
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amewataka wanasiasa na viongozi wa serikali wenye mamlaka ya kikatiba na sheria kutoingia utendaji wa Mahakama na kuheshimu Muhimili huo.
Jaji Ibrahimu ameyasema hayo jijini Dar es salaam, wakati akifafanua siku ya maadhimisho ya siku ya sheria nchini itakayo adhimishwa Februali Mosi Mwaka huu.
“Nadhani hayo ni mambo ambayo yamekuwa yanatakiwa kwa mujibu wa Katiba unapokuwa na Katiba kazi moja ni kugawa mamlaka na mamlaka moja inapoingia kwenye mamlaka nyingine tayari unaondoka kwenye misingi ya Katiba.Mimi naomba Mahakimu ambao amri zao zinavunjwa na hawaonekani wakichukua hatua nadhani tuwe tunafanya kama Bunge wanavyofanya ukiingia kwenye anga la Bunge utaitwa mbele ya Kamati utaulizwa maswali na hatua huwa zinachukuliwa,” alisema Jaji Mkuu.
“Ninawasihi viongozi wote wa Serikali wenye mamlaka za kikatiba na kisheria wabaki ndani ya maeneo yao ya kikatiba na wajiepushe na kingilia maeneo yaliyo ndani ya haki, hadhi na mamlaka ya kikatiba ya Mahakama.”
“Mahakama tuna nguvu kama hiyo na sio Jaji ndio Mwenye nguvu hiyo ila nguvu hiyo iko kwenye kila Mahakama asitokee mtu akajivika kofia ya kimahakama atachukuliwa sheria”,aliongeza.
Wiki ya sheria mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment