Monday, 4 December 2017

Madaktari watangaza kimakosa kuwa mtoto amefariki



Mtoto ambaye alikuwa ametangazwa kuwa amefariki na madaktari mara baada ya kuzaliwa kwenye hospitali moja huko Delhi India, alipatikana akiwa hai wakati akipelekwa kufanyiwa mazishi.

Madaktari kwenye hospitali ya kibinafsi ya Max walikuwa wamemtangaza mtoto kuwa amefariki saa chache baada ya pacha mwenzake kutangazwa kufariki baada ya kuzaliwa.

Wazazi wake walisema kuwa walifahamu kuwa mtoto huyo alikuwa hai ndani ya mfuko ambao madaktari walikuwa wamemweka.

Kisa hicho kimezua hasira na mjadala kuhusu hali ya viwango katika hospitali za kibinafsi ambazo mara nyingi ni ghali mno.

Mkuu wa jimbo la Delhi aliandika katika Twitter kuwa ameamrisha kisa hicho kufanyiwa uchunguzi.

Kulingana na babu yake mtoto, familia hiyo iliyokuwa imepigwa na mshangao ilimkimbiza mtoto kwenda hospitali iliyokuwa karibu ambapo waliambiwaa kuwa mtoto huyo alikuwa hai.

Katika taarifa kwa waandishi wa hababi , hospitalia ya Max ilishangazwa na kisa hicho na kuongeza kuwa daktari huyo amepewa likizo huku uchunguzi ukifanywa

No comments:

Post a Comment