Mzee Kingunge Ngombale Mwiru enzi za uhai wake.
RATIBA ya mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, iliyotolewa na familia yake leo inaonyesha atazikwa kesho Jumatatu katika shughuli itakayoanza saa 9:30 hadi 11:30 katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati maalum ya shughuli hiyo, Omary Kimbau, inaonyesha kwamba mwili wa marehemu utatolewa leo saa 10 jioni Hospitali ya Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwake Victoria/Makumbusho ambako ibada na mila zitafanywa usiku mzima.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shughuli zitakazofanywa kesho ni kama ifuatavyo:
Jumatatu tarehe 5/2/2018
– Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
– Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi kupata kifungua kinywa
– Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani kwa marehemu
– Saa 6:00 mwili kuwasili Karimjee Hall kuagwa
– Saa 6:00 mchana 9;00 kuaga mwili wa marehemu
– Saa 9:00 alasiri mpaka 9:30 kuelekea makaburini Kinondoni
– Saa 9:30 mpaka 11:30 maziko
– Saa 11:30 jioni 12:30 kuelekea nyumbani kwa chakula cha jioni
1:30 usiku mpaka. 2:45 chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 usiku- waombolezaji wote hitimisho la shughuli nzima
Kingunge Ngombale-Mwiru alifariki Ijumaa wiki hii katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akitibiwa majeraha baada ya kuumwa na mbwa wake.
No comments:
Post a Comment