Friday, 3 November 2017

Waziri Nchemba ameonekana mazoezi ya Singida Utd kulekea mechi vs Yanga




 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba ambaye ni mdau mkubwa timu ya Singida United leo Ijumaa asubuhi alikuwepo kwenye mazoezi ya mwisho ya timu hiyo kwenye uwanja wa Namfua Singida kuelekea mechi yao ya kesho dhidi ya Yanga.

Waziri Nchemba amekuwa karibu na Singida United tangu ikiwa ligi daraja la kwanza, baada ya timu hiyo kupanda kucheza VPL kwa mara nyingine baada ya muda mrefu bado amekuwa akionekana viwanjani kuisapoti kwa karibu.

Kumbuka kuwa, Waziri Nchemba ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi (Singida) mahali ambapo ni nyumbani kwa Singida United.

Waziri Nchemba pia alipiga penati kadhaa katika mazoezi hayo ya mwisho ambayo yalishuhudiwa na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo ambayo wataishuhudia kwenye uwanja wao wa nyumbani Namfua mjini Singida.

Uwanja wa Namfua utakuwa ukitumika kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu, Singida United walikuwa wakiutumia uwanja wa Jamhuri Dodoma kupisha ukarabati wa uwanja wa Namfua.

Kwa mujibu wa Ibrahim Mohamed maneja wa Singida United, Nizar Khalfani ndio mchezaji pekee mwenye majeraha ambaye hajafanya mazoezi ya mwisho ya pamoja kwa hiyo ataukosa mchezo wa kesho.

“Nizar Khalfani ndio mchezaji pekee ambaye hata kuwa sehemu ya mechi ya kesho kwa sababu anasumbuliwa na majeraha, wachezaji wengine wote wako vizuri kabisa na wamefanya mazoezi ya pamoja.

TANGAZO: TUNZA GARI YAKO NA KICHOCHEO CHA NANO ( NANO ENERGIZER )

TANGAZO: TUNZA GARI YAKO NA KICHOCHEO CHA NANO ( NANO ENERGIZER )


Tunakitambulisha kichocheo madhubuti cha Nano  kilichothibitishwa ubora wake na shirika la 
viwango la kimataifa (ISO 9001:2015). Hii ni teknolojia ya kipekee na ya kimapinduzi kwenye tasnia ya magari na mitambo. kichocheo cha Nano kimetengenezwa na teknolojia ya kisasa duniani ya Nano (Nano technology) kwa ajili ya kuikarabati na kuipa ulinzi injini ya gari yako bila kuifungua. Kichocheo cha Nano huziba mikwaruzo yote ndani ya injini na kuirudisha nguvu ya injini kama ilivyokuwa mpya. Wasiliana nasi kupitia Namba 0715480174


Kichocheo cha Nano kinaipa injini ganda au tabaka gumu la ceramic na platinum. Tabaka hili linafanya muunganiko wa kudumu na chuma cha injini (cylinder wall) na kina uwezo madhubuti wa kuhimili uchakavu na michubuko itokanayo na msuguano. Inarudisha uwezo wa kusukuma wa injini (compression ratio) kwa kuweka ganda gumu kwenye ukuta wa cylinder.

FAIDA ZA KICHOCHEO CHA NANO.

  1. Hupunguza matumizi ya mafuta kwa 8% - 21%.
  2. Huongeza nguvu ya injini hadi kufikia 100%.
  3. Hupunguza mlio na makelele ya injini na mtetemo hadi Mara 5 zaidi.
  4. Inatoa ulinzi wa injini hadi kufikia 40000 km.
  5. Husaidia Kuboresha uhai wa injini na vifaa vingine.
  6. Hulinda injini na kuirudisha kwenye ubora wake kama ilivyokuwa mpya.
  7. Huongeza msukumo wa injini na kuboresha uunguaji wa mafuta.
  8. Hulainisha usukani na gear box.
  9. Hupatikana kwa magari ya aina zote, generator, compressor, pikipiki, bajaji na kila aina ya mtambo.
  10. Hupunguza utoaji wa moshi kati ya mara 3 hadi 9.
  11. Ina garantii ya utendaji kazi kwa 100%.
  12. Haiharibiki kwa nanma yoyote ile.
  13. Bidhaa bora kabisa iliyothibitishwa kimataifa na kitaifa.
  14. Inakupa faida ya kutoifungua injini hivyo kuongeza thamani ya gari hata ukitaka kuiuza.
  15. Inakupa faida ya kupata mafuta bure kila unapoweka kwa mara ya 9.
  16. Faida isiyolinganishwa ya ulinzi wa gari lako hadi kufikia km 40000 kwa sh 60000 tu ukilinganisha na gharama za  mafuta na services kwa kipindi hicho.


MATUMIZI

  1. Injini inatakiwa iwe imetumika kwa km 3000.
  2. Kichocheo cha Nano kinatumika kwa injini za aina yoyote inayotumia oili ya aina yoyote (mineral or synthetic oils).
  3. Ili kupata matokeo bora zaidi weka unapofanya service.
  4. Ipashe injini yako.
  5. Tikisa kichocheo cha Nano kabla ya kuweka kwenye injini.
  6. Fungua kifuniko cha injini oili halafu mimina kichocheo cha Nano.
  7. Funga kifuniko. Hongera, umefanikiwa.
  8. Baada ya kumimina kichocheo cha Nano usibadili oili ya injini mpaka kipindi cha matumizi yafuatayo (kilomita 400 kwa pikipiki na bajaji, kilomita 1200 - 1500 kwa magari madogo na kilomita 3000 kwa malori na mabasi).


MAPENDEKEZO.
Kichocheo cha Nano kimefanyiwa majaribio na kukubaliwa na taasisi zifuatazo.

  • Chuo kikuu cha Taifa cha Kyungpook - Korea.
  • Chuo Kikuu cha Taifa cha Seoul - Korea.
  • Taasisi ya Korea ya Mashine na Vifaa.
  • Chuo Kikuu cha Yeungnam - Korea.
  • Taasisi ya Korea ya Teknolojia ya magari.
  • Jeshi la ulinzi wa Taifa la Korea.
  • Kituo cha Jeshi la Anga la India.


UTHIBITISHO WA UBORA.
Kichocheo cha Nano kimefanyiwa majaribio maabara, kuthibitishwa, kukubalika na kutunukiwa vyeti vya ubora na taasisi zifuatazo.


  1. Shirika la Ubora la Kimataifa ISO 9001:2015.
  2. Shirika la viwango la Tanzania - TBS.
  3. Mkemia mkuu wa serikali ya Tanzania - GCLA.
  4. Maabara ya kimataifa ya SGS.
  5. Maabara ya kimataifa ya TUV SUD Industrie Service GmbH.


USHUHUDA / MAPENDEKEZO.
Kichocheo cha Nano kimefanyiwa majaribio na makampuni ya kutengeneza magari, kimethibitishwa na kupendekezwa kutumika na makampuni yafuatayo.
  • MERCEDES BENZ
  • TOYOTA
  • GM DAEWOO
  • VOLVO
  • HONDA
  • HYUNDAI
  • AUDI
kichocheo cha Nano sasa kinapatikana Tanzania na kusambazwa na POWER ENERGY ENGINEERING COMPANY LTD. Tunakaribisha mawakala kutoka wilaya zote za Tanzania. Wasiliana nasi kupitia Namba 0715480174.

Kwa wafanyabiashara: usiikose fursa hii ya kibiashara.
Kwa wamiliki wa vyombo vya moto (Magari, pikipiki, bajaji nk): Tumia Kichocheo cha Nano kwa ulinzi madhubuti wa chombo chako.




WASAMBAZAJI WA NANO MIKOANI- TANZANIA

DAR ES SALAAM
UBUNGO OIL COM Jengo la oil com juu kwenye bango la Bima 0715 480 174   
RealMaps Mtaa wa sikukuu/mkunguni kariakoo 0755 366 658 0713 360 040                  
Dubai traders Livingston/mafia Kariakoo 0716 302 626   
Luesha central Mtaa wa msimbazi/ mvita jingo la kisangani 0768 820 344   
Japan auto spare parts Mwenge( karibu na Maryland bar) 0714 363 637   
Bk japani auto spare parts Segerea stand karibu na Fantasy park 0653 519 653  0758 519 653   
Darajani Geraji Darajani ubungo karibu na Land Mark Hotel 0765 447 803  0686 615 298   


MOSHI KILIMANJARO
Mshiu 0714 229 079
  
MOROGORO
Jumbo Lubnzants Morogoro eneo la Fine Mazimbo Road 0715 003 738   
Nuba auto Auto Accessories Mtaa wa Fine morogoro 0653 129 307
  
DODOMA
Temu auto parts Mtaa wa mji mpya chenja Dodoma 0754 265 211  0715 265 211   
Nuba auto Accessories Eneo la CBE Dodoma 0653 746 907
  
MWANZA
GT. Sahara general supplies Pamba Road mwanza0754 560 284   0754 560284   
Libety mkabala na Coconut Hotel mwanza 0626 450 450   

GEITA  
Kashakara auto spare parts Nyerere Road Geita
  
SHINYANGA
Green Star Expresses Stendi ya mikoani 0766 876 057     0759 933 290   
Phanuel  jeremia  Machinjioni eneo la viwanda shinyanga 0755 042 505  0787 592 871   

SINGIDA
Bingo spare Centre Standi ya zamani C Bomba la maji mkabala na Asma Hotel Singida  0755 961 679 0712 504 579
   
ZANZIBAR
Bengkok Accessories Kwa Biziredi mkabala na Bin Rashid Madawa 0779 959 850   0788 106 469   

Kwa maelezo zaidi na kutaka uwakala katika wilaya na mikoa ya Tanzania piga simu No: 0715 480 174


Republican wabuni mbinu za marekebisho ya kodi

Wanachama wa Republican nchini Marekani wamebaini mpango wa marekebisho ya kodi kubwa kwa kipindi cha miaka 30 ijayo.

Marekebisho hayo ya kodi, yamekuwa kipaumbele cha ajenda za Rais Donald Trump.
Mapendekezo yaliyotolewa ni pamoja na kupunguza kodi katika biashara kutoka asilimia 35 hadi asilimia 20 na kupandisha posho binafsi ya kodi.

Marekebisho mengine yaliyopendekezwa ni kuondoa viwango vya kodi katika magari ya umeme, hali itakayo waathiri watengenezaji wa magari kama vile kampuni ya general Motors,Tesla na Nissan.

Mpango huu wa Republican ambao unapaswa kuidhinishwa na bunge Congress, unatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa deni la taifa

Mawaziri wawekwa kizuizini Catalonia



Raia wa jimbo la Catalonia wanaotaka kujitenga wameandamana nje jengo la bunge la jimbo hilo mjini Barcelona baada ya jaji mjini Madrid kuwaweka kizuizini mawaziri nane wa serikali ya jimbo la Catalonia.

Taarifa zinasema kuwa hadi sasa kuna jumla ya wanasiasa kumi wa Catalonia waliowekwa kizuizini nchini Hispania wakiwemo pia viongozi wa kitamaduni wawili ambao nao wanashikiliwa.

Jaji Carmen Lamela amesema kuwa aliamua kuwaweka kizuizini viongozi hao nane kwa kuhofia kwamba wanaweza kutorokea nje ya nchini ama kuharibu ushahidi.

Waendesha mashitaka wanawatuhumu wanasiasa hao kwa makosa mawili ambayo ni mapinduzi na uchochezi katika jaribio la kutaka kujitenga na Hispania.

Hata hivyo jaji bado hajatoa kibali cha kukamatwa nje y nchi kwa kiongozi wa watu wa jimbo la Catalonia Carles Puigdemont na wenzake wane ambao wote wapo nchini Ubelgiji.



MAGAZETI YA LEO 3/11/2017


MAGAZETI YA LEO 3/11/2017




Audio | Enock Bella – Sauda | Mp3 Download

Audio | Enock Bella – Sauda | Mp3 Download


Enock Bella - Sauda

Audio | Enock Bella – Sauda | Mp3 Download

                                       
https://my.notjustok.com/track/download/id/287696/by/eM_J1W76fP

Audio | Nyandu Tozzy Ft. Young Dee , Chin Bees – Double Double | Mp3 Download

Audio | Nyandu Tozzy Ft. Young Dee , Chin Bees – Double Double | Mp3 Download

Nyandu Tozzy Ft. Young Dee , Chin Bees - Double Double

Audio | Nyandu Tozzy Ft. Young Dee , Chin Bees – Double Double | Mp3 Download


https://my.notjustok.com/track/download/id/287534/by/6NAtshXQUW

Audio | Ibrah Nation Ft. Switcher Baba – Batani | Mp3 Download

Audio | Ibrah Nation Ft. Switcher Baba – Batani | Mp3 Download

Ibrah Nation Ft. Switcher Baba - Batani

Audio | Ibrah Nation Ft. Switcher Baba – Batani | Mp3 Download


https://my.notjustok.com/track/download/id/287525/by/EaKQ6xEaRm

Video | Enock Bella – Sauda | Download Mp4

                          Video | Enock Bella – Sauda | Download Mp4

Video Enock Bella - Sauda



Video | Enock Bella – Sauda | Download Mp4





Thursday, 2 November 2017

Jela miezi 6 kwa kuoa mke wa pili Pakistan




Mahakama nchini Pakistan imemfunga mwanamume mmoja miezi sita jela ya kuoa mke wa pili bila ya idhini kutoka kwa mke wake.

Mahakama hiyo ya mjini Lahore pia ilimuamrisha Shahzad Saqib, kulipa faini ya dola 1,900, na kukataa maoni yake kuwa dini ya kiislamu inamruhusu kuoa hadi wake wanne.

Mke wa kwanza wa Sadiq Ayesha Bibi, alikuwa amefanikiwa kujitetea kuwa kuoa bila idhini yake ulikuwa ni ukiukaji wa sheria za familia nchini Pakistan.

Wanaharakati wa masuala ya wanawake wabasema kuwa kesi hiyo ni pigo kwa ndoa za wake wengi.
Mfasiri wa FBI afunga ndoa na mwajiri wa IS

Pia walisema kuwa itawapa wanawake zaidi walio katika hali kama hizo motisha ya kupeleka kesi mahakamani.

Nchini Pakistan, wanaume wanaotaka kuoa wanawake kadhaa hufanya hivyo baada ya miaka kadhaa na ni lazima wapate idhini kutoka kwa mke wa kwanza.

Baraza la kiislamu nchini Pakistan ambalo hutoa ushauri wa serikali kuhusu masuala ya kiislamu, mara kwa mara limekosoa sheria za familia nchini humo.

Sadiq ana haki ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo ya siku ya Jumatano.

Watu 34 wahukumiwa kunyongwa



Watu 34 wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, (Albino), ambapo matukio 67 ya ukatili dhidi ya albino yakiwa yameripotiwa.

Takwimu hizo zimetolewa katika muendelezo wa mkakati wa kitaifa wa kupiga vita ukatili, mauaji na unyanyasaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo Wakili kutoka Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka, Beatrice Isembo, amesema, pamoja na adhabu za vifo, watuhumiwa 17 wamehukumiwa vifungo tofauti huku kesi nyingine zikiendelea.

"Tumegundua mikoa ya kanda ya Ziwa ndiyo iliyoongoza kwa matukio ya aina hii  na yote ni kutokana na imani za kishiriki kama kutaka utajiri kwenye uvuvi, mazao nk." Mwanza inaongoza kwa kuwa na kesi za aina hii 15, na jumla ya matukio 67 yameripotiwa katika kipindi cha miaka 11" amesema Bi. Isembo.

Kwa upande wake, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Ralph Meela, kutoka Makao Makuu ya jeshi la polisi Idara ya Upelelezi kitengo cha makosa dhidi ya binadamu na usalama barabarani, amesema, asilimia kubwa ya mauaji hayo yanatokana na imani za kishirikina hasa maeneo ya migodini na uvuvi pembezoni mwa ziwa Victoria.

Julio aanza majigambo




KOCHA MKUU WA TIMU YA DODOMA FC YA DODOMA, JAMHURI KIHWELU ‘JULIO’,.

KOCHA Mkuu wa timu ya Dodoma FC ya Dodoma, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, amesema matokeo mazuri ambayo timu yake inapata katika mechi za Ligi Daraja la Kwanza yanatokana na wao kujipanga na si kubebwa kama baadhi ya wadau wanavyosema.

Akizungumza na gazeti hili jana, Julio, alisema kuwa anaamini kikosi chake kina nafasi ya kupanda daraja na kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao kwa sababu wamejipanga kuendelea kupambana ili watimize malengo waliyoyaweka.

Beki na kocha huyo wa zamani wa Simba alisema pia ligi hiyo ni ngumu na ina changamoto mbalimbali huku akiweza wazi kukukutana na ushindani kwenye michezo yote wanayocheza.

“Hakuna mechi rahisi, tunapambana katika kila mechi, hatubebwi, hata ukiangalia matokeo yetu, mechi nyingi tulizoshinda tumecheza ugenini, tutaendelea kupambana tutakaporudi kumalizika michezo ya nyumbani," alisema Julio.

Baada ya juzi kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Toto Africans, Dodoma FC imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 18, ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine katika kundi lao ikiwamo Alliance ambayo imekuwa mshindani.

Timu sita kutoka katika Ligi Daraja la Kwanza zitapanda daraja na kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao wa 2017/18

Omog hafukuzwi ng’o: Simba



KAIMU RAIS WA KLABU HIYO, SALIM ABDALLAH "TRY AGAIN.

WAKATI mkataba wa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, ukiwa umebakiza miezi minne kumalizika na hakuna mazungumzo yoyote ya kusaini mkataba mpya yaliyofanyika, Kaimu Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah "Try Again", ameibuka na kusema kuwa kocha huyo hafukuzwi.

Minong'ono ya kutimuliwa kwa Omog imeendelea kwa kasi baada ya kutua kwa Mrundi Masoud Djuma Irambona, ambaye amerithi mikoba ya Jackson Mayanja aliyeamua kuachia ngazi na kurejea kwao Uganda kumaliza matatizo ya kifamilia.

Akizungumza na Nipashe jana, Salim, alisema kuwa Omog bado ni kocha wa Simba na hakuna kikao chochote ambacho kimefanyika na kufikia uamuzi wa kumtimua kocha huyo raia wa Cameroon.

Salim alisema kuwa mpaka sasa timu yao haijapoteza mchezo wowote kwenye ligi na anawaomba wote ambao wanafikiria Omog ataondoka kwenye klabu hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, kwa sasa waache kuwaombea "mabaya".

"Kuna watu wana ndoto na matarajio ambayo hatuwezi kuwazuia kuyafikiria, hatujafungwa, tunaongoza ligi, ligi ni ngumu msimu huu, sio ya kawaida, timu nne zote zinalingana pointi, haijawahi kutokea," alisema Salim ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Friend's of Simba.

Hata hivyo, Salim alikataa kuweka wazi kama klabu ina mpango wa kumpa mkataba mpya Omog ambaye aliwahi kuifundisha Azam FC, lakini akikiri kuwa waliwahi kufanya mazungumzo na Kocha Mkuu wa Lipuli FC, Selemani Matola ili kuchukua nafasi ya Mayanja.

"Mkataba ni siri kati ya sisi na kocha, hatuwezi kuweka hadharani, ila tuna mkataba naye mrefu, hatuna mpango wa kumfukuza, pia siwezi kusema kesho kitatokea nini, anaweza yeye akaamua kuachana na sisi na kwenda mahali kwingine," alisema Salim.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa Omog na msaidizi wake wanafanya kazi kwa ushirikiano na tayari wameshaanza kutoa mapendekezo ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo kuelekea dirisha dogo la usajili.

"Omog ametupa ubingwa wa FA, tukamaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita, kwa sasa Simba iko vizuri, hakuna migogoro na viongozi tunajenga mifumo imara na sahihi, tunataka kuiendesha klabu kisasa, tunaachana na kufanya mambo kwa mazoea," aliongeza kiongozi huyo.

Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka jijini kesho kuelekea Mbeya kwa ajili ya kuwafuata wenyeji wao Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo