Thursday, 30 November 2017

Imani za kishirikina zasababisha Nyumba 7 Kuchomwa Moto LINDI



Na. Ahmad Mmow.
WAKATI serikali ikiwa haiamini uchawi, na ikiwataka wanachi kutochukua sheria mkononi. Wananchi wanaoamini ushirikina na wanaojichukulia sheria mkononi wamechoma moto nyumba saba za makazi katika kijiji cha Nahukahuka A, wilaya na mkoa wa Lindi.

Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia tukio hilo lilitokea jana alfajiri kijijini hapo, walisema sababu ya wananchi hao kuchoma moto ulioteketeza nyumba hizo saba za wananchi wenzao ni kutokanana kuamini kwamba mwenzao mmoja  aliyepotea kijijini hapo katika mazingira ya kutatanisha siku tatu zilizopita na kuonekana ghafla juzi saa sita usiku alichukuliwa kichawi na wananchi waliowachomea moto nyumba zao.

"Kuna mtu alipotea katika mazingira ya kutatanisha siku tatu zilizopita, jana majira ya saa sita usiku alionekana akiwa katika hali mbaya nahajitambui. Wananchi wenye hasira kali walichukizwa na kitendo hicho, mapambazuko (alfajiri) wakachoma nyumba hizo moto, "alisema mmoja wa mashuhuda ambae hakutaka kutaja jina lake.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Mussa Bakari Namwanga bila kutaja jina wala umri wa aliyepotea na kuonekana katika mazingira ya kutatanisha alikiri kuwa tukio hilo limetokea katika kijiji chake. Ambapo hadi alipozungumza na Muungwana kutoka katika kijiji hicho hakukuwa na mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

"Nikweli tukio hilo limetokea, wananchi wamechoma moto nyumba za wananchi wenzao kwa imani za kishirikina. Tukio hilo lilitokea alfajiri ya leo (jana) hivi navyozungumza nawewe, mheshimiwa diwani amekwenda Mtama kuripoti tukio hilo. Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo. Kwasasa bado hatujua kiasi cha mali ziliteketea na moto huo ," alisema Namwanga.

Maelezo ya mwenyekiti huyo juu ya mazingira ya tukio hilo na sababu za wananchi hao kufanya ukatili huo dhidi ya wananchi wenzao, hayakutofautiana na maelezo yaliyotolewa na shuhuda ambae alikataa jina lake liandikwe kwenye habari hii.

Kwa upande wake kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga  alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema hadi wakati huo alikuwa hana taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo. Huku akihaidi kufuatilia ili kupata ukweli.

"Mimi sina taarifa, ngoja nifuatilie kwawasaidizi wangu. Maana tumeamka kukiwa shwari, kwakifupi tumeamka kukiwa shwari, sasa kama kuna hilo acha nifuatilie, "alisema kamanda Mzinga.

Miongoni mwa vitendo ambavyo serikali imekuwa ikionya visivywe na wananchi ni kujichukulia sheria mkononi. Huku pia ikionya jamii kuacha imani za kishirikina. Ikiwamo ramli chonganishi.

Video | Alikiba – Maumivu Per Day(Unofficial Release Video).| Mp4 Download

Video | Alikiba – Maumivu Per Day(Unofficial Release Video).| Mp4 Download

Video | Alikiba – Maumivu Per Day(Unofficial Release Video).| Mp4 Download




                                                    DOWNLOAD HERE

Video | Abdu Kiba Ft Alikiba – Single.| Mp4 Download

Video | Abdu Kiba Ft Alikiba – Single.| Mp4 Download

Video | Abdu Kiba Ft Alikiba – Single.| Mp4 Download




                                                 DOWNLOAD HERE

Audio | Abdu Kiba ft Alikiba – Single.| Mp3 Download

Audio | Abdu Kiba ft Alikiba – Single.| Mp3 Download

Audio | Abdu Kiba ft Alikiba – Single.| Mp3 Download



                                           DOWNLOAD HERE

Mizengo Pinda awapa somo wanasiasa vijana



Dodoma. Vijana wametakiwa kufanya siasa za kistaarabu na wajikite katika ujasiriamali.

Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ametoa rai hiyo leo Jumatano Novemba 29,2017 alipofungua mkutano wa uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dodoma.

Pinda amesema siasa bila kujishughulisha zinakosa tija na matokeo yake ni vijana kuishia kulalamika.

Pia, amezungumzia suala la vijana kuhama CCM akisema wanapotea. Amewataka kutulia kwa kuwa wataweza kupaza sauti zao.

Pinda amewataka wagombea kuwa kitu kimoja na kushirikiana na watakaoshinda kwa kuwa huo ndiyo msingi wa CCM.

Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya yaanza kuyumba




Kwa habari za kunyapia nyapia ni kwamba Irene Pancras Uwoya (Sheila Abdul) aanza kumchukia dogo janja kiasi cha kuyumbisha penzi lao na mbaya zaidi amekuwa akimnyima penzi dogo janja na mara nyingi hupenda kumkwepa kwepa janjaro na kiasi fulani anahisi kama janjaro ndo chanzo cha mumewe kipenzi Hamadi Kataut.

Dogo janja mara kwa mara akitafutwa kujibu suala hili la kunyimwa penzi na uwoya amekuwa akibabaika sana na muda mwengine hupenda kujibu nje ya mada ili asiendelee kuulizwa.

Masikini.... Wema Sepetu



 Muigizaji mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amesema kuna muda anatamani Mungu amchukue afe ili aweze kupumzika na mambo ya dunia ambayo yanamnyima raha.

Wema Sepetu ameyasema hayo kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram, akisema ingawa anajua ipo siku atakufa, lakini anatamani ingetokea sasa ili aweze kupumzika na mambo yanayomuumiza nafsi yake ikiwemo kutakanwa bila sababu za msingi kwenye mitandao ya kijamii.

Wema Sepetu amendeelea kusema kuwa kutokana na mambo ambayo anayapitia anatamani hata asingetokea duniani, na kuamua kukaa nje ya mitandao ya kijamii kwa muda.

"Ipo siku nitakufa, hakuna anaeishi milele... Sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndo itakuwa, “Maskini ya Mungu, Dada wa watu alikuwa hivi na vile, Mungu ailaze Roho yake mahali pema...” Kuna muda mwingine huwa natamani Allah Subhannah wata’allah anichukue tu... Ya Duniya ni mengi sana", ameandika Wema Sepetu.

Wema ameendelea kuadniak akisema.." Kuna muda mwingine nakufuru mwenyezi Mungu na kutamani labda hata nisinge exist... Ila acha niendelee kumtegemea yeye... Kila jambo hutokea kwa sababu.... Hili nalo litapita... I think I need a Time Off Social Media... Kwa mara nyingine Tena.... Siwezi jamani".

Licha ya hayo Wema Sepetu hajaweka wazi moja kwa moja ni jambo gani ambalo limemkwaza zaidi, kwani kitendo cha kutukanwa na kusemwa vibaya kwake sio jambo geni.





Baba wa Neymar aponda taarifa za mwanaye kuamia Real Madrid



Baba mzazi na wakala wa Neymar Jr, Neymar Santos Sr amesema yeye na mwanae hawana wazo la kuhamia Real Madrid kwa wakati huu.

Neymar Sr amesema hawafikirii kuhamia Real Madrid kama inavyodaiwa, akisisitiza kuwa mkataba wa Neymar Jr ndani ya PSG bado ni mrefu sana hivyo kwasasa wanaangalia kufanya vizuri ndani ya PSG.
Hatuna wazo hilo kwasasa, Neymar ana mkataba wa miaka mitano na PSG unaanzaje kuzungumzia mambo ya kuhama kwasasa, sio rahisi hivi vitu vinazungumzwa tu lakini havina uhalisia”, amesema Neymar Sr.

Paris Saint-Germain ilimsajili Neymar Jr kwa dau la kuvunja rekodi ya dunia ya €222 takribani bilioni moja za Tanzania ukijumulisha na gharama zote zilizohusika kukamilisha usajili huo.

Neymar Jr mwenye miaka 25 amekuwa akihusishwa kujiunga na Real Madrid ya Hispania kwa dau la €250 mwishoni mwa msimu wa 2017/18.

Kilimanjaro Stars yaongeza wachezaji watatu



Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Ammy Conrad Ninje, ameongeza nyota watatu katika kikosi chake baada ya Baraza la Soka la Afrika Mashariki (CECAFA), kuridhia kuongezwa wachezaji watatu kwa kila timu.

Awali CECAFA ilihitaji wachezaji 20 tu, lakini sasa wameongeza watatu na kufanya idadi mpya ya wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ya Chalenji kwa mwaka huu kuwa 23. Wachezaji walioongezwa ni Kipa Ramadhani Kabwili kutoka Yanga, Amani Kiata  wa Nakuru All Stars ya Kenya na Yahya Zayd kutoka Azam FC.

Wachezaji 20 walioitwa awali na kocha Ninje ni makipa Aishi Manula (Simba SC) na Peter Manyika (Singida United). Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphace Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Kennedy Juma (Singida United), Erasto Nyoni (Simba SC) na Mohammed Hussein (Simba SC).

Viungo wa kati ni Himid Mao ambaye ni Nahodha (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Young Africans), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Ibrahim Ajib (Young Africans). Washambuliaji ni Mbaraka Yussuph (Azam FC), Elias Maguri (Dhofar/Mascat, Oman), Daniel Lyanga (Fanja FC/Mascat) na Yohana Mkomola (Ngorongoro Heroes).

Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 3, mwaka huu, Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi A pamoja wenyeji Kenya, Rwanda na Libya ambayo ni timu mwalikwa kutoka Kaskazini mwa Afrika. Kilimanjaro Stars imewahi kutwaa mara tatu taji hilo tangu kuanzishwa kwake.

Petr Cech ataka Kuzeekea Arsenal



KIPA Petr Cech hana mpango wa kuondoka Arsenal kwa mujibu wa kocha Mfaransa wa klabu hiyo, Arsene Wenger.

Wenger amesema mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 35 amepunguza uzito ili kuongeza muda wake wa kuendelea kucheza kadri iwezekanavyo.

"Anazeeka, na wote tunazeeka,"amesema Wenger. "Lakini wakati anazeeka, pia anakuwa fiti kuliko alivyowahi kuwa,".

"Ameweka msistizo mwingi kwenye maandalizi. Amekuwa mwembamba kuliko alivyokuwa. Nafikiri ananufaika na hilo,".

"Amepunguza uzito fulani. Siyo sana, kilo mbili au tatu tu. Lakini ni nyingi ikiwa unakwenda kupanda farasi, unaweka kitu nyua kuongeza uzito na farasi anakuwa mkubwa,".

Kocha wa Arsenal anaanza kumfananisha kipa wake huyo na mlinda mlango wa zamani wa Manchester United, Edwin Van Der Sar.

Mholanzi huyo anashikilia rekodi ya mchezaji mzee zaidi kucheza Ligi Kuu ya England alipoidakia Manchester United hadi akiwa ana umri wa miaka 40 na siku 205.

"Cech amefanya hivyo kwa sababu anajisikia vizuri na anataka kuwa bora," amesema Wenger.

"Petr Cech ni mtu sahihi. Na huwezi kufika alipofika yeye kama hautakuwa hivyo, wakat wote uwe katika uborsa wako,".

"Namkumbuka Van der Sar alipokuwa Manchester United, Namfananisha naye. Ni weledi na wana maumbo yanayoshabihiana pamoja a ubora,".

"Na Van der Sar aliacha soka kwa sababu aliamua mwenyewe kustaafu. Kwa sababu Manchester United walimtaka aongeze mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Sikatai hioo, lakini itategemea na kiwango chake,"amesema.

RC Amos Makalla akanusha taarifa hii


MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amekanusha taarifa kuwa, anakusudia kuandika barua ya kumuomba radhi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. John Magufuli kwa kushindwa katika uchaguzi Kata ya Ibighi.

Mhe. Makalla amenusha taarifa hizo zilizosambaa mtandaoni kuwa na kuripotiwa na Gazeti la Mwananchi tofauti na alichokisema yeye katika mkutano wa (UWT) mkoa uliofanyika jana ambapo alikuwa msimamizi Mkuu wa uchaguzi.

“Nilichowaasa wajumbe wa mkutano na wanaCCM, watafakari kwanini Chama cha Mapinduzi kimeshindwa katika uchaguzi Kata ya Ibighi na zaidi nilisema Chama mkoa wa Mbeya kifanye tathmini kwanini mikoa mingine wamefanikiwa kushinda na CCM Mkoa wa Mbeya kushindwa Kata ya Ibighi,  nikashauri Chama kifanye tathmini ngazi ya kata , Wilaya na Mkoa kujua tatizo ni nini,” alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya.

Alisema, ni kwa ajili hiyo akashauri Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya wamuombe radhi Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Magufuli kwa kupoteza Kata hiyo.

“Mimi sikuhaidi kuandika barua ya kuomba radhi na habari zichukuliwe ni za uongo na uzushi,” alisema Mhe. Makalla.


Azam FC yafunga dirisha la usajili



Uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, umesema kuwa kwa sasa hautasajili wachezaji wengine ndani ya kikosi hicho baada ya kumalizana na Mghana, Bernard Arthur aliyesaini mkataba wa miaka miwili.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffar Idd amesema: “Kwa sasa nTumefunga usajili kwenye kikosi chetu hatutasajili mchezaji mwingine nafasi zimeja.”

“Tumemuongeza mkataba kiungo wetu, Steven Kingue Mpondo raia wa Cameroon.”

Dirisha la usajili lilifunguliwa Novemba 15 na kutarajiwa kufungwa mwezi ujao.

Kampuni ya Dabaga yanunuliwa na kampuni ya Chai Bora



Katika kutekeleza sera ya uwekezaji nchini ili kuendana na kasi ya serikali ya kuwa na Tanzania ya Viwanda ifikapo mwaka 2025, kampuni ya Chai Bora imeinunua kampuni ya Dabaga iliyokuwa ikitamba na bidhaa za kuongeza ladha za vyakula kama vile Dabaga tomato sauce , Pilipili Mbuzi, Mango pickle na bidha nyinginezo.

Kampuni ya Chai Bora imekuwa ikifanya shughuli zake hapa nchini tangia mwaka 1990, Chai Bora inaogoza kama chata ya kuzalisha majani ya chai, Ikijikita zaidi katika uzalishaji wa bidhaa kama vile majani kama vile Black Tea, Green Tea pia Kahawa aina ya Café Bora. Kwa kuwa imeanza kazi tangia mwaka 1990 hadi sasa ni takribani miaka 27 inaashiria ukuaji katika sekta husika ya bidhaa za Chai . Katika hiyo miaka 27 Chai Bora imeinunua kampuni ya Dabaga, imeongeza uzalishaji wa bidhaa tofauti na imeboresha kiwanda cha Dabaga Iringa na teknolojia za kisasa.

Uwekezaji huo ambao umehusisha teknolojia za kisasa na mitambo ya kisasa zaidi ni wazi kuwa itaongeza ufanisi kwenye uzalishaji wa bidhaa husika na kusukuma ongezeko la ajira nchini. Kupitia uzalishaji huo kwa sasa kiwanda hicho kimetoa ajira ya moja kwa moja na ajira isiyokuwa ya moja kwa moja kwa wakazi wa kijiji cha Ikokoto cha wilayani Ilula, Iringa. Wakulima ambao wanaojihusisha na shughuli za malighafi za viwanda kama hicho hasa wakulima, wasambazaji wa bidhaa za kilimo pamoja na watoa huduma wengine kama vile kampuni za ulinzi, usafi na hata watoa huduma za vyakula nao watanufaika na uwekezaji huo.

Mkurugenzi wa Chaibora, Mr.Kapila Mr.Kapila Ariyatilakakaalisema wakulima watanufaika kwa kuuza mazao yao hasa nyanya kwa kuwa kwa sasa kiwanda hicho kinahitaji nyanya tani 300 hadi 400 kwa mwezi. "Hii inaashiria kuwa wakulima wa nyanya wa ndani na nje ya Iringa watanufaika na uwepo wa kiwanda hicho hasa kwa kuuza bidhaa zao humo" anasema Mr.Kapila Ariyatilaka.

Anasema wasambazaji wanaojihusisha na bidhaa za kilimo nao wamepata mwanya wa kuuza bidhaa zao na hasa wanaweza kununua kwa wakulima na kisha kuuza kwenye kampuni hiyo na hivyo kuongeza wigo wa ajira.