Monday, 4 December 2017

Diamond Platnumz aomba radhi kwa wanachuo,,,

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz jana alikuwa kwenye orodha ya wasanii wa WCB ambao walitakiwa kutumbuiza kwenye Party maalumu ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam lakini cha ajabu hakutokea jukwaani.
Sasa leo kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platnumz amewaomba radhi mashabiki wake kwa kutotokea kwenye party hiyo ya Dar Freshers ambayo iliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda kwa kusema kuwa, hata yeye alikuwa na hamu ya kujumuika na vijana wenzake lakini haikuwa riziki kwake.
Najua wengi mlikuwa na Shauku kubwa ya uwepo wangu pale Mlimani City jana ila amini kuwa, shauku yangu ya kuwepo pale kuimba na kufurahi pamoja nanyi, ilikuwa ni kubwa kuliko yenu na ndiomaana nilijitahidi sana kuhamasisha kwa uwezo wangu wote ili kwa wingi tufike pale….lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu sikuweza kufanikiwa kufika. Pengine Haikuwa Riziki yangu ama Labda Mwenyezi Mungu hakuniandikia siku ya jana kujumuika nanyi pale. Hivyo tusisononeke wala kuchukia…Niwaombe radhi na kuwapa pole wote ambao waliokwazika jana…Inshaallah Mwenyez Mungu siku akiniandikia kuwa pamoja nanyi ntawataarifu….. nimpongeze pia Mkuu wa mkoa pamoja na waandaaji wote, Wanavyuo, Media , na wasanii wote kwa kuifanikisha #FreshersParty. Hakika Historia iliandikwa🔥🔥🔥
Dar Freshers Party ilifanyika jana katika ukumbi wa Mlimani City na ilitumbuizwa na wasanii kutoka WCB, na wengine ni Dully Sykes, Ray C, Lady JayDee, Ruby, Christian Bella, Fid Q na Mwana FA.

No comments:

Post a Comment