Wanaume watatu waliokunywa dawa za kuongeza nguvu za kiume huko nchini Zambia wamejikuta wakilazwa hospitali baada ya kuanza kutapika nakuharisha mfululizo baada ya kutumia dawa hizo.
Vyombo vya habari nchini Zambia vimeeleza kuwa wanaume hao walilazwa kwa makosa kwenye vituo vya zahanati za kuhudumia wagonjwa wa kipindu pindu wakidhaniwa kuwa wanaugua kipindu pindu hadi baadaye walipokuja kukiri kuwa walikunywa dawa za kuongeza nguvu za kiume na ndio zimepelekea waharishe na kutapika.
Kwa mujibu wa mtandao wa The Mast Online wa nchini humo umeeleza kuwa wanaume hao walikuja kubainika kuwa hawaugui kipindupindu wakati Kiongozi Mkuu wa Jimbo la Mashariki nchini Zambia, Chanda Kasolo alipotembelea kujua idadi ya wagonjwa juzi (Jumatano) katika Hospitali ya Katete jimboni humo..
“Mpaka kufikia jana kulikuwa na kesi mbili za wagojwa waliolazwa kutoka Lusaka, hivyo idadi ya wagonjwa imeongeka kutoka 24 hadi 26 jambo ambalo limeongeza hofu kwenye jamii yetu. Na kingine cha kushangaza jana tumepata wagonjwa wengine watatu kutoka Katete eneo ambalo halijawahi kupatwa kabisa na kipindu pindu lakini baada ya uchunguzi wa madaktari tumebaini kuwa Wagonjwa hao hawakuwa wanaugua Kipindu Pindu,“amesema Kasolo na kuelezea kilichowakumba.
“Baada ya majibu ya vipimo kupatikana , inaonekana kuwa wanaume hao walikutwa na mchanganyiko wa pombe, vyakula na dawa za kienyeji ambazo zilisababisha mchafuko wa mfumo wa chakula na hivyo ikahusishwa na kipindupindu lakini baada ya kuwauliza maswali, baadaye walikiri kuwa walikunywa dawa ya kuongeza nguvu,”amesema Kasolo.
Hata hivyo tayari wanaume hao wamehamishwa kwenye hospitali hiyo inayolaza wagongonjwa wa kipindu pindu na kulazwa kwenye hospitali ya kawaida.
Mpaka sasa vifo vya watu wapatao 70 vimeripotiwa kutokea tangu mwaka jana kwa kesi za ugonjwa wa kipindu pindu .
Mwishoni mwa mwaka jana Rais wa Zambia, Edgar Lungu alitangaza kuwa ugonjwa huo ni janga la taifa huku akitaka kila mwananchi kuwajibika kwa usafi.
No comments:
Post a Comment