Saturday, 3 February 2018

Esma aweka wazi mahaba yake kwa Wema Sepetu


Esma Abdul ‘Esma Platnumz’

MWANADADA Esma Abdul ‘Esma Platnumz’ ameonesha mahaba yake kwa staa mkubwa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akidai kuwa, amekuwa shosti wake kwa muda mrefu na hivyo hawezi kujitenga naye.

Akipiga stori na gazeti hili, Esma alisema Wema ametoka naye mbali kiasi kwamba leo hii hawezi kumuweka pembeni na kujiweka zaidi kwa wifi wake wa sasa,  Zarina Hassan ‘Zari’.

“Jamani Wema hata kidogo siwezi kumuweka pembeni, hata kama aliachana na kaka yangu lakini kwangu bado ana umuhimu. Kama kila anayeachana na kaka basi
niwe naye mbali, nikifa inabidi nikazikwe Uganda au Sauzi maana Bongo sitakuwa na rafiki,” alisema Esma

Kauli ya kocha wa Simba yamwacha mdomo wazi Tambwe


KAULI ya Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, aliyedai kwamba atafurahi zaidi kama straika wake Emmanuel Okwi atafunga mabao 30 msimu huu, imemshitua mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe.

Tambwe ambaye anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika msimu wa 2015/16 akifunga mabao 21, baada ya kusikia kauli hiyo ya Djuma alisema; “Siyo kazi rahisi Okwi kufunga mabao 30.”

Akizungumza na Championi Jumamosi, Tambwe alisema ili Okwi ambaye hivi sasa anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 12, aweze kufikisha mabao 30, anatakiwa kufunga katika kila mechi atakayocheza.

“Siyo kazi rahisi kwa Okwi kufunga mabao 30, kwani mzunguko wa pili ligi huwa ni ngumu sana, kila timu hupambana kuhakikisha inafanya vizuri ili kuwania ubingwa, nyingine zinapambana zisishuke daraja.

“Inabidi Okwi apambane kwelikweli na ajitahidi pia kufunga katika viwanja vya mikoani lakini kama ataendelea kutegemea Uwanja wa Uhuru na ule wa Taifa pekee, itakuwa ni vigumu kufikisha mabao hayo,” alisema Tambwe.

Uchebe akana madai ya kuwa Sangoma



Mwanamuziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’ akiwa na mume wake Ashrafu Uchebe.

MUME wa mwanamuziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’ Ashrafu Uchebe amekana kuwa mganga (Sangoma) wa kutumia vitabu na kuweka wazi kuwa kazi yake ni ufundi wa magari.

Maelezo hayo yamekuja kutokana na madai yaliyokuwa yumeenea kwamba, mbali na kufanya mambo mengine lakini pia anatibu kwa kutumia Quran na amekuwa akifanya hivyo tangu alipokuwa Zanzibar.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Uchebe alifunguka hivi: “Kama unavyojua kumuombea mtu dua ni jambo la kawaida lakini anayesaidia ni Mungu, hata wewe nakuombea tu dua na Mungu ndiye anasaidia ila hilo la kuwa mganga sijawahi, kazi yangu ni fundi wa magari,” alisema Uchebe

Jokate afunguka kuanzisha familia mwaka huu



Jokate Mwegelo

MWANAMITINDO ambaye ni kada wa CCM, Jokate Mwegelo baada ya kuanika kuwa mwaka huu ni sahihi kuingia kwenye maisha ya ndoa, ameibuka tena na kuanika kuwa 2018 ni mwaka wa kuwa na familia pia.

Akiongea na Risasi Jumamosi Jokate alisisitiza kuwa mwaka huu ni wa neema kwake na kufafanua kuwa ana mpango wa kuanzisha familia yake.

“Watu wajue tu kuwa mwaka huu nitaanzisha familia, sio kama ninawafumba lakini kwa uwezo wake Mungu wataona tu, wakae wakisubiri kwani lisemwalo lipo kama halipo linakuja,” alisema Jokate ambaye hakuweka wazi mwanaume atakayemuoa na kuanzisha naye familia

Mrema awatolea uvivu UKAWA


Mwenyekiti wa chama cha TLP Lyatonga Augustino Mrema amefunguka na kusema kuwa UKAWA hawampendi wala hawamtaki ndiyo maaana walifanya kila namna kuhakikisha wanampokonya jimbo la Vunjo kwa kumsimamisha James Mbatia katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Mrema amesema hayo jana Januari 2, 2018 akiwa kwenye kampeni za kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia chama cha TLP, Dokta Godfrey Malisa na kusema kuwa wapinzani nchi hii wamekuwa wakimchukia.

"Ni kweli kwamba UKAWA hawanipendi, hawanitaki wakaninyang'anya lile jimbo wakampa James Mbatia angekuwa basi anafanya kazi za wananchi wa Vunjo wala nisingelalamika. Angelikuwa mwaminifu kwa Rais wetu wala nisingehangaika wala kulalamika, lakini walininyang'anya jimbo kwa ulaghai na utapeli kwa maneno ili kunimaliza kwa wananchi wa Vunjo wakasema Mrema ni mzee na kweli ni mzee ila kuwa mzee siyo kosa wala siyo dhambi kwamba wazee hawana manufaa" alisema Mrema

Mbali na hilo Mrema aliendelea kusema

"Hawa UKAWA wananiita marehemu mtarajiwa ndiyo wenzangu kwa hiyo wakaninyanyasa, wakanizodoa na ndiyo maana nawaambia UKAWA wakiendelea na tabia hii ya kuwakataa wazee kama Mrema kama hawana lolote, hamtakaa mpate kura za wazee wa nchi hii kwa sababu maneno yenu waliyasikia. Kwanini mnatukataa sisi wazee"


Aliyewabagua Waaafrika afutwa kazi


Klabu ya soka ya West Ham imemfuta kazi mkurugenzi wa uajiri wa wachezaji wa timu hiyo Tony Henry kutokana na kauli yake ya kuwabagua wachezaji kutoka Afrika.

Tony Henry hivi karibuni alinukuliwa akisema kuwa timu hiyo haiwezi kusaini wachezaji kutoka Afrika kutokana na wachezaji hao kutowajibika vizuri kwenye baadhi ya majukumu yao.

Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa maneno ya Tony Henry sio msimamo wa klabu kwasababu timu haiamini katika ubaguzi wa aina yoyote ndio mana imeamua kumfuta kazi Henry ili hatua zingine zichukuliwe.

West Ham ina wachezaji sita kwenye kikosi cha kwanza wenye asili ya Kiafrika ambao ni  Cheikhou Kouyate, Pedro Obiang, Joao Mario, Angelo Ogbonna, Arthur Masuaku na Edimilson Fernandes.

Wengine ni mshambuliaji wa Senegal Diafra Sakho ambaye ameondoka kwenye dirisha dogo la Januari akajiunga na Rennes ya Ufaransa huku Andre Ayew wa  wa Ghana akielekea Swansea.

Mose Iyobo awachezeshea kichapo Shilawadu


 Watangazaji wa Kipindi maarufu cha Shilawadu kinachorushwa na Clouds tv,Soudy Brown na Kwisa wamechezea kichapo kutoka kwa Dancer wa Diamond,Mose Iyobo,usiku wa kuamkia  ijumaa,baada ya kutaka kumuhoji kuhusu matukio yaliyotokea hivi karibuni kati ya familia yake na mwanadada Tunda.

Wakithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Shilawadu wameandika katika ukurasa wao wa instagram:

Kazi yetu ina changamoto kubwa sana..asilimia kubwa ya ma star wanatuunga mkono.

Usiku wa Leo wakati tukiwa kazini tumenusurika kumwagwa damu na mtu tuliemfuata kumuomba kufanya naye mahojiano,kati yetu kuna walioumia viuno,mikono, etc.kuna uharibifu wa vifaa vyetu vya kazi umetokea pia,wenzetu wanaendelea na matibabu Mungu  ni mwema  Mungu ni wetu sote na hili litapita bado tuna wasiwasi tu kama mhusika ataendelea kututafuta kwa ajili ya kutudhuru zaidi,tunasikitishwa sana na matumizi ya nguvu dhidi yetu sisi Wanyonge #Shilawadu

Kuna watu watasema Shilawadu wamezidina kusahau kuwa sisi ni wana Habari kama wanahabari wengine na kupata habari ni haki ya kila mwananchi kama ilivyo haki nyingine yoyote ile.Kifungu cha 18 cha katiba  ya Jamhuri ya Muungano 1977 na hatimaye kufanyiwa marekebisho mwaka 2005 inampa haki mtu na uhuru wa kujieleza na kutoa mawazo,uhuru wa kutafuta habari,kupata habari,na kuneza habari bila kujali mipaka,pia sheria hiyo inampa haki mtu ya kuwasiliana bila kubughudhiwa na mawasiliano na kufahamishwa wakati wowote masuala yoyote muhimu yahusuyo maendeleo yake na yahusuyo jamii yake kwa ujumla.

Imeandikwa na Mtayarishaji wa Kipindi cha Shilawadu Benedict Noel

Mourinho atoa ujumbe huu kwenye birthday ya mtoto wake


 Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amemtakia furaha ya kuzaliwa mwanawe wa kiume Zuca baada ya kutimiza miaka 18 huku akiposti picha ya utotoni inayomuonyesha wakiwa pamoja katika kiboti.

Meneja huyo wa Man United ameposti picha hiyo huku akiandika “Furaha ya kuzaliwa Zuca sasa unamiaka 18 huitaji uwepo wangu tena kwenda kuogelea pamoja katika kiboti,”ameandika Mourinho kupitia mtandao wake.

Picha hiyo inamuonyesha Mourinho akiendesha kiboti hicho huku akiwa na Zuca.

Mwaka jana Mourinho aliwahi kumtakia furaha ya kuzaliwa mwanawe kwa kuposti ujumbe unao fanana na huo.

Zuca anacheza nafasi ya goli kipa katika academy ya Fulham akiwa amesaini kandarasi ya miaka miwili  akiwa na umri wa miaka 16.

Hapo hawali Zuca alikuwa akiitumikia klabu ya Chelsea na Real Madrid wakati timu hizo zikitumikiwa na baba yake.

Baada ya kumdiss Donald Trump, Diego Maradona yamkuta makubwa


Gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutoswa visa ya kwenda nchini Marekani kutokana na matamshi aliyoyatoa dhidi ya raisi Donald Trump.

Maradona ana kesi na aliyekuwa mke wake aitwaye Claudia Villafane na alipaswa kwenda hadi Miami kusikiliza kesi hiyo lakini maofisa wa uhamiaji walimuwekea ngumu kupata visa ya kwenda nchini humo.

Maradona siku zilizopita alisikika katika moja ya interview zake akimuita raisi Donald Trump “chirolita” jina ambalo kwa Waargentina linatumika kwa watu ambao ni vibaraka wa watu wengine.

Baada ya Maradona kushindwa kwenda nchini Marekani sasa itabidi wakili wake akwee pipa kuelekea Miami kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo huku ikiwa bado haijafahamika kwamba inawezekana ukawa mwisho wa Maradina kwenda Marekani ama laa.

Huu ni muendelezo wa matukio na visa vya Maradona nje ya uwanja, kwani miaka ya karibuni amekuwa akiyafanya na kwa sasa mchezaji huyo yuko falme za kiarabu kama kocha wa klabu ya Al Fujairah.

Manula, Bocco, Ndemla wapokea tuzo za mwezi


KIPA chaguo la kwanza wa Simba, Aishi Manula amekabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa Wekundu wa Msimbazi katika sherehe fupi iliyofanyika juzi  nyumbani kwa Balozi wa Uturuki, Ali Davotuglu.

Manula, ambaye pia ni kipa chaguo la kwanza la timu ya Taifa (Taifa Stars) alishinda tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mechi nne zilizopita za ligi hiyo inayotarajiwa kuingia kwenye raundi ya pili kuanzia leo.

Mbali na Manula, wachezaji wengine waliopata tuzo katika sherehe hiyo pamoja na nahodha na mshambuliaji aliye kwenye kiwango cha juu, John Bocco na kiungo, Said Ndemla.

"Hizi ni tuzo ambazo zinatolewa na klabu yetu katika kuhamasisha wachezaji wafanye vizuri katika kila mechi wanayocheza na vile vile kusaidia kuipa timu ushindi," alisema Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara.

Aliongeza kuwa katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na viongozi wa klabu hiyo pamoja na mwekezaji na bilionea, Mohamed Dewji "Mo", walifanya mazungumzo mbalimbali na kubadilishana mawazo ili kuifanya timu ifikie malengo yake msimu huu.

"Tunaamini hatua hii tuliyofika, itakuwa na matokeo chanya kwa sababu tutaimarisha mahusiano," Manara aliongeza.

Mume aliyeweka pilipili kwenye nguo ya mkewe aadhibiwa


Mahakama moja wilayani Lira nchini Uganda imemuhukumu mwanamume kifungo cha siku 40 kutumikia jamii baada ya kupatikana na hatia ya kupaka pilipili nguo ya ndani (chupi) ya mkewe.

Akisoma hukumu, hakimu Hilary Kiwanuka alisema ushahidi uliotolewa mahakamani umejitosheleza pasipo kuacha shaka kwamba mtuhumiwa Moses Okello alitenda kosa hilo.

Okello, mkazi wa Kijiji cha Barmola, Kaunti Ndogo ya Bala wilayani Kole atatakiwa kufanya kazi za kijamii katika kipindi cha siku 40 kutokana na kosa hilo.

Mahakama ilielezwa Januari 20,2018, Okello alipaka pilipili kwenye nguo hiyo na baadaye alimshauri mkewe aivae.

“Alinishauri kuivaa siku hiyo, nilipoivaa nilianza kuwashwa na mwasho huo haukuisha hata nilipooga,” mwanamke huyo aliieleza Mahakama.

Haikuelezwa ni kwa nini Okello aliamua kufanya kitendo hicho kwa mkewe ingawa baadaye alidai alikuwa akimtania.

Magufuli awatunuku 197


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 197 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Sherehe hizo zimefanyika leo Februari 3, 2018 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo maofisa hao wapya ni wa Tanzania na kutoka nchi marafiki,  waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha.

Katia tukio hilo ambalo lilipambwa na magwaride kutoka kwa Wanajeshi hao, lilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kitaifa.

Miongoni mwa waliotunukiwa kamisheni hizo wanawake ni 28, na waliobaki ni wanaume.

Majeruhi wailiza Azam FC


Kuelekea mchezo wa marudiano raundi ya pili ya ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC, klabu ya soka ya Azam FC imesema inakabiliwa na majeruhi wengi akiwemo nahodha wa kikosi hicho Himid Mao.

Akiongelea mchezo huo msemaji wa timu hiyo Jaffary Idd amesema pamoja na majeruhi hao lakini timu ina kikosi kipana hivyo mwalimu Aristica Cioaba amewaandaa wengine kupambana kwaajili ya kupata alama tatu.

Wachezaji wengine ambao ni majeruhi ndani ya kikosi hicho ni Waziri Junior, Joseph Kimwaga na Joseph Mahundi, wakati Abubakar Salum 'Sure Boy' anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

Azam FC inaingia katika mchezo wa leo utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex ikiwa katika nafasi ya pili na alama 30, nyuma ya Simba yenye alama 35 kileleni. Ndanda inashika nafasi ya 8 ikiwa na alama 16.