Asasi za kiraia zimetakiwa kufuata taratibu kabla ya kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananchi ili kukwepa udanganyifu, ikiwa ni pamoja na kuwachangisha fedha na kutokomea kusikujulikana.
Kauli hiyo imetolewa leo Februari 3, 2018 na ofisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Temeke, John Bwana wakati akizindua mradi wa kuwajengea wanawake uwezo kuhusu ujasiriamali ili kujiinua kiuchumi ulioandaliwa na asasi ya Iwapoa.
Amesema kuna lundo la asasi za kiraia zinazotoa mafunzo kiholela na kuwatapeli wanawake kwa kuwachangisha michango na kutokomea na fedha zao.
“Iwapoa mmefanya jambo la maana kufuata taratibu za kuonana na mamlaka husika na kupata wataalamu kutoka katika kata mtakazofanya kampeni hii ya kupunguza umasikini kwa kuwajengea wanawake uwezo,|” amesema na kuongeza,
“Nawaunga mkono na ninatoa rai kwa asasi nyingine zisizofuata utaratibu zifanye hivyo mara moja kwa sababu tunazifuatilia na tukizibaini tutazizuia kufanya kazi zake katika maeneo yetu.”
Mratibu wa mradi huo kutoka Iwapoa, Yusuph Kutegwa amesema mradi huo utatekelezwa katika kata sita za Manispaa ya Temeke.
Amezitaja kata hizo kuwa ni Buza, Keko, Chamazi, Vituka, Azimio na Charambe.
Amesema utawafikia wanawake 150 kutoka katika maeneo hayo waliyoyachagua kutokana na kuwa na wingi wa watu, wakiwamo wanawake wasiokuwa na shughuli za kudumu.
“Ili kuwapatia masoko na mitaji tutawaunganisha katika vikundi vya watu watano watano, ili iwe rahisi kuwapa ujuzi kwa pamoja, ”amesema Kutegwa.
Mlinda mlango namba mbili wa Simba, Said Mohammed 'Nduda' wiki ijayo anatarajia kujiunga na wenzake tayari kuanza mazoezi baada ya kuwa nje kwa miezi mitano, kufuatia kufanyiwa upasuaji wa goti Oktoba mwaka jana nchini India.
Mbunge mwingine nchini Kenya, amekamatwa kuhusiana na mzozo unaozunguka kujiapisha kwa aliyekuwa waziri mkuu Raia Odinga kwa kile anachokitaja kama rais wa watu wa Kenya.
Msanii Radio wa nchini Uganda ambaye alifariki Februari 1, amezikwa leo kijijini kwao Nakawuka nchini Uganda, na kuhdhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali za nchi hiyo na wasanii wa nchi jirani.




Serikali mkoani Lindi imeunda timu ya kuchunguza matukio ya baadhi ya wakulima kuchanganya mchanga na korosho kwa nia ya kuongeza uzito wakati wa kupima kwenye mizani, ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakaobainika kufanya hhujuma hiyo.
Rais wa Marekani Donald Trump amewapigia simu viongozi wa Japan na Korea Kusini siku chache kabla ya michezo ya Olimpiki kuanza nchini Korea Kusini.
Watu watatu waripotiwa kufariki nchini Uswidi kutokana na baridi kali Kaskazini mwa Uswidi.
Singida United wameshinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Mwadui FC katika mechi kali ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeridhia kuhamishwa kwa vituo 46 vya kupigia Kura katika kata tatu za jimbo la Kinondoni zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Ubunge Februari 17 mwaka huu.
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata tija.