Sunday, 15 October 2017

Clement Sanga Wa young Africans Amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya Wa TPLB

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amempongeza Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ligi Kuu, Clement Andrew Sanga wa Young Africans kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa TPLB baada ya kupata kura 10 kati ya 16.
Katika katika uchaguzi uliofanyika leo Oktoba 15, 2017 kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mpinzani wa Sanga, Hamad Yahya Juma wa Mtibwa Sugar alipata kura sita kati ya 16 za Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Wakati Sanga akichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Shani Christoms Mligo wa Azam FC alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa TPLB. Shani aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo alipata kura 15 kati ya 16 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Nafasi tatu za kuwakilisha klabu za Ligi Kuu kwenye Kamati ya Uongozi zilivutia wagombea wawili; Hamisi Mshuda Madaki (Kagera Sugar) na Ramadhani Marco Mahano (Lipuli) ambao wote wameshinda. Madaki alipata kura 12 na Mahano 13.
Almasi Jumapili Kasongo kutoka Ashanti United FC ni mgombea pekee aliyejitokeza kuwania nafasi ya uwakilishi wa klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 35 kati ya 40 zilizopigwa.
Edgar William Chibura kutoka Abajalo FC alishinda nafasi ya Ujumbe kutoka Klabu za Ligi Daraja la Pili ambako zina nafasi moja kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB. Chibura alipata kura 35 kati ya 40.
“Natuma salamu zangu za pongezi kwa wote walioshinda. Nina imani nao kwamba tutashirikiana vema, kufanya kazi katika sekta ya mpira wa miguu, najua wanajua changamoto za ligi yetu hivyo naamini wataweza,” amesema Rais Karia mara baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli kutangaza matokeo.
Mapema kabisa leo asubuhi, Rais Karia aliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Kamati mpya ya Uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) waliochaguliwa leo Oktoba 15, 2017.
Rais Karia aliyeambatana na Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred alitoa ahadi hiyo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Baraza la TPLB uliofanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
“Tupo kwenye kikao hiki ambacho pia kitachagua viongozi wakaoongoza miaka minne ijayo, viongozi watakaochaguliwa leo kwa nia njema wataongoza Bodi kwa miaka minne…
“Bahati nzuri nilikuwa mmoja wa viongozi wa kwanza wa Bodi ya Ligi. Kwa hiyo najua changamoto tangu uundwaji wake. Hivyo nakifahamu chombo hiki vema, najua kwa undani malengo ya chombo hiki, lazima tuyafikie.
“…Lakini niwahakikishie tu kwamba hatutafika kama tutaendesha shughuli zetu bila uwazi, uadilifu na uwajibikaji,” amesema Rais Karia.
“Naahidi kuona kamba chombo hiki kipo huru. TFF itakuwa ikifanya monitoring. Tukiona mambo hayaendi sawa, hatutasita kukaa nanyi watu wa Bodi ili tushirikiane kuweka mambo sawa, mvumiliane huku mkifuata taratibu,” amesema.
Rais Karia amesema kwamba uadilifu, uwazi na uwajibikaji upo zaidi kwa lengo la mpira wa miguu kuchezwa kwa weledi ili tupate mabingwa wa kweli katika mashindano yanayosimamiwa na kuendeshwa na TFF.
Rais Karia aliasa viongozi wa klabu kubadilika na hasa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa TPLB, “Nami nitatoa ushirikiano kwenu.”
Awali kabisa Mwenyekiti wa TPLB, Hamad Yahya akimkaribisha Rais Karia, aliwakaribisha viongozi wote waliohudhuria huku akiwapa pole kwa safari ndefu hadi kuja kwenye mkutano.
Baada ya matokeo, Yahya alirudi tena kuzungumza na Wajumbe ambako aliwashukuru kwa ushirikiano waliompa wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa TPLB na kuahidi, “Nipo bado kwenye mpira tutaendelea kushirikiana. Uchaguzi umekwisha, hakuna makundi.”
Kwa upande wake, Sanga alimshukuru Mungu na wajumbe wote kwa uchaguzi wa amani na utulivu, ishara inayompa nguvu kutekeleza vema majukumu yake mapya.

RC Gambo Amesema hana mpango Wa kugombea ubunge mkoa Arusha,,,,,

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema hana mpango wa kugombea ubunge Arusha Mjini ila anachofanya sasa ni kutekeleza ahadi za Rais John Magufuli za kutatua kero za wananchi.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana, Gambo alisema wanaosambaza uvumi kuwa atagombea ubunge ni wanasiasa ambao hawajiamini na wameshindwa kutatua kero za wananchi.
“Kazi ambazo nafanya kwa kushirikiana na wasaidizi wangu wakuu wa wilaya ni kutatua kero na tumeachana na mambo ya kisiasa, sisi tunachapa kazi,” alisema.
Alifafanua kuwa baadhi wabunge hawaonekani majimboni na kuwaachia viongozi wa Serikali kufanya kazi zilizopaswa kufanywa na wabunge.
Akizungumzia tuhuma za kununuliwa madiwani wa Chadema zilizotolewa na wabunge wa chama hicho, alisema anaamini hakuna masuala ya rushwa.
Gambo alisema madiwani hao wamejiuzuru baada ya kuridhishwa na utendaji kazi mzuri wa Rais Magufuli.
“Kuna madiwani wa Arusha, Monduli, Ngorongoro, Arumeru, Hai, Iringa na maeneo mengine hawa wote wameridhishwa na utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano,” alisema.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro alisema wilaya hiyo imefanikiwa kutatua kero za wananchi ikiwamo upatikanaji wa huduma muhimu.
Hata hivyo, alitoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza katika shughuli ya uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa

Waziri Mwigulu : Tutahakikisha sheria inabadilishwa,,,,,,,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema wizara yake itahakikisha inawabana ipasavyo wahamiaji haramu pamoja na kubadilisha sheria ili ziwabane zaidi.
Waziri Mwigulu ameyasema hayo alipotembelea Gereza la Kigongoni wilayani Bagamoyo na kugundua robo tatu ya wafungwa ni wahamiaji kutoka nchi jirani ikiwemo Ethiopia.
Taarifa ya Mkuu wa magereza Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, SACP Boyd Mwambingu imebainisha kuwa wafungwa ambao ni raia wa Ethiopia waliofungwa katika Magereza ya Mkoa huo ni 334, Mahabusu 12 na wanaosubiri kusafirishwa ni 91 ambao jumla ya raia kutoka Etheopia ni 437 wa Malawi ni 1 Msomali ni 1 wa DRC ni 1 wa Burundi 2 na Kenya ni 2.
Kufuatia taarifa hiyo Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesema haiwezekani wahamiaji haramu wagharamikiwe na taifa ikiwemo kusafirishwa kwa gharama za serikali pamoja na kupatiwa Chakula na Matibabu.
“Tutafanyia kazi ili sheria iseme kama watakamatwa watafungwa au mambo mawili, nchi yao iwachukue au warudi kwa gharama zao wenyewe lakini sheria lazima iwe kali itakayotoa fundisho kwa wengine”, amesema Mwigulu.

MICHEZO : WACHAMBUZI WA SOKA WAUPONDA MFUMO WA MOURINHO,,,,

Msimu wa ligi kuu Uingereza wakati unaanza kila mtu alimsifu Jose Mourinho kwa kuibadilisha United, walionekana wanacheza soka la kuvutia sana tofauti na msimu wa mwaka juzi.
Lakini baada ya mechi 7 ambazo hawakucheza na timu ngumu sana, jana United walipata kipimo chao cha kwanza baada ya kukanyaga katika uwanja wa Anfield kucheza dhidi ya majogoo wa London Liverpool.
Mambo yalibadilika na United walicheza ambavyo hakuna aliyetarajia, wakawa United wale wale wa kurudi nyuma kusubiri mipira ije huku wakiwaacha Liverpool kuushikilia mchezo wote.
Baada ya mchezo huo kuisha sasa sio mashabiki tu bali hata wachambuzi wa soka walianza tena kubeza mfumo wa kocha Mourinho dhidi ya timu kubwa na kudai kwamba unaboa sana kuangalia kama walivyocheza jana.
Mourinho mwenyewe amewaambia wanaoponda kwamba kila mtu auchukulie huo mchezo auchukuliavyo na hakwenda Anfield kujaribu kumburudisha mtu yeyote bali walikwenda kucheza soka.
Mourinho anadai kama kipindi cha pili aliona ugumu kufanya mabadiliko kutokana na Liverpool walivyokuwa wakicheza huku baadhi ya wachezaji wake muhimu akiwemo majeruhi mpya Eric Bailly wakiwa hawamo ndio maana akacheza mchezo huo unaokera kuangalia.
Cha kushangaza zaidi kuhusu Mou na Manchester United yake ni mashuti mawili tu waliyopiga golini kwa Liverpool katika michezo miwili, yaani shuti moja kila mchezo suala linaloonesha ni jinsi gani United wamekuwa wanajilinda tu.
Liverpool hawako katika kiwango kizuri sana na ni wazi kwamba kwa uwezo wa United ilitarajiwa jana wangejaribu kuwasukuma na kucheza mpira lakini wao wakacheza kama wanacheza na Barcelona au Real Madrid.
Mou anaonekana labda ni muoga kufungwa kutokana na alivyoanza msimu kwa mbwembwe lakini pamoja na yote United wamepata alama 1 Anfield inayowaweka nafasi ya pili nyuma ya vinara wa ligi Manchester City.

Larry Flynt atangaza zawadi ya dola milioni 10 kumuondoa Trump Madarakani

Mchapishaji wa jarida la picha chafu za utundu, Larry Flynt, amechapisha tangazo katika gazeti la Washington Post, akiahidi kulipa zawadi ya dola milioni 10, kwa mtu mwenye habari, zitazopelekea Rais Trump kushtakiwa na kuondoshwa madarakani.
Bwana Flynt, anayemiliki jarida la "Hustler", amesema ni wajibu wa kila Mmarekani, kumuondoa Bwana Trump, kabla ya kuchelewa.
Tangazo hilo, linatoa nambari ya simu ya kupiga na anuani ya barua pepe.
Larry Flynt, ambaye alikuwa mfuasi mkubwa wa Hillary Clinton katika kuania urais, ametoa matangazo kama hayo kabla, lakini hakuwahi kutoa zawadi kubwa kama hiyo.

Idadi ya waliofariki kwenye milipuko Mogadishu yazidi kuongezeka

Sasa imebainika kuwa idadi ya watu waliouawa katika mashambulio mawili ya mabomu mjini Mogadishu, Somalia, imepanda na kuwa zaidi ya 80.
Haijulikani nani alihusika, lakini kwa idadi ya maafa, hayo yalikuwa kati ya mashambulio makubwa kabisa nchini Somalia, tangu kundi la wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabab, kuanza mapigano yao mwaka 2007.
Katika shambulio la kwanza, bomu lilokuwa kwenye lori, lililipuka kwenye njia panda, iitwayo Kilomita-5, ambapo kuna ofiisi za serikali, mahoteli na maduka, vyote viliporomoka katika mlipuko huo.
Saa mbili baadaye, bomu jengine lilikalipuka katika mtaa wa Medina.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Madina, Mohamed Yusuf Hassan, anasema, alishtushwa na ukubwa shambulio hilo

Bodi mpya ya ligi kuu kujulikana leo

Kamati ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), leo inatarajiwa kupata viongozi wapya kufuatia uchaguzi mkuu utakaofanyika leo Oktoba 15 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salam.
Jumla ya wajumbe 44 wanashiriki Mkutano huo wa uchaguzi wa Baraza Kuu la TPLB. Wajumbe hao ni klabu 16 za Ligi Kuu, klabu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na wawakilishi wanne wa klabu za Ligi Daraja la Pili.
Wanaowania nafasi ya Mwenyekiti wa TPLB ni Clement Andrew Sanga kutoka Yanga na Hamad Yahya Juma wa Mtibwa Sugar. Nafasi ya makamu mwenyekiti inawaniwa na Shani Christoms Mligo wa Azam FC.
Nafasi tatu za kuwakilisha klabu za Ligi Kuu kwenye Kamati ya Uongozi zinawaniwa na wagombea wawili ambao ni Hamisi Mshuda Madaki (Kagera Sugar) na Ramadhani Marco Mahano (Lipuli).
Almasi Jumapili Kasongo kutoka Ashanti United FC amejitokeza kuwania nafasi ya uwakilishi wa klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Wakati Edgar William Chibura kutoka Abajalo FC anawania nafasi ya uwakilishi ya klabu za Ligi Daraja la Pili kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB.

Trump hana uwezo wa kufuta mkataba wa nyuklia na Iran - Mogherini

Muakilishi wa Umoja wa Ulaya wa mambo ya njee Federica Mogherini asema kuwa rais Trump hana uwezo wa kufıuta mkataba wa nyuklia uliosainiwa bain aya Marekani na Iran
Federica Mogherini akiwakilisha Umoja wa Ulaya asema kuwa msimamo wa rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mkataba wa nyuklia uliosaini na Iran amesema kuwa rais wa Marekani hana uwezo wa kufut mkataba huo.
Mogherini aliyazungumza hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini Brussels nchini Ubelgiji kunakopatikana ofisi za Umoja huo.
Umoja wa Ulaya umepinga msimamo wa Donald Trump kuhusu mkataba wa nyuklia.
Mogherini aliendelea kusema kuwa mkataba huo hauhusu taifa moja pekee kufuta mkataba huo.

Burudani : Nuh Mziwanda Afunguka maumivu anayoyapata,,,,,

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuh Mziwanda ambaye hivi karibuni ameachana na mke wake, amesema kuwa kitendo hicho kinamuumiza sana kwani anakosa muda wa kuwa na mtoto wake, na anahisi mtoto wake atakuwa bila kupata malezi yake.
Kwenye ukurasa wake wa instagram Nuh Mziwanda ameandika ujumbe akionyeshwa kuumizwa na kuwa mbali na mtoto wake huku akilelewa na watu wengine, wakati yeye baba yake yupo, lakini anashindwa kutimiza wajibu wake wa kumlea kutokana na ugomvi uliopo kati yake na mama mtoto wake ambaye wameshaachana, huku akijtahidi
"Nakumiss sana Mwanangu Anya, yani Mungu anajua jinsi gani Moyo wangu unaenda mbio nikikukumbuka au ukinijia akilini, maana najua haufurahi, najua hauhisi upendo kama uliokua unahisi kipindi upo karibu yangu, napenda ningekukuza kwenye misingi yangu, sheria zangu na kanuni zangu kama baba yako, ukweli nipo kwenye wakati mgumu sana sana kwa ajili yako wewe tu, najitatahidi kucheka ila ukweli naumia na majonzi mengi juu yako", ameandika Nuh Mziwanda.
Nuh Mziwanda ameendelea kuandika ujumbe huo akisema anamwachia Mungu kwa yote yanayotokea, huku akimlaumu mama mtoto wake kwa malezi ambayo anampa, kwani sio yale anayostahili mtoto wa umri wake kuyapata.

NEWS : Watu 10 wamefariki katika Ajari ya moto Saudi Arabia,,,,,,,

Moto umeripotiwa kuwaka katika warsha ya useremala mjini Riyadh nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa habari,moto huo umesababisha vifo vya watu 10 huku wengine watatu wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
Sababu ya moto haijajulikana mpaka sasa.

MICHEZO: Ibrahim Ajib Azidi kumpoteza Niyonzima,,,,,,

Haruna Niyonzima na Ibrahim Ajib ni wachezaji waliozungumzwa sana wakati wa dirisha la usajili kabla ya kuanza kwa msimu huu kwa sababu ya kuhama kutoka klabu zao na kujiunga na mahasimu wa klabu walizozihama. Ajib kutoka Simba kwenda Yanga Niyonzima kutoka Yanga kwenda Simba.
Inatajwa kwamba Ajib alisajiliwa na Yanga kwa Tsh. 50 Mil pamoja na gari ndogo ya kutembelea (Toyota Brevis). Wakati huo ikielezwa Niyonzima ndiye mchezaji ghali kusajiliwa msimu huu baada ya kuvuta mtonyo unaokadiriwa kufika Tsh. 120 Mil.
Baada ya ligi kuanza Ajib ameshafunga magoli matatu na ku-assist moja katika mechi sita alizocheza huku Yanga ikiwa imefunga magoli sita kwenye ligi wakati Niyonzima bado hajafunga wala kutoa assist katika magoli 14 ambayo Simba imefunga hadi sasa, amecheza mechi nne kati ya tano.
Ibrahim Ajib
Njombe Mji 0-1 Yanga (Ajib)
Yanga 1-0 Ndanda (Ajib)
Kagera Sugar 1-2 Yanga (Ajib-assist goli la kwanza likafungwa na Chirwa, yeye akafunga la pili).
Haruna Niyonzima
Simba 7-0 Ruvu Shooting (hakufunga wala ku-assist)
Azam 0-0 Simba
Mbao 2-2 Simba (hakufunga wala kutoa assist)
Stand United 1-2 Simba (hakufunga wala ku-assist)
Ligi bado inaendelea bado kuna fursa ya kuona mambo mengi kutoka kwa mafundi hawa wawili ndani ya ligi yetu, Niyonzima anaweza akanyanyuka na kumfikia Ajib hata kumwacha lakini pia inawezekana Ajib akaendelea kumkimbiza Niyonzima kama ilivyo sasa hivi.

RB Leipzig yaiyadhibu Borussia Dortmund 3-2

Borussia Dortmund (4-3-3): Burki; Toljan (Pulisic 45), Papastathopoulos, Toprak, Zagadou; Castro, Sahin (Weigl 45), Gotze; Yarmolenko, Aubameyang, Philipp (Bartra 51)
Subs not used: Weidenfeller, Isak, Dahoud, Kagawa
Goals: Aubameyang 4, 64
Yellow Cards: burki 48; Gotze 72
Red Cards: Papastathopoulos 47
RB Leipzig (4-2-2-2): Gulacsi; Fernandes, Ilsanker, Upamecano, Halstenberg; Kampl, Keita (Demme 45); Sabitzer (Orban 86), Bruma; Poulsen, Augustin (Laimer 65)
Subs not used: Forsberg, Werner, Schmitz, Mvogo
Goals: Sabitzer 10; Poulsen 25; Augustin 49 (pen)
Yellow Cards: Fernandes 30; Ilsanker 54; Keita 15; Demme 83
Red Cards: Ilsanker 56

MAGAZETI YA LEO,,, OCTOBER 15