Tuesday, 31 October 2017

Mvua kubwa zatarajiwa kuanza kunyesha usiku wa leo

Mvua kubwa zatarajiwa kuanza kunyesha usiku wa leo




Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa(TMA) imetangaza vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya masaa 24 vinatarajiwa kuanza usiku wa kuanzia leo Jumanne.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Jumanne imeeleza kuwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani pamoja visiwa vya Unguja na Pemba yataaririka.

“Mvua hiyo inatarajiwa kusambaa katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Lindi kuelekea siku ya Ijumaa ya tarehe 3 Novemba 2017.”

“Hali hii inatokana na kuwepo na kuimarika kwa ukanda wa mvua (Inter Tropical Convergency Zone –ITCZ) katika maeneo hayo.”

Mamlaka hiyo imewataka wakazi wa maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa

“Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi

Meya wa jiji la Mwanza afunguka

Meya wa jiji la Mwanza afunguka



Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire amefunguka juu ya sababu zilizomfanya akamatwe na polisi wakati wa msafara wa Rais Magufuli alipokuwa Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari Meya huyo amesema sababu ya kukamatwa kwake alielezwa ni amri kutoka kwa viongozi wa juu ili asiwepo kwenye msafara wa Rais, na kupata fursa ya kuzungumza yale ambayo anayajua.

Meya Bwire ameendelea kwa kusema kwamba katika jiji hilo kuna vitendo vya matumizi mabaya ya fedha pamoja na kudhulumu haki za wananchi, na kamwe hatoacha kuzungumza hata kama anahatarisha kibarua chake

Simba wampa Omog nafasi nyingine

Simba wampa Omog nafasi nyingine



Pamoja na taarifa kuendelea kuzagaa kwamba Kocha Joseph Omog kiota kimeanguka,

Kamati ya Utendaji ya Simba imekutana na kukubaliana Kocha Joseph Omog kuendelea kukinoa kikosi hicho.

Omog amekuwa katika hali ya hatihati kama vile atafukuzwa kazi kutokana na mwenendo wa timu yake.

Lakini taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza, katika kikao hicho wamekubaliana Omog kuendelea na kazi yake.

“Lakini ametakiwa kubadili mambo na kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, Simba inataka ushindi,” kilieleza chanzo.

Mwenendo wa Simba katika mechi nane ilizocheza imekuwa ni milima na mabonde kwa kupitia ushindi, sare, ushindi sare.

Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa taarifa nyingi ambazo zinaeleza kwamba Omog anakaribia kutimuliwa.

Hata hivyo, bado hali inaonekana kuwa haijatulia na Omog atalazimika kufanya kazi ya ziada kuhakikisha anabadili mambo.

Yanga kumkosa Juma Abdul kwenye mechi dhidi ya Singida United

Yanga kumkosa Juma Abdul kwenye mechi dhidi ya Singida United



Wakati Yanga itakuwa na kibarua cha kuivaa Singida United kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida, wikiendi hii, taarifa za uhakika zinaeleza, itamkosa beki wake wa kulia, Juma Abdul.

Abdul ana kadi tatu za njano, ya mwisho akiwa ameipata katika mechi dhidi ya Simba, Jumamosi.

"Juma ana kadi tatu, kadi ya tatu ameipata dhidi ya simba baada ya kupata nyingine dhidi ya Kagera. Hivyo hatacheza mechi ya Singida," taarifa zilieleza.

Hakuna mtu wa benchi la ufundi la Yanga alipatikana kuzungumzia baada ya simu zao kuwa zinaita bila majibu.

Lakini taarifa nyingine zikaeleza kuwa, tayari Yanga wana taarifa kuhusiana na Juma Abdul.

"Hatakuwa katika mipango ya safari, benchi la ufundi linajua Juma ana kadi tatu.

Mavugo akalia kuti kavu Simba

Viongozi wa Simba wameonyesha kutofurahishwa na uchezaji wa mshambuliaji wao Laudit Mavugo hasa kutokana na kushindwa kuonyesha juhudi uwanjani.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza, viongozi wa Simba wamemtaka Mavugo kujituma na kama inashindikana basi wataachana nao.

"Viongozi hawajafurahishwa na Mavugo kwa kuwa hajaonyesha juhudi zozote katika mechi dhidi ya Simba.

"Unajua hata katika upangaji, awali kocha alionekana kama nafasi ya kuanza angempa Bocco. Lakini alibadili ikawa ni Mavugo," kilieleza chanzo.

"Viongozi wao hawana uwezo wa kumuingilia kocha lakini wanakerwa na namna Mavugo asivyoonyesha kama ana uchungu. Hivyo walitaka kama ameshindwa aende zake.

"Tayari kaelezwa kuwa lazima ajitume na acheze kuitumikia timu na kuisaidia kwa kuwa kama ilivyo kwa wengine anapata kila kinachotakiwa."

Lisu afunguka kuhusu Nyalandu






Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki(CCM), Lazaro Nyalandu kwa kupata ujasiri wa kuchukua hatua kubwa ambayo hata wabunge wengi waliopo ndani ya CCM wanashindwa kuichukua.

Lissu ambaye yuko kwenye matibabu jijini Nairobi  amempongeza Nyalandu kwa kuwa ni alikuwa mbunge jirani yake na kuwa ujasiri wa kufanya hivyo.

Mbali na kumpongeza Nyalandu pia Lissu amezungumzia  uchaguzi wa madiwani katika kata 43 akieleza kuwa kuwapa CCM kura katika kata hizo ni sawa na kukubaliana na yanayoendelea nchini.

“Kuwapa CCM kura sasa hivi ni sawa na kuwapa CCM mamlaka ya kutapanya mali zetu kama wanavyotaka,”amesema Lissu leo Jumanne akiwa jijini Nairobi

VIDEO: Makonda amjibu Nyalandu

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewata wanasiasa  kukubaliana na hali ya mabadiliko kwani sasa ni muda wa kufanya kazi na sio wakati wa kutafuta umaarufu na maneno mengi.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI

Msigwa: Nyarandu amewaonyesha watanzania mambo saba muhimu

Msigwa: Nyarandu amewaonyesha watanzania mambo saba muhimuMbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kumpongeza Lazaro Nyalandu na kumwambia kuwa amechukua uamuzi sahihi kuachana na chama hicho na kusema amewaonyesha watanzania mambo saba muhimu.


Msigwa amesema kitendo cha Nyalandu jana kuamua kuachana na Chama Cha Mapinduzi ni wazi kuwa amethibitisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) si chama tena bali kimekuwa chini ya dola na hakina uwezo wa kuikosoa serikali tena. Msigwa aliainisha mambo hayo saba kama ifuatavyo

1. Nyalandu umethibitisha kwamba CCM sio Chama Cha siasa tena. CCM iko chini ya miguu ya dola na haina uwezo wa kuikosoa serikali tena

2. CCM imepoteza mwelekeo wake. Imeshindwa kusimamia uchumi, siasa na uongozi wa nchi
3. Misingi ya nchi yetu imebomolewa chini ya utawala wa CCM na umeitisha mwito wa kila mmoja wetu kuijenga upya misingi ya nchi yetu

4. Tanzania imekithiri ukiukwaji wa haki za binadamu , dhulma na kutekwa na serikali mhimili wa bunge pamoja mahakama.

5. Watanzania wapate fursa ya kuchagua itikadi wanayoona inafaa na sio kutishiwa na kulazimishwa.

6. Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini yatapatikana kwa mfumo wa demokrasia na Uhuru wa mawazo.

7. Mwisho umeonesha umuhimu wa kupata Katiba Mpya kwa sasa katika Nchi yetu
Mbali na hilo Mbunge Msigwa alimaliza na kusema kuwa "Kuishi nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inawezekana"

CCM kupeleka vijana Ulaya

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa fursa ya kuwapeleka barani Ulaya vijana watakaochaguliwa na shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kwaajili ya kupata mafunzo ya kuchezesha soka.

Hilo limedhibitishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho ndugu Humphrey Polepole kwenye mahojiano na eatv.tv ambapo amebainisha kuwa fursa hiyo imetolewa na vyama rafiki vya chama hicho kwenye nchi za Ulaya.

Polepole amesema kupitia kikao kikubwa cha vyama vyote vya kijamaa barani Afrika na Ulaya kilichofanyika mapema mwaka huu ilitolewa fursa kwa CCM kuweza kupeleka vijana kwenye baadhi ya nchi barani Ulaya ili kupatiwa mafunzo hayo.

Aidha Polepole amebainisha kuwa zoezi hilo litasimamiwa na TFF kwasababu wao ndio wana dhamana ya kupitisha watu wanaohusiana na soka hivyo watashirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha vijana wanatumia fursa hiyo ambapo baada ya mafunzo hayo watarudi kuitumikia sekta ya michezo nchini.

Baada ya Uwoya kuonekana ameolewa, mume wake ajibu mapigo

Baada ya Uwoya kuonekana ameolewa, mume wake ajibu mapigoAliyekuwa mume halali wa muigizaji wa filamu bongo Irene Uwoya, mcheza soka kutoka nchini Burundi Hamad Ndikumana, ameonyesha kujibu mapigo baada ya mwenza wake kuonekana kuolewa, kwa kupost picha akiwa na mwanamke mwengine.


Kwenye ukurasa wake wa instagram Ndikumana amepost picha hizo, huku akiandika ujumbe kama ambao unaonekana ni kurusha vijembe kwa mwenza wake huyo, ambaye hivi karibuni alimuandikia waraka kuanika yale aliyokuwa akithubutu kuyafanya, na kusema yuko tayari kutoa talaka.

Wawili hao walitfunga ndoa takatifu katika kanisa la Mtakatifu Joseph la Jijini Dar es salaam, na kutengana baada ya muda mfupi wa ndoa yao, huku kukiwa na tetesi kuwa hakuna maelewano baina yao.

Tazama mapicha aliyopost Ndikumana

Mtandao wa WhatsApp Waruhusu Kufuta Ujumbe

Ilishawahi kukutokea kutuma ujumbe, picha au video au documenti yeyote kwa mtu usiyemkusudia kwa bahati mbaya kupitia programu ya WhatsApp? kama huwa unapatwa na matatizo hayo sahau kabisa kwani tayari programu hiyo imeshaongeza sehemu ya kufuta jumbe hizo.

WhatsApp is rolling out the Delete for Everyone (Recall) feature for all users! 🎉https://t.co/3bnbgxtPvU

— WABetaInfo (@WABetaInfo) October 26, 2017

WhatsApp tayari imezindua huduma hiyo ambayo imeongezwa kwenye programu kwa jina ‘Delete For Everyone’ ambapo mtumaji wa ujumbe, picha au video atachagua kufuta kwake au kwa mtu aliyemtumia kimakosa.



Kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwa watumiaji wote wa iOS na Android kama bado basi cha kufanya update programu yako ya WhatsApp ili uanze kutumia.

Hii inakuwa hatua nyingine ya maboresho ya programu hiyo baada ya kutangaza kuongeza sehemu ya Live Chart  ndani ya mwaka huu.

Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu WhatsApp Inc walitangaza kuwa wataleta mabadiliko makubwa manne ndani ya mwaka huu ambayo yataifanya programu ya WhatsApp kuwa ya kisasa zaidi.

Twambie wewe mtumiaji wa programu pendwa ya WhatsApp umeyapokeaji mabadiliko haya.

Majibu ya joti kwa Waliomsema Kafunga Ndoa na Kiduku

Jumamosi iliyopita ilikua harusi ya Mchekeshaji maarufu Tanzania Lucas Muhavile maarufu kama Joti ambapo gumzo lilikua pia nywele zake alizonyoa kwa staili ya kiduku na kuingia nacho Kanisani jambo ambalo lilifanya baadhi ya watu kuongea sana kwenye mitandao.

Joti kwenye Exclusive Interview ambapo amewajibu waliomsema kuhusu kiduku chake, >>> “Sidhani kama kuna sheria au kuna maandiko yameandika kwamba ukinyoa hivi hutakiwi kufunga ndoa, hii sanasana iko kwenye maadili tu“

“Nilimuomba Padri na akanielewa na kuniambia wewe ni Msanii tunajua cha kufanya usisuke tu, fumua hizo nywele ziwe tu kawaida zibanebane vizuri

Polepole: Nyalandu amejimaliza mwenyewe

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amemponda aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akisema walishamweka pembeni kwa kuwa hakuwa mtu wa muhimu kwao.

Akizungumza jana Jumatatu usiku katika kipindi cha Msemakweli kinachorushwa na Channel Ten, Polepole aliyekuwa akizungumzia mafanikio ya Rais John Magufuli kwa kipindi cha miaka miwili, alimtakia heri Nyalandu huku pia akisema amejimaliza mwenyewe.

“Ameondoka mwanachama mmoja wa CCM leo (jana) amekwenda upinzani. Katiba yetu hii ya Jamhuri ya Muungano inasema kila mtu ana uhuru wa kujiunga na chama chochote. Tunaheshimu uamuzi wake, tunamkatia heri katika chama anakokwenda,” alisema Polepole.

“Aliyeondoka leo ni ‘very insignificant’ yaani kwa Kiswahili hatujaona utofauti. Ndiyo maana sisi tumetoa maelekezo kwa Serikali kwamba, watu ambao hawakuweza kutukimbiza katika awamu ya tano kwenye maendeleo ya Taifa letu kwenye uongozi wa awamu ya tano wawekwe benchi kwanza. Sasa wamewekwa benchi,” alisema Polepole.

Hata hivyo alisema Nyalandu ana haki ya kikatiba kuamua kwenda chama chochote anachokitaka na kwa kuwa CCM ni chama cha kidemokrasia hakitamlazimisha kubaki.

“Chama chetu kina watu wengi wakongwe na wa muda mrefu na kitaendelea kuwepo na kinafanya kazi watu wanaona,” alisema.

Alisema kwa kuwa Nyalandu alishawekwa benchi alipaswa ajitafakari na kujipanga upya.

“Unajua unapowekwa benchi uelewe kwamba ama uongeze mazoezi au umeongezeka kilo mbio zako zimepungua, kwa hiyo tunakuweka benchi ujitafakari kwamba hauna msaada kwenye timu,” alisema na kuongeza:

“Sasa ukiwekwa benchi kwa muda mrefu ukapata timu ya mchangani, wanacheza chandimu, wewe unafahamu chandimu? Unatoka daraja la kwanza unakwenda daraja la nne na ndiyo chandimu na ndiyo umekwenda na maji.”
                                                                                                   
Aliendelea kujisifu akisema CCM haina wasiwasi kwa kuwa kiwango chake ni cha juu na wachezaji wake ni wa kimataifa na wametengenezwa vizuri kuwahudumia Watanzania.

Huku akipekua katiba ya CCM, Polepole alimsikitikia Nyalandu akisema anakwenda kwenye chama kisicho na itikadi akiacha CCM yenye itikadi ya ujamaa na kujitegemea.

“Unamtazama mtu amekwenda kutafuta itikadi pahala ambapo kuna itikadi isiyojulikana. CCM itikadi yetu ni nini? Ibara ya nne, ibara ndogo ya tatu, anakwambia itikadi ya CCM ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru,” alisema na kuongeza:

“Sisi ni wajamaa kwa maneno na kwa matendo. Uliza chama anachokwenda itikadi yao ni nini? Kuna malango ya mbinguni na malango ya jehanam. Sisi tunamtakia mafanikio mema