Monday, 22 January 2018

Mwenyekiti UVCCM amtupia kombora Salum Mwalimu


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Kheri James amemfananisha Mgombea Ubunge, Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CHADEMA, Salum Mwalimu sawa na bibi harusi na kuwa wao CCM watashinda uchaguzi huo.

James amesema kuwa Watanzania wanakipenda sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati huu kuliko wakati mwingine wowote hivyo ni lazima Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya (CCM), Maulid Mtulia ashinde.

"Kinondoni tunakwenda kushinda nimesikia Kamati ya harusi imemchagua Bibi harusi mmoja, hawa wanacheza siasa ya diblo dibala mara wamo mara hawamo lakini faida tuliyopata safari hii wametuletea mtu mwenye historia ya kushindwa, kaomba Ubunge kwao huko visiwani kapigwa, kaomba Ubunge wa Afrika Mashariki kapigwa na Kinondoni atapigwa, nachohitaji Kinondoni nataka kipigo kitakatifu ili baada ya kushindwa Salum Mwalimu aache siasa atafute biashara nyingine" alisema Kheri James

Mbali na hilo Mwenyekiti wa UVCCM amedai kuwa Salum Mwalimu ni mbuzi wa kafara wa CHADEMA kuwa kila shughuli ngumu wanamtuma yeye ili akafe wao wabaki.

No comments:

Post a Comment