Saturday, 3 February 2018

Majeruhi wailiza Azam FC


Kuelekea mchezo wa marudiano raundi ya pili ya ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC, klabu ya soka ya Azam FC imesema inakabiliwa na majeruhi wengi akiwemo nahodha wa kikosi hicho Himid Mao.

Akiongelea mchezo huo msemaji wa timu hiyo Jaffary Idd amesema pamoja na majeruhi hao lakini timu ina kikosi kipana hivyo mwalimu Aristica Cioaba amewaandaa wengine kupambana kwaajili ya kupata alama tatu.

Wachezaji wengine ambao ni majeruhi ndani ya kikosi hicho ni Waziri Junior, Joseph Kimwaga na Joseph Mahundi, wakati Abubakar Salum 'Sure Boy' anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

Azam FC inaingia katika mchezo wa leo utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex ikiwa katika nafasi ya pili na alama 30, nyuma ya Simba yenye alama 35 kileleni. Ndanda inashika nafasi ya 8 ikiwa na alama 16.

Mafuta ya Petroli kuanza kuchimbwa Septemba mwaka huu Morogoro


Serikali imesema mradi wa uchimbaji mafuta katika Kisima kilichoanishwa kuchimbwa kwenye eneo la kijiji cha Ipera Asilia, kwenye hifadhi tengefu ya bonde la Kilombero, mkoani Morogoro, unatarajiwa kuanza rasmi mwezi Septemba, 2018 ambapo kisima hicho kinakadiriwa kuwa na mafuta kuanzia lita milioni 180 hadi 200.

Akizungumza jana Februari 2, 2018 katika kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha nne cha mkutano wa 10 wa Bunge mjini Dodoma, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kinachosubiriwa ni kibali kutoka Baraza la Mazingira nchini (NEMC) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), ili uchimbaji huo uanze rasmi.

“Mkataba ulishasainiwa tangu mwaka 2012 kilihobaki ni utekelezaji wa uchimbaji na ugunduzi wa mafuta, mafuta yanayotarajiwa kuchimbwa kwenye eneo hilo yanafikia milionii 180 hadi 200, mtaji ni mkubwa na utakua na manufaa kwa wananchi wako na nchi kwa ujumla,” alisema na kuongeza.

“Kinachosubiriwa ni kibali cha mazingira kutoka NEMC na mamlaka ya TAWA, mwezi Julai mwaka huu tumehakikishiwa mkataba utapatikana na Septemba uchimbaji utaanza rasmi.”

Serikali kupitia shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) liliingia mkataba wa utafiti na uchimbaji wa gesi na uvunaji mafuta na Kampuni ya Mafuta na gesi ya Swala (Swala Oil), ambapo katika utekelezaji wa mkataba huo iligundulika kuwepo kwa wingi mafuta ya petrol na gesi katika vijiji vya Mtimbira.

VIDEO: Ifahamu Dini Ya Kingunge Na Mengine Usioyajua



Enock Ngombale ambae ni mdogo wa Kingunge Ngambale Mwiru amefunguka kuhusu maisha ya kaka yake tangu alipozaliwa  na kusema kuwa kuna wakati unaweza ukawa huna dini lakini kuna wakati itakulazimu urudi kwenye imani yako, hivyo kaka yangu atazikwa Kikatoliki kama kanisa watakubali tunachosema sisi ndugu zake tunayemjua.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

VIDEO: Aunty Ezekiel Aomba msamaha Shilawadu


Baada ya shilawadu, kunusurika kugongwa na gari ya mose iyobo na kuharibu mali ikiwemo, gari na kamera aunty ezekiel apiga simu na kuomba msamaha shilawadu pamoja na kutaka kuwa wavumilivu akirudi wayamalize


TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..............USISAHA KUSUBSCRIBE.......................

Friday, 2 February 2018

DC Matiro akabidhi hundi za mikopo mil 25 vikundi vya vijana na wanawake

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi hundi za mikopo shilingi milioni 25 kwa vikundi vitatu vya vijana na kimoja cha wanawake zilizotolewa na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Fedha hizo zinatokana na asilimia 10 ya makusanyo kutoka katika vyanzo vya mapato ndani ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Julai 2o17 hadi Disemba 2017.

Vikundi vilivyokabidhiwa hundi ni kikundi cha Wanawake na Maendeleo kilichopo katika kijiji cha Ishololo kata ya Usule na vikundi vya vijana vya Umoja wa bodaboda, Jikwamue, Shukrani Group vilivyopo katika kijiji cha Didia kata ya Didia katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Akikabidhi hundi hizo kwa wawakilishi wa vikundi hivyo leo Ijumaa Februari katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo,Matiro aliwataka walionufaika na mikopo hiyo watumie pesa walizopata kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Kila mtu aliyepata pesa akafanye kile alichokusudia kufanya, serikali inajitahidi kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo ili mjikwamue kiuchumi,naomba mfanye kazi kwa bidii ili kubadilisha maisha yenu”,alieleza Matiro.DC

Utawala wa Jordani umekata mahusiano ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.


Katika gazeti rasmi, imeandikwa kuwa "Baraza la Mawaziri lilipitisha Azimio No. 6056 la Januari 15, ambalo linasema kusimamishwe kwa mahusiano ya kidiplomasia na Korea ya Kaskazini".

Kwa mujibu wa habari,balozi wa Korea Kaskazini nchini Jordan atasimamishwa kazi.

Afisa Mkuu wa Jordan amesema  kwamba uamuzi wa kukata mahusiano na Korea Kaskazini ni kutokana na maslahi ya serikali.

Umoja wa Mataifa umeiwekea Korea Kaskazini vikwazo kutokana na majaribio yake ya makombora ya nyuklia.

Helikopta mbili zagongana nchini Ufaransa


Ndege mbili za jeshi la Ufaransa zimegongana na kusababisha vifo vya watu watano,katika mji wa Marseille kusini mwa Ufaransa.

Gazeti la Var Metin limeripoti kuwa ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi karibu na ziwa la Carces.

Ripoti zinaonyesha kuwa helikopta zilikuwa na jumla ya abiria sita na hivyo mmoja bado hajulikani alipo.

Timu za uokoaji zinaendelea kumtafuta abiria wa sita.

Gavana wa mkoa huo amesema kuwa helikopta hizo zilikuwa za shule ya kujifunza Urubani ya jeshi la Ufaransa na ajali hiyo imetokea mile 50 kutokea mji wa kitalii wa Saint Tropez.

Meli ya mizigo yapinduka


Meli ya mizigo imetipotiwa kupinduka na kusababisha kifo cha mtu mmoja China.

Kwa mujibu wa habari,wafanyakazi sita wa meli hiyo walianguka katika maji baada ya ajali hiyo kutokea.

Shirika la Shingua limetangaza kuwa ajali hiyo imetokea katika mto wa Yangtze katika mji  wa Huanggang.

Meli hiyo ilikuwa ina wafanyakazi sita,mmoja wao akiwa amefariki huku watano wengine hawajulikani walipo mpaka sasa.

Timu ya uokoaji iliweza kumtoa mmoja wao katika maji lakini haikuwezekana kuyanusuru maisha yake.

Juhudi za kuwatafuta wafanyakazi watano waliobaki zinaendelea.

Tundu Lissu amlilia Mzee Kingunge


Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia kifo cha Kingunge Ngombale Mwiru akisema historia itamkumbuka.

Akizungumza leo Februari 2, 2018 na Mwananchi akiwa nchini Ubelgiji anakoendelea na matibabu ya viungo, Lissu akizungumzia kifo hicho ameanza kwa kusema “namtakia mapumziko mema.”

Amesema Mzee Kingunge alikuwa miongoni mwa wazee wenye historia kubwa na alionyesha ujasiri mkubwa wa kuhama chama chake cha CCM bila kuhofia kuhudhuriwa kutokana na mazingira yalivyokuwa.

“Ni mmoja wa wazee walioonyesha ujasiri mkubwa katika mazingira ya siasa za Tanzania yalivyokuwa, akahama chama tena CCM bila hofu za kuhudhuriwa  akaeleza madhabi yake kuwa hiki chama (CCM) kinatupeleka kuzimu,” amesema Lissu na kuongeza “historia itamkumbuka.”

Kingunge aliyekuwa kada wa CCM mwenye kadi namba nane, Oktoba 4, 2015 alitangaza kukihama chama hicho na kusema hatojiunga na chama chochote lakini mara kadhaa alionekana akipanda majukwaa ya upinzani kumnadi aliyekuwa mgombea urais wa Chadema/Ukawa, Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015..

Humud aipeleka KMC ligi kuu Bara


KMC imeongeza idadi ya timu zinazotokea Dar es Salaam katika Ligi Kuu Bara baada ya ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mlale waliokuwa vinara wa Kundi B la Ligi Daraja la Kwanza.

Ushindi huo unaifanya KMC kupanda Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza huku shujaa wake akiwa ni kiungo mkongwe Abdulhalim Humud aliyefunga bao hilo pekee.

Huenda furaha kuu itakuwa kwa kocha Fred Felix Minziro maarufu kama Majeshi ambaye aliipandisha Singida United na sasa amejiunga na KMC na kuipandisha pia.

JKT Mlale iliyokuwa nyumbani ilionekana ina nafasi kubwa zaidi ya kupanda kwa kuwa ndiyo ilikuwa kinara ikiwa na pointi 25 sawa na KMC.


Lakini ushindi huo wa KMC umeifanya ifikishe pointi 28 na kupaa kileleni ikifuatiwa na Coastal Union iliyoshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Mawezi mjini Morogoro. Coastal imemaliza ikiwa na pointi 26 wakati Mlale wanabaki na 25.


KUNDI B
                                P   W   D   L   F   A  GD  Pts
1. KMC                     14   8   4   2   17  13  4    28
2. Coastal Union       14   7   5   2   18   9   9   26
3. JKT Mlale             14   7   4   3   13   7   6   25
4. Polisi Tanzania     14   6   6   2   18   12  6   24
5. Mbeya Kwanza      14   6   4   4   14   10  4   22
6. Mufindi            14   3   4   7   13   21 -8  13

Thursday, 1 February 2018

Papii kuanza kuachia ngoma mfululizo

MKALI wa Dansi Bongo, Johnson Nguza ‘Papii’ amesema kuanzia mwezi huu wa Februari, ataanza kuachia ngoma mfululizo kwani tayari wameshaanza kurekodi nyimbo za kutosha.

Papii alisema mpaka sasa tayari amesha-fanya ngoma nne ambazo amezipika kwa staili tofauti katika dansi la kisasa ambalo halich-oshi.

“Tumefanya staili kama ya wanayofanya Yamoto Band, tumefanya moja kama ya dini na pia tumerudia Seya ambazo kimsingi zitawateka tu mashabiki,” alisema Papii.

Akifafanua zaidi, Papii alisema, atakuwa na mfululizo wa kutoa ngoma mbilimbili zenye ujazo wa hali ya juu.

“Nitakuwa naachia ngoma mbilimbili mfululizo ambazo karibia zote nimefanya na mzee wangu (Nguza). Nimezifanyia katika Studio ya Wanene iliopo Mwenge,” alisema Papii.

Mwana FA: sijawahi kuvaa suruali za kubana

MKONGWE kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Hamisi Mwinjuma, ‘MwanaFA’ amesema, katika maisha yake ya kisanii, hajawahi kuvaa suruali za kubana kama ilivyo kwa vijana wenzake wa kileo kwa kile alichodai nguo hizo zinamfanya ashindwe kupumua.

Akipiga stori na Showbiz Xtra, MwanaFA alisema, tamaduni za Muziki wa Hip Hop ndizo zilizomfanya ashindwe kabisa kuvaa suruali za kubana kwa kuwa kila anapojaribu kuvaa hujikuta anashindwa kupumua.

“Unajua nguo zetu sisi watu wa Hip Hop ni ile suruali pana na tisheti kubwa, nimekulia katika mavazi hayo, licha ya kwamba dunia inabadilika lakini mimi nashindwa kabisa kuvaa suruali za kubana kwa kuwa nguo hizo hunifanya nishindwe kuhema,” alisema MwanaFA.

Lulu Diva arudisha mahari kwa mikono yake



MWANAMUZIKI wa kike anayekuja kwa kasi Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amerejesha kwa mikono yake mwenyewe mahari aliyokuwa ametolewa na mchumba wake aliyedumu naye kwa takriban miaka mitatu.

Chanzo chetu makini kilisema kuwa, mwanamuziki huyo alikuwa afunge ndoa mwishoni mwa mwaka jana lakini kutokana na kuvuja kwa habari kuwa anatoka na mwanamuziki mwenziye wa Bongo Fleva, mwanaume huyo akadai mahari yake.

“Kama kuolewa basi Lulu angeolewa mwaka jana mwishoni lakini mchumba huyo alibaini anatoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake akaomba mahari yake irudishwe,” kilisema chanzo.

Gazeti hili lilipompigia simu Lulu na kumuuliza madai hayo alisema, ni kweli alirudisha mahari lakini si kwamba mwanaume huyo alijua anatoka na mwanaume mwingine bali alipata shinikizo kutoka kwa ndugu zake.

“Aliposhinikizwa sana nikaona isiwe tabu nikamrudishia mahari yake kwa maana alikuwa akiwasikiliza sana ndugu zake ambao walikuwa hawataki anioe,” alisema Lulu.