Tuesday 5 December 2017

Afrika Kusini: Ugonjwa wa Listeriosis waua watu 36



Takriban watu 36 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Listeriosis Afrika ya Kusini.

Waziri wa afya Aaron Motsoaledi ametangaza kuwa kesi nyingi za mlipuko huo zimeripotiwa kutoka katika maeneo ya Gauteng,Western Cape na KwaZulu Natal.

Kwa mujibu wa habari,chanzo kabisa cha mlipuko wa ugonjwa huo bado kinafanyiwa utafiti wa kina.

Ugonjwa wa Listeriosis ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na kula chakula chenye bakteria Listeria.

Maafisa wa mazingira wanafanya utafiti kuangalia sampuli za vyakula waliokula wagonjwa hao.

Ripoti zinaonyesha kuwa zaidi ya kesi 557 za ugonjwa huo zimeripotiwa toka kuanze kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment