Salum Njwete maarufu Scorpion akiwa chini ya ulinzi.
Kesi ya kumjeruhi mpaka kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho inayomkabili mwalimu wa sanaa ya kujihami, ‘Martial Arts’ na msanii wa filamu za kibongo, Salum Njwete maarufu Scorpion hatimaye imefikia tamati ambapo hukumu inatarajiwa kusomwa januari 10 mwakani.
Kesi hiyo iliendelea jana katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala jijini Dar ambapo Scorpion alikuwa akibanwa maswali na wakili wa utetezi, Nassoro Katuga kufuatia utetezi wake alioutoa kipindi kilichopita akiongozwa na wakili wake, Juma Nassoro.
Katika utetezi wake wa awali Scorpion alisema alishurutishwa kutoa maelezo katika kituo cha polisi cha Buguruni ambapo wakili Katuga alimuuliza kwanini alisaini.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Flora Haule aliifunga kwa kuahidi kuitolea hukumu Januari 10 mwakani ambapo kabla ya hukumu hiyo kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Desemba 27 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment