Mwanamuziki maarufu nchini Afrika Kusini, Hugh Masekela anayefahamika kama baba wa muziki wa Jazz amefariki dunia baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya saratani ya tezi dume.
Hugh Masekela amefariki dunia baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya saratani ya tezi dume.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Afrika Kusini. Masekela amabaye hadi kifo chake kinamkuta alikuwa na umri wa miaka 78.
Katika kipindi chake cha zaidi ya miongo mitano kwenye fani hiyo ya muziki alijijengea umaarufu kimataifa kutokana na utunzi wa nyimbo zake za muziki wa Jazz ukiwemo wimbo uliotumika katika harakati za kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.
Hugh Masekela alitumbuiza katika hafla ya ufunguzi wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 zilizofanyika nchini Afrika Kusini ikiwa ni mara ya kwanza fainali hizo kufanyika barani Afrika.
No comments:
Post a Comment