Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kesho Januari 27, 2018 watakuwepo katika uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Kinondoni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo inasema kuwa viongozi hao watakuwepo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni kumtambulisha Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Salum Mwalimu.
Uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika viwanja vya Mapilau kuanzia saa nane mchana mpaka saaa kumi na mbili jioni ambapo wageni rasmi watakuwepo Lowassa pamoja na Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA.
Tarehe 17 Februari mwaka huu unatarajiwa kufanyika uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Siha na Kinondoni kutokana na wabunge wa majimbo hayo kujiuzulu nafasi zao za Ubunge wakiwa katika vyama vya upinzani na kuingia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa wanagombea nafasi hizo wakiwa chini ya CCM.
No comments:
Post a Comment