Mlinda mlango wa kimataifa wa klabu ya Simba Said Mohamed Nduda amewataka mashabiki na wapenzi wa wekundu wa msimbazi kuwa na subira katika kipindi hiki kwa madai ana matumaini timu yake watachukua ubingwa safari hii.
Nduda ameeleza hayo wakati akizungumza na mwandishi wa 'East Afrika Television' baada ya kuwepo nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kutoka na matatizo ya goti aliyoyapata akiwa mazoezini pindi timu yake ilipokuwa ikijiandaa kwa mchezo dhidi ya watani wao jadi.
"Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu hali yako kwa sasa naendelea vizuri na ninafuata maelekezo ya daktari ya kufanya mazoezi kama anavyoniambia, hapa nasubiri tu kauli yake kama ataniruhusu nianze mazoezi uwanjani ili niungane na wenzangu", alisema Said Nduda.
Pamoja na hayo Nduda aliendelea kwa kusema "nahisi mwezi Februari utakaoanza ninaweza nikawa nimerejea uwanjani, napenda kuwaambia mashabiki wa Simba kuwa na subira katika kipindi hichi kwa kuwa nina imani timu yetu itafanya vizuri na kukinyakua kikombe"
Kwa upande mwingine timu ya Simba itarajia kushuka dimbani alasiri ya leo (Jumatatu) kuvaana na Kagera Sugar katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa 14.
No comments:
Post a Comment