Saturday, 25 November 2017

Beka Flavour - Sarafina (Official Video)


Shambulio la Msikiti laua 235 Misri




Wanamgambo wametekeleza shambulio la bomu na ufyatuaji wa risasi katika msikiti mmoja uliopo kaskazini mwa eneo la Sinai na kuwaua takriban watu 235 kulingana na chombo cha habari cha taifa.

Walioshuhudia wanasema kuwa msikiti wa al-Rawda katika mji wa Bir al-Abeid , karibu na al-Arish ulilengwa wakati wa ibada ya Ijumaa.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa wanaume wanne waliokuwa ndani ya gari moja waliwafyatulia risasi waliokuwa wakiabudu kulingana na chombo cha habari cha AP.

Misri imekuwa ikikabiliana na wanamgambo katika eneo hilo tangu 2013.
Kumekuwa na mshambulio ya mara kwa mara yanayolaumiwa kutekelezwa na wanamgambo katika rasi ya Sinai lakini hilo ni shambulio baya zaidi kuwahi kufanyika.

Ripoti moja inasema kuwa waliolengwa ni wafuasi wa maafisa wa usalama waliokuwa wakitekeleza ibada katika msikiti huo.

Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa wafuasi wa madhehebu ya Sufi hukongamana katika msikiti huo.

Makundi ya wanajihad likiwemo lile la Islamic State wanawaona wasufi kama watu wasioamini.
Rais Abdul Fattah al-Sisi anatarajiwa kukutana na maafisa wa usalama kuzungumzia kisa hicho .

Kocha K'Njaro Stars kuwapeleka wachezaji Ulaya




Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars Ammy Ninje, amesema yupo tayari kuwasaidia wachezaji wa Tanzania kwenda kucheza soka barani Ulaya.

Ammy Ninje ambaye ataiongoza timu hiyo kwenye michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya mapema mwezi ujao amesema yeye yupo tayari kutumia uzoefu wake barani Ulaya kuwatafutia timu wachezaji watakaoonesha viwango.

“Mimi nina ‘Network’ ya walimu wenzangu kwenye nchi za Ulaya kama Sweden, hivyo nitawasaidia wachezaji wenye vipaji vya kucheza Ulaya kuweza kupata vilabu ili wakacheze soka la kulipwa, na kama nchi tuwe na ‘professional’ wengi”, amesema Ammy Ninje.

Kocha huyo ameyasema hayo kwenye mahojiano na kipindi cha Hotmix  jioni ya leo Novemba 24, ambapo amesema yupo tayari kutumia uzoefu wake wote ili nchi ifanikiwe na kufikia viwango vya mataifa kama Uganda na zaidi ya hapo.

Kuhusu michuano ya Challenge Ninje, amesema atajipanga vyema na kikosi cha wachezaji 20 ambao aliwataja hivi karibuni kwaajili ya michuano hiyo na anaamini wakishirikiana vyema wataibuka mabingwa.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Desemba 3 na kumalizika Desemba 17 nchini Kenya ambapo Tanzania ipo kundi moja na timu za Zanzibar Heroes, Rwanda, Libya na wenyeji Kenya. Kilimanjaro Stars itacheza mchezo wa ufunguzi Desemba 3 dhidi ya Libya.

Kumbe Cantona anamkubali Pep zaidi ya Mourinho



Mchezaji nguli wa zamani wa Manchester United Eric Cantona amesema anamkubali kocha wa timu hiyo Jose Mourinho lakini anapenda kuiona klabu yake hiyo ya zamani inacheza kama kikosi cha Pep Guardiola, Manchester City.

Cantona, ambaye alicheza Manchester United kwa  miaka mitano kati ya 1992 na 1997,amemwelezea Mourinho kama kocha mwenye mbinu nyingi za kushinda lakini si kuifanya timu icheze vizuri kama ilivyo kwa Pep Guardiola ambaye huvifanya vyote kwa pamoja.

"Wote Guardiola na Mourinho ni makocha wazuri, lakini mimi napendelea mchezo wa kushambulia zaidi kuliko kujihami kama ambavyo Mourinho anafundisha na huo sio utamaduni wa Manchestweerr United”, amesema Cantona.

"Sielewa kwa nini United ilichukua meneja ambaye anacheza kwa mbinu za kujihami kila wakati.Nampenda Mourinho, lakini napenda kutazama Barcelona ikiwa inacheza kwasababu soka lao linavutia”, ameongeza Cantona.

Cantona amemaliza kwa kuweka wazi kuwa anapenda kuangalia timu inayofundishwa na Guardiola na angependa kuona Mhispania huyo anaifundisha Manchester United kwasababu mara zote soka lake huwa ni lakuvutia zaidi.

Serikali yatoa muongoza wa upigaji chapa



Serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi imetoa muongozo wa upigaji chapa mifugo kufuatia kuibuka kwa changamoto ya upigaji holela unaoharibu ngozi hali inayoweza kuifanya bidhaa hiyo kukataliwa kwenye soko la ndani na nje ya nchi

Akizungumza mjini Dodoma wakati wa utoaji elimu wa zoezi hilo, kaimu mkurugenzi wa utafiti mafunzo na ugani katika wizara ya  mifugo na uvuvi, Dk. Erastus Mosha, amesema sehemu ambayo ni salama na isiyo na madhara ya upigaji chapa katika zao la ngozi ni mguu wa nyuma kulia mwa mnyama juu kidogo ya goti wakati.

Naye afisa mifugo manispaa ya Dodoma, Kiboma John, amesema zoezi hilo linatarajiwa kufikiwa na kata 40 lakini linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo la uhaba wa fedha, vitendea kazi na rasilimali watu, na kusababisha kwenda kwa kusuasua hivyo wameiomba serikali kuisaidia manispaa katika zoezi hilo.

Mkutano wa Chadema wavamiwa na watu wasiojulikana




Watu  wasiofahamika  wamevamia  na kuvunja vifaa vya muziki vilivyopangwa kutumika katika mkutano wa kampeni za udiwani wa Kata ya Mbweni wilayani Kinondoni.

Meya wa Ubungo, Boniface Jacob  akiwa pamoja na Mbunge , Tarime Vijijini John Heche na Mbunge wa Kawe Halima Mdee ameliambia gazeti hili  leo Novemba 24, 2017 kuwa tukio lilitokea saa 9 alasiri katika uwanja wa  Mbweni Vijijini.

 Jacob ambaye pia ni diwani wa Kata ya Ubungo, amesema  wakati watu wakiwa pembeni wakisubiri viongozi na wanachama kufika eneo hilo ghafla lililotekea gari ndogo lililobeba vijana hao ambao walishuka na kufanya uharibifu huo.

“Walivunja muziki wote uliokuwa uwanjani kisha kuvunja kioo cha gari la matangazo  lililokuwa likitumika kuhamasisha watu kuhudhuria mkutano huu,” amesema Jacob.

Amesema hadi sasa bado hawajawatambua  watu hao ambao wamefanya uharibifu huo na kwamba, hali ya utulivu imerejea katika eneo baada ya polisi kuwasili na wakati wowote mkutano utaanza wa kumnadi mgombea wao.

Waziri Ummy ahimiza wananchi kuwa na Bima ya Afya



Waziri wa Afya,  Ummy Mwalimu amesema mrundikano wa wagonjwa wengi katika meli ya Wachina, umetokana na wananchi wengi kukosa bima za afya.

Kufuatia hilo Ummy ametoa siku 60 kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuhakikisha wanaanza kutoa bima za afya kwa watoto za kulipa kidogokidogo,  huku akiwataka kuongeza idadi ya wanachama.

Ameyasema hayo leo Novemba 24 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima ya afya, vyeti vya kuzaliwa na kadi za benki kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

"Ile meli ya Wachina watu wamejazana pale maana yake watu hawawezi kufikia gharama za matibabu na ndiyo maana wanakwenda kule ni bure, kama watu wana bima huna haja kusubiri meli ya Wachina mtu anakuja Muhimbili lakini watu wanasubiri vya bure," amesema.

Amesema mfuko huo unapaswa kuunganisha watu na kulipa kidogokidogo ili kila mwananchi aweze kupata kadi ya matibabu itakayomuwezesha kutibiwa kwa wakati.

Amesema alishawaambia NHIF kuanzisha fao la wajawazito kujifungulia popote, ambapo amewataka walikamilishe kabla hajawasilisha bajeti ya wizara hiyo bungeni.   

Ametoa rai kwa wananchi kujiunga na mifuko ya bima ya afya huku akiitaka mifuko mingine ya bima za afya kutengeneza mazingira rahisi na yenye bei za kiushindani ili kuvutia watu kujiunga.

"Mimi mtu akiwa tayari kutengeneza fao la watoto nipo tayari kwa hospitali zetu na hata kadi za mama na mwana,  wakina baba hawatashindwa kuchangia 50400 hadi mtoto atakapofikisha mwaka mmoja haiwezekani," amesema.

Ametoa wito kwa wazazi, walezi kuhakikisha watoto wao wanakuwa na uhakika  wa matibabu  kabla ya kuugua kwa kumkatia kadi ya bima ya afya  ya sh50400.

Lukuvi awataka walionunua viwanja wakadai fedha zao Halmashauri


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefuta viwanja vilivyokuwa vimepimwa katika  eneo la Mawelewele pamoja na mchoro wake kwa madai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu.

Lukuvi amewataka  watu wote walionunua viwanja katika eneo hilo waende ofisi za Halmashauri ya Manispaa kudai fedha zao.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM kupitia Chama hicho  Baraka Kimata  kwenye kata ya Kwiru.

 Lukuvi amesema  amefikia uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali na pia kufanya uchunguzi wake binafsi.

 “Nimefuta mchoro  wa upangaji eneo lile na ule wa upimaji yote nimefuta leo(jana) na nimeagiza watu waliouziwa eneo lile waende wakadai fedha zao halmashauri iwarudishie” amesema Lukuvi na kuongeza

“Haiwezekani leo hatuna vyumba vya madarasa vya kutosheleza halafu unachukua eneo kubwa kama lile unaligawa kwa watu wachache” amesema

Katika hatua nyingine Lukuvi aliwataka wakazi wa Kitwiru kuchagua Kimata na kwamba mara atakapoichaguliwa yeye atafika katika kata hiyo kusikiliza kero za ardhi.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo Alex Kimbe amesema  uamuzi huo ni wa kisiasa na umelenga kurudisha nyuma maendeleo katika halmashauri hiyo.

Amesema  eneo hilo ni  mtu binafsi ambaye ni Japan Kiluka  ambaye alilitoa  kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Msingi Mawelewele.

Amesema  mmiliki alikuwa na malalamiko yake ya muda mrefu Alisema mmiliki huyo aliomba katika viwanja vilivyopimwa apewe viwanja 18 na vinavyobaki iwe mali ya halmashauri jambo ambalo walilitekeleza.

 “Niwatoe hofu wananchi wa Iringa ,wale wote walionunua viwanja tutajipanga tutawarejeshea fidia zenu, lakini nisisitize kuwa uamuzi huo utaigharimu  Manispaa zaidi ya Sh 40 milioni kwani kila kiwanja kiliuzwa kwa Sh 5 milioni” amesema

Naye  Diwani wa kata ya Mshindo Ibrahimu Ngwada amesema hatua ya upimaji wa viwanja hivyo ililenga kuwanufaisha watu wachache na kwamba yeye alikuwa analishitaki suala hilo kwa waziri.

 Mwananchi.


Huu ndiyo Ugonjwa Utokanao na Msongo wa Mawazo


Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi, kutokuwa na mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi.

Masuala ya kijamii ambayo hupelekea msongo ni kama kupoteza mtu umpendaye, ndoa kuvunjika, kupoteza kazi, kuongezeka majukumu ya kifedha, magonjwa sugu, matatizo ya familia na mengineyo mengi.

Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe  na siyo sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo.

Ufuatayo ni ugonjwa unaosabishwa na msongo:

Magonjwa ya moyo
Watu walio na msongo (Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya moyo. Magonjwa haya ya moyo ni kama shinikizo la juu la damu, moyo kwenda mbio na mengineyo.

Matabibu wanafahamu kuwa, msongo wa ghafla waweza kusababisha magonjwa hatari ya moyo kama shambulizi la moyo. Watu wenye matatizo ya moyo hawana budi kuepuka hali ya msongo na kujifunza jinsi ya kukabiliana na maisha katika hali ya utulivu kwa kadiri iwezekanavyo.

Hivyo ili uweze kuepuka ugonjwa huu unachoptakiwa kufanya ni kuhakisha unaepuka visababishi vyote vya ugonjwa  huu vya msongo, ambavyo nimekwisha vielezea hapo awali.


IGP Sirro awaasa wananchi kufanya uchaguzi kwa amani


MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro amewatahadharisha wananchi kote nchini kutokuvuruga uchaguzi wa marudio wa udiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sirro amesema kuwa, jeshi lake limejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa zoezi hilo la uchaguzi litafanyika kwa amani na utulivu na kwamba ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya uchaguzi ili kuzuia aina yoyote ya uvunjifu wa amani utakaojitokeza.

“Natoa rai kwa wananchi walioko kwenye maeneo hayo kushiriki zoezi hili la uchaguzi kwa amani na utulivu na wakishapiga kura warejee kwenye maeneo yao na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa huku wakisubiri kutangazwa kwa matokeo,” alisema Sirro.

Kamanda Sirro vilevile amezungumzia hali ilivyo kwa sasa katika maeneo ya kibiti na Rufiji kuwa hali ni shwari na wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.

“Kuhusiana na uharifu wa kutumia silaha katika Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji tumefanikiwa kuwakamata waharifu waliokuwa wakijihusisha na matukio haya ambao wamekiri kufanya matukio mbalimbali ya mauaji na baadhi yao wamekimbilia nchi za jirani ikiwemo Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya CONGO lakini hata hivyo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi. Lakini tutaendelea kuwashughulikia hata huko walikokimbilia.

Friday, 24 November 2017

Ronaldo na wachezaji wenzake wa Real Madrid wapewa Magari



 Cristiano Ronaldo na wachezaji wenzake wa Real Madrid wamekabidhiwa magari yao.

Wachezaji hao wamepewa magari kutoka kwa mdhamini wao Audi ambaye kila mwaka hutoa magari kwa wachezaji wa klabu hiyo.

Wakati wanakabidhiwa magari hayo kila mtu akikabidhiwa lake, Madrid walikuwa bado wanasherekea ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Apoel katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.







Mugabe na mkewe wasusia sherehe ya kuapishwa kwa Mnangagwa



Robert Mugabe na mkewe Grace walikosa kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Emmerson Mnangagwa baada ya wananiasa hao kukubaliana kwamba Mugabe anaweza kupumzika.

Sababu kuu ilioteolewa ni kwamba bwana Mugabe alikuwa amechoka.

Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana hadharani tangu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 kujiuzulu kama rais kufuatia shinikizo kutoka kwa jeshi na raia.

Hatua hiyo inajiri baada ya Mugabe na mkewe kufumta kazi rais huyo mpya wakati alipokuwa makamu wa rais kwa madai kwamba alikuwa akipanga njama za kutaka kumuondoa madarakani rais Mugabe

Aliyekuwa makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa amewataka raia wa Zimabwe kusalia watulivu na kuweka amani na kutolilipiza kisasi.

Umati mkuwa wa takriban raia 60,00 wa Zimbabwe wakiwemo viuongozi wa kimataifa na wanadplomasia walihudhuria sherehe ya kumuapisha Mnangagwa katika uwanja wa michezo wa mjiini harare.

Upinzani umemtaka rais mpya kukabiliana na ufisadi.wakati rais Mugabe alipolazimishwa kuondoka madarakani siku ya Jumanne baada ya jeshi kuchukua mamlaka kulikuwa na sherehe matika maeneo tofauti ya taifa hilo.

VIDEO: Full video ya Wasomali walionaswa na TCRA



Raia watatu wa Somalia wamekamatwa kwa kosa la kuingiza vifaa vya mawasiliano  bila leseni, na kuunganisha mitambo hiyo bila kufuata sheria za nchi.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..... USISAHAU KUSUBSCRIBE