Monday, 22 January 2018

Kagera Sugar imejiandaa kuikwamisha Simba


Klabu ya Simba SC leo inarejea kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, sehemu ambayo ina kumbukumbu ya kukwamishwa mipango yake ya kusaka ubingwa msimu uliopita.

Kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime, amesema timu yake imejiandaa kwa muda mrefu hivyo leo inaingia uwanjani kupambana na vinara wa ligi Simba SC huku lengo likiwa ni kusaka alama tatu.

''Hali ya hewa leo hapa Bukoba ni jua tu na hali ya uwanja ni nzuri, tumefanya maandalizi kwa muda mrefu leo tuna kazi moja tu ya kucheza mpira kwaajili ya kupata alama tatu kwasababu mpira ndio kazi yetu'', amesema Mexime.

Timu hizo zinakutana kwenye mchezo wa raundi ya 14 ambapo Simba wanahitaji alama tatu ili kuweza kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi. Simba kwa sasa ina alama 29 nyuma ya Azam FC yenye alama 30.

Msimu uliopita Simba ikiwa inaelekea kwenye hatua za mwiosho za kusaka ubingwa ilitibuliwa mipango na Kagera Sugar April 2, 2017 ilipokubali  kipigo cha mabao 2-1 hivyo kuiacha Yanga katika mazingira mazuri ambayo mwisho wa ligi waliibuka mabingwa.

Magogo yaliyokosa mmiliki bandarini kuuzwa wakati wowote kuanzia sasa



Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema magogo 938 yaliyopo Bandari ya Dar es Salaam yatauzwa wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukosa wamiliki wa mzigo huo.

Maamuzi hayo yamekuja  baada ya Waziri Kigwangalla mwezi uliopita kufanya ziara ya kushitukiza bandarini hapo baada ya kupata taarifa kuwa kuna shehena hiyo ya magogo ambayo umiliki wake ulikuwa na utata.

Mhe. Kigwangalla alieleza kuwa magogo hayo yamekuwa bandarini kwa miaka 10 huku mengine yakiwa kwenye makontena 55 .

Kutokana na utata huo, Kigwangalla alitoa siku 30 kwa wamiliki wa makontena 55 kujitokeza wakiwa na nyaraka zote ili kuthibitisha kama kweli yalivunwa Zambia kama ilivyodaiwa au laah!.

“Kulikuwa na vikao mbalimbali ndani ya serikali kujadili suala hilo, na tumekubaliana kuyauza baada ya wahusika kutojitokeza kuthibitisha umiliki wake,” amesema Waziri Kigwangalla.

Waziri Kingwangalla amesema jukumu la kuyauza magogo hayo wamepewa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) wanaoruhusiwa kisheria kufanya kazi hiyo, ambapo watashirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS).

Kauli ya Salum Mwalimu kuhusu wanaodai kuwa sio mkazi wa Kinondoni


Mgombea ubunge wa Kinondoni kupitia Chadema, Salum Mwalimu amwajibu baadhi ya watu wanaodai kuwa yeye si mkazi wa wilaya ya Kinondoni, hivyo hana sifa za kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Akizungumza leo Januari 22, 2018 katika mahojiano na kituo cha tevisheni cha Azam, Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema- Zanzibar amesema ni mkazi wa wilaya hiyo na anajua matatizo ya wananchi wake.

 “Nilianza maisha Kinondoni baada ya kumaliza chuo. Nimeishi kwa miaka 14 na niko Kinondoni kwa miaka zaidi ya 30. Kwa nini Kinondoni? Si kwamba fursa zimejitosheleza lakini ninaifahamu na ninayajua matatizo ya Kinondoni kuhusu barabara, afya na elimu.”

Amesema alipomaliza Chuo Kikuu mwaka 2008 aliishi mtaa wa Togo kisha  akahamia Hananasif, kufafanua kwamba madai kwamba si mkazi wa Kinondoni hazina ukweli wowote.

Kuhusu suala la kugombea ubunge akiwa na wadhifa Chadema amesema, “Ninachotafuta ni uwakilishi wa wananchi, kwa sasa ni mwakilishi ndani ya chama. Hata  CCM kuna wenye vyeo viwili. Tunatafuta mwakilishi madhubuti ndani ya Bunge na katika chama chetu hakuna changamoto ya kofia moja au mbili.”

“Kama ni kofia mbili au moja mbona kuna mawaziri ambao ni wabunge, ili uwe  mbunge ni lazima uwe raia wa Tanzania,  lakini mbona Rais John Magufuli ni mwenyekiti wa CCM, mbona Rais wa Zanzibar ni makamu mwenyekiti wa CCM, kwa hiyo hilo la vyeo halitupi shida.”

Amesema yeye kiuhalisia ni mzaliwa wa Kikwajuni Zanzibar huku akigusia kwa kifupi kwamba anaungwa mkono na CUF.


AT: Tuzo zangu za Marekani siwezi kuzipasua


Msanii wa muziki Bongo, AT amesema hawezi kuzipasua tuzo zake alizoshinda nchini Marekani November mwaka jana, 2017.

Muimbaji huyo katika mahojiano na kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm amesema awali alipanga kupasua tuzo zake za Kilimanjaro Music Award (KTMA) zilizokuwa zikitolewa hapa nchini lakini baadaye akagundua kuwa tuzo hizo ni mali ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

“Ni baada ya kuomba msaada ili nisaidiwe kwenda Kongo nikafanye kolabo na Koffi Olomide, wakanizungusha sana, ilikuwa hasira tu, ila hizi tuzo zangu za Marekani siwezi kuzipasua,” amesema AT.

November mwaka jana AT alishinda tuzo mbili katika ‘B&K Music & Video Music Awards’, vipengele alivyoshinda ni International Artist na Best Music Video kupitia wimbo wake ‘Sili Feel’.

Kingozi CCM awataka Wananchi Kuwaombea JWTZ Waliopo Kongo


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewasihi wananchi wa Tanzania   kuendelea kuwaombea Dua na visomo mbali mbali Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanaouawa  wakilinda Amani katika nchini mbali mbali ikiwemo DRC Kongo.

Pia ameliomba Jeshi hilo pamoja na familia za ndugu wa marehemu Askari 10 waliofariki waliofariki siku za hivi karibuni wakilinda Amani Kongo, kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Wito huo ameutoa leo mara baada ya kumalizika shughuli ya kisomo cha Khitma na Dua ya pamoja ya Arubaini ya kuwaombea marehemu hao iliyoandaliwa na Kamati ya Amani Kitaifa Zanzibar huko katika Msikiti wa Noor Muhammad (SAW) kwa Mchina Mwanzo Zanzibar.

Dk.Mabodi ameeleza kwamba Askari hao watakumbukwa daima kwa mchango wao wa kutetea na kulinda maisha ya Waafrika katika Nchi ya Kongo ambapo walikuwa wakiiwakikisha Tanzania kupitia Jeshi la Pamoja la Umoja wa Mataifa lililopo nchini humo kwa ajili ya kulinda Amani.

Aliwambia wananchi kuwa Mashujaa hao hakuna cha kuwalipa kwa sasa kwani wamepoteza uhai wao kutokana na uzalendo uliotukuka hivyo kilichobaki ni kuwaombea Dua wao Mwenyezi Mungu awapumzishe pahala pema peponi Amini na kuziombea familia zao ziendelee kuwa na subra.

Amefafanua kuwa msiba huo mzito ni sehemu ya Askari wa Majeshi mbali mbali ya Ulinzi na Usalama nchini wanaoendelea na kazi zao za kawaida wawe imara Kifkra na Kimwili bila kukata tamaa ili kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa Kituo kikuu cha Amani Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

Akizungumzia matunda ya kulinda misingi ya Amani nchini Dk.Mabodi amesema ni kuwepo kwa maendeleo katika Nyanja mbali mbali za Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii.

“Wananchi tulinde tunu ya Amani na Utulivu tuliokuwa nao katika Taifa letu, ili tuweze kuwa Mabalozi wazuri wa kulinda Amani kwa nchi jirani na Mataifa mengine.”, amesisitiza.

“Nawapongeza Kamati ya Amani ya Taifa Zanzibar kwa maandalizi yao mazuri ya kuandaa shughuli ya kuwaombea Dua kubwa kama hii vijana wetu waliouwawa na watu wanaosadikiwa kuwa Waasi huko Nchini Kongo.”, amesema Dk.Mabodi.

Aidha ameeleza kuwa wananchi wanatakiwa kujenga utamaduni wa kuenzi Amani na Utulivu, uliopo nchini kwa lengo la kuepuka machafuko na migogoro isiyokuwa ya lazima nchini.

Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Hussein Mwinyi, amewashukru wananchi mbali mbali waliojitokeza katika Khitma hiyo kwa lengo la kuwaombea Dua Marehemu Askari hao.

Amesema licha ya Tanzania kuwapoteza Mashujaa hao bado Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) litaendelea kuwa imara na kulinda mipaka na kushiriki harakati mbali mbali za kulinda amani hata nje ya Tanzani kwa lengo la kudumisha mahusiano mema na nchi nyingine Duniani

Baada ya kuona picha ya mtoto akiomba jezi yake, Samatta afunguka


 Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta licha ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili lakini ameonesha kuzidi kupendwa na mashabiki wa club yake.

Moja kati ya ujumbe unaosambaa kwa sasa katika mitandao ya kijamii ni pamoja na post ya bango ya shabiki mtoto wa KRC Genk ikiwa imeandikwa “Mbwana Can I have Your Shirt Pendeza” akiwa kamaanisha “Mbwana unaweza kunipa jezi yako? Pendeza”

Baada ya Mbwana Samatta kuona post ya picha ya mtoto huyo akajibu “Ndio naweza kukupa kwa nini ishindikane” hiyo imezidi kudhihirisha mapenzi ya dhati ya mashabiki kwa Mbwana Samatta maana sio kila mchezaji soka huwa anapata nafasi ya kupendwa na mashabiki kwa kiwango hicho.

Wenger atakuwepo George Weah akiapishwa?


Wananchi wa Liberia wanasubiria kwa hamu tukio la kuapishwa kwa Rais mteule George  Weah, ambapo wengi wamekesha katika uwanja wa mpira wa taifa hilo, mahali ambapo leo January 22, 2018 anategemea kuapishwa na kuandika historia mpya kutoka kung’aa kwenye soka hadi kuwa Rais

George Weah, maisha yake ya utoto, yalikuwa katika mazingira duni katika mji mkuu wa Liberia Monrovia, alipata mafanikio makubwa katika  soka na kufanikiwa kuchezea timu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Chelsea, Monaco na AC milan.

Ni Muafrika pekee kuwahi kushinda tuzo mchezaji bora wa FIFA na tuzo ya Ballon. Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa Maseneter katika bunge la Liberia.

Aligombea urais mwaka 2005 na alimshinda Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini akashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki.

Aliyewahi kuwa meneja wa George Weah katika klabu ya Monaco ya ligi kuu ya Ufaransa Arsene Wenger amealikwa na atakuwepo katika tukio la kuapishwa.

Wazazi wanashikiliwa na Polisi kwa kupokea mahali ya Ng'ombe saba


JESHI la Polisi mkoani Geita linawashikilia watu  wawili wakazi wa  Kijiji cha Kasubuya  wilayani Nyang’wale kwa kula njama wakiwa wazazi  kupokea mahari ya ng’ombe saba na kumwozesha  mwanafunzi wa  kidato cha pili.

Binti huyo  aliyekuwa anasoma katika shule ya sekondari Nyijundu, sasa ana ujauzito.

Aliyethibitisha kukamatwa kwa wazazi hao wa pande zote mbili ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Mponjoli Lotson na kuwataja ni baba mzazi wa msichana huyo, Herman Makanika (48) na Maximillian Makila ambaye ni baba mzazi wa mtuhumiwa aliyemuoa mwanafunzi huyo.

Ingawa hakulitaja jina la mtuhumiwa, Kamanda Mpojoli alimpongeza mwalimu wa shule ya sekondari aliyetoa taarifa  za kuwapo kwa tukio hilo na akabainisha  jinsi wazazi wa pande zote mbili walivyoshiriki  kutenda kosa licha ya mtuhumiwa kutoroka.

Alisema wazazi wa pande zote mbili wanahusika ingawa mtuhumiwa (muoaji) anaendelea kusakwa, hivyo wanapaswa kuwajibika kutokana na kufanya makubaliano kwa kutoa mahari ya ng’ombe saba na mzazi wa msichana kuwapokea ng’ombe hao kama mahari.

Aliongeza kuwa baada ya polisi kuarifiwa ilichukua hatua za haraka na watuhumiwa kukamawta na hadi jana walikuwa wanaendelea kushikiliwa huku juhudi za kumsaka mtuhumiwa zikiendelea kuhakikisha anapatikana na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Ronaldo apasuliwa uso



LICHA ya ushindi wa bao 7-1 dhidi ya Derpotivo la Coruna walioupata Real Madrid katika La Liga, mshambuliaji wake, wa Kimataifa Raia wa Ureno, Cristiano Ronaldo alikutana na dhoruba baada ya kuumia kwa kupasuka usoni.

Ronaldo aliumia kwa kuchanipa sehemu ya usoni baada ya kugongwa wakati akijaribu kufunga.

Alikuwa ameruka kichwa kwa lengo la kufunga lakini akagongana na mchezaji wa Derpotivo. Hata hivyo, Ronaldo alipata huduma nzuri na kilichovutia zaidi ni yeye kutumia simu ya daktari kuangalia kama alikuwa ameumia au la.

Nduda awasihi mashabiki na wapenzi wa Simba SC



Mlinda mlango wa kimataifa wa klabu ya Simba Said Mohamed Nduda amewataka mashabiki na wapenzi wa wekundu wa msimbazi kuwa na subira katika kipindi hiki kwa madai ana matumaini timu yake watachukua ubingwa safari hii.

Nduda ameeleza hayo wakati akizungumza na mwandishi wa 'East Afrika Television' baada ya kuwepo nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kutoka na matatizo ya goti aliyoyapata akiwa mazoezini pindi timu yake ilipokuwa ikijiandaa kwa mchezo dhidi ya watani wao jadi.

"Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu hali yako kwa sasa naendelea vizuri na ninafuata maelekezo ya daktari ya kufanya mazoezi kama anavyoniambia, hapa nasubiri tu kauli yake kama ataniruhusu nianze mazoezi uwanjani ili niungane na wenzangu", alisema Said Nduda.

Pamoja na hayo Nduda aliendelea kwa kusema "nahisi mwezi Februari utakaoanza ninaweza nikawa nimerejea uwanjani, napenda kuwaambia mashabiki wa Simba kuwa na subira katika kipindi hichi kwa kuwa nina imani timu yetu itafanya vizuri na kukinyakua kikombe"

Kwa upande mwingine timu ya Simba itarajia kushuka dimbani alasiri ya leo (Jumatatu) kuvaana na Kagera Sugar katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa 14.

Sunday, 21 January 2018

Audio | Best Nasso – Sabuni Ya Roho | Mp3 Download

Audio | Best Nasso – Sabuni Ya Roho | Mp3 Download

Audio | Best Nasso – Sabuni Ya Roho | Mp3 Download

DOWNLOAD Mp3

Audio | Best Nasso _ SABUNI YA ROHO | Official Song

Audio | Best Nasso _ SABUNI YA ROHO | Official Song

Audio | Best Nasso _ SABUNI YA ROHO | Official Song

Faiza ampa somo Diamond



Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Faiza Ally amempa ushauri msanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kuwa kwa sasa ni muda wake wa kula ujana na kuizunguuka dunia na sio muda wa kujipa majukumu mazito ile hali umri wake bado mdogo.

Faiza Ally amesema Diamond bado hajamaliza hata robo ya dunia hivyo ingawaje ana jina kubwa barani Afrika hivyo angefanya kwanza vitu kama hivyo kuizunguuka dunia ikibidi ajiweke kando na mambo ya mahusiano.

“Diamond kijana mdogo sana anahitaji kuhave funny na watoto wenzie na sisi wadada wazima lazima taungalie watu wa kutoka nao, Go baba have a funny enjoy the world ndio useto down,“ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumshauri kuwa ikibidi ajiweke mbali na mahusiano.

“Jiachie uwe huru ikibidi usiwe na mahusiano, bado hujaiona dunia hata robo wewe ni star hela ipo there is alot to see nasema with clean heart no hate kwa Zari au kwa yeyote.“ameandika Faiza.

Ushauri huo umekuja ikiwa ni wiki sasa imepita tangu kuenee tetesi kuwa Diamond Platnumz yupo kwenye mahusiano na msichana maarufu kwenye mitandao ya kijamii anayejulikana kwa jina la Tunda.