Saturday, 3 February 2018

Watatu wafariki kutokana na baridi kali

Watu watatu waripotiwa kufariki  nchini Uswidi kutokana na baridi kali Kaskazini mwa Uswidi.

Baridi kali katika eneo hilo la Kaskzini mwa Uswidi ilifuatiwa na theluji kali ambapo nyuzi joto ilikuwa 20 chini ya sifuri.

Uongozi wa eneo la Vesternorrland nchini Uswidi umefahamisha kuwa bariki kali katika eneo hilo imesababisha vifo vya watu watatu.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Uswidi imetoa tahadhari kwa raia  kutokana na kiwango kĊŸkubwa cha theluji ambacho kinatarajiwa katika za usoni.

Singida United yaipiga Mwadui FC 3-2

Singida United wameshinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Mwadui FC katika mechi kali ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Wageni Mwadui walitangulia kwa mabao mawili kabla ya Singida kusawazisha na kufunga la ushindi.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya kushambuliana kwa zamu ingawa Singida United walifanya mashambulizi mengi zaidi mwishoni.

Shuja wa Singida United alikuwa Kenny Ally Mwambungu ambaye alifunga bao kwa shuti kali ndani ya dakika 3 za nyongeza baada ya mwamuzi kuongeza dakika 5.


Shuti kali alilopiga na kumshinda kipa Massawe wa Mwadui ni baada ya kupokea pasi nzuri ya Mudathiri Yahya.

Mabao mawili ya Singida United ikisawazisha, yalifungwa na Salum Chuku na Deus Kaseke aliyeng'ara katika mchezo huo.

Vituo 46 vya kupigia kura kinondoni kuhamishwa

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeridhia kuhamishwa kwa vituo 46 vya kupigia Kura katika kata tatu za jimbo la Kinondoni zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Ubunge Februari 17 mwaka huu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima ameeleza kuwa uamuzi wa NEC kuridhia kuhamishwa kwa vituo hivyo, umetokana na makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Msimamizi  wa Uchaguzi wa  jimbo la Kinondoni na Vyama vya siasa juu ya kuhamishwa kwa vituo hivyo vilivyokuwa kwenye nyumba za Ibada, Zahanati na maeneo ya majengo ya watu binafsi.

Amesema Tume imeridhika na uamuzi huo kwasababu hatua zilizochukuliwa ni sahihi kwa mujibu sheria na kanuni namba 21 ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambayo inaeleza kuwa ;  Vituo vya Kupigia Kura havitakiwi kuwekwa katika majengo ya nyumba za Ibada, kambi za jeshi, nyumba za watu binafsi na  ofisi za vyama vya siasa.

“ Tumejiridhisha kuwa baadhi ya vituo katika Kata ya  Kigogo vilikuwa katika nyumba za Ibada na vingine kuwa katika maeneo yenye ufinyu wa nafasi hivyo tumeridhia vituo hivyo vihamishwe na kupelekwa katika majengo ya umma” Amesema.

Amesema kuwa baadhi ya vituo vya kupigia Kura vilivyokuwa katika majengo ya umma ikiwemo Zahanati vimehamishwa katika shule za msingi za umma zilizo katika kata hizo  ili kuondoa usumbufu kwa wagonjwa.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Mwananyamala Bi. Barima Omari ameeleza kuwa kata ya Mwananyamala ina vituo vya kupigia kura 65 na wapiga kura 27,589 na kuongeza kuwa vituo nane (8) vilivyokuwa katika shule ya Sekondari Kambangwa mtaa wa msisiri A vimehamishwa. Kati ya hivyo 6 vimehamishiwa katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa ya Msolomi na 2 kuhamishiwa uwanja wa kwakopa.

Naye Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi  Kata ya Kijitonyama Elizabeth Minga ameeleza kuwa Kata hiyo ina jumla ya vituo vya kupigia Kura 101, kati ya hivyo vituo 22 vimehamishwa.

Akifafanua kuhusu vituo hivyo amesema vituo 6 vilivyokuwa katika shule ya Sekondari Kenton vimehamia shule ya Msingi Mapambano na vituo 5 vilivyokuwa nje ya Ofisi ya serikali ya Mtaa wa Bwawani vimehamishiwa mbele ya ofisi hiyo.

Aidha, vituo 6  vilivyokuwa nje ya soko la Makumbusho vimehamia ndani ya Ofisi ya Meneja wa Soko hilo na vituo 5 vilivyokuwa  katika Ofisi ya Serikali za mitaa kijitonyama vimehamishiwa katika shule ya msingi kijitonyama.

Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kigogo Bw. Singoro Mdegela ameeleza kuwa kata yake ina idadi ya Wapiga kura 27,000 na Vituo vya Kupigia Kura  59.

Amesema katika Kata hiyo vituo 16 vimehamishwa ambapo vituo 5 vilivyokuwa eneo la Kiwenge kwenye Msikiti wa Shiha vimehamia Uwanja wa People na Vituo 6 vilivyokuwa kwenye Zahanati ya Kigogo vimehamishiwa katika Shule ya Msingi Kigogo ili kuruhusu shughuli za matibabu kwa wagonjwa kuendelea.

Aidha, vituo 5 katika ofisi ya serikali ya mtaa wa Mkwajuni vimehamishiwa katika  shule ya secondari Kigogo.

Masoko ya mazao kuimarishwa

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata tija.

Taarifa iliyotolewa leo Februari 3, 2018  na ofisi ya Waziri Mkuu inaeleza kuwa ametoa kauli hiyo jana Januari 2, 2018 wakati akikagua Kampuni ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha masoko.

Amesema kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.

“Kupitia Wizara ya Kilimo tunataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini. Wakati umefika kwa wakulima nchini kuona tija ya mazao wanayolima,” amesema.

Ametoa mfano zao la pamba ambalo wakulima walikuwa wanaingia mikataba na wanunuzi, mfumo ambao ulikuwa unawanyonya badala ya kuwanufaisha.

Awali, ofisa mtendaji mkuu wa TMX, Godfrey Malekano amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa wamejipanga vyema kuanza minada ya mazao.

“Tutaanzia na zao la ufuta mwezi Mei, 2018 na kuendelea na mazao mengine kwa kadiri ya misimu ya mazao hayo ilivyo,” amesema.

Amesema kufanikiwa kwa soko la bidhaa na mfumo wa stakabadhi ghalani kunategemea msaada wa Serikali, “Soko la bidhaa la Ethiopia linalotajwa sana kwa mafanikio limefikia malengo yake kutokana na mkono wa Serikali.”

Tshishimbi apiga bao, Yanga ikiiua Lipuli 2-0


YANGA SC imejivuta kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Lipuli Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 31 baada ya kucheza mechi 16, ikipanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikiwazidi kwa pointi Azam FC ambao wanacheza mechi yao ya 16 usiku dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Yanga pia imepunguza pengo la pointi inazozidiwa na vinara, Simba SC hadi kubaki tano – lakini Wekundu wa Msimbazi nao watacheza mechi yao ya 16 kesho dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Erick Onoka aliyesaidiwa na Geoffrey Kihwilio na Janeth Balama, Yanga ilipata bao moja kila kipindi.

Na mabao hayo yalikuja baada ya Yanga kupata pigo dakika ya 17 kufuatia kipa wake wa kwanza Mcameroon, Youthe Rostand kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na chipukizi, Ramadhan Awam Kabwili.

Kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Papy Kabamba Tshishimbi alifunga bao la kwanza dakika ya 19 kwa kichwa akimalizia mpira uliotemwa na kipa Agathon Anthony Mkwando baada ya kichwa cha kuparaza cha winga Emmanuel Martin kufuatia kona ya kiungo Pius Charles Buswita

Kipindi cha pili, Yanga ya kocha Mzambia, George Lwandamina ilirudi na mchezo mzuri na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Buswita dakika ya 55, aliyempiga chenga kipa Mkwando baada ya pasi nzuri mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa kutokea pembeni kulia na kufunga bao zuri.

Yanga ilijitahidi kuendelea kusaka mabao zaidi, lakini Lipuli walikuwa imara na kumaliza mchezo kwa kipigo cha mabao 2-0.

Lipuli FC; Agathon Mkwando, Stephen Mganga, Ally Mtoni, Martin Kazila, Joseph Owino, Novaty Lufunga, Seif Karihe/Tola Mangonela dk69, Mussa Nampaka/Zawadi Mawiya dk71, Adam Salamba, Malimi Busungu na Jamal Mnyate/Jerome Lembele dk78.

Yanga SC; Youthe Rostand/Ramadhani Kabwili dk17, Hassan Kessy, Gardiel Michael, Kelvin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Papy Kabamba Tshishimbi, Emmanuel Martin, Raphael Daudi/Raphael Daudi dk86, Obrey Chirwa, Pius Buswita na Geoffrey Mwashiuya/Maka Edward dk81.

Man City yaambulia sare mikononi mwa Burnley

Mshambuliaji wa Manchester City, Raheem Sterling akikosa bao la wazi kipindi cha pili katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya wenyeji, Burnley leo Uwanja wa Turf Moor timu hizo zikitoka sare ya 1-1. Man City ilitangulia kwa bao la Danilo dakika ya 22 kabla ya Johann Berg Gudmundsson kuisawazishia Burnley dakika ya 82.

New VIDEO: Justin Timberlake – Man Of The Woods

New VIDEO: Justin Timberlake – Man Of The Woods

New VIDEO: Justin Timberlake – Man Of The Woods

Justin Timberlake just delivered his fifth studio album Man Of The Woods and now he doubles down with an official music video for the project’s title-track featuring a cameo by his wife Jessica Biel, directed by Paul Hunter.


Audio | Chidinma X Young D X Toby Grey X Daphne – Egwu | Mp3 Download

Audio | Chidinma X Young D X Toby Grey X Daphne – Egwu | Mp3 Download
Audio | Chidinma X Young D X Toby Grey X Daphne – Egwu | Mp3 Download

Audio | Marisa – UKARONDA | Mp3 Download

Audio | Marisa – UKARONDA | Mp3 Download

Audio | Marisa – UKARONDA | Mp3 Download

DOWNLOAD MP3

Yanga yajihakikishia ushindi dhidi ya Lipuli leo



KOCHA wa Yanga, George Lwandamina, amesema kama watashindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Lipuli ya Iringa watajiweka pabaya katika kuutetea ubingwa wao msimu huu.

Lwandamina, alisema kuwa kwenye mchezo wa leo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa, wana kila sababu za kuhakikisha wanapata ushindi ili kuendelea kuifukuzia Simba inayoongoza ligi.

Yanga itaingia kwenye uwanja huo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 18 tangu Lipuli ilishuka daraja mwaka 1999 na kuwafanya mashabiki wa mkoa wa Iringa kushindwa kuziona timu kubwa na kongwe zenye mashabiki wengi, ikiwemo Yanga.

“Ni mchezo mgumu kama ilivyo michezo mingine, tupo ugenini lakini kwa namna mambo yalivyo ni lazima tupambane ili kutoongeza pengo la pointi na wanaoongoza ligi,” alisema Lwandamina.

Yanga imeachwa kwa pointi saba na Simba wenye pointi 35 huku Azam wanaoshika nafasi ya pili wakiachwa kwa pointi tano na vinara hao, kikosi cha Lwandamina kinashika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 28.

Mchezo wa leo utamshuhudia mshambuliaji Ibrahim Ajibu akirejea uwajani baada ya kuukosa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Ihefu, muunganiko wake na Obrey Chirwa unatazamiwa kuwa chachu ya ushindi kwa mabingwa hao watetezi.

Canavaro anena

Kuelekea kwenye mchezo wa leo, nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Canavaro’, amesema watahakikisha wanapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha wanapata ushindi.

“Tulitoka sare kwenye mchezo wetu wa kwanza Dar es Salaam, hiyo inaonyesha Lipuli si timu ya kuibeza, kama wachezaji tutahakikisha tunakuwa makini na kupambana muda wote,” alisema Canavaro.

Naye kocha wa Lipuli, Selemani Matola, aliiambia Nipashe kuwa wamejiandaa vyema kuwakabili mabingwa hao watetezi.

Askari Magereza watiwa mbaroni wakidaiwa kuua

KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA, EDWARD BUKOMBE.

ASKARI 12 wa Jeshi la Magereza wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wanahojiwa na polisi kwa tuhuma za mauaji yaliyochochewa na ugomvi wa mapenzi.

Askari hao wanadaiwa kumshambulia mkazi wa kijiji cha Kerenge wilayani hapa, Aloys Makalla na kusababisha kifo chake mwishoni mwa mwezi uliopita huku wakiwa wamevaa kininja.

Katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, imedaiwa kuwa saa chache kabla ya kifo chake, marehemu alikuwa amepigana na mmoja wa askari.

Kamanda Bukombe alisema tukio hilo lilitokea Januari 28 na kwamba askari 12 wa Magereza wanahojiwa na polisi katika upepelezi wake.

“Ni kweli tumepata taarifa za tukio hilo la mauaji ya mwanakijiji huyo na askari 12 tunawachunguza kupata ukweli wake, ili kuona kama kuna wanaohusika hatua ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi,” alisema Kamanda Bukombe.

Akihadithia mkasa wa mauaji hayo, mkazi wa kijiji cha Kerenge, Juma Salim, alisema marehemu alikuwa na mzozo wa muda mrefu na askari Magereza mmoja (jina tunalihifadhi) wakituhumiana kuingiliana katika penzi la mmoja wa wanawake kijijini hapo.

"Na siku hiyo (mzozo huo) ulizusha vurugu kubwa," alisema Salim.

Salim alisema katika ugomvi huo kati ya askari na Makalla, Magereza huyo alijeruhiwa na kurudi kwenye makazi yao lakini baada ya muda alirejea kijijini hapo na wenzake wakiwa wamevalia kininja na kuwapiga wenyeji.

Baadaye walimkamata Makalla waliyemtuhumu kumpiga mwenzao na kuondoka naye, alisema Salim.

Naye Jeniffer Leonard, mkazi mwingine wa Kerenge alisema askari hao waliondoka na Makalla kwa madai ya kumpeleka kituo cha polisi lakini walishangaa kupata taarifa za kifo chake baadaye.

HAKUMTAJA JINAAkielezea tukio hilo, Kamanda Bukombe alisema taarifa zinaonyesha kutokea ugomvi baina ya askari ambaye hata hivyo hakumtaja jina wala cheo chake na marehemu huyo, hali iliyosababisha Magereza kujeruhiwa.

Bukombe alisema baada ya kujeruhiwa, askari huyo alikwenda kambini kuchukua wenzake ambapo walirudi kwa mara ya pili na kumkamata marehemu, kumpakia kwenye gari na kuondoka naye kwa madai ya kumpeleka kituo cha polisi.

Kamanda Bukombe alisema taarifa kutoka kwa askari Magereza zinadai wakati wakiwa njiani, marehemu aliruka kutoka kwenye gari hiyo na kuanguka barabarani ambako alifikwa na mauti.

“Tunachunguza upi (ndiyo) ukweli wa marehemu," alisema Kamanda Bukombe. "Kauawa kwa kipigo cha askari hao ama (ni) kifo kinachotokana na kuanguka kwa kuruka kwenye gari."Mambo hayo ndiyo tunayoyachunguza tupate ukweli.”

Alisema matokeo ya uchunguzi huo ndiyo yatakayoamua kama kuna hoja na ukweli kwamba askari wamehusika na kifo cha marehemu na hatua zitachukuliwa, ikiwemo kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote.

Makamu wa Rais aguswa na Cover ya wimbo wa Nandy na Aslay



Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa na wasanii Nandy na Aslay.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana jioni aliwakaribisha nyumbani kwake wasanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ na Faustina Charles maarufu kama Nandy kwa ajili ya mazungumzo mafupi na chakula cha jioni.

Katika mazungumzo yake na wasanii hao, Bi Samia alieleza kuvutiwa sana na marudio ya kibao cha SUBALKHERI kilichorudiwa na wakali hao wa Bongo Fleva hivi karibuni na kuwapa wosia wa kuendelea kufanya kazi nzuri zaidi na kujiepusha na makundi mabaya.

Esma aweka wazi mahaba yake kwa Wema Sepetu


Esma Abdul ‘Esma Platnumz’

MWANADADA Esma Abdul ‘Esma Platnumz’ ameonesha mahaba yake kwa staa mkubwa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akidai kuwa, amekuwa shosti wake kwa muda mrefu na hivyo hawezi kujitenga naye.

Akipiga stori na gazeti hili, Esma alisema Wema ametoka naye mbali kiasi kwamba leo hii hawezi kumuweka pembeni na kujiweka zaidi kwa wifi wake wa sasa,  Zarina Hassan ‘Zari’.

“Jamani Wema hata kidogo siwezi kumuweka pembeni, hata kama aliachana na kaka yangu lakini kwangu bado ana umuhimu. Kama kila anayeachana na kaka basi
niwe naye mbali, nikifa inabidi nikazikwe Uganda au Sauzi maana Bongo sitakuwa na rafiki,” alisema Esma