Thursday, 25 January 2018

JPM amwagiwa pongezi na Rais wa Benki ya maendeleo

Rais John Magufuli amepongezwa na mjumbe maalum wa Rais wa Rwanda na aliyewahi kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka kwa kuweza kuweza kusimamia ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

Pongezi hizo zimetolewa leo wakati Rais Magufuli alipokutana na mjumbe na kufanya mazungumzo katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Tanzania na umoja wa Afrika (AU), yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

"Nimefurahi sana jinsi Tanzania inavyokwenda mbele, maendeleo yanakwenda kwa kasi na Mhe. Rais anafahamu kabisa kwamba katika Afrika nchi zetu zinahitaji kuwa na uchumi bora, ningependa kumpongeza Mhe. Rais na watanzania wote kwa kazi nzuri wanayofanya", alisema Dkt. Kaberuka.\

No comments:

Post a Comment