Tanzania\'s leading online News Edition (The National Newspaper). Get access to the most current and latest authoritative news on local issues, politics, events, celebrations, editorial, columnists, features, people and business.
Saudi Arabia imelaani hatua ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel huku pia shutuma zikizidi kuongezeka kufuatia hatua hiyo.
Katika taarifa, taifa hilo la ghuba lilisema kuwa tangazo hilo la Trump sio la haki.
Lakini waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alilitaja tangazo hilo kuwa la kihistoria.
Hatma ya mji wa Jerusalem ni moja masuala makuu kwenye mzozo katika ya Israel na Palestina.
Mataifa 8 kati ya 15 ambayo kwa sasa ni wanachama wa baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa yametaka shirika hilo kufanya mkutano wa dharura kufuatia uamuzi huo wa Marekani.
Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ni jambo ambalo halijatambuliwa kimataifa na hadi sasa nchi zote zimeweka balozi zao kweny mji wa Tel Aviv.
Jerusalem una semue takatifu kwa dini tatu za kiyahudi, kiislamu na kikristo.
Wapalestina walichoma picha za Trump
Dar es Salaam. Wananchi wanaonekana kukubaliana na vita dhidi ya rushwa inayoendeshwa na Rais John Magufuli, matokeo ya utafiti yamebainisha.
Utafiti huo kuhusu hali ya rushwa nchini uliofanywa na taasisi ya Repoa kwa kuwezeshwa na taasisi ya Afro Barometer, ulihusisha wananchi 2,400 katika mikoa yote.
Utafiti huo unaoitwa “Mtazamo wa Wananchi Katika Rushwa wa 2017”, unaonyesha kuwa ushiriki wa Serikali katika kupambana na vita dhidi ya rushwa umeongezeka.
Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo yaliyotangazwa jana, wananchi saba kati ya 10 (asilimia 71) ya waliohojiwa walisema ushiriki wa Serikali katika kupambana na vita dhidi ya rushwa ni mzuri, imani hiyo ikiongezeka kutoka asilimia 37 kulingana na matokeo ya mwaka 2014/15.
Akiwasilisha matokeo hayo, Profesa Pellizzio Riccard kutoka Repoa alisema utafiti huo unaonyesha imani ya wananchi kuongezeka katika vita dhidi ya rushwa ndani ya taasisi za Serikali.
Kwa mujibu wa utafiti huo, rushwa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepungua hadi asilimia 14 kutoka 37, Takukuru (asilimia 11 kutoka 29), Jeshi la Polisi (asilimia 36 kutoka 50), mahakimu na majaji imepungua hadi asilimia 21 kutoka 35.
Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani mwaka 2015, imekuwa ikiwafikisha mahakamani watu wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa kubwa kama uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Pia imepambana na ufisadi katika mashirika ya umma, ukwepaji kodi, utoroshaji makontena bandarini na kutimua wafanyakazi wa umma wanaojihusisha na ufisadi.
Hata hivyo, mmoja wa wasomi waliohudhuria hafla ya kutangazwa kwa matokeo hayo jana, Dk Simeon Mesaki alisema mtazamo huo unaweza kuwa tofauti na hali halisi.
“Kama utafiti unahusu mtazamo, matokeo yanaweza kuwa tofauti na hali halisi. It is the all about perception against reality (ni suala la mtazamo dhidi ya uhalisia),” alisema.
“Lakini, pili inawezekana kwamba jinsi Serikali inavyofanya kazi na watu wakaona, basi imani ni wazi itaongezeka. Kwa mfano, wananchi wanaona vigogo wa Escrow wanapandishwa mahakamani basi imani inaongezeka.”
Dk Mesaki alihofia kama kasi hiyo inaweza kudumu. “Je, vita hii itaendelea na kasi yake au ni povu tu kwa sababu Serikali iliyopo imeamua kutengeneza legitimacy (uhalali) yake?” alihoji.
Mbali ya Profesa Riccard, uwasilishaji wa matokeo hayo uliohudhuriwa na wasomi, wadau kutoka balozi na taasisi mbalimbali ulifanywa pia na mtafiti Lulu Silas kutoka Repoa.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakaluka alisema kupungua kwa vitendo vya rushwa kumetokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kuimarisha nidhamu na kurejesha imani ya polisi kwa wananchi.
Mwakaluka alisema wapo askari waliochukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kufukuzwa kazi, kupewa onyo kali huku kiwango cha uelimishaji kikiongezeka kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.
Jeshi la Polisi na mahakama zimekuwa zikitajwa mara kwa mara kuwa taasisi ambazo wananchi wanaziona kuwa zinaongoza kwa vitendo vya rushwa.
Mbali ya matokeo hayo, mkurugenzi mkuu wa Repoa, Dk Donald Mmari alisema pamoja na imani kuongeza, bado wananchi wanaogopa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa.
Dk Mmari alisema hiyo inatokana na woga wa kujulikana endapo watatoa taarifa hizo.
Dodoma. Wafanyabiashara wametoa kilio chao cha wingi wa kodi zinazotozwa na Serikali na mazingira yasiyo ya ushindani sawa wa kibiashara nchini, jambo linalowafanya kushindwa kuchangia ipasavyo katika maendeleo.
Mambo mengine waliyolalamikia ni kutozwa kodi mara mbili, baadhi ya wafanyabiashara kuingiza nguo kutoka nje ya nchi kwa njia za panya, utaratibu wa utoaji wa vibali kwa mamlaka za Serikali na kodi na ushuru katika sekta ya kilimo.
Wakizungumza jana katika mkutano wao na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wafanyabiashara hao walisema hawawezi kushindana kibiashara kama hakutakuwa na ushindani ulio sawa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania, Felician Kilahama alisema kuna wafanyabiashara wa mbao ambao wamekuwa wakitozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) lakini wengine hawatozwi, jambo ambalo haliweki ushindani sawa wa kibiashara nchini. “Unakuta wale wanaotozwa VAT bidhaa zao zinakuwa juu ya wale ambao hawatozwi kodi jambo ambalo halileti ushindani sawa katika biashara,” alisema Kilahama.
Alisema pia kuna tatizo la wafanyabiashara kuidai Serikali fedha za VAT inazotakiwa kurejesha na kuitaka kuangalia jinsi ya kutatua tatizo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mahoteli, Nura Karamagi alilamikia tozo ya Serikali ya kuingia katika mageti ambayo wanatozwa watalii kwamba inapunguza ufanisi katika sekta hiyo.
Licha ya Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere kusema kuwa kodi hiyo ilishafutwa tangu Julai, Karamagi alisema bado wenye hoteli wamekuwa wakitozwa na inajionyesha katika karatasi za malipo.
Mwenyekiti wa Wasindikaji Mafuta (Tasupa), Ringo Ringo alilamikia kiwango kikubwa cha kodi kinachotozwa cha VAT ikilinganishwa na nchi nyingine kama za Kenya. “Kenya wao wanatoza asilimia 14 tu lakini sisi hapa tunatozwa asilimia 18,” alisema.
Akijibu hoja hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James alisema changamoto iliyojitokeza katika urejeshaji wa VAT ni udanganyifu na kwamba ili kuwalipa malipo halali, Serikali inakagua madai hayo.
Alisema wameanza kuirejesha na kwamba Oktoba walirudisha Sh33 bilioni na Novemba Sh15 bilioni. “Na Desemba tunatarajia kulipa zaidi ya Sh10 bilioni, bado tunapitia hesabu.”
Dk Mpango alisema kukutana na wafanyabiashara hao kulilenga kuwasikiliza na kujumuisha hoja zao katika bajeti ijayo.
Dar es Salaam. Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye ametoa siku 30 kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (Taa) kuziondoa familia 59 zilizo ndani ya eneo la Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA).
Pia, ameitaka Taa kuhakikisha hatimiliki za ardhi za kampuni ya Puma Energy na Tanzanair zinafutwa kwa sababu ziko ndani ya uwanja huo ambao nao una hatimiliki yake.
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutembelea kampuni hizo, Nditiye alisema haiwezekani kukawa na watu wengine wanaomiliki ardhi katikati ya uwanja huo na wana hatimiliki.
Pia, aliitaka mamlaka hiyo kuwaondoa watu wote waliojenga karibu na uzio wa uwanja huo bila kuacha mita tatu kama inavyotakiwa katika sheria ya ardhi au mita 10 kwa mujibu wa sheria ya viwanja vya ndege.
Naibu waziri huyo aliagiza viwanja vyote viwekewe mipaka na kwamba, vile ambavyo havina hatimiliki navyo vitafutiwe.
“Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba inazirudisha na kuzitambua mali zake zote. Hakikisheni viwanja vyote nchini vinakuwa na hatimiliki, mpaka sasa uwanja wa Mwanza hauna hatimiliki,” alisema. Nditiye aliitaka Taa kuhakikisha kwamba inapata taarifa zote za Puma Energy inayouza mafuta ya ndege ili waweze kukusanya tozo zao na pia kuimarisha usalama kwa usafiri wa ndege. “Wekeni watu wenu pale Puma kwa saa 24 ili mjue mafuta hayo yanatumikaje na mnapata stahiki yenu. Sasa kama mtu anaagiza mafuta na hakuna mtu anayemsimamia inakuwaje? Hiyo ni hatari hata kwa usalama,” alisisitiza.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Taa, Richard Mayongela alisema watatekeleza maagizo yote.Hata hivyo, alishauri kwamba mamlaka hiyo ipokee tozo zao bandarini wakati mafuta yakishushwa kama ilivyo kwa mamlaka zingine za Serikali kama vile TRA.
Alisema hatua hiyo itapunguza gharama nyingine na kurahisisha ukusanyaji wa mapato wanayostahili kupata kutokana na mafuta ya ndege.
Kuhusu fidia kwa wananchi, Mayongela alisema mamlaka yake kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji wameandaa ardhi kwa ajili ya kaya zaidi ya 1,000 zilizoathirika na mradi wa upanuzi wa uwanja na tayari wamelipa Sh3.7 bilioni.
Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba timu yake imekutana na Waziri Lukuvi ambaye amewataka kupeleka nyaraka muhimu kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
Kuhusu Puma Energy na Tanzanair kumiliki viwanja katikati ya uwanja wa JNIA, Mayongela alisema zilipata ardhi kihalali kwa sababu Serikali haikuwa na utaratibu wa kupima maeneo yake na mengi yalianzishwa kwa matamko.
Alisisitiza kuwa taratibu za kufuta hatimiliki zao zinaendelea ili sehemu yote ya uwanja imilikiwe na Taa.
Baada ya kuenea kwa picha katika mitandao ya kijamii za Muingizaji na Msanii Zuwena Mohamed,maarufu kama Shilole zikionyesha kuwa amefunga ndoa na mpenzi wake Uchebejana usiku , aliyekuwa mpenzi wa Shilole, Nuh Mziwanda ametuma dongo.
Nuh Mziwanda ameandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram ambao unatafsiriwa kama amebeza ndoa hiyo.
Mpenzi huyo wa Zawadi wa Shilole, Nuh Mziwanda ameandika,
"Aliyelala na bibi harusi wiki moja kabLa ya harusi’, na wala sio bwana harusi bado mnanishauri harusi, (all girls are pretenders )."
Siku chache zilizopita Shilole alisisitiza kuwa atafunga ndoa kabla ya mwaka huu kuisha japo watu walimbeza, hayawi hayawi yamekuwa.
Tabora. Aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Mkoa wa Tabora, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Bhoke Bruno na wenzake saba jana Jumatano walihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la kuiba bunduki nane aina ya SMG, mali ya mwajiri wao.
Wengine waliohukumiwa kifungo katika hukumu iliyosomwa na Kaimu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Sharmira Sarwatt ni Koplo Idd Abdalah, PC Mwinyi Gonga na Said Mgonela, wote kutoka kikosi cha FFU Tabora.
Kwa pamoja, waliokuwa waajiriwa hao wa jeshi la polisi kwa pamoja walitiwa hatiani kwa makosa matatu ya kula njama, kuiba na kushindwa kuzuia tukio.
Mahakama pia iliwapa adhabu kama hiyo washtakiwa wengine watatu Shaban Haruna, Shaban Kabanika na Idd Supu waliodaiwa kushirikiana na waliokuwa maofisa hao wa polisi.
Washitakiwa wengine watatu kati ya 10 waliokuwa wakishtakiwa, Charles Abihud, Emmanuel Festo na Nicholaus Mlelwa, waliachiwa huru baada ya ushahidi dhidi yao kukosekana.
“Ushaihidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri umeithibitishia Mahakama pasipo shaka kuwa washtakiwa saba kati ya 10 walihusika na makosa yanayowakabili, hivyo wanahukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kila kosa,” alisema Sarwatt.
Kutokana na adhabu ya makosa yote matatu yanaenda pamoja, washtakiwa watakaa magereza kwa miaka mitano.
Awali upande wa mashtaka ulioongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Juma Masanja uliiambia Mahakama kuwa kwa pamoja, wahtakiwa walitenda makosa hayo kati ya Aprili 2013 hadi Aprili 2014.
Katika shtaka la kwanza, ilidaiwa kuwa washtakiwa kwa nyakati tofauti, walikula njama ya kuiba bunduki aina ya SMG zilizokuwa zikihifadhiwa katika ghala la kituo cha FFU mjini Tabora.
Upande wa mashitaka ulidai katika shitaka la pili kuwa katika kipindi hicho washitakiwa kwa pamoja washtakiwa bila kuwa na uhalali, walichukua bunduki nane kwenye ghala hilo, wakati shtaka la tatu likiwa ni kushindwa kuzuia uhalifu kutendeka ambalo.
Katika shauri hilo la jinai namba 104/2015, washtakiwa waliwakilishwa na mawakili Kelvin Kayaga na Mussa Kassimu wa mjini Tabora.
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amesema kuwa, anamuunga mkono muigizaji Faiza Ally kwa kitendo chake cha kuweka picha inayomuonyesha akiwa mtupu katika chumba cha kujifungulia (leba).
Wolper alisema anawashangaa watu wanaomponda Faiza aliyeposti picha hiyo hivi karibuni katika ukurasa wake wa Instagram, wakati yeye amevutiwa sana na kitendo hicho na ipo siku atamuiga.
“Wabongo ni washamba, ushamba unawasumbua sio kingine. Sioni ubaya wa hiyo picha hata kidogo, eti katudhalilisha, kamdhalilisha nani sasa pale, mimi nimefurahi mno tena nitamuiga nikijaaliwa kupata mtoto,”alisema Wolper.
Kilimanjaro Stars leo watacheza na Zanzibar Heroes katika michuano ya Chama cha soka Afrika Mashariki na kati (CECAFA) yanayofanyika nchini Kenya majira ya saa nane mchana, nani kubuka mshindi leo?
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania bara maarufu kama Kilimanjaro Stars amesema wanaingia uwanjani wakiwa na hofu kubwa kwa kiwango walichoonesha Zanzibar katika mchezo wao wa awali.
"Tunaingia katika mchezo mgumu kwetu, tumejiandaa vizuri ili kupata alama tatu kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata" , Ammy Ninje amesema
Kwa upande wa kocha mkuu wa Zanzibar Heroes amesema ni mchezo wa kihistoria hivyo watajitahidi wapate matokeo mazuri.
"Ni mchezo wa kihistoria kwetu sio rahisi kutabiri, lengo letu kushinda, kila mmoja ana mawazo hayo" , amesema Hemed Morocco
Timu mbili katika kundi "A" zitakazopata alama za juu zitapata nafasi ya kusonga mbele, kundi hilo lina timu tano ikiwemo wenyeji Kenya, Kilimanjaro Stars, Zanzibar Heroes, Libya na Rwanda.
Mchezo huu utakuwa mkali na mgumu pande zote kutokana na wachezaji wengi wa timu hizo kujuana na wengi wao kucheza ligi kuu Tanzania bara.
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), imelaani vikali huku ikipaza sauti ya kutaka arejeshwe akiwa hai mwandishi wa habari wa kujitegemea wa gazeti Mwananchi, Azory Gwanda aliyechukuliwa na watu wasiojulikana.
Gwanda ambaye kituo chake cha kazi ni Kibiti na Rufiji mkoani Pwani, alitoweka katika mazingira ya kutatanisha Novemba 21, 2017 baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana akiwa Kibiti majira ya saa 4:00 asubuhi.
MCL ilipata taarifa za kupotea kwa mwandishi huyo Novemba 30, 2017 kutoka kwa ndugu zake na mkewe baada ya kushindwa kumpata kwenye simu yake.
Juhudi za kuhakikisha Gwanda anapatikana chini ya uongozi wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama, wizara husika na wadau wa tasnia hiyo ya habari hazijafanikiwa hadi leo.
Kutokana na mazingira hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai akiwa ameongozana na timu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na viongozi wa Jukwaa la Wahariri(TEF) leo Alhamisi asubuhi ameitisha mkutano wa vyombo vya habari kueleza jinsi kampuni inavyoendesha harakati za kumtafuta mwandishi huyo kupitia jeshi la polisi na wizara ya habari.
“Tumefuatilia tukio hilo hadi kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Kanda Maalumu ya Rufiji ambaye amesema hawana taarifa na kwamba atafuatilia kisha kutoa taarifa. Mpaka leo hatujapata taarifa yoyote,” amesema Nanai.
Katika tukio hilo, waandishi wote na wafanyakazi wa kampuni hiyo inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen wamevalia mavazi meusi huku wakiwa wameinua juu magazeti na mabango yenye ujumbe unaosema kwa maandishi makubwa ‘Bring Back Azory’, #MrudisheniAzory.
Waandishi wa habari walihitaji kujua ni sababu au dalili gani ambazo kampuni inaamini zimesababisha kupotea kwa Gwanda, aina ya habari alizokuwa amepewa kufuatilia za uchunguzi na habari ya mwisho kuripoti katika gazeti la Mwananchi ilikuwa ya aina gani.
Nanai amejibu maswali hayo kwa nyakati tofauti lakini akasema habari ni nyingi zinazoandikwa na vitisho vimekuwapo kwa waandishi wa habari katika mazingira tofauti.
Kupotea kwake
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Nanai amesema kwa mujibu wa Anna Pinoni, ambaye ni mke wake, Azory alichukuliwa na watu ambao hawafahamu waliomfuata eneo ambalo hupenda kukaa kwa ajili ya maongezi na wenzake katika mji wa Kibiti.
Amesema kwa maelezo ya Anna watu hao waliokuwa na gari nyeupe aina ya Toyota Land Cruiser walienda naye shambani kumfuata. Walipofika shambani, Azory alimuuliza mkewe mahali zilipo funguo za nyumba yao na kuelezwa sehemu zinapowekwa siku zote.
Nanai amesema baadaye watu hao na Azory wakaondoka na kumuacha mkewe shambani. Kabla ya kuondoka, Azory alimwambia mkewe kwamba anaenda kazini na atarudi jioni ya siku hiyo (Jumanne Novemba 21, 2017) au siku inayofuata (Jumatano Novemba 22, 2017).
“Mkewe aliporudi nyumbani alikuta nyumba imefungwa na funguo zikiwa mahali alipoziweka, lakini alipoingia ndani alikuta dalili za kupekuliwa kwani vitu mbalimbali vilikuwa vimerushwa shaghalabaghala ndani ya nyumba. Mkewe anasema hakuwa na wasiwasi mpaka siku iliyofuta baada ya kuona simu zake zote hazipatikani,” anaendelea kusimulia Nanai.
Amesema Alhamisi ya Novemba 23, 2017 alikwenda(mkewe) kuripoti Kituo cha Polisi Kibiti na kupewa RB Na:Kibiti/RB/1496/2017 ambako walimweleza kuwa hawajui alipo na kumwomba awape namba yake ya simu ili wampigie iwapo watapata taarifa zinazomhusu, lakini mpaka sasa hajapewa taarifa yoyote wala kuitwa.
“Baada ya hapo, juhudi za kumtafuta ziliendelea ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari vya ndani na nje, baadhi vikatangaza na kuchapisha. Pia kampuni ilituma ujumbe wake kwa mkewe Kibiti kumpa pole na kupata taarifa zaidi ili kujua kinachoendelea.”
Nanai amesema pamoja na hatua hiyo, MCL imeshaandika barua rasmi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Wengine waliopata barua ni Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Taasisi ya MISA-TAN, Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na wadau wengine kuhusu kupotea kwa mwandishi huyo.