Thursday, 30 November 2017

Diwani wa CCM afariki ajalini



Songea. Diwani wa viti maalumu (CCM), Mariam Yusuph (53) amefariki dunia katika ajali iliyojeruhi wengine wawili mkoani Ruvuma.

Ajali ilitokea walipokuwa wanakwenda kwenye uchaguzi wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Ruvuma.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Songea, Dk Magafu Majura amesema amepokea majeruhi wawili na mwili wa diwani huyo leo Alhamisi Novemba 30,2017 saa 3:30 asubuhi.

Amesema majeruhi waliowapokea ni Asia Sapwela (52) ambaye ni diwani wa viti maalumu aliyevunjika mkono wa kulia, mbavu na ana michubuko miguuni.

Dk Majura amesema majeruhi mwingine ni Atingala Ally (48), ambaye ni diwani mstaafu wa Tunduru aliyeumia mbavu na mguu wa kulia. Amesema majeruhi wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushi akizungumzia ajali hiyo amesema imetokea katika Kijiji cha Lumecha wilayani Songea ikihusisha gari aina ya Toyota Carina.

Amesema gari hilo lilikuwa likitokea wilayani Tunduru kwenda Songea.

Kamanda Mushi amesema gari hilo likiendeshwa na Osam Ulaya liligonga kingo za barabara kabla ya kupinduka.

Amesema Mariam alifariki dunia papo hapo baada ya kujigonga kichwani.

Dereva Ulaya amepelekwa katika Hospitali ya Peramiho kwa matibabu na polisi wanaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.

Alexandre Lacazette atakaa nje kwa muda



Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anahofia mshambuliaji Alexandre Lacazette ''hatakuwa uwanjani kwa muda'' baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu siku ya Jumatano, katika mecho ambayo walipata ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya Huddersfield.

Lacazette, 26, alifunga bao la kwanza lakini alitolewa uwanjani wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Oliver Giroud.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amefunga magoli saba kwa Gunners tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Lyon mwezi Julai kwa kitita cha £46.5m.

''Ni bayana hatashiriki mechi ya wikendi hii,'' Wenger amesema.

''Alipata jeraha kwenye kifundo cha mguu wake. Atakuwa nje ya mchezo kwa muda.''

Gigy Money ampa makavu Rado.


Msanii Gigy Money amemtolea povu muigizaji wa filamu wa bongo Rado, ambaye wiki iliyopita alisikika akisema wasanii wa kike wa bongo fleva hawana vigezo vya kuolewa, na kusema kwamba ndoa siku hizi haina dili kwani wanwake wanajioa wenyewe.

Gigy ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Radio, na kusema kwamba suala la kuolewa halina dili sana kwani wanawake wanaoa wenyewe kwa kujilipia mahari, na kumtaka Rado apambane na hali yake kwa kutokuwa na hela ya kuweza kuwapata watoto wazuri.


Emmanuel Okwi atarajiwa kujiunga na wenzake Jumatatu



Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anaweza kurejea nchini kati ya Jumamosi au Jumapili kuungana na wenzake.

Taarifa zinaeleza Okwi amepata nafuu kwa kiwango kizuri kabisa na anaweza kuanza mazoezi.

"Inawezekana akarejea wikindi hii, Jumamosi au Jumapili. Kama atakuwa fiti kabisa ataanza mazoezi Jumatatu," habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza.

Lakini taarifa nyingine zinaeleza, pamoja na nafuu, Okwi anaweza kuchelewa kwa kuwa mkewe alikuwa amejifungua mtoto wa pili.

"Pamoja na kuwa majeruhi, kumbuka mkewe alijifungua. Hivyo anaweza kutaka kuhakikisha mambo yamekaa vizuri katika msitari kabla ya kuondoka," kiliongeza chanzo.

Kombe la Cecafa Challenge kuonyeshwa live na Azam TV



KAMPUNI ya Azam Media, imeingia mkataba na Baraza la Vyama vya Soka Afika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa ajili ya kuonyesha mechi zote za michuano ya kombe la Chalenji, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 3 hadi 16 mwaka huu nchini Kenya, yakishirikisha jumla ya timu tisa.

Akizungumza na Wanahabari jana katika studio za Azam Tv, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Tido Mhando, alisema kuwa, baada ya kuafanya vizuri katika Ligi Kuu Bara na mashindano mbalimba ya Ukanda wa Afrika Mashariki, zikiwemo nchi za Uganda, Rwanda na Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, Azam TV sasa imeamua kupiga hatua zaidi na kuingia katika michuano mikubwa zaidi Afrika.

Alisema huo ni moja ya mipango ya Azam kwenye mikakati yao ya muda mrefu kuonyesha michuano mikubwa zaidi ya soka kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana (AFCON) wa umri chini ya miaka 17, itakayofanyika Tanzania mwaka 2019.

“Kwa upande wetu maandalizi yanaendelea vizuri na timu nzima ya utayarishaji na urushaji matangazo ya moja kwa moja (Mubashara) tayari ipo katika vituo vyote nchini Kenya ambavyo vitatumikwa kwa mashindano ya mwaka huu,” alisema Mhando.

Aliongeza kuwa, Azam Tv wamejipanga kwa ajili ya kutoka burudani nzuri kwa wapenzi wa soka wa Afrika Mashariki na Kati kwa kuhakikisha wanafikisha matangazo hayo kwa uborea wa hali ya juu.

Mhando alisema huo ni mwanzo tu kwao kwao tayari wameanza mazungumzo na CECAFA kwa ajili ya kutangaza mashindano ya Kagame Cup yanayoshirikisha klabu mbalimbali.

Morogoro: Wabunge wa chadema wakosa dhamana



Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, imewanyima dhamana, Wabunge Peter Lijualikali, Suzan Kiwanga na wafuasi wengine 34 wa Chadema wakiwepo madiwani, na kuwarudisha mahabusu hadi Disemba 04 mwaka huu.

Wabunge hao walikamatwa mapema wiki hii kwa tuhuma za kufanya vurugu katika uchaguzi wa madiwani ikiwa ni pamoja na kuchoma shule na rasilimali nyingine za umma
Mapema wiki hii Polisi wa mkoani Morogoro inawatia mbaroni watu 41 akiwemo mbunge wa Mlimba (Chadema), Susan Kiwanga, madiwani wawili kwa madai ya  kufanya fujo na kuchoma moto majengo ya shule baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Sofi
Kamanda wa Polisi Ulrch Matei alisema kwambaViongozi hao walikuwa wakiwachochea wafuasi wa chama hicho kuchoma moto  nyumba ya walimu wa shule ya Sofi na ofisi ya mtendaji kata na pia hataa baada ya kuchoma majengo hayo kwa kutumia petroli, walidhamiria pia kwenda katika zahanati lakini askari waliwakamata.

Mbunge Lijualikali yeye alijisalimisha baada ya kupata taarifa kwamba anatafutwa.

VIDEO: RC Makonda abeba jukumu la matibabu ya Ahmed Albaity



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amejitolea kumsaidia kijana Ahmed Albaity  anayesumbuliwa na tatizo la Uti wa Mgongo lililompelekea kulala kitandani kwa takribani miaka 10.
TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Kijana huyo anatakiwa kwenda kutibiwa nchini China kwa muda wa wiki tatu akiambatana na wasaidizi wawili ambapo gharama za matibabu zinazohitajika ni zaidi ya dola 40,000 za marekani ambapo sindano moja aliyoandikiwa inagharimu kiasi cha dolla 27,000.

RC Makonda amesema atafanya jitihada zote kuhakikisha Ahmed anapatiwa Matibiwa ili aweze kupona na kutimiza ndoto zake akiwa na Afya Njema.

Mapema leo RC Makonda ametembelewa ofisini kwake na Balozi mpya wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke ambae amekuja kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa ambapo katika mazungumzo RC Makonda amemgusia balozi huyo suala la matibabu ya AHMED ALBAITY ambapo Balozi WANG KE alieambatana pia na Daktari Bingwa wa China aliebaki Nchini kwaajili ya Shughuli ya Serikali ya China ambapo wamemtazama na kupitia Ripoti ambapo wameahidi kulifanyia kazi suala hilo.


Katika Mazungumzo hayo pia wamejadili Masuala mbalimbali ikiwemo Kuimarisha Usalama, Kampeni ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu na kuongeza huduma kwa Wananchi.

MAKONDA pia ameishukuru Serikali ya China kwa kuleta Meli ya Jeshi la China yenye Hospital ndali ambayo imesaidia kutoa vipimo na Matibabu kwa wananchi wengi.

Kwa Upande wake Bolozi Mpya wa China Nchini Tanzania WANG KE amesema Serikali ya China itaendelea kusaidiana na Tanzania katika masuala yote ya maendeleo


Simba kufanya usajili mwingine


Simba ina mpango wa kumsajili mtu ambaye atamaliza tatizo la umaliziaji.

Kocha Msaidizi wa Simba, Djuma Masoud amesema mpango wao msimu huu ni kuhakikisha wanafanya usajili bora.

Dirisha dogo la usajili lilifunguliwa hivi karibuni na linatarajiwa kufungwa Desemba 15, mwaka huu.
Djuma alisema kuwa wanahitaji wachezaji wanne wa nguvu ambao ni kipa, beki wa kati, winga pamoja na straika.

Masoud amesema kuwa licha ya uhitaji huo wa wachezaji hao, hata hivyo mchezaji ambaye wanamuhitaji zaidi ni mshambuliaji.

Alisema sifa ambazo wanataka mshambuliaji huyo wanayemhitaji awe nazo ni awe anajua kuzitumia vizuri nafasi za kufunga ambazo atakuwa anazipata uwanjani, awe na uwezo mkubwa wa kupambana na mabeki wa timu pinzani lakini pia awe anajua kutafuta nafasi za kufunga.

“Tunataka kuhakikisha tunafanya vizuri msimu huu na kuvunja utawala wa Yanga, lakini pia ukiachana na ligi kuu pia tunakabiliwa na mashindano wa kimataifa kwa hiyo tunataka kuwa na mshambuliaji wenye uwezo mkubwa na mwenye sifa hizo.

“Tunaendelea na harakati zetu na muda si mrefu naamini tutampata lakini pia wachezaji hao wengine ambao tunawahitaji,” alisema Masoud ambaye ni raia wa Burundi aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akichukua mikoba ya Mganda, Jackson Mayanj


Azam FC ruksa kumtumia Mghana



Azam FC itakuwa imetibu lile suala lake la ushambulizi na kuhakikisha inapata mabao mengi zaidi.

Hii inatokana na ruhusa waliyoipata ya kumtumia straika wake mpya, Bernard Arthur raia wa Ghana baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili ikiwemo kuwasili kwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).

Azam imemsajili straika huyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Klabu ya Liberty Proffessionals ya nchini Ghana ili kuchukua nafasi ya Mghana mwenzake, Yahaya Mohammed aliyefungashiwa virago hivi karibuni.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema walitoa ruhusa ya mchezaji huyo kuanza kuitumikia Azam kabla hata ya mchezo wao wa juzi Jumatatu wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Hivi sasa Azam inaweza kumtumia straika wao mpya kwani wamekamilisha kila kitu kinachotakiwa kufanyika ikiwemo kuwasili kwa ITC yake.

“Hivi sasa mchezaji akisajiliwa kisha taratibu zikafanyika haraka, basi sisi tunamruhusu kuanza kuitumikia timu yake mpya wakati usajili ukiendelea,” alisema Lucas.



Malinzi na Aveva warudishwa rumande


 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeziahirisha kesi za utakatishaji fedha inayowakabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na ile inayomkabili aliyekuwa Rais (TFF), Jamal Malinzi hadi December 14,2017 kwa sababu upelelezi haujakamilika.

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Vitalis Peter amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi ya Aveva na Malinzi zimeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi hizo bado haujakamilika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hizo hadi December 14/2017.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya March 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa  USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli


Nape Nnauye afunguka haya



Ilikua ni wakati wa kuufungua Msikiti mpya uliojengwa katika jimbo la Mtama linaloongozwa na Mbunge Nape Nnauye ambapo waliohudhuria ni pamoja na Mufti wa Tanzania mwenyewe, Waziri wa zamani Benard Membe na wengine.

Kwenye ufunguzi huo Nape Nnauye alinukuliwa akisema “Sisi Wanasiasa wakati mwingine tunawasha moto mwingi mno tunashindwa kuuzima lakini kupitia Dini zetu hizi kama mambo yakiwekwa vizuri mioto mingi inazimika na mambo yanakwenda vizuri“

“Tumeanza kuona wakati mwingine tunafanya chaguzi zetu, watu wanakatana mapanga, watu wanapigana…. wanashutumiana, hili jambo sisi Wanasiasa tunaweza tukashindwa kulihimili lakini nyinyi viongozi wa dini mkisimama mkatusaidia inawezekana sababu watu hawa wanatoka miongoni mwetu humuhumu“

Manchester City yamuongezea mkataba wa mwaka mmoja David Silva




David Silva ametia saini mkataba wa mwaka mmoja zaidi kukaa Manchester City hadi mwaka 2020.
Kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Man City kutoka Valencia kwa kitita cha £24m mwaka wa 2010.

Kiungo huyo ameshinda taji la ligi ya Premia mara mbili, kombe la FA na vikombe viwili vya ligi akiwa na City.

Klabu hiyo ya Pep Guardiola imo alama nane mbele kileleni mwa ligi ya Premia baada ya ushindi wa mechi 12, ushindi wao wa hivi karibuni ukiwa siku ya Jumatano dhidi ya Southamton.

Silva, ambaye amesaidia ufungaji wa magoli manane, usaidizi ambao hakuna mchezaji yeyote wa kiwango chake ametimiza, amesema anatarajia kuongeza tuzo zaidi Etihad.

''Najivunia kwa kile nilichojivunia na City kwa misimu saba na nusu hapa pamoja na Pep akiwa meneja. Najihisi tuko katika nafasi nzuri kushinda vikombe msimu huu na kuendelea,'' alisema Silva.

''Mbinu tunayoitumia kucheza soka ni nzuri na ni furaha yangu kuwa miongoni mwao na natarajia kushinda mataji mengi miaka ijayo

Israel inatarajia kufungua ubalozi wake nchini Rwanda



Waziri mkuu wa Isreal katika hafla ya kutawazwa Uhuru Kenyatta kuwa rais wa Kenya  alifahamisha kuwa Israel inatarji kufungua ubalozi wake nchini Rwanda.

Taarifa hiyo kuhusu kufunguliwa kwa ubalozi wa Israel nchini Rwanda  inaonesha kuwa  ushirikiano bain aya Rwanda na Israel unazidi kuimarika.

Katika mazungumzo yake na viongozi wa bara la Afrika, Netanyahu a alizungumza pia na rais  Paul Kagame.

Netanyahu amesema kuwa  Paul Kagame  ni mhandisi  katika kuboresha ushirkiano bain aya Israel na bara l a Afrika.

Rwanda ni taifa mshirika wa Israel.

Ikumbukwe kuwa Rwanda  haikuonesha msimamo wake  baraza la usalama la Umoja wa mataifa lilipo omba kura ipigwe kuitaka Israel  kusitisha kukalia kimabavu ardhi ya wapalestina.