Friday, 1 December 2017

Breaking News: Wema Sepetu ang'atuka rasmi Chadema



Muigizaji wa filamu za kibongo na Miss Tanzania 206 Wema Sepetu ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi huku akidai kwamba hawezi kuishi kwenye nyumba inayomkosesha amani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amesema kwamba anatangaza rasmi kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambacho alitangaza kujiunga nacho Februari mwaka huu.

"Siwezi Kuendelea kuishi kwenye nyumba inayo nikosesha amani... Peace of mind is everything for me. Natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani" . Wema Sepetu.




Mambo ya kuzingatia ili kujinga na ugonjwa wa Figo



Ugonjwa huu umekuwa ukiwakosesha furaha watu wengi sana hii ni kwa sababu wapo baadhi ya watu mara baada ya kufanyiwa vipimo huambiwa figo zao zina mawe.

Wapo baadhi ya watu huambiwa figo zao hazifanyi kazi, na maneno mengine kama hayo. Pamoja na sababau mbalimbali ambazo ni chanzo ugonjwa huu, ipo kauli isemayo kinga ni bora kuliko tiba hivyo siku yale nitakupa dondoo ya nini kifanyike ili kuzua ugonjwa huu wa figo kama ifuatavyo

1.Usichelewe kwenda haja. 
Kutunza mkojo kweye kibofu chako  kwa muda mrefu ni wazo baya. Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu  huzidisha bakteria haraka. Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha  maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.

2. Kula Chumvi kupita kiasi.Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku.

3. Kula nyama nyekundu kupita kiasi.
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia-  sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi  inaleta uharibifu zaidi wa figo.

4. Unywaji mwingi wa "Caffeins".
Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso. Unapaswa kupunguza kiwango  cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.

5. Kutokunywa maji.
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri. Endapo hatunywi ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, kama hakuna kimiminika cha  kutosha kutoa kwa njia ya figo. Inashauriwa Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku. Kuna njia rahisi ya kuangalia kama  unakunywa maji ya kutosha. Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vzuri.

6. Kuchelewa matibabu.
Tibu matatizo yako yote ya kiafya kwa uhakika na uwe unachunguza afya yako mara kwa mara

Jifunze jambo hili ili kuyadumisha mahusiano yako ya mapenzi



Unapokuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu sahihi, kila wakati jitahidi kuwa na mawasiliano ya karibu na mtu huyo mara kwa mara. Haijarishi upo busy kiasi gani, kwani ukweli ambao upo wazi unasema ya kwamba mapenzi ya kweli hujengwa na mawasiliano thabiti.

Nasema hivi nikiwa na maana ya kwamba hivi ukimpigia simu mpenzi wako zaidi ya mara tatu bila kupokea huwa unajisikiaje? Bila shaka huwa huwa unajisikia vibaya sana, achilia mbali kutokupokea  simu, vipi tena ukitumia mpenzi wako ujumbe mfupi wa maandishi (sms) na asijibu kwa wakati, bila shaka suala hilo nalo litakufanya unisikie vibaya.

Kwa dalili hizo utaona ni kwa kiasi gani mawasiliano yalivyo na nguvu katika suala la kuhakikisha mahusiano yako yanasonga mbele. Hivyo haijalishi upo mbali au karibu na mpenzi wako kiasi gani,  hivyo unachotakiwa ili kulifanya penzi lenu liwe imara ni lazima uhakikishe ya kwamba unajibu sms za mpenzi wako kwa wakati, na hata simu zake ni lazima uzipokee kwa wakati pia.

Hii ni kwa sababu ipo  kauli isemayo mapenzi ni hisia. Inawezekana fika wakati mpenzi wako anakautumia sms hiyo, anakuwa na hisia kali na wewe na hivyo endapo utachelewa kujibu utafanya ajisikiye vibaya, kwani dawa ya njaa ni chakula, hivyo jifunze kuwa karibu na mpenzi wako kwa kumjibu na kupokea simu yako kwa wakati hii itasaidia kuamsha hisia mpya za kimapenzi.

Lakini pia epukana na kumjibu mpenzi wako kauli ambazo zitamfanya mpenzi wako huyo kukushusha hadhi ya kuendelea kukupenda wewe na kumfanya aweze mawazo hasi juu yako.

Mwisho nimalize kwa kusema mawasiliano ya kweli ni chachu dhidi ya kuongeza hamasa na mvuto wa kimapenzi.

LIVE TBC 1: Viongozi wa CCM Waliohusika Katika ubadhirifu Kuchukuliwa Hatua

LIVE TBC 1: Viongozi wa CCM Waliohusika Katika ubadhirifu Kuchukuliwa Hatua



Live: Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara Afungukia Mkutano wa Jumapili

Live: Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara Afungukia Mkutano wa Jumapili



Shilole amjibu Nuh Mziwanda... "najisikia kuharibu ndoa ya mtu"

Shilole amjibu Nuh Mziwanda... "najisikia kuharibu ndoa ya mtu"



Ati Zari hana kazi ya kufanya ????? ( KWA SAUTI YA ZARI)



Ati Zari hana kazi ya kufanya ????? ( KWA SAUTI YA ZARI)



Watu Sita washikiliwa kwa kukutwa na mifupa ya albino, ulimi wa simba



Mbozi. Watu sita wanashikiliwa na polisi mkoani Songwe kwa tuhuma za kukutwa na vipande vitatu vya mifupa ya mtu wanayedai kuwa ni albino, pamoja na mafuta na ulimi unaodhaniwa kuwa wa simba.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Mathias Nyange alisema jana kuwa watu hao walikamatwa juzi saa 7:00 mchana katika mji wa Tunduma wilayani Momba na askari waliokuwa doria.

Alisema watuhumiwa hao walikutwa na mafuta ya simba, mifupa mitatu ya albino, mfupa mmoja wa mnyama ambaye hajajulikana, na vipande viwili vya ulimi, vitu vinavyosadikiwa kuwa ni vifaa vya tiba asili.

Kamanda Nyange alidai kuwa baada ya kuhojiwa, watuhumiwa walikiri kuwa mifupa waliyokutwa nayo ni ya albino waliyemkata mkono mkoani Morogoro.

Alisema kati ya watuhumiwa hao wawili ni wakazi wa Morogoro, wawili wakazi wa Mbozi, mmoja ni mkazi wa Wilaya ya Momba na mwingine ni kutoka Nakonde nchini Zambia.

Nyange alisema watuhumiwa hao wanatarajia kupelekwa mkoani Morogoro ambako ndiko wanakotuhumiwa kutenda kosa.

Wakati huohuo, Nyange amesema watu watatu wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30 wamefariki dunia baada ya kupigwa risasi na askari waliokuwa doria saa 4:00 usiku wa Novemba 30 baada ya kukaidi amri ya kusimama ya polisi ambao waliwatilia shaka.

Baada ya kukataa kutii amri ya kusimama, polisi waliwafuatilia na baadaye watu hao walianza kuwafyatulia risasi, jambo ambalo kamanda huyo alisema liliwalazimisha askari kuanza kujibizana nao.

Alisema baada ya kuwapekua walikutwa na silaha moja aina ya bastola iliyotengenezwa kienyeji inayotumia risasi za short gun ikiwa na risasi moja na pia walikutwa na mapanga mawili pamoja na kipande kimoja cha nondo.

Mbunge Prof. Jay Aangua Kilio Hadharani


Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ameangua kilio hadharani kwenye mkutano aliokuwa amefanya na wananchi wa kijiji cha Ruhembe wilayani Kilosa na kuwaomba Waziri wa mambo ya ndani na waziri mkuu wachukue hatua kabla ya wananchi kujichukulia hatua

Wananchi hao pia waligoma kuzika mwili wa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Salim Said Mheka mwenye umri wa miaka 17 aliyeuawa na polisi wa kitengo maalumu kwa madai kuwa alikuwa ni mhalifu wa Kibiti

Kijana huyo alimaliza kidato cha nne katika shule ya sekondari Ruhembe,

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro amesema kijana huyo alikuwa anajihusisha na ugaidi

Dr. Shika aandaliwa tamasha la ‘Usiku wa 900 itapendeza’




Dkt. Louis Shika ambaye amejizolea umaarufu baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu, Said Lugumi, na kushindwa kuzilipia, ameandaliwa usiku wake maalum ambao ataongea na Watanzania juu ya maisha yake.

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema jana  Novemba 30, 2017, Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Dkt. Shika, Catherine Kahabi aliweka wazi kuwa wamekuja na wazo hilo la kuandaa tamasha maalum ili watu wote wamtambue Dkt. Shika kama mmoja wa watu wakubwa ambao wameweza kuibuka katika mazingira ya chini na baadae kuwa gumzo kila kona.

“Usiku wa 900 Itapendeza ni usiku maalum ambao unatarajiwa kufanyika Desemba 9, mwaka huu. Watu wote wanakaribishwa pale ndani ya uwanja wa burudani, Dar  live. Usiku huo ni maalum na Dkt. Shika ataweka wazi kila kitu pamoja na historia yake alianzia wapi mpaka kufika Nchini Urusi na baadae kurejea Tanzania” amesema Catherine

Pia aliongeza kuwa, kwa sasa wanamuangalia Dkt. Shika kama ni mmoja wa Watanzania wenye bahati na muonekano wa tofauti licha ya kila mmoja kusema lake.

Mbali na Dkt. Shika, kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazosindikizwa na bendi ya Twanga Pepeta, Jahazi Modern Taarab na wasanii wengine kibao wakiwemo wa Bongo fleva na wachekeshaji akiwemo MC Pilipili.

Kwa upande wake msimamizi wa masuala ya burudani wa Dar Live, Rajabu Mteta (KP Mjomba) amesemakuwa usiku huo utapambwa na shamrashamra mbalimbali kwani utakuwa ni wa aina yake kwa kila mmoja atakayefika siku hiyo.

“Wengi bado wapo njia panda kuhusiana na ukweli wa mabilioni ya Dkt. Shika, tumeshuhudia hivi karibuni amelipia bima fedha zilizopo nje ya nchi. Kabla fedha hizo hazijatua ameona awashangaze wananchi ambapo ukija Dar Live utaishuhudia,” amesema Mteta  KP Mjomba.

Usiku huo pia unatarajiwa kuwa na mgeni rasmi ambaye atafungua halfa hiyo, Mkurugenzi wa Global Group, Erick Shigongo kama mtu aliyemsaidia kwa namna moja ama nyingine Dkt. Shika.

Mbao yagonga mwamba kwa Yanga



Kila timu sasa inahangaika kusaka wachezaji watakaowasaidia huku timu nyingi zikiwa zinawawinda wachezaji wa Yanga na Simba walio benchi au wasiopata nafasi ya kutosha ya kucheza.

Lakini Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amegoma kuwatoa wachezaji wake, Maka Edward ambaye ni kiungo na Yusuph Mhilu anayechezea nafasi ya ushambuliaji kwenda kwa mkopo katika timu ya Mbao FC kutokana na kuwahitaji katika kikosi chake.

Mbao FC iliwasilisha barua katika Klabu ya Yanga kuwaomba wachezaji hao kwa mkopo katika usajili wa dirisha dogo unaoendelea hivi sasa kwa lengo la kuongeza nguvu katika kikosi chao.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema walipokea barua kutoka Mbao ya kuwataka wachezaji wao Mhilu na Maka, lakini kocha Lwandamina amekataa kuwatoa.

Zimbabwe yateua wakuu wa Jeshi kuwa Mawaziri



Rais Emmerson Mnangagwa amewateua wakuu wa jeshi katika baraza lake jipya la mawaziri

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amelitaja baraza lake la mawaziri akimteua afisa mkuu wa jeshi kwa wadhfu mkuu katika serikali yake.

Waziri mpya wa fedha ni Sibusiso Moyo , jenerali aliyetangaza katika runinga ya taifa hilo wiki mbili zilizopita kwamba jeshi limechukua udhibiti.

Mkuu wa jeshi la angani Perence Shiri ataongoza wizara ya fedha na kilimo.

Kiongozi mmoja wa upinzani Tendai Biti amesema kuwa fungate iliokuwa ikisherehekewa

Bwana Mnangagwa aliapishwa wiki moja iliopita kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe ambaye alikuwa mamlakani kwa takriban miaka saba.

Apigwa faini kwa kuchora alama zake za barabarani


Apigwa faini kwa kuchora alama zake za barabarani China

Mtu mmoja raia wa China amepigwa faini baada ya kupatikana katika kamera akipaka rangi ishara mpya za barabarani ili kurahisisha safari yake kuwa rahisi.

Gazeti la Modern Express limeripoti kwamba mtu mwenye umri wa miaka 28 kwa jina Surnamed Cai, alipigwa faini ya Yuan 1000 mashariki mwa mji wa Lianyungang mkoani Jiangsu .

Alipatikana katika kamera mnamo mwezi Septemba 27 akiwa na mkebe wa rangi akipaka mistari mipya katika barabara ili kubadilisha mwelekeo wa trafiki na kuwaambia maafisa wa polisi kwamba alichukua hatua hiyo ili kupunguza tatizo la milolongo mirefu ya magari swala ambalo limekuwa likimchelewesha kila siku anapoelekea kazini.

Niliona kwamba barabara iliokuwa ikielekea moja kwa moja ilikuwa na mlolongo mrefu wa magari , huku barabara inayoelekea upande wa kushoto ikiwa na nafasi kubwa., aliambia maafisa wa polisi.

Nilidhani kubadilisha ishara hizo za babarabara kutarahisisha usafiri wangu kuelekea kazini.

Maafisa wa idara ya trafiki waliambia gazeti hilo kwamba walidhani kwamba tabia ya bwana Cai ilikuwa hatari na kwamba ingesababisha ajali.

Tayari wametuma wafanyikazi kuhadilisha ishara hizo za trafiki.

Hii sio mara ywa kwanza kwamba raia ametumia ujuzi wake wa sanaa kuweka ishara zao za barabara.

Mnamo mwezi Mei ,dereva mmoja mashariki mwa mji wa Zhejiang alipigwa faini baada ya kamera kumpata akichora eneo lake la kuegesha gari kwa kutumia chaki.