Askari mbaroni kwa kumuua mwenzake kisa 'mapenzi
Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia kwa mahojiano askari Magereza wa Gereza la Kisongo jijini Arusha, Koplo Faustine Masanja kwa tuhuma za kumuua mwenzake wakiwa kazini.Akizungumza na Vyombo vya Habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa limetokea Desemba 14,2017 majira ya saa 2:00 asubuhi.
Kamanda Mkumbo amesema baada ya Masanja kumjeruhi mwenzake kwa risasi, alipelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu ambako alifariki dunia.
Mkumbo ameahidi kutoa taarifa zaidi baada ya uchunguzi kukamilika ili kubaini chanzo na sababu za tukio hilo. Ingawaje taarifa za awali zinaonesha kuwa tukio hilo linaviashiria vya wivu wa mapenzi.
No comments:
Post a Comment