Saturday, 3 February 2018

Mose Iyobo awachezeshea kichapo Shilawadu


 Watangazaji wa Kipindi maarufu cha Shilawadu kinachorushwa na Clouds tv,Soudy Brown na Kwisa wamechezea kichapo kutoka kwa Dancer wa Diamond,Mose Iyobo,usiku wa kuamkia  ijumaa,baada ya kutaka kumuhoji kuhusu matukio yaliyotokea hivi karibuni kati ya familia yake na mwanadada Tunda.

Wakithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Shilawadu wameandika katika ukurasa wao wa instagram:

Kazi yetu ina changamoto kubwa sana..asilimia kubwa ya ma star wanatuunga mkono.

Usiku wa Leo wakati tukiwa kazini tumenusurika kumwagwa damu na mtu tuliemfuata kumuomba kufanya naye mahojiano,kati yetu kuna walioumia viuno,mikono, etc.kuna uharibifu wa vifaa vyetu vya kazi umetokea pia,wenzetu wanaendelea na matibabu Mungu  ni mwema  Mungu ni wetu sote na hili litapita bado tuna wasiwasi tu kama mhusika ataendelea kututafuta kwa ajili ya kutudhuru zaidi,tunasikitishwa sana na matumizi ya nguvu dhidi yetu sisi Wanyonge #Shilawadu

Kuna watu watasema Shilawadu wamezidina kusahau kuwa sisi ni wana Habari kama wanahabari wengine na kupata habari ni haki ya kila mwananchi kama ilivyo haki nyingine yoyote ile.Kifungu cha 18 cha katiba  ya Jamhuri ya Muungano 1977 na hatimaye kufanyiwa marekebisho mwaka 2005 inampa haki mtu na uhuru wa kujieleza na kutoa mawazo,uhuru wa kutafuta habari,kupata habari,na kuneza habari bila kujali mipaka,pia sheria hiyo inampa haki mtu ya kuwasiliana bila kubughudhiwa na mawasiliano na kufahamishwa wakati wowote masuala yoyote muhimu yahusuyo maendeleo yake na yahusuyo jamii yake kwa ujumla.

Imeandikwa na Mtayarishaji wa Kipindi cha Shilawadu Benedict Noel

Mourinho atoa ujumbe huu kwenye birthday ya mtoto wake


 Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amemtakia furaha ya kuzaliwa mwanawe wa kiume Zuca baada ya kutimiza miaka 18 huku akiposti picha ya utotoni inayomuonyesha wakiwa pamoja katika kiboti.

Meneja huyo wa Man United ameposti picha hiyo huku akiandika “Furaha ya kuzaliwa Zuca sasa unamiaka 18 huitaji uwepo wangu tena kwenda kuogelea pamoja katika kiboti,”ameandika Mourinho kupitia mtandao wake.

Picha hiyo inamuonyesha Mourinho akiendesha kiboti hicho huku akiwa na Zuca.

Mwaka jana Mourinho aliwahi kumtakia furaha ya kuzaliwa mwanawe kwa kuposti ujumbe unao fanana na huo.

Zuca anacheza nafasi ya goli kipa katika academy ya Fulham akiwa amesaini kandarasi ya miaka miwili  akiwa na umri wa miaka 16.

Hapo hawali Zuca alikuwa akiitumikia klabu ya Chelsea na Real Madrid wakati timu hizo zikitumikiwa na baba yake.

Baada ya kumdiss Donald Trump, Diego Maradona yamkuta makubwa


Gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutoswa visa ya kwenda nchini Marekani kutokana na matamshi aliyoyatoa dhidi ya raisi Donald Trump.

Maradona ana kesi na aliyekuwa mke wake aitwaye Claudia Villafane na alipaswa kwenda hadi Miami kusikiliza kesi hiyo lakini maofisa wa uhamiaji walimuwekea ngumu kupata visa ya kwenda nchini humo.

Maradona siku zilizopita alisikika katika moja ya interview zake akimuita raisi Donald Trump “chirolita” jina ambalo kwa Waargentina linatumika kwa watu ambao ni vibaraka wa watu wengine.

Baada ya Maradona kushindwa kwenda nchini Marekani sasa itabidi wakili wake akwee pipa kuelekea Miami kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo huku ikiwa bado haijafahamika kwamba inawezekana ukawa mwisho wa Maradina kwenda Marekani ama laa.

Huu ni muendelezo wa matukio na visa vya Maradona nje ya uwanja, kwani miaka ya karibuni amekuwa akiyafanya na kwa sasa mchezaji huyo yuko falme za kiarabu kama kocha wa klabu ya Al Fujairah.

Manula, Bocco, Ndemla wapokea tuzo za mwezi


KIPA chaguo la kwanza wa Simba, Aishi Manula amekabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa Wekundu wa Msimbazi katika sherehe fupi iliyofanyika juzi  nyumbani kwa Balozi wa Uturuki, Ali Davotuglu.

Manula, ambaye pia ni kipa chaguo la kwanza la timu ya Taifa (Taifa Stars) alishinda tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mechi nne zilizopita za ligi hiyo inayotarajiwa kuingia kwenye raundi ya pili kuanzia leo.

Mbali na Manula, wachezaji wengine waliopata tuzo katika sherehe hiyo pamoja na nahodha na mshambuliaji aliye kwenye kiwango cha juu, John Bocco na kiungo, Said Ndemla.

"Hizi ni tuzo ambazo zinatolewa na klabu yetu katika kuhamasisha wachezaji wafanye vizuri katika kila mechi wanayocheza na vile vile kusaidia kuipa timu ushindi," alisema Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara.

Aliongeza kuwa katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na viongozi wa klabu hiyo pamoja na mwekezaji na bilionea, Mohamed Dewji "Mo", walifanya mazungumzo mbalimbali na kubadilishana mawazo ili kuifanya timu ifikie malengo yake msimu huu.

"Tunaamini hatua hii tuliyofika, itakuwa na matokeo chanya kwa sababu tutaimarisha mahusiano," Manara aliongeza.

Mume aliyeweka pilipili kwenye nguo ya mkewe aadhibiwa


Mahakama moja wilayani Lira nchini Uganda imemuhukumu mwanamume kifungo cha siku 40 kutumikia jamii baada ya kupatikana na hatia ya kupaka pilipili nguo ya ndani (chupi) ya mkewe.

Akisoma hukumu, hakimu Hilary Kiwanuka alisema ushahidi uliotolewa mahakamani umejitosheleza pasipo kuacha shaka kwamba mtuhumiwa Moses Okello alitenda kosa hilo.

Okello, mkazi wa Kijiji cha Barmola, Kaunti Ndogo ya Bala wilayani Kole atatakiwa kufanya kazi za kijamii katika kipindi cha siku 40 kutokana na kosa hilo.

Mahakama ilielezwa Januari 20,2018, Okello alipaka pilipili kwenye nguo hiyo na baadaye alimshauri mkewe aivae.

“Alinishauri kuivaa siku hiyo, nilipoivaa nilianza kuwashwa na mwasho huo haukuisha hata nilipooga,” mwanamke huyo aliieleza Mahakama.

Haikuelezwa ni kwa nini Okello aliamua kufanya kitendo hicho kwa mkewe ingawa baadaye alidai alikuwa akimtania.

Magufuli awatunuku 197


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 197 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Sherehe hizo zimefanyika leo Februari 3, 2018 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo maofisa hao wapya ni wa Tanzania na kutoka nchi marafiki,  waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha.

Katia tukio hilo ambalo lilipambwa na magwaride kutoka kwa Wanajeshi hao, lilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kitaifa.

Miongoni mwa waliotunukiwa kamisheni hizo wanawake ni 28, na waliobaki ni wanaume.

Majeruhi wailiza Azam FC


Kuelekea mchezo wa marudiano raundi ya pili ya ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC, klabu ya soka ya Azam FC imesema inakabiliwa na majeruhi wengi akiwemo nahodha wa kikosi hicho Himid Mao.

Akiongelea mchezo huo msemaji wa timu hiyo Jaffary Idd amesema pamoja na majeruhi hao lakini timu ina kikosi kipana hivyo mwalimu Aristica Cioaba amewaandaa wengine kupambana kwaajili ya kupata alama tatu.

Wachezaji wengine ambao ni majeruhi ndani ya kikosi hicho ni Waziri Junior, Joseph Kimwaga na Joseph Mahundi, wakati Abubakar Salum 'Sure Boy' anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

Azam FC inaingia katika mchezo wa leo utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex ikiwa katika nafasi ya pili na alama 30, nyuma ya Simba yenye alama 35 kileleni. Ndanda inashika nafasi ya 8 ikiwa na alama 16.

Mafuta ya Petroli kuanza kuchimbwa Septemba mwaka huu Morogoro


Serikali imesema mradi wa uchimbaji mafuta katika Kisima kilichoanishwa kuchimbwa kwenye eneo la kijiji cha Ipera Asilia, kwenye hifadhi tengefu ya bonde la Kilombero, mkoani Morogoro, unatarajiwa kuanza rasmi mwezi Septemba, 2018 ambapo kisima hicho kinakadiriwa kuwa na mafuta kuanzia lita milioni 180 hadi 200.

Akizungumza jana Februari 2, 2018 katika kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha nne cha mkutano wa 10 wa Bunge mjini Dodoma, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kinachosubiriwa ni kibali kutoka Baraza la Mazingira nchini (NEMC) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), ili uchimbaji huo uanze rasmi.

“Mkataba ulishasainiwa tangu mwaka 2012 kilihobaki ni utekelezaji wa uchimbaji na ugunduzi wa mafuta, mafuta yanayotarajiwa kuchimbwa kwenye eneo hilo yanafikia milionii 180 hadi 200, mtaji ni mkubwa na utakua na manufaa kwa wananchi wako na nchi kwa ujumla,” alisema na kuongeza.

“Kinachosubiriwa ni kibali cha mazingira kutoka NEMC na mamlaka ya TAWA, mwezi Julai mwaka huu tumehakikishiwa mkataba utapatikana na Septemba uchimbaji utaanza rasmi.”

Serikali kupitia shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) liliingia mkataba wa utafiti na uchimbaji wa gesi na uvunaji mafuta na Kampuni ya Mafuta na gesi ya Swala (Swala Oil), ambapo katika utekelezaji wa mkataba huo iligundulika kuwepo kwa wingi mafuta ya petrol na gesi katika vijiji vya Mtimbira.

VIDEO: Ifahamu Dini Ya Kingunge Na Mengine Usioyajua



Enock Ngombale ambae ni mdogo wa Kingunge Ngambale Mwiru amefunguka kuhusu maisha ya kaka yake tangu alipozaliwa  na kusema kuwa kuna wakati unaweza ukawa huna dini lakini kuna wakati itakulazimu urudi kwenye imani yako, hivyo kaka yangu atazikwa Kikatoliki kama kanisa watakubali tunachosema sisi ndugu zake tunayemjua.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

VIDEO: Aunty Ezekiel Aomba msamaha Shilawadu


Baada ya shilawadu, kunusurika kugongwa na gari ya mose iyobo na kuharibu mali ikiwemo, gari na kamera aunty ezekiel apiga simu na kuomba msamaha shilawadu pamoja na kutaka kuwa wavumilivu akirudi wayamalize


TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..............USISAHA KUSUBSCRIBE.......................

Friday, 2 February 2018

DC Matiro akabidhi hundi za mikopo mil 25 vikundi vya vijana na wanawake

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi hundi za mikopo shilingi milioni 25 kwa vikundi vitatu vya vijana na kimoja cha wanawake zilizotolewa na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Fedha hizo zinatokana na asilimia 10 ya makusanyo kutoka katika vyanzo vya mapato ndani ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Julai 2o17 hadi Disemba 2017.

Vikundi vilivyokabidhiwa hundi ni kikundi cha Wanawake na Maendeleo kilichopo katika kijiji cha Ishololo kata ya Usule na vikundi vya vijana vya Umoja wa bodaboda, Jikwamue, Shukrani Group vilivyopo katika kijiji cha Didia kata ya Didia katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Akikabidhi hundi hizo kwa wawakilishi wa vikundi hivyo leo Ijumaa Februari katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo,Matiro aliwataka walionufaika na mikopo hiyo watumie pesa walizopata kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Kila mtu aliyepata pesa akafanye kile alichokusudia kufanya, serikali inajitahidi kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo ili mjikwamue kiuchumi,naomba mfanye kazi kwa bidii ili kubadilisha maisha yenu”,alieleza Matiro.DC

Utawala wa Jordani umekata mahusiano ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.


Katika gazeti rasmi, imeandikwa kuwa "Baraza la Mawaziri lilipitisha Azimio No. 6056 la Januari 15, ambalo linasema kusimamishwe kwa mahusiano ya kidiplomasia na Korea ya Kaskazini".

Kwa mujibu wa habari,balozi wa Korea Kaskazini nchini Jordan atasimamishwa kazi.

Afisa Mkuu wa Jordan amesema  kwamba uamuzi wa kukata mahusiano na Korea Kaskazini ni kutokana na maslahi ya serikali.

Umoja wa Mataifa umeiwekea Korea Kaskazini vikwazo kutokana na majaribio yake ya makombora ya nyuklia.

Helikopta mbili zagongana nchini Ufaransa


Ndege mbili za jeshi la Ufaransa zimegongana na kusababisha vifo vya watu watano,katika mji wa Marseille kusini mwa Ufaransa.

Gazeti la Var Metin limeripoti kuwa ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi karibu na ziwa la Carces.

Ripoti zinaonyesha kuwa helikopta zilikuwa na jumla ya abiria sita na hivyo mmoja bado hajulikani alipo.

Timu za uokoaji zinaendelea kumtafuta abiria wa sita.

Gavana wa mkoa huo amesema kuwa helikopta hizo zilikuwa za shule ya kujifunza Urubani ya jeshi la Ufaransa na ajali hiyo imetokea mile 50 kutokea mji wa kitalii wa Saint Tropez.