Friday, 26 January 2018

Watu zaidi ya 30 wafariki katika ajali ya moto Korea Kusini


Hospitali yaungua moto Korea Kusini

Zaidi ya watu 30 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya moto uliyotokea katika Hospitali moja nchini Korea Kusini. Hata hivyo maofisa wanasema idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kutoka katika ya majeruhi hao.

Imefahamika kuwa moto huo ulianzia katika chumba cha dharura cha Hospitali ya Sejong, kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Zaidi ya majeruhi 100 wanasemakana wamo katika jengo la hospitali hiyo.

Picha za mitandao ya jamii, zinaonyesha vikosi vya zima moto wakijaribu kukabiliana na moto huo huku kukiwa na moshi mkubwa.

Mwaka jana watu 29 walikufa katika mji wa Echeon, Korea Kusini, na wengine kujeruhiwa baada ya moto kuzuka katika sehemu ya mazoezi ya wazi.

No comments:

Post a Comment