Wednesday, 13 December 2017

Wanandoa wauawa kwa kupigwa mapanga na watu wasiojulikana


Mume na mke wakazi wa kitongoji cha Kidogue wilayani Mkalama wamefariki dunia kwa madai ya kukatwa mapanga shingoni na kichwani na watu wasiojulikana.

Mauaji ya wanandoa hao, Kija Kitundu (53) na mkewe Mwajuma Ramadhan (59) yalitokea Desemba 10 saa sita usiku nyumbani kwao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba alisema watoto wa wanandoa hao, Ramadhani (14) na Namagalu (12), wamepelekwa hospitali kwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo.

Magiligimba alisema siku ya tukio wauaji hao walitumia ngazi kupanda juu ya paa la nyumba ya Kija kisha kuingia chumbani kwa wanandoa hao na kuwacharanga mapanga.

Alifafanua kuwa kabla ya tukio hilo, kuna mtu alikwenda nyumbani kwa Kija kuomba pampu lakini aliponyimbwa ndipo ugomvi ukaanza baina yao.



No comments:

Post a Comment