Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Edward Lowassa jioni leo amemnadi Mgombea wa Ubunge wa Kinondoni kupitia chama hicho, Salumu Mwalimu huku akiwataka wakazi wa Kinondoni kuacha kumuongelea mgombea wa CCM, Maulid Mtulia maana amekuwa msaliti kwao.
Lowassa alitumia wakati huo pia kuwashukuru wananchi wa Kinondoni kwa kumpigia kura wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, na kuwaomba zile kura walizompigia 2015 basi wazielekeze kwa Mwalimu ambaye anaamini ni msomi mwenye kuweza kuwatetea wakazi wa Kinondoni.
" Msiogope vijana wa Kinondoni wenzetu wamekuwa wajanja wakilinda kura zao sasa na sisi kama ambavyo wazungumzaji wengine wamesema basi tunaomba mlinde kura zetu ikiwezekana tulale katika vituo vya kupigia kura kuhakikisha hatuibiwi.
Nae Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu, Fredrick Sumaye alisem, " Hakikisheni mnamchagua Mwalimu huyu ndie mtu safi wa kuhakikisha analeta maendeleo katika jimbo lenu,"
Kwa upande wake Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, alisema " Achaneni na wao wanaosema mimi sio mkazi wa hapa nachoomba ni kura zenu ambazo zitanifanya nikawatetee kuwajengea shule, kuhakikisha ajira kwa vijana,"
Kampeni za chama hicho zitaendelea kesho katika eneo la Kigogo jijiji Dar es Salaam ambapo zitaongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe.
No comments:
Post a Comment