Monday, 4 December 2017

MAGAZETI YA LEO 4/12/20

MAGAZETI YA LEO 4/12/20












Madaktari watangaza kimakosa kuwa mtoto amefariki



Mtoto ambaye alikuwa ametangazwa kuwa amefariki na madaktari mara baada ya kuzaliwa kwenye hospitali moja huko Delhi India, alipatikana akiwa hai wakati akipelekwa kufanyiwa mazishi.

Madaktari kwenye hospitali ya kibinafsi ya Max walikuwa wamemtangaza mtoto kuwa amefariki saa chache baada ya pacha mwenzake kutangazwa kufariki baada ya kuzaliwa.

Wazazi wake walisema kuwa walifahamu kuwa mtoto huyo alikuwa hai ndani ya mfuko ambao madaktari walikuwa wamemweka.

Kisa hicho kimezua hasira na mjadala kuhusu hali ya viwango katika hospitali za kibinafsi ambazo mara nyingi ni ghali mno.

Mkuu wa jimbo la Delhi aliandika katika Twitter kuwa ameamrisha kisa hicho kufanyiwa uchunguzi.

Kulingana na babu yake mtoto, familia hiyo iliyokuwa imepigwa na mshangao ilimkimbiza mtoto kwenda hospitali iliyokuwa karibu ambapo waliambiwaa kuwa mtoto huyo alikuwa hai.

Katika taarifa kwa waandishi wa hababi , hospitalia ya Max ilishangazwa na kisa hicho na kuongeza kuwa daktari huyo amepewa likizo huku uchunguzi ukifanywa

Mbunge amchumbia mwanaume mwenzie Bungeni



Tim Wilson

Mbunge mwanamume nchini Australia ameposa kwa mpenzi wake wa kiume wakati wa kikao cha bunge cha kujadili kuhalalishwa ndoa za jinsia moja.

Tim Wilson alimchumbia Ryan Bolger ambaye alikuwa ameketi eneo la umma. Wawili hao wamekuwa wapenzi kwa miaka 9.

Mswada huo wa kuhalalisha ndoa ya jinsia moja uliwasilishwa bungeni siku ya Jumatatu baada ya kupitia bunge la Senate wiki iliyopita.

"Katika hotuba yangu ya kwanza, ninatambua uhusiano wetu kwa pete iliyo kwenye mikono yetu yote ya kushoto. Pete hii ni jibu kwa maswalii ambayo hatutawezi kuyauliza," Bw Wilson alisema.

"Kwa hivyo kuna kitu kimoja tu ambacho kimebaki kufanywa. Ryan Patrick Bolger utakubalia nikuoe ?"

Swali hilo lilizua shangwe na pongezi, kaala ya Bw Bolger kujibu kwa sauti na kusema "ndiyo"
Mapema Bw. Wilsni alizungumzia maisha yake ya kukua kama kijana mpenzi wa jinsia moja na kukumbana na unyanyapaa .

Bw Wilson ni miongoni mwa wabunge 77 ambao watajadili mswada huo.

Wafanyabiashara waishauri Halmashauri kuboresha huduma ya Kodi


Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mbeya, kimeshauri Jiji la Mbeya kuangalia namna bora ya kuboresha na kukusanya tozo za kodi ya huduma kutoka kwa wafanyabiashara ili kuboresha kiwango cha huduma.

Mratibu wa TCCIA Mkoa wa Mbeya, Emily Malinza alibainisha hilo juzi jioni kwenye mkutano uliowakutanisha uongozi wa jiji la Mbeya, wadau wa masuala ya kodi na wafanyabiashara kwenye majadiliano ya pamoja kuhusu programu ya kukuza uwekezaji na biashara kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kwa jiji hilo.

Malinza alisema wafanyabiashara wamekuwa wakifika TCCIA kuuliza tozo za kodi wanazotozwa na jiji namna zinavyowanufaisha, kwa kukuwa wanatozwa tu lakini hawaoni huduma.

Wafanyabiashara wengi wanauliza tozo wanazolipa zinakokwenda, wakati hakuna huduma wanayoipata kutoka jiji kwa mujibu wa sheria inayoelekeza.

“Sasa jibu ni rahisi tu kwamba kodi inayochukuliwa ni chache kiasi hata matokeo yake hayawezi kuonekana,” alisema Malinza na kuongeza:

“Lakini TCCIA tunaamini kabisa kama kutaboreshwa huduma zitokanazo na tozo hizo, mapato yakaongezeka na hata huduma nyingine ambazo jiji linatoa zitaboreshwa.”

Akichangia katika mkutano huo, ofisa biashara Mkoa wa Mbeya, Stanley Kibakaya alisema licha ya majadiliano hayo kujitikiza zaidi kushusha kiwango vya tozo ili kupata makusanyo mengi zaidi, jiji liwe na mpango mkakati kukuza na kutangaza kujua umuhimu wa vyanzo vingine vya mapato.

“Ukiangalia kwenye ada za leseni za biashara, kila mara wanatangaza umuhimu wa kulipa ada za leseni na kuna mbinu kabisa kama hujalipa hatua zinazotakiwa kuchukuliwa,” alisema.

Naye mhasibu wa Jiji la Mbeya, Andrew Kiyungu alisema tayari wameandaa mpango mkakati wa kuwafikia wafanyabiashara ambao hawasajaliwa kwenye mfumo wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (Vat) na wana leseni za biashara.

Kiyungu alisema mkakati huo umegawanywa katika makundi matatu ambayo ni wafanyabiashara wakubwa ambao wamesajaliwa na Vat hawataguswa na punguzo la kodi, watabakia kwenye tozo ya asilimia 0.3.

“Kundi la pili ni wafanyabiashara wa kati ambao wanalipa leseni kuanzia Sh100,000 hadi Sh200,000, menejimenti ya jiji ilipendekeza wakilipa Sh30,000 kwa kila mwezi itakuwa na afya kwa halmashauri na watawafikiwa wengi zaidi kwa bei nafuu na itasaidia kukuza mapato ndani,” alisema.

Alisema kundi la tatu ni wafanyabiashara wadogo ambao wanalipa leseni za biashara kuanzia Sh40,000 hadi Sh80,000, menejimenti ya jiji ilipendekeza kundi hiyo kulipa Sh15,000 kwa mwezi.

Alisema hatua zote hizo ni mkakati wa kuwafikia wafanyabiashara wengi wanaopaswa kulipa tozo ili kukuza mapato yatakayosaidia kuboresha huduma mbalimbali za jamii.

Naye kaimu mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Afrael Manase alisema ili wasonge mbele na kuboresha huduma kwa jamii, lazima sekta binafsi zishirikishwe kila hatua tofauti na hapo watashindwa kumudu utoaji huduma.

Jinsi ghorofa 10 jengo la Tanesco zitakavyobomolewa



Wakati ukumbi wa mikutano na ofisi za mapokezi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), vikivunjwa Wakala wa Majengo (TBA) umeeleza namna jengo la ghorofa 10 litakavyobomolewa.

Meneja wa Kikosi cha Ujenzi wa TBA, Humphrey Killo alisema jana kuwa uvunjaji wa ofisi na ukumbi ulifanyika usiku wa kuamkia juzi ikiwa ni maandalizi ya kuvunja sehemu ya jengo la ghorofa 10 lililoko eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam ambalo liko kwenye hifadhi ya Barabara ya Morogoro.

Ubomoaji huo unafanyika pia ili kupisha utekelezaji wa mradi wa barabara za juu eneo la Ubungo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli.

Novemba 15, Rais Magufuli aliagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuweka alama za X kwenye jengo hilo katika sehemu zilizo katika hifadhi za barabara.

Akizungumzia uvunjaji wa jengo hilo, Killo alisema kwa sasa wanafanya maandalizi yakiwemo ya vifaa kama vile mitambo na malori ya kubebea vifusi. “Maandalizi haya ni pamoja na kubomoa majengo madogo kama vile ofisi za walinzi na ukumbi wa mikutano na sehemu ya mapokezi,” alisema Killo aliyekuwa akisimamia mchakato huo.

Killo alisema maandalizi yanatarajiwa kukamilika kesho na utaratibu utakaofuata ni kubomoa jengo la ghorofa akisema kazi hiyo inaweza kufanyika kwa mwezi mmoja.

Alisema kabla ya kubomolewa ghorofa hilo, jengo lote litawekwa vyuma na kuzungushiwa nyavu maalumu ili kuzuia vumbi kusambaa katika maeneo mengine ya jirani.

“Nyavu hizi zitasaidia pia kuzuia vitu au vipande vidogovidogo vitakavyokuwa vikitoka wakati wa ubomoaji,” alisema Killo.

Alisema ubomoaji ni hatari hivyo timu ya wataalamu 10 wa fani mbalimbali wakiwamo wasanifu wa majengo watapelekwa kusimamia kazi hiyo itakapoanza.

“Wataalamu wengine watakuwa ni wa fani ya uhandisi wa majengo, wakadiriaji wa majenzi na mafundi sanifu. Pia, watakuwepo maofisa usalama kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama,” alisema Killo.

Alisema jengo hilo lina sehemu tatu; ya mbele, katikati na nyuma hivyo ubomoaji utahusisha sehemu ya mbele pekee.

Novemba 27, uongozi wa Tanesco ulitoa taarifa kwa umma ukisema utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli umeanza kuhusu kubomolewa jengo.

Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji, Novemba 28 alisema wafanyakazi wa shirika hilo wamehamia ofisi zingine za shirika hilo zilizoko jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais ameitaka Jamii kuwapa kipaumbele walemavu kwenye maendeleo



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameitaka jamii kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu hawaachwi nyuma kwenye nyanja zote za maendeleo.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Watu wenye ulemavu duniani iliyofanyika mkoa wa Kusini, Unguja, Zanzibar.

Akihutubia mamia ya watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu kwenye kwenye viwanja vya Skuli ya Uzini, Makamu wa Rais alisema tumejumuika leo hapa kuungana na wenzetu duniani kote kuadhimisha kilele cha siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo imebeba kauli mbiu isemayo “Mabadiliko kuelekea jamii Jumuishi na Maendeleo Endelevu kwa wote”­­­­­­ ujumbe huu unalenga kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanajumuishwa katika mipango yote ya maendeleo ili kuweza kufikia malengo endelevu ya dunia ifikapo mwaka 2030 pia inakwenda sambamba na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2020; Ilani ya Chama Tawala na mpango wa kukuza Uchumi na kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA III) ambapo masuala ya watu wenye ulemavu yamezingatiwa.”

Tanzania iliridhia mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu ambao umeweka misingi madhubuti wa utekelezaji wa masuala mbali mbali kwa ajili ya watu wenye ulemavu, ikiwemo; Usawa, Ushirikishwaji kikamilifu katika mipango ya hifadhi ya jamii na kupunguza umasikini na kuwapatia huduma pamoja na kufanya kazi na taasisi zinazoshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu,” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais alitoa rai kwa kusema “kuanzia leo(jana) kila mmoja miongoni mwetu awe askari wa mwenzie katika kuhakikisha kuwa tunalinda haki na usawa wa watu wenye ulemavu”.

Makamu wa Rais aliwaasa wanafamilia kutoficha maovu wanayofanyiwa watu wenye ulemavu, alisema Serikali kwa nguvu zote inakemea vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu kwani si vitendo vya kiungwana hata kidogo na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia kikamilifu wahalifu hawa na wakithibitika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ikiwemo mahakama na kutoa adhabu kali dhidi ya wale watakaobainika.

Makamu wa Rais alisema Serikali kwa kushirikiana na Wadau wengine wa Maendeleo pamoja na wananchi itaendelea kuhakikisha kuwa ‘digital technology’ inakuwa rafiki kwa walemavu hususan katika kuwawezesha kupata elimu, vitendea kazi katika maendeo yao pamoja na kuhakikisha wanafikia kirahisi huduma zote za kijamii.


  • Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilisema itaendelea kuweka mipango thabiti na mathubuti yenye kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki za kisiasa, kiuchumi, kijamii na fursa sawa kama wengine na kuahikisha watu wenye ulemavu wanashiriki kikamilifu katika ngazi mbali mbaliza uongozi za kitaifa.

Yanga kurejea mazoezini leo



 
Kikosi cha Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, kinatarajia kurejea mazoezini leo Jumatatu baada ya mapumziko ya zaidi ya siku tatu.

Uongozi wa Yanga uliamua kuwapumzisha wachezaji wake kwa muda wakati michuano ya Chalenji inaanza huko Kenya.

Awali ilielezwa kuwa mazoezi yangeanza Ijumaa, lakini baadaye ilibadilishwa na mazoezi kupelekwa hadi leo.

Baadhi ya wachezaji wako katika kikosi cha Tanzania Bara maarufu kama Kili Stars kinachoshiriki Chalenji.

Wengine pia wako katika kikosi cha Zanzibar Heroes pia kianshiriki michuano hiyo ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kat


Bi. Hindu ajisalimisha kwa MO



Kama unakumbuka, shabiki na mwanachama mkongwe wa Simba Chuma Suleiman maarufu kama Bi. Hindu alikuwa hataki kusikia kabisa habari za mambo ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ndani ya klabu yao hususan masuala ya hisa na kampuni.

Leo December 3, 2017 MO ameshinda kwa kishindo zabuni ya kuwekeza ndani ya Simba, baada ya MO kutangazwa mshindi na wanachama wengi waliohudhuria mkutano huo kuridhia, Bi Hindu alijitokeza na kwenda hadi MO kumpongeza.

ShaffiDauda.co.tz ikapiga story na bibi huyo kutaka kujua msimamo wake upo kwa sasa baada ya kuwa miongoni mwa wanachama waliokuwa wakipinga mchakato huo.

“ Tuliambiwa wanachama tutafukuzwa tutakuwa hatukanyagi klabuni, ndio kitu kilichokuwa kinaniuma rohoni kwa sababu klabu hii imejengwa na wauza vitumbua, wapasua kuni, lakini baada ya kueleweshwa nimeelewa na nipo safi. Atakaenifata  kuniuliza nitamweleza akielewa ataungana na sisi kama hataki basi namuacha.”

Bi. Hindu amesema wapo watu watakaosema amevuta ‘mtonyo’ ili kukubali mabadiliko hayo ambayo yameridhiwa pia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) sambamba na serikali kupitia wizara inayosimamia masuala ya michezo.

“Kuna watu wanaweza wakasema nimepewa ‘kitita’ lakini mimi sipo huko, nipo katika kujenga Simba kwa sababu aibu inatukuta kila siku sisi mikono kichwani.”

Wakulima watakiwa kuheshimu mkataba wa Kampuni za ununuzi








Chama Kikuu cha Ushirika (Kacu), kimewatahadharisha wakulima wa tumbaku kuheshimu mkataba wa kampuni za ununuzi ili kusijitokeze kama yaliyowakuta msimu uliopita, baada ya zaidi ya kilo milioni tatu kukosa soko.

Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa Kacu, Emmanuel Peter baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa uchaguzi.

Alisema mwaka huu wakulima wameingia mkataba na kampuni za ununuzi kuzalisha kilo milioni nane za tumbaku, hivyo wanapaswa kulima bila kuzidi.

Mwaka jana, tumbaku iliyozidi kwa Kahama ilikuwa kilo milioni 3.25 ambayo ilikuwa ni ziada ya mkataba wa kuzalisha kilo milioni sita ambazo kampuni ziligoma kununua ziada hiyo.

Hata hivyo, baada ya mazungumzo ya muda mrefu zilikubali kwa masharti ya kununua kwa bei ya dola 1.25 za Marekani (Sh2,700) kwa kilo kwa tumbaku ya daraja la kwanza badala ya Sh5,000 au Sh6,000 kwa bei iliyotumika awali.

“Wakulima acheni kulima nje ya idadi iliyopo kwenye mkataba wa kampuni za kununua, ili kujiepusha na usumbufu uliojitokeza kwa nchi nzima ni zaidi ya kilo milioni 20 zilizozidi hali iliyosababisha tumbaku kukaa muda mrefu ghalani na kukosa ubora,” alisema Peter.

Wanunuzi wakuu wa zao hilo ni kampuni ya TLTC na Alliance One.

Katika uchaguzi huo, Peter alifanikiwa kutetea nafasi yake baada ya kupita bila kupingwa huku makamu wake akichaguliwa Geofrey Mbuto.

Wajumbe wa bodi wanaokamilisha safu ni Tano Nsabi, Cecilia Shigemo, Patrick Songoro na Elias Madata huku mjumbe mwakilishi kutoka nje ya bodi akichaguliwa Benedicto Bulugu.

Marekani yatakiwa isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel



Ayman Safadi alisema alimuambia waziri wa mashauri wa nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson kuwa hatua kama hiyo inaweza kuzua ghadhabu kubwa kwa nchi za kiarabu na ulimwengu wa kiisalmu.

Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni.

Jared Kushner, mkwe wa Trump alisema kuwa bado hakuna uamuzi uliofanywa.

Ubalozi wa Marekani kuhamia Jerusalem?

Palestina: Uhamisho wa ubalozi utaathiri amani

Katika mtandao wa Twitter, Bw Safadi alisema: #Nilizungumza na waziri Rex Tillerson kuhusu hatari ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Hatua kama hiyo inaweza kusababisha ghadhabu kwenye nchi za kiarabu na kwa ulimwengi wa kiislamu na kuzua misukosuko na pia kuhujumu jitihada za amani."

Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni.

Hakuna jibu lolote kutoka kwa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani.

Naye rais wa Palestina Mahmoud Abbas anajaribu kupata uungwaji mkono wa kimataifa katika kumshawishi Trump asifanye tangazo kama hilo.

Ofisi yake ilisema kwa aliwapigia simu Jumapili viongozi wa dunia wakiwemo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Askofu aliyewapatia silaha Wapalestina dhidi ya Israel afariki

"Alitaka kulezea harari za uamuzi wowote wa kuhamisha ubalozo wa Marekani kwenda Jerusalem au kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Isael," mshauri wa Bw. Abbas, Majdi al-Khalidi aliliambia shirika la AFP.Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Jardan ameonya Marekani kuhusu hatari ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Polepole amesema Chama chake hakitampokea Mtu adi afuate taratibu



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole  amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) hakitampokea yeyote anayetaka kurudi ndani ya chama hicho bila kufuata utaratibu. Kauli hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni(CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia kutangaza kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi alizokuwa akizishikilia kwenda CCM

Polepole aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa CCM mkoa wa Mara katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama.

“Ameamua kule aliko haoni itikadi,haoni siasa, haoni mwelekeo, Chama kina baba wawili huwezi kuwa na nyumba ina baba wawili alafu utasikiliza watoto watamsikiliza nani, basi amehama,” alisema Polepole.

“Sasa mimi niko hapa Musoma mimi nitumie fursa hii anayemuunga mkono ni Rais wetu ambaye ni mwana CCM kwelikweli na ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ikimpendeza afuate utaratibu akiona mazuri ya Rais yule asione vinaelea kwa mazuri yale asione vimeshushwa vimeundwa na wanaounda mambo mazuri ya Magufuli ni Chama cha Mapinduzi.

Audio | Young Dee Ft Dayna Nyange _ Ki Ben Ten | Mp3 Download

Audio | Young Dee Ft Dayna Nyange _ Ki Ben Ten | Mp3 Download

Audio | Young Dee Ft Dayna Nyange _ Ki Ben Ten | Mp3 Download

                 DOWNLOAD NOW

Diamond Platnumz aomba radhi kwa wanachuo,,,

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz jana alikuwa kwenye orodha ya wasanii wa WCB ambao walitakiwa kutumbuiza kwenye Party maalumu ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam lakini cha ajabu hakutokea jukwaani.
Sasa leo kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platnumz amewaomba radhi mashabiki wake kwa kutotokea kwenye party hiyo ya Dar Freshers ambayo iliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda kwa kusema kuwa, hata yeye alikuwa na hamu ya kujumuika na vijana wenzake lakini haikuwa riziki kwake.
Najua wengi mlikuwa na Shauku kubwa ya uwepo wangu pale Mlimani City jana ila amini kuwa, shauku yangu ya kuwepo pale kuimba na kufurahi pamoja nanyi, ilikuwa ni kubwa kuliko yenu na ndiomaana nilijitahidi sana kuhamasisha kwa uwezo wangu wote ili kwa wingi tufike pale….lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu sikuweza kufanikiwa kufika. Pengine Haikuwa Riziki yangu ama Labda Mwenyezi Mungu hakuniandikia siku ya jana kujumuika nanyi pale. Hivyo tusisononeke wala kuchukia…Niwaombe radhi na kuwapa pole wote ambao waliokwazika jana…Inshaallah Mwenyez Mungu siku akiniandikia kuwa pamoja nanyi ntawataarifu….. nimpongeze pia Mkuu wa mkoa pamoja na waandaaji wote, Wanavyuo, Media , na wasanii wote kwa kuifanikisha #FreshersParty. Hakika Historia iliandikwa🔥🔥🔥
Dar Freshers Party ilifanyika jana katika ukumbi wa Mlimani City na ilitumbuizwa na wasanii kutoka WCB, na wengine ni Dully Sykes, Ray C, Lady JayDee, Ruby, Christian Bella, Fid Q na Mwana FA.