Monday 4 December 2017

Aliyekuwa Waziri Mkuu Misri hajulikani alipo



 Familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Misri, Ahmed Shafiq imesema haina taarifa wapi aliko ndugu yao baada ya kutangaza ana azma ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu mwakani.

Shafiq ambaye ni kamanda wa zamani wa jeshi la anga la Misri na waziri mkuu katika utawala wa Hosni Mubarak, anaonekana kuwa mgombea mwenye nguvu ya kuchuana na Rais Abdel Fattah al Sisi ambaye anatarajiwa kugombea muhula wa pili katika uchaguzi huo.

Familia ya Shafiq aliyerejea mjini Cairo jana kwa kutumia ndege binafsi imesema haijui lolote kuhusu hatima yake.

Wakili wake pia amesema hajawasiliana naye, huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ikisema haihusiki na suala la Shafiq.

Ripoti zinasema Shafiq aliwasili Misri jana jioni na alionekana mjini Cairo.

Maofisa wa Falme za Kiarabu wamethibitisha kuwa Shafiq aliondoka nchini humo.

No comments:

Post a Comment