Tuesday, 5 December 2017

Kenya inampango wa kuzalisha kawi ya nyuklia kufikia 2027



Kenya imesema kwamba itaendelea na mpango wake wa kuhakikisha kwamba ina kiwanda cha kuzaliwa umeme kwa kutumia nguvu za nyuklia kufikia 2027.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Umeme wa Nyuklia ya Kenya Collins Juma ameambia mkutano wa wadau kuhusu kawi jijini Nairobi kwamba ujezi wa kiwanda cha kuzalisha kawi hiyo unatarajiwa kuanza 2024.

Bodi hiyo imesema nishati hiyo itatumiwa kuongeza uzalishaji wa umeme nchini humo na si kuchukua nafasi ambayo imekuwa ikitekelezwa na vyanzo vingine vya kawi nchini humo.

Kufikia mwaka 2030, ambapo Kenya inatazamia kuwa taifa lenye viwanda la mapato ya wastani kufikia wakati huo, Kenya itakuwa ikihitaji megawati 17,000.

Kawi ya mvuke itachangia megawati 7,000. Kwa sasa, kawi hiyo kwa sasa hutumiwa kuzaliwa megawati 2,400 za umeme nchini humo.

Kaimu afisa mkuu mtendaji wa kukinga dhidi ya miali nururishi nchini Kenya Joseph Maina amesema Wakenya hawafai kuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa nishati ya nyuklia.

"Kumekuwa na ajali tatu pekee kubwa za nyuklia katika historia. Kisiwa cha Three Mile Marekani, 1978; Chenorbyl nchini Ukraine, 1986 na Fukushima nchini, Japan, 2011. Usalama umeimarishwa kutokana na mafunzo kutoka kwa mikasa hiyo," amesema.

Kenya imekuwa na mpango wa kuzalisha kawi ya nyuklia kwa muda.

Machi mwaka huu, Waziri wa nishati na mafuta wa nchi hiyo Bw. Charles Keter alisema Kenya itatimiza vigezo vikali vilivyowekwa na Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki IAEA kabla ya kutekeleza mpango huo.

Alikadiria kwamba Kenya itatumia dola 5 bilioni za Marekani kujenga kiwanda cha kuzalisha kawi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya IAEA ya mwaka 2015, zaidi ya nchi 30 duniani, theluthi moja zikitoka Afrika zinajiandaa kuanzisha mipango ya nyuklia kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa usaidizi wa wataalamu kutoka shirika hilo.

VIDEO: Walichosema Witness na Tea kuhusiana na uzalendo

Hiki ndicho walichokisema Witness A.K.A kibonge mwepesi na Ndumbagwe misayo A.KA Tea kuhusiana na uzalendo ambapo waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Mh. Harrison Mwakyembe

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.........USISAHAU KUSUBSCRIBE.

VIDEO: Polisi wamnasa komandoo wa Burundi akiwa na AK.47 akifanya matukio ya ujambazi


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es alaam mnamo tarehe 28/11/2017 na tarehe 30/11/2017 askari walifanya oparesheni maalum ambayo ilifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa watatu ambao wanajihusisha na matukio ya uporaji na mauaji mbalimbali katika jiji la Dar es salaam.

TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Kamanda SACP Lazaro Mambosasa amesema hayo leo  alipozungumza na waandishi wa habari, na kusema kuwa baada ya  mahojiano name watuhumiwa hao walikubali kuonyesha silaha moja aina ya AK.47, Magazine mbili 2 na risasi 57 ambayo walikuwa wameificha kwenye kichaka karibu na eneo la Ubungo Mawasiliano, pia walionyesha pikipiki mbili aina ya Boxer zenye namba za usajili MC 757 BCT rangi nyekundu na MC 946 BSE  rangi nyeusi ambazo walizipora katika matukio mbalimbali.


Pia Kamanda Mambosasaaliongeza kuwa walipohojiwa zaidi walisema wanazo silaha nyingine ambazo wamezificha kwenye kichaka eneo la Ununio na wako tayari kwenda kuonyesha silaha hizo, walipofika huko wakati wakishuka kwenye gari jambazi mmoja raia wa Burundi aliyefahamika kwa jina la Fanuel Luchunda Kamana @Mrundi alimvamia askari kwa lengo la kumpora silaha huku wenzake wawili wakijaribu kutoroka na ndipo walijeruhiwa kwa risasi.

Aidha majambazi hao waliwahishwa katika hospitali ya Mwananyamala ili kupatiwa matibabu na ndipo madaktari wakabaini kuwa tayari wameishafariki dunia.

Miili hiyo imehifadhiwa hospitalini hapo kwa hatua za uchunguzi wa kitaalamu, aidha majambazi hao walikiri kufanya matukio kadhaa ya uporaji na mauaji likiwemo tukio la mauaji huko Kunduchi Mtongani la tarehe 19/11/2017 ambapo huwaua madereva bodaboda na kupora pikipiki zao na kuziuza kwa TSHS.800, 000/=.

Majambazi wengine waliofariki ni Gallus Clement, (31) na Fredrick Wilbord Acholo mkazi wa Gongo la Mboto.

VIDEO: Waziri Mwakyembe amkabidhi Ibrahim Classic TSH 18 Milioni


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe leo ameonesha uzalendo wake baada ya kumkabidhi Bondia Ibrahim Classic kiasi cha Tsh Milioni 18 kama malipo yake ya pambano na Bondia Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini ambapo Ibrahim alishinda pambano hilo na kutetea ubingwa wake wa Dunia wa CBG.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Dhamana ya Wabunge Lijualikali na Susan Kiwanga kujulikana kesho


Morogoro. Wabunge Susan Kiwanga na Peter Lijualikali waliofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro pamoja na washtakiwa wengine 36 wamerejeshwa rumande.

Mahakama iliyokuwa itoe uamuzi wa dhamana leo Jumanne Desemba 5,2017 imekwama kufanya hivyo kutokana na kuibuka hoja za kisheria.

Upande wa mashtaka na ule wa utetezi unavutana kuhusu hati ya kiapo ya kupinga dhamana iliyowasilishwa mahakamani hapo.

Kutokana na mvutano wa kisheria, hakimu Ivan Msack ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano Desemba 6,2017 ili kutoa fursa kwa pande zote mbili kujibu hoja kuhusu hati hiyo.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka nane likiwamo la kuchoma moto ofisi ya Kata ya Sofi iliyopo wilayani Malinyi.

Washtakiwa wanatetewa na mawakili Peter Kibatala, Ignas Punge, Fredrick Kiwelo na Bartholomew Tarimo.

Upande wa mashtaka unawakilishwa na mawakili wa Serikali, Edga Bantulaki na Sunday Hyera.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Frederick Sumaye walihudhuria mahakamani.

Wengine waliofika mahakamani ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na wa Viti Maalumu, Devota Minja.

Usiku wa Kitendaliwili kuzinduliwa Disemba 8 Dodoma


Usiku wa Kitendawili unaotarajiwa kufanyika Disemba 8 mwaka huu huko mkoani Dodoma ndio habari ya mjini kwa sasa, kwani watanzania wanashahuku kubwa ya kusikia kauli za viongozi mbalimbali wastaafu na walioko madarakani kuhusu harakati za Tanzania kupata uhuru pamoja na jinsi watanzania walivyoonganika na kuwa kitu kimoja licha ya kuwa na makanila 120.

Viongozi wa zamani wa serikali, walipo madarakani pamoja na wadau wakiwa wamekaa chini kwenye mikeka ya asili na vigoda watapata fursa ya kueleza namna serikali kupitia viongozi wake ilivyoweza kuondoa mambo ya ukabila ambayo yanayatesa mataifa mengi ya Afrika.

Akiongea na TBC katika kipindi cha Tanzania Mpya, Mrisho Mpoto amesema kuwa siku hiyo mgeni rasmi ambaye ni Rais John Pombe Magufuli atapata fursa ya kueleza maisha yake ya utoto na namna alivyoweza kusimama katika mstari ambao kila mmoja kwa sasa akiangalia matendo yake anaona rais kweli ni mzalendo wa kweli.

“Usiku wa Kitendawili ni ukurasa mpya wa kujifunza mambo mapya kuhusu uzalendo na kuanza utekelezaji mara moja, na kama unavyojua tutakuwa na viongozi mbalimbali katika huo usiku, Mhe. Rais wetu John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu pamoja na Waziri Mkuu na wote watapata fursa ya kueleza mawili machache kuhusu uzalendo, wao waliwezaje kuwa wazalendo wa kweli, tunapokuwa kuna jambo la kitaifa tuungane kwa pamoja kama watanzania, wanapotokea watu wachache wakajitenga huo sio uzalendo ndio maana nikasema hiyo siku tutamsikiliza Rais wetu amewezaje kuwa mzalendo ambaye kila mtu akimuangalia anaona kabisa huyo ni mzalendo na apaswa kuungwa mkono na watanzania wote kwa manufaa ya taifa leo na la kesho,” alisema Mpoto.

Aliongeza, “Lakini pia tumeomba protocol zisiwe kali sanaa kwa upande watanzania na viongozi ili watu wafunguke, tunataka Rais wetu atuambie kwanini yupo vile, kwa nini anakuwa na uchungu na watanzania hasa watanzania wa chini, kwa nini anawafikiria wanyonge zaidi.

 Kuna wakati Mhe Rais anasema Tanzania ya Viwanda watu wanaona kama haeleweki, lakini sasa hivi viwanda vimeongezeka kila mtu amenza kuamini kwamba Tanzania ya Viwanda inawezekana, kwa sababu imetoka kwenye ubongo kama wazo imeenda kwenye uhalisia.

 Kwahiyo ninachosema kwamba tutakaa kwenye mikeka na vigoda, tutakula ugali ya muhogo, kisamvu na madafu , Majaliwa pale, Mama Samia pale , tunakaa pale na ule ukumbi umetengenezwa kama kuna vijiji na mitaa, Mhe atapita pale kwenda kusalimia kijiji cha jirani watuambie tu wamewezaje kuondoa suala la ukabila, nchi za wenzetu wanapigana kila siku, kwahiyo kama tukitumia nguvu iliyotumiaka kuwaonganisha watanzania ambao kwa wingi wetu tuna makabila 120, lakini wote tukawa kitu kimoja kwanini tushindwe watanzania na wote tuimbe wimbo mmoja wa Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’,”

Mpoto amesema kwa sasa kuna haja ya kuwa na nyimbo za hamasa ambazo zitawajenga watanzania kuwa wazalendo na kukataa rushwa pamoja na kuacha kufanya kazi kizembe.

Usiku wa Kitendawili umeanzishwa na msanii wa huyo wa muziki wa asili nchini baada ya kuachia wimbo wake ‘Kitendawili’ na baadaye kufikiria kuanzisha usiku wa wimbo huo kwaajili ya kuwakutanisha wadau na kujadili kuhusu Uzalendo.

Alisema baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo, itayokuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julis Kambarage Nyerere, wataanza kuzungumza katika mikoa mbalimbali kupaza sauti kuhusu uzalendo.

Mpoto alisema mambo yatayopambaniwa katika kampeni hiyo ni pamoja na kudhibiti na hatimaye kukomesha kabisa mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa umma, kupunguza tuhuma za rushwa, ufisadi, ubadhilifu wa mali za umma pamoja kuongeza hari ya kufanya kazi na Uzalendo.

Rais Mwinyi amtembelea Lissu, Nairobi


RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi leo Desemba 5, 2017 amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika, Tundu Lissu katika Hospitali ya Nairobi anakotibiwa baada kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, Mjini Dodoma.


Rais Mstaafu Kikwete afanya uteuzi huu


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete amemteua Profesa William-Andey Anangisye kuwa makamu mkuu wa chuo hicho.

Prof. Anangisye ameteuliwa katika nafasi hiyo kuitumikia kwa miaka mitano kuanzia leo Desemba 5, 2017. Makamu mkuu huyo mpya wa chuo anachukua nafasi ya Profesa Rwekaza S. Mkandala ambaye anamaliza muda wake.

Mkuu huyo wa chuo Dkt. Kikwete amefanya uteuzi huo baada ya kushauriana na bodi ya chuo kwenye kikao kilichofanyika Novemba 30 na baadae kumjulisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Kampuni ya CNBM Group yaunga mkono jitihada za Makonda



Kampuni ya China Nationali building Material Group leo imekabidhi hundi ya Shilingi Milioni kumi ili kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kusaidia Watu wenye uhitaji wa miguu bandia na zoezi la upimaji afya.


Akizungumza na Waandishi wa habari leo mara baada ya kupokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa,  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dakta Grace Magembe amesema Serikali ya Mkoa imekusudia kutatua changamoto za kiafya kwa wananchi pamoja na kusaida watu wenye ulemavu,ambapo amebainisha kuwa hapo awali Serikali ya Mkoa ilikusudia kusaidia watu wenye ulemavu miambili lakini idadi ya wenye uhitaji wa miguu ni zaidi ya watu elfu moja hivyo amewataka wadau kuendelea kujitokeza kusaidia.

Dakta Magembe ameongeza kuwa tokea kuingia madarakani Serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais Dakta John Magufuli imekuwa ikishughulikia changamoto mbalimbali za wananchi hivyo amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya China National building Material Group Wang Shupeng amesema kampuni hiyo imeridhishwa na juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na imetambua umuhimu wa kusaidia watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo miguu bandia hivyo mbali na msaada huo wa shilingi milioni kumi za kitanzania itaendelea kutoa misaada mbalimbali kuunga mkono serikali.

Mbunge wa kibamba Mnyika akana taarifa za kujiuzulu


Mbunge wa Kibamba, John Mnyika amesema taarifa kwamba amejiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema -Bara hazina ukweli.

Mnyika ambaye amekuwa akitajwa tajwa kwamba atakihama chama hicho, ametoka kauli hiyo baada ya kuwapo taarifa kwamba  amejiuzulu wadhifa huo.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Desemba 5,2017 jioni kuhusu taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu; Mnyika amesema, ‘’Si kweli ni taarifa za uongo.’’

Afrika Kusini: Ugonjwa wa Listeriosis waua watu 36



Takriban watu 36 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Listeriosis Afrika ya Kusini.

Waziri wa afya Aaron Motsoaledi ametangaza kuwa kesi nyingi za mlipuko huo zimeripotiwa kutoka katika maeneo ya Gauteng,Western Cape na KwaZulu Natal.

Kwa mujibu wa habari,chanzo kabisa cha mlipuko wa ugonjwa huo bado kinafanyiwa utafiti wa kina.

Ugonjwa wa Listeriosis ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na kula chakula chenye bakteria Listeria.

Maafisa wa mazingira wanafanya utafiti kuangalia sampuli za vyakula waliokula wagonjwa hao.

Ripoti zinaonyesha kuwa zaidi ya kesi 557 za ugonjwa huo zimeripotiwa toka kuanze kwa mwaka.

California yakumbwa na moto mkali


Mtu mmoja ameripotiwa kupoteza maisha huku maelfu ya watu wakiwa wamekimbia manyumba yao kutokana na moto mkali ulioikumba California

Kwa mujibu wa habari,moto huo umesababishwa na hali ya hewa iliyosababisha moto ho kusambaa kwa kasi.

Moto huo wa "Thomas" unasemekana kuchochewa na upepo mkali,hali ambayo inausababisha kusambaa kuelekea mji wa Ventura.

Ripoti zinaonyesha kuwa moto huo unasambaa kwa kasi na manyumba pamoja na mali za watu vipo katika hatari ya kuangamizwa.

Mpaka sasa watu 27,000 tayari wameyahama makazi yao.

Moto huo umeripotiwa kuwa ni hatari na umekuwa vigumu kuudhibiti.

Huyu ndiye refa atakayechezesha mechi ya mahasimu wa Manchester Jumapili



REFA Michael Oliver ameteuliwa kuchezesha mchezo wa ujao mahasimu wa Jiji la Manchester.
Uwanja wa Old Trafford unatarajiwa kuhimili vishindo vya mpambano wa mahasimu, Manchester United na Manchester City Jumapili, moja kati ya mechi zinazotarajiwa kuwa na ushindani mkali msimu huu.

Timu hizo mbili kwa sasa zinafuatana juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, huku United wakionekana kama washindani kweli wa City kwenye mbio za ubingwa.

Pointi nane zinazitenganisha kwa sasa timu hizo mbili bvaada ya mechi 15, na City haijaonja ladha ya kipigo msimu wote huu.

Oliver atasaidiwa na washika vibendera Gary Beswick na Simon Bennett, wakati mezani atakuwapo Jon Moss.

Huu si mchezo wa kwanza wa mahasimu hao kwa mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 32, aliyeibukia Ashington, kwani awali alichezesha mechi ya Machi timu hizo zilipokutana.

Oliver ndiye aliyekataa penalti ya Marcus Rashford ambayo mashabiki wa Man United wanaamini ilikuwa ni halali.

Katika mechi zilizotangulia za mahasimu hao, Oliver alimtoa kwa kadi nyekundu beki wa Man United, Chris Smalling timu hizo zilipokutana mwaka 2014.

Mechi ya Jumapili Man United watamkosa kiungo wao, Paul Pogba aliyetolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Arsenal Uwanja wa Emirates baada ya kumchezea vibaya, Hector Bellerin.

United imeamua kutokata rufaa, hivyo itakutana na kikosi cha Pep Guardiola bila mchezaji wake huyo ghali iliyemnunua kwa Pauni milioni 89.