
Kwa hali yoyote ile ambayo inatokea nje ya wewe haina mchango mkubwa sana wa kuweza kukukwamisha au kukufanya ushindwe kufikia mafanikio yako. Kitu ambacho kitakufanya ushindwe kufanikiwa ni ile hali inayotokea ndani mwako tu.
Hali hiyo inayotokea ndani mwako, ndiyo ina nguvu kubwa sana ya kubadillisha maisha yako na kuwa ya mafanikio kabisa. Hebu jiulize kila unapowaza mafanikio, ndani mwako unajionaje? Unajiona ni kwamba utafanikiwa au utashindwa? Kipi unachokiona ndani mwako?
Haijalishi watu wanasemaje au watasema nini juu yako, hata watu dunia nzima waseme kwamba utafanikiwa, lakini kama ndani yako huoni hivyo ni wazi huwezi kufanikiwa, pia hata dunia nzima iseme kwamba wewe ni wa kushindwa, lakini ikiwa ndani yako unajiona wewe ni mtu wa mafanikio, utafanikiwa.
Kiti kikubwa hapa, jifunze kutokulaumu hali yoyote ile, inayotokea nje katika maisha yako kwamba ndio imekukwamisha. Anayejizuia na kujikwamisha sio mwingine bali ni wewe mwenyewe na hali hasi nyingi ulizozibeba. Kuanzia leo amua kujenga hali bora ndani mwako itakayokupa mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment