Thursday, 30 November 2017

Punda wanane watupwa jela kwa kuharibu mimea yenye thamani nchini India



Punda wanane wametupwa gerezani kwa muda wa siku nne nchini India kwa kosa la kuharibu mimea yenye thamani katika bustani .

Kituo cha runinga cha New Delhi kimefahamisha kuwa  uongozi wa jimbo la Uttar Pradesh uliwatupa jela punda hao kwa lengo la kuwaadhibu.

Mlinzi wa gereza la Jalaun  RK Mishra amesema kuwa wanayama hao waliharibu mimea yenye thamani katika bustani hiyo.

Mlinzi huyo aliendelea kusema kuwa mmiliki wa wanyama hao alipewa tahadhari kuhusu wanyama wake.

Wananyama hao waliachwa huru baada ya mwanasiasa mmoja kujitolea kulipa gharama zote zilizosababishwa na wanyama hao.

Sam Allardyce ndio kocha mpya wa Everton



KOCHA mpya wa Everton, Sam Allardyce amesema kwamba wachezaji wamepoteza hali ya kujiamini na ameiagiza klabu kusajili mbadala wa Romelu Lukaku.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 63 leo amethibitishwa kuwa kocha mpya wa Everton na mwanahisa mkuu wa klabu, Farhad Moshiri amemtaja kama kiongozi wa nguvu' na amemtabiria ataifikisha timu panapohitajika.'

Lakini kuelekea utambulisho rasmi, Allardyce ameandika kwenye safu ya Paddy Power kutoa maoni yake juu ya kufanya vibaya kwa timu hiyo msimu huu.

The Toffees wanashika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England pointi mbili tu kutoka nafasi za kuteremka daraja, licha ya kutumia Pauni Milioni 140 kufanya usajili mzuri kwa lengo la kumaliza ndani ya sita bora.

Allardyce amekiri klabu ipo katika nafasi mbaya kwa sasa na amesema jukumu lake la kwanza litakuwa ni kurejesha hali yab kujiamini.

Allardyce mwenye umri wa miaka 63, amerejea kutoka mapumzikoni leo na kukutana na Moshiri kusaini mkataba wa kufundisha Everton.

Atakuwa anapokea mshahara Pauni Milioni 6 kwa mwaka katika miezi 18 ya mkataba wake na ataanza rasmi kazi jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Huddersfield Town Uwanja wa Goodison Park.

Lakini leo atakwenda kushuhudia mchezo dhidi ya West Ham.

Katika kutimiza miaka 20 ya ndoa yao, Lissu ampa ujumbe mzito mkewe



Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu leo ametimiza miaka 20 ya ndoa akiwa bado hospitalini Nairobi akijiuguza  ambapo pia amemshukuru mke wake Alicia na kusema kwamba ni mke ambaye anaishi katika kiapo cha siku walichofunga ndoa.

Kwa mujibu wa Diwani wa Sombetini-Arusha, Ally Bananga amesema kwamba Mh Lissu amemtaja Alicia kama kipande chake sahihi kwa upande wake.

"Leo Tundu Lissu na mkewe Alicia wametimiza miaka 20 ya ndoa yao. Mume yuko kitandani na mke amebaki pembeni yake kumuhudumia. Ndoa yenye baraka hii,  na Mh Lissu amemtaja Alicia kama kipande chake sahihi"  Bananga.

Aidha Diwani Bananga ameongeza kwamba "Lissu amesema mkewe anakiishi kiapo chao siku walipofunga ndoa kuwa watayakabili maumivu na vikwazo pamoja mpaka mwisho".

Haya Ndiyo Madhara ya Kufanya Mapenzi na Mwanamke aliyopo kwenye Hedhi




Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana. Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si madhuri kwa afya ya wote wawili.Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi.

Zifuatazo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati KE yupo katika siku zake{period}.

 MADHARA KWA MWANAUME.

  1. Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.
  2. Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.
  3. Kuziba kwa njia ya mkojo.
  4. Utasa au ugumba.
  5. Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.
  6. Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.Pia hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.

MADHARA KWA MWANAMKE.

  1. Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID( PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.
  2. Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).
  3. Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.
  4. Utasa au Ugumba.
  5. Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.
  6. Athari mbaya ya kisaikolojia:Mwanamke atahisi kuwa mumewe hamjali wala mpendi bali anajali hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu.Pia kuona kuwa mumewe ajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu mume anataka KU-DO.

Njia 7 Za Kuwa Mafanyabiashara Mkubwa



Je unataka kuwa kama MO ??  Fuata hatua hizi 7 utafika alipo MO..

1. Chagua wazo bora la kibiashara.
Wazo bora la kibiashara ndilo litakalo kufanya kuwa mfanyabiashara wa mkubwa. Mara nyingi nimekuwa nikikutana na watu wakisema wanataka kuwa wafanyabiashara na kuishia kusema tu. Ila ukweli ni kwamba katika kuchagua wazo bora la kibiashara ni lazima ujiulize je unataka kuwa mzalishaji wa bidhaa au huduma? Je unataka kuwa mnunuzi na muuzaji?au  je unataka kuwa msambazaji tu ? Hayo yanaweza kuwa miongoni mwa maswali ya msingi ya kujiuliza.

2. Fanya uchunguzi juu ya washindani wako.
Hapa ndipo jicho la tatu linaposhindwa kufanya kazi mara nyingi. Tumekuwa si wachunguzaji wazuri juu ya washindani wetu ila tumekuwa wasikilizaji tu kwa watu wengine juu ya washindani wetu. Ila ikumbukwe ya kwamba fanya uchunguzi wa kutosha ili kujua washindani wako wanatumia mbinu zipi kukuza biashara zao. Hii itakusadia pia kujua ni wapi wanapokosea ili uweze kulizipa pengo hilo. Kwa kufanya hivi kutakufanya ndoto zako za kuwa mfanyabiashara wa kimataifa zitimie.

3. Tafuta mtu wa kukuongoza. (Helpful mental).
Tafuta mtu sahihi wa kukuongoza  na si mtu wa kukukwamisha. Watu wengi tunashindwa kuwa wafanyabishara wakubwa hii ni kutokana tunatafu watu ambao sio sahihi katika kutushauri. Stuka mapema juu ya jambo hili. Na anza kukaa na watu ambao tayari wamefanikiwa kwenye biashara zao watakusaidia sana kufika kule unakotaka kufika kibiashara. Siku zote ukitaka kuruka kama tai, ni lazima ujifunze kama tai wanavyoruka. Kwa maana huyo ukitaka kuwa mfanyabiashara mkubwa kubali kuchukua mwongozo wa wafanyabiashara waliofanikiwa.

4. Tambua biashara inayokua.
 Ukilijua hili ni jambo jema zaidi. Moja ya tatizo kubwa ni kwamba tumekuwa tukishuhudia biashara hazikuwi miaka nenda miaka rudi. Hii ni sababu kubwa ambayo inachangia tusiweze kujua ni kwa jinsi gani tusiwe wafanyabiashara wakubwa. Natamani kuona malengo yako yanabadilishwa kila wakati. Kwa mfano leo unauza nguo kwa kutembeza, ili kuona biashara inakuwa tunataka kuona unapata chumba kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo napo kweli tunasema biashara inakua. Kama unafanya biashara mkoa wako mzima tunatamani kuona unaongeza mkoa mwingine na mwingine katika kusambaza huduma au bidhaa.

5. Panga malengo na mipango ya biashara yako.
Hapa inahusiana na juu ya kuuza, kununua bidhaa au huduma. Lazima malengo ya biashara yako uyapange kila robo ya mwaka ili kugundua kama biashara yako inakuwa au haikui. Na lazima pia katika kupanga malengo yako, utambue baada ya muda fulani biashara yako itakuwa imefika wapi. Kwa mfano ni muhimu kujua biashara yako itakapokuwa baada ya miaka miwili au mitatu mbeleni.

6. Tangaza biashara yako.
Wateja wako ni lazima wajue bidhaa na huduma ambayo unazalisha. Si kujua tu, lengo jingine la kutangaza bidhaa au huduma inamfanya mtumiaji aweze kujua jinsi ya kutumia kitu hicho. Kwa kutangaza biashara wateja huongezeka kwa asilimia kubwa sana na kufanya huduma au bidhaa yako kuweza kupendwa na wengi pia. Matangazo ni njia mojawapo bora ya kukufanya kuwa mfanyabiashara wa kimataifa ikiwa utaitumia vizuri.

7. Jenga mahusiano mazuri na wateja wako.
Jitahidi kulizingatia hili ya kwamba Kauli katika biashara ni mali kuliko hata  pesa. Jali wateja wako na kuwafanya wajihisi kama wanapata bidhaa bure. Kwa kadri utakavyozidi kujenga mahusiano bora na wateja hiyo itapelekea wao kupenda bidhaa zako na hiyo itakusaidia kukuza wateja wengi siku hadi siku.

Ni matumaini yangu umenielewa vizuri hizo ni baadhi ya siri chache kati nyingi zitakazokufanya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Asante sana na usisite kumshirikisha mwingine.

Matumizi Mabaya Ya Fedha Ni Adui Wa Mafanikio




Kuna wakati mwingine Katika maisha yetu ya kila siku tunasema pesa ndo kila kitu.Ni kweli lakini kuwa na pesa bila wazo mahususi katika matumizi ni sawa na kuzima moto kwa chafya. Unashangaa huo ndo ukweli watu wengi tunapata pesa lakini hatujui tuitumie vipi pesa hiyo ili iweze kujisalisha. zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha matumizi mabaya ya fedha.

Pesa hii ina majina mengi hii ni kutokana na mahali husika wapo wanaita pesa ni sababuni ya roho, mtonyo, mapene, ankara  na majina mengine mengi.  Leo katika makala haya nitakwenda kukuelezea juu ya matumizi mabaya ya pesa yanayofanya kila siku tuwe katika hali ya umaskini.
Yafuatayo ndiyo matumizi mabaya ya pesa.

Kutokuwa na mpangilio wa matumizi ya pesa.
Moja ya changamoto kubwa inayowakumba wengi wetu ni kwamba hatuana mapangalio sahihi juu ya matumizi ya fedha. Tupo baadhi yetu ambao hutamani kila kitu ambacho tunakiona mbele yetu na kukinunua hata kama ulikuwa hauna mapngo wa kununua kitu hicho. Tupo baadhi yetu tukiwa tunatembea tukiona hiki na kile ni lazima tununue hiyo siyo nidhamu ya fedha.

 Pia kuna baadhi ya watu wakipata mishara utajua tu kwa kuona matumizi yao wanayoyafanya. Kufanya hivo ni Kujirudisha nyuma mwenyewe jambo lamsingi la kufanya juu ya matumizi sahihi ni kuwa na mapagalio mzuri wa pesa nunua kitu ambacho umepanga kununua. Pia Hakikisha ya kwamba kila pesa unayoipata na kuitumia Unaiandika katika daftari lako la kumbumbuka hii itakusaidia kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha maana utakuwa unajua kila faida na hasara ya jambo unalolifanya.

Kukopa pesa ovyo
Hili ndilo kosa kubwa ambao linawaelemea watu wengi sana. Nadhani utakuwa shaidi mzuri ni jinsi gani!  madeni yanavowatesa au yanavokutesa. Wapo baadhi ya watu wanakopa pesa katika taasisi za kifedha lakini hawana elimu ya kutosha juu ya mikopo hiyo hasa katika kuangalia mkopo utakuwa na faida au hasara. Wengi Hawaelewi kuhusiana na mkopo hasa swala zima la kulipa riba.

Utashangaa kwa mfano mtu anakopa shilingi laki tisa na anatakiwa kurudisha milioni moja ndani ya mwezi mmoja.  Kwa kuwa pesa hiyo haukujua juu ya riba hiyo pindi unaposhindwa kuirejesha utajikutana unanguna na wale wanaosema pesa ni shetani.

Maana yangu ni kwamba kukopa sio kubaya ila jaribu kupata elimu ya kutosha juu ya mikopo na jaribu kufanya uchunguzi wa mkopo hasa swala la riba. Jaribu kufanya mlinganisho kutoka taasisi moja na nyingine hii itakusaidia kujua ni mkopo gani unakufaa.

Tukiachana maswala ya mikopo katika mataasisi ya kifedha wapo baadhi ya watu ni wakopaji wazuri kwa watu wengine kama vile nguo, viatu na pesa. Usiwe na madeni ambayo yamezidi kwa kiwango kikubwa kwani kuwa na madeni kwa kiasi kikubwa yanakurudisha nyuma kwa namna moja au nyingine.

Baada ya Wimbo mpya wa Diamond, Hamisa asema "maisha yanaendelea uwepo au usiwepo”



Baada ya Wimbo mpya wa Diamond, Hamisa asema "maisha yanaendelea uwepo au usiwepo”


Wednesday, 29 November 2017

Nandy asema ukweli kuhusu yeye kununua nyimbo kwa mashabiki zake



Nandy asema ukweli kuhusu yeye kununua nyimbo kwa mashabiki zake



Tanzania imepewa BILIONI 75 na Finland leo


Tanzania imepewa BILIONI 75 na Finland leo



Chrisbrown, T.I , Vanessa Mdee, Peter P Square wapigia Libya kelele


Chrisbrown, T.I , Vanessa Mdee, Peter P Square wapigia Libya kelele



Nafasi za kazi leo November 29

Mchakato wa hisa za Simba kuanikwa



JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU, THOMAS MIHAYO

MWENYEKITI wa Kamati ya Zabuni ya Klabu ya Simba, Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu, Thomas Mihayo, amesema kamati yake imepanga kuweka wazi kila kitu juu ya mchakato wa kutoa zabuni ya kununua hisa  za klabu hiyo.

Akizungumza jana, Mihayo alisema kuwa kamati yake bado haijamaliza mchakato huo, lakini wataweka wazi walipofikia na nini kinaendelea.

Alisema hayo yote watayaweka wazi kwenye mkutano mkuu wa dhararu wa wanachama wa klabu hiyo ulioitishwa na uongozi huku ukitarajiwa kufanyika Desemba 3, mwaka huu.

“Naomba niweke wazi, hatuendi kwenye mkutano kutaja mshindi kwa sababu kazi bado haijamalizika, ila kumekuwa na minong'ono na presha ya kujua nini kinaendelea, kwenye huu mkutano ambao sisi tumewaomba viongozi wauitishe, tutaweka wazi kila kitu,” alisema Jaji Mihayo.

Alisema kamati yake itaeleza kila kitu bila kuficha na kutaja ni watu wangapi wamejitokeza kuomba kununua hisa za klabu hiyo.

Simba ipo kwenye mchakato wa kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo ambapo wanataka kuendeshwa kwa hisa.

Mmoja wa wanachama wanaotajwa kutaka kununua hisa hizo asilimia 50 ni mfanyabiashara na mdau wa soka wa siku nyingi, Mohamed ‘Mo’ Dewji.

Wakulima Kilombero wametakiwa kutumia Viwanda kuongeza thamani ya Mazao


Wakazi wa Wilaya ya Kilombero wametakiwa kutumia viwanda vilivyopo kuongeza thamani mazao wanayozalisha na kuyauza.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Denis Londo alitoa rai hiyo jana wakati akizindua kiwanda cha kati cha kukoboa, kupanga madaraja na kuuza mchele (Jatu) katika Kijiji cha Igima.

Alisema ujio wa kiwanda hicho ambacho kipo karibu na mashamba ya wakulima wa mpunga ni neema kwa kuwa malighafi zinapatikana kwa urahisi na kutawezesha kunufaika kwa kuuza ziada ya chakula.

Kwa mwaka jana pekee wilaya hiyo ilipata wastani wa mazao mchanganyiko tani 572,000 wakati mahitaji yalikuwa ni tani 138,0000 hivyo kuvuka lengo.

Londo alisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho cha kati ni juhudi za Serikali za kutaka kila Mkoa kuhakikisha inafikisha viwanda 100, agizo lililotolewa hivi karibuni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jaffo.

Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Petter Isare alisema baada ya kuhitimu masomo ya sheria ya elimu ya juu, waliamua kuanzisha asasi iliyolenga kutoa msaada wa kisheria na katika majukumu yao, wakagundua sehemu kubwa ya waliohitaji ni kutoka kundi la watu maskini wa kipato.

Isare alisema ndipo wakaamua kuangalia namna ya kusaidia kundi kubwa hilo kiuchumi na kiafya kwa wakati mmoja kwa kupitia fursa ya mazao mchanganyiko ndipo wakaanzisha kiwanda hicho.

Mwenyekiti wa kijiji cha Igima Timothy Mwakitalu alisema licha ya kusogea kwa kiwanda hicho kitakachosaidia pia kuhifadhi bure mazao kwenye ghala, kuna changamoto ya barabara.