Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Wilaya wa Kinondoni, Harold Maruma amesema mgombea ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya chama hicho, Maulid Mtulia atatumia uzinduzi wa kampeni kueleza mikakati yake ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
CCM inazindua kampeni leo Jumamosi Januari 27,2018 kuanzia saa 10:00 jioni katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
Maruma amesema baadhi ya changamoto zitakazozungumzwa na mgombea huyo ni barabara na mikopo kwa akina mama.
"Tunaomba wakazi wa Kinondoni kujitokeza kwa wingi na Jeshi la Polisi limetuhakikishia kuwa hakuna mtu atakayedhurika wakati wa kampeni na wakati wa kurudi nyumbani," amesema.
Wengine wanaoshiriki uzinduzi wa kampeni hizo ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba na wabunge wake wa mkoa wa Dar es Salaam.
Tayari viongozi wakuu wa chama hicho tawala waliofika katika uwanja wa Biafra wametambulishwa na kuipisha bendi ya bendi ya TOT inayotoa burudani ya nyimbo za kuhamasisha wana CCM.
No comments:
Post a Comment