Tuesday, 21 November 2017

Dk Kaunda kwenda kumshawishi Mugabe ajiuzulu


Harare, Zimbabwe. Chama tawala cha Zanu-PF kimewaita wabunge wake ili kuwapanga waanzishe mchakato wa kumshtaki bungeni Rais Robert Mugabe huku kukiwa na taarifa kwamba rais wa zamani wa Zaimbia, Kenneth Kaunda anakwenda kumshawishi mpigania uhuru mwenzake ajiuzulu.

Taarifa kutoka Lusaka, Zambia zinasema Rais Edgar Lungu amemtuma Dk Kaunda kwenda Harare kujaribu kumshawishi Rais Mugabe “ajiuzulu kwa heshima” baada ya jeshi kutwaa madaraka wiki iliyopita.

"Dk Kaunda alisafiri kwa ndege ya rais na ametua Harare," ofisa mwandamizi wa serikali ya Zambia aliliambia jana shirika la habari la Reuters. Kaunda ana umri wa miaka 93 sawa na Mugabe.

Hazijapatikana habari zaidi juu ya safari hiyo. Lakini ndani ya makao makuu ya Zanu PF, gazeti la NewsDay la Zimbabwe limripoti kwamba mbunge mmoja aliyezungumza kwa sharti la kutoandikwa jina alisema kikao cha wabunge wa chama tawala kiliitishwa kujadili hatua ya kumshtaki mwanampinduzi huyo ambaye taifa linamtaka astaafu.

"Tumeitwa na tumeambiwa tufike kwenye makao makuu ya chama kabla au ifikapo saa 8:30 mchana leo (jana)” alisema. Mnadhimu mkuu wa Zanu-PF Lovemore Matuke alithibitisha habari hizo na kwamba kikao kilitarajiwa kuanza saa 10:00 jioni.

Chama cha Zanu PF, ambacho Mugabe alikiasisi na kukiongoza kwa miongo kadhaa Jumapili kilitoa tamko la kumfuta uongozi wa chama na kikamtaka awe amejiuzulu urais kufikia saa 6:00 mchana jana vinginevyo asubiri kushtakiwa na kuondolewa bungeni.

Mugabe alipuuza hali ambayo Rais Lungu ameamua kumtumza Dk Kaunda ili mkongwe huyo aliyetawala kwa miaka 37 tangu Zimbabwe ilipopata uhuru asiondolewe katika namna itakayomwondolea heshima.



Muda wa mwisho

Muda wa mwisho wa kujiuzulu kwa hiari ambao Rais Mugabe alikuwa amepewa na chama chake cha Zanu PF ulipita bila kutolewa taarifa rasmi huku uvumi ukienea kuhusu hatima yake

Japokuwa haijatolewa taarifa yoyote chanzo kilichokaribu na timu ya majadiliano upande mmoja wakiwemo majenerali waliotwaa madaraka wiki iliyopita kimeliambia shirika la utangazaji la CNN kwamba Rais Mugabe amekubali kung’atuka na kwamba ameshaandaa barua ya kujiuzulu.

Chanzo hicho kilidokeza kwamba majenerali wameridhia matakwa mengi ya Mugabe ikiwa ni pamoja na kupewa kinga ya kutoshtakiwa yeye na mkewe Grace, na abaki na mali zake.

CNN limeambiwa kwamba chini ya makubaliano hayo, Mugabe na Grace hawatashtakiwa. Pia, viongozi wawili waandamizi wa serikali ya Mugabe waliliambia shirika la habari la Reuters Jumapili kwamba Mugabe alikuwa amekubali kujiuzulu lakini hawakuwa wanajua yaliyomo katika mkataba wa kuondoka kwake.

Ili ionekane amejiuzulu rasmi, utaratibu ni kwamba barua lazima iandikwe kwenda kwa Spika wa Bunge, chanzo kingine kimeongeza.

Mugabe ambaye anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kutoka kila kona aliwashangaza watu Jumapili alipokataa kufanya hivyo alipolihutubia taifa kwa njia ya televisheni akiwa ikulu.

Chama chake cha Zanu PF kimempa Mugabe, ambaye amekuwa katika kizuizi cha nyumbani na jeshi lililotwaa madaraka kimempa hadi mchana leo kuondoka vinginevyo atashtakiwa bungeni.

Jumamosi, maelfu ya Wazimbabwe walijimwaga mitaani kupaza sauti zao wakimtaka mzee huyo mwenye umri wa miaka 93, ajiuzulu.

Agoma

Jumapili mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 93 aliwashtua watu alipokataa wito wa kujiuzulu na hivyo kuitumbukiza Zimbabwe katika wiki ya pili ya mgogoro wa kisiasa huku juhudi za kuhitimisha utawala wake wa miaka 37 mfululizo zikikwama.

Chama cha Zanu PF alichoasisi na kukiongoza kwa miongo kadhaa kilitangaza kumwondoa kama kiongozi na kilimpa muda hadi Jumatatu mchana kuachia urais vinginevyo atashtakiwa bungeni.

Kabla ya kumwondoa Mugabe katika nafasi ya uongozi, Zanu PF ilitangaza kumrejesha katika chama makamu wa rais aliyefukuzwa Emmerson Mnangagwa kisha kikamteua kuwa kiongozi wake mpya. Mugabe alimfukuza Mnangawa Novemba 6 kwa madai ya usaliti hali iliyochochea mgogoro wa kisiasa.


Maneno ya Mama Lulu baada ya mwanae kwenda jela

Maneno ya Mama Lulu baada ya mwanae kwenda jela





Elizabeth Michael ‘Lulu’.

SIKU tano baada ya mwanaye ambaye ni staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ mama yake mzazi, Lucresia Karugila, kwa mara ya kwanza amefunguka baada ya mtoto wake huyo kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia staa mwenzake, Steven Kanumba aliyekuwa pia mwandani wake.

Awali, kulienea lawama nyingi mitandaoni baada ya Lulu kuhukumiwa kuwa huenda kuna mahali wazazi walikosea malezi ndiyo sababu ya mtoto wao huyo kujihusisha na masuala ya kimapenzi akiwa na umri wa chini ya miaka 18 ambao hakubaliki.

Kufuatia hali hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta mama Lulu ili kujua mtazamo wake juu ya mwanaye kwenda jela na madai ya mitandaoni ndipo akafunguka mazito. Mama Lulu aliliambia gazeti hili kuwa, kwa sasa hapendi kuzungumza hovyo na watu na anahitaji muda mwingi wa kupumzika kwa kuwa hayuko vizuri. “Nafikiri kwa kipindi hiki nahitaji zaidi kupumzika kwa muda mwingi na sipendi kuzungumza hovyohovyo, siko vizuri kabisa,” alisema mama Lulu kwa sauti ya unyonge.

Lulu akiwa na mama yake Lucresia Karugila.
Akiendelea kuzungumza, mama huyo alisema kuwa, tangu apate majanga ya mtoto wake huyo hadi kwenda jela hayupo vizuri na wala hapendi kuongea kwa sababu hajisikii kufanya hivyo kwani anahisi anaiona dunia chungu. “Najua watu watanishangaa sana, lakini ndiyo nimeamua kuwa hivyo, siko sawa na sijisikii vizuri kabisa. “Sidhani kama kuna mzazi yeyote anaweza kupata usingizi wakati mwanaye yupo kwenye mateso kama ilivyokuwa zamani, kiukweli ninaumia sana,” alisema mama Lulu.

DAKTARI NAYE ANENA!

Naye daktari wa magonjwa ya binadamu, Dk Godfrey Chale, akizungumzia hali ya Lulu baada ya hukumu hiyo alisema kuwa, kuna magonjwa ambayo huweza kumpata mtu mwenye matatizo ya kimaisha ikiwemo kufungwa jela ikiwa ni pamoja na kuwa kichaa kutokana na msongo.

Dk Chale alisema mara nyingi watu ambao hupatwa na majanga makubwa kama la Lulu, huwa kwenye uwezekano mkubwa wa kukumbwa na msongo ambao husababisha mpangilio mbovu wa homoni kiutendaji na mhusika kuchanganyikiwa endapo atashindwa kukubaliana na mazingira ya tatizo.
Alisema kuchanganyikiwa kwa watu wenye matatizo kama ya Lulu, hutokana na kuzidiwa na huzuni na mgandamizo wa hisia (depression) hivyo kushindwa kabisa kuzuia mfumo wa kufikiri na kutafakari na ndiyo maana unakuta mtu anaongea peke yake au kufanya vitendo vya ajabu kama kuokota vitu mbalimbali kama sehemu ya kujifariji na hapo ndipo tatizo la kuchanganyikiwa huanzia.

Tatizo kubwa jingine ambalo linaweza kumpata Lulu ni kupoteza popularity momentum (nguvu ya umaarufu) na kushuka kwa uchumi atakapomaliza kifungo kwani kwa kipindi ambacho yuko jela atapoteza mikataba yake ya kikazi kama matangazo na uigizaji, vitega uchumi ambavyo vilikuwa vikimuingizia kipato cha kuyaendesha maisha yake

Dereva wa daladala abomolewa nyumba zake nne Dar es Salaam



picha ya mtandao

Jasho linamtiririka. Mikono yake na mdomo vinatetemeka, vishikizo viwili vya shati lake la mistari ya rangi ya zambarau na nyeupe vimeachia.

Sehemu kubwa ya tumbo lake ipo wazi, macho yake mekundu yanalengalenga machozi. Ghafla anaaza kulia huku akijiviringisha chini.

Licha ya kuwa na mwili mkubwa, anaonekana kuwa mwepesi kwa namna anavyoviringika chini. Kitendo hiki kinawavutia watu waliokaribu kusogea kuangalia kitu kinachoendelea.

Baada ya dakika kama mbili au tatu, akiwa amejaa vumbi mwilini anasimama na kuwafuata maofisa wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) waliokuwa wakibomoa nyumba mtaani kwake.

Anapiga magoti huku akizungumza na maofisa hao: “Msinibomolee nyumba zangu. Nitakwenda wapi na watoto wangu?” Ghafla anadondoka chini na kuzimia.

Huyu ni Nicomed Leo (61), mkazi wa Kimara Stop Over jijini Dar es Salaam na mwathirika wa bomoabomoa ya zaidi ya nyumba 1,000 zinazodaiwa kujengwa ndani ya hifadhi ya Barabara ya Morogoro mita 121.5 kila upande kuanzia Kimara hadi Kiluvya.

Siku hiyo ndiyo ambayo nyumba zake nne; mbili za ghorofa moja na mbili za kawaida alizodai zilikuwa na thamani ya Sh900 milioni zilikuwa kwenye ratiba ya kubomolewa, lakini kabla hazijafikiwa yakamkuta yaliyomkuta.

Baada ya kuzimia Leo alibebwa na kuwekwa sehemu ya wazi na kuanza kupepewa ili apate hewa ya kutosha. Baada ya muda mfupi anazinduka.

Baada ya kuzinduka akahoji: “Wamebomoa? Nyumba zangu jamani, nyumba zangu.”

Hata hivyo, msimamizi wa bomoabomoa hiyo, Janson Rutechula akawaamuru maofisa wenzake wasibomoe nyumba za Leo kisha akamfuata mmiliki huyo na kumweleza hawatabomoa nyumba zake kwa wakati huo.

Rutechula na wenzake waliondoka eneo hilo na kusitisha ubomoaji wa nyumba za Leo kwa muda.

“Tumeamua kuacha kwanza lakini haimaanishi hatutaboamoa. Tutazibomoa tu,” anasema Rutechula wakati akizungumza na Mwandishi wetu.

Siku ya pili baada ya tukio hilo, gazeti la Mwananchi likafunga safari tena kwenda nyumbani kwa Leo ili kumjulia hali na kumkuta mke wake Maria Nicomed.

“Sijui kama ataweza kuongea, hali yake bado haiko sawa maana baada ya tukio la jana amekesha baa anakunywa pombe mpaka muda huu ninaozungumza amelala,” anasema.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi Leo alitoka nje huku akionekana amevimba macho, amevaa shati nyeupe ambalo halikufungwa vyema vishikizo na kusababisha tumbo lake kubaki wazi.

Akapita mbele ya mwandishi bila kuzungumza chochote na kutoka nje ya geti la nyumba yake. Akiwa nje akasimama karibu na nyumba za jirani zake ambazo zilibomolewa jana yake.

Ameweka mikono nyuma na kutembea huku na kule, mara akapita mtoto mdogo mbele yake akamuuliza swali.

“Mage leo haujaenda shule eeh! bomoabomoa imekuzuia?”

Mwandishi wetu anamsongelea kumsalimia akitaka kujua hali yake:

“Leo sitaki kabisa kuongea naomba uniache, hata nikiongea haisaidii zaidi nitachochea nyumba yangu ibomolewe,” anasema Leo.

Baada ya muda Leo anapokea taarifa ya zuio la Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi juu ya ubomoaji wa nyumba 278. Alisikika akijisemea mwenyewe, “zuio limetoka tuwaone sasa kama watabomoa.”

Baada ya wiki moja

Leo aliona kama muujiza, hakudondosha hata chozi wala kugalagala tena. Alikuwa na ujasiri wa aina yake ambao uliwashangaza hata waathirika wenzake.

Huku nyumba yake ikiwa imebandikwa karatasi za zuio la mahakama kutaka isibomolewe, Tanroads waliibomoa. Leo alihaha huku na kule kuokoa baadhi ya mali za nyumba yake kama vile nondo, mabati na mbao pamoja na milango.

“Kuanzia leo sina imani tena na Mahakama wala Serikali, nimekosa tumaini kabisa, nimekubali Serikali imeshinda,” anasema Leo huku akiokota tofali zilizoangushwa na tingatinga na kuzikusanya.

Kabla ya bomoabomoa

Baada ya kupata taarifa ya ubomoaji wa nyumba zaidi ya 1,000 zilizondani ya hifadhi ya barabara hiyo, mwandishi wetu alifunga safari hadi Kimara Stop over ili kujua kinachoendela. Akiwa eneo hilo aliona umati wa watu ukiwa umekusanyika karibu na nyumba ya Leo.

Katika umati huo Leo alionekana akiwa amesimama nje ya geti la nyumba yake. Pia, walionekana wafanyakazi wa Tanesco wakiwa na vifaa vyao vya kazi.

Katika kudodosa mwandishi wetu akapewa taarifa kuwa Tanesco wamefika hapo kung’oa mita zao na kukata umeme kwenye nyumba zinazotakiwa kubomolewa yaani zenye alama ya X.

Miongoni mwa nyumba iliyotakiwa kukatiwa umeme siku hiyo ilikuwa ni ya Leo. Hata hivyo, wakati wafanyakazi hao wakijiandaa kuanza kazi hiyo katika nyumba ya Leo, wananchi waliokuwa wamekusanyika walikubaliana kuwafukuza wafanyakazi wa Tanesco.

Makubaliano yao hayo yalizaa matunda kwani walifanikiwa kutimiza lengo lao, baada ya kuwafukuza mwandishi wetu alimtembelea Leo nyumbani kwake ili kujua amejipangaje kukabiliana na bomoabomoa hiyo.

Mwandishi alipofika nyumbani alimkuta Leo akiwa amehamisha baadhi ya vitu vyake vikiwamo nyaraka muhimu na kuvifungia ndani ya buti za magari yake mawili.

Leo alionyesha baadhi ya vitu alivyofungia kwenye magari kuwa ni pamoja na televisheni kubwa ya kisasa ya nchi 60, spika, nguo na baadhi ya vyombo.

“Nimeshajiandaa kisaikolojia, wakimaliza kubomoa nyumba zangu mimi nachukua mabati na tofali nasimamisha tena kibanda hapa hapa. Nitalala na kuishi na wanangu hadi umauti utakaponikuta,” anasema na kuongeza:

“Nimetandika magodoro chini ya sakafu ndiyo nalalia na nimeacha vyombo vichache vya kupikia, nawasubiri waje kubomoa.”

Nyumba za Leo zilikuwa na wapangaji saba wakiwamo wamiliki wa kituo cha tiba asilia cha  Samaritarian Nutracetical  Services  ambao walikuwa wakimlipa kodi ya nyumba  Sh10 milioni kwa mwaka.

Pia, alikuwa na wapangaji wengine ambao walimlipa Sh50,000 hadi Sh100,000 kwa mwezi fedha alizodai zilimtosheleza kuendesha maisha yake ikiwamo kusomesha watoto wake. “Nyumba yangu ilikuwa na wapangaji wote wameondoka na walipoondoka  watatu waling’oa milango ya nyumba na kuondoka nayo kwani  walikuwa wamelipia kodi ya miezi sita na walipotaka niwarudishie sikuweza hivyo wakangoa milango,” anasema.

Alivyojenga nyumba zake

Leo anaeleza kuwa mwaka 1988 alifika Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Kilimanjaro, wakati huo alikuwa akijishughulisha na kazi ya ufundi wa magari.

Akiwa Dar es Salaam alibahatika kununua daladala kutokana na kazi yake hiyo. Baada ya kununua gari hiyo ya biashara aliachana na ufundi na  kuwa dereva wa gari yake.

Mwaka 1994 alipata fedha akanunua nyumba kwa mtu aliyemtaja kuwa ni Paulo Kihampa, baada ya kujiridhisha kwa kutumia kiogozi wa Serikali ya Mtaa Stop Over, Abuu Mbasi  kuwa haiko ndani ya hifadhi ya barabara.

“Nilinunua nyumba kwa bei ya Sh2 milioni. Baada ya hapo nikajenga nyumba ya ghorofa moja na baada ya miaka mitano  aliongeza nyingine ya gorofa moja.” anasema.

“Nilikaa miaka miwili nikaanza kujenga taratibu nyumba ya tatu ambayo haikuwa ya ghorofa, nilitumia miaka mitatu kukamilisha ujenzi huo nikiwa bado na kazi yangu ya udereva,” anasema.

Nilipokamilisha tu nikaanza tena kujenga nyumba ya nne ambayo pia niliijenga kidogokidogo mpaka sasa kiwanja chake kilikuwa na nyumba nne ndani ya eneo moja,” anasema.

Maisha mapya baada ya kubomolewa

“Najiuliza sijui kwanini bado naishi hapa, lakini sipati jibu. Nikilala nikiamka najikuta nipo hapa,” anasema Leo ambaye licha ya nyumba yake kubomolewa bado anaendelea kuishi katika mabaki ya nyumba yake.

“Nalala kwenye pagale hili, watoto wangu nimewapeleka kwa ndugu na jamaa, naamimi nimebaki hapa sina pakwenda napambana na hali yangu,” anasema.

Bilioni tano zaokolewa

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kufuata matibabu.



Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alipotembelea MOI na kukagua hali ya utoaji wa huduma, mazingira , miundombinu na kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kukutana na menejimenti.

Dkt. Mpoki amesema kuwa fedha hizo zimeokolewa baada ya MOI kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali zilikua hazipatikani hapa nchini, hivyo kulazimu wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi hivyo kuongeza gharama.

Akizungumza na uongozi wa MOI, Dkt. Ulisubisya amepongeza kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea watanzania kupata huduma bora za kibingwa ambazo wangepaswa kuzifuata nje ya nchi.

Aidha, Dkt Ulisubisya amesema MOI imepunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa asilimia 95% na asilimia 5% iliyobaki MOI inaweza kuimaliza kabisa na kusiwepo na mgonjwa wa kwenda nje ya nchi.

Monday, 20 November 2017

Kaburi lafukuliwa kwa utata



Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na madaktari wa hospital ya rufaa ya KCMC limesema linaendelea na uchunguzi wa mwili uliofukuliwa kwenye makaburi ya Karanga mji mdogo wa Himo mjini Moshi.

Mwili huo ulifukuliwa jumapili chini ya usimamaizi wa Jeshi la Polisi na kufuatia utata uliojitokeza baada ya mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Scholastica iliyopo Himo kupotea kwa siku kadhaa bila kuonekana.

“Tunaendelea na uchunguzi juu ya mwili huo na tayari kuna watu tumewakamata hivyo kila kitu kitakapokuwa sawa tutatoa ripoti kamili ya tukio hilo na wenzetu wa KCMC wanaendelea na uchunguzi wa mwili tulioufukua ili kujiridhisha kama ni wenyewe au sio”, amesema Kamishna Msaidizi wa Polisi Hamis Issa.

Humphrey Makundi, mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Scolastica anatajwa kupotea tangu Novemba 7 mwaka huu akiwa shuleni.

Kutokana na kuwepo kwa taarifa za kuokotwa kwa mwili katika mto Ghona uliopo mita 300 kutoka shule hiyo na kukosekana kwa ndugu walioutambua, mahakama ililazimu kukubali ombi la familia ya Humphrey la kufukua kaburi hilo ili kuweza kutambua kama mwili huo ni wa mtoto wao.

Kocha wa Mbeya City akubali matokeo



Kocha mkuu wa kikosi cha Mbeya City Nsanzurwimo Ramadhani amekubali kubeba lawama kutokana na kipigo cha 5-0 ilichokumbana nacho timu yake ilipocheza ugenini dhidi ya Yanga mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Kocha huyo ametoa pole kwa uongozi wa timu yake, wachezaji na mashabiki kutokana na matokeo mabaya ya kupoteza mchezo kwa kufungwa magoli mengi msimu huu Mbeya City ikiwa timu ya pili kuruhusu magoli mengi kwenye uwanja wa Uhuru baada ya Ruvu Shooting kufungwa 7-0 na Simba mwanzoni mwa msimu.

“Nitoe pole kwa Mbeya City kuanzia uongozi wa juu, wachezaji na watu wote, ni vigumu kucheza katika mazingira haya, kama unacheza ligi hii na kufanya makosa yanayopelekea kufungwa magoli mawili ya mapema, lakini kwa upande mwingine pongezi ziende kwa Yanga kwa sababu walitumia vizuri makosa yetu wakatufunga.”

“Mbinu zetu hazikufanikiwa kabisa, hatukucheza vizuri, inaumiza, kwa sababu tulijiandaa vizuri na wachezaji walikuwa na ari kabla ya mchezo lakini wakati wa mchezo zaidi ya asilimia 80 ya wachezaji hawakuwa bora, unategemea nini?”

“Kwa hiyo hatukupaswa kujiandaa? Timu zote zinazojiandaa ni lazima zishinde? Matokeo yaha ni sehemu ya mchezo, hata kama tungeenda Brazil au sehemu yoyote. Timu haikucheza vizuri nakubali na ninabeba mzigo wa lawama kama kocha wa timu, kufungwa goli 5-0 nakubali na ninabeba lawama.”

“Tumepoteza mechi hatujashindwa ligi, bado ligi inaendelea tunarudi kujipanga na kuangalia makosa yetu bado kuna nafasi ya kufanya marekebisho kuona kwa namna gani tutaboresha kiwango chetu.

Ukiangalia utaona kulikuwa na makosa mengi binafsi ya mchezaji mmoja mmoja kuliko makosa kama timu na inatokea kwenye mchezo. Kwa mara nyingine nawapa pole mashabiki wetu.”

Wanafunzi waliolipukiwa na bomu shuleni, sasa hawaoni

Wanafunzi waliolipukiwa na bomu shuleni, sasa hawaoni




Zikiwa ni siku 12 baada ya mlipuko wa bomu uliotokea Shule ya Msingi Kihinga mkoani Kagera, majeruhi wawili wamerejeshwa hospitali baada ya kupata tatizo la kuona.

Majeruhi hao wawili ni miongoni mwa wanafunzi 43 waliojeruhiwa akiwamo mwalimu katika mlipuko wa bomu uliotokea Novemba 8 na kuua wanafunzi watano baada ya mmoja wao kuliokota na kwenda nalo shuleni akidhani kuwa ni chuma chakavu ambacho angekiuza.

Mganga mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Rulenge, Dk Mariagoreth Frederick alisema jana kuwa, watoto hao waliruhusiwa kurejea nyumbani Novemba 10 na walirejeshwa tena Novemba 14 kutokana na kuathirika machoni. Aliwataja watoto hao kuwa ni Irene Sherehe na Domina Wabandi (10).

Dk Mariagoreth alisema Domina anafanyiwa utaratibu na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ili apelekwe Hospitali ya Rufaa ya KCMC ili kuwekewa jicho la bandia.

Bomu hilo lililipuka wakati wanafunzi wa darasa la kwanza wakiingia darasani na liliokotwa na mwanafunzi ambaye alilihifadhi kwenye begi la madaftari kwa lengo la kwenda kuliuza kwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu.

Mbali ya hao, Dk Mariagoreth alisema watoto wengine wawili jana walihamishiwa Hospitali ya Kagondo wilayani Muleba ambako kuna madaktari bingwa wa mifupa.

Pia, alisema leo watawaruhusu majeruhi watano kurejea nyumbani kutokana na afya zao kuimarika, hivyo watabaki watano.

Majeruhi waliohamishiwa Hospitali ya Kagondo ni Emanuel Hilali (13) ambaye anahitaji uchunguzi zaidi wa mguu wa kushoto na ambaye pia alipoteza jicho la kulia lililoondolewa kutokana na kuharibika.

Mwingine ni Simon Boniface (10), mwenye tatizo kwenye kidevu na anahitaji kuchunguzwa meno huku akiwa na maumivu mguu wa kulia. Dk Mariagoreth alisema bado wanahitaji dawa na vifaa tiba.

Alisema gharama za matibabu zilizotumika kwa majeruhi 33 walioruhusiwa ni Sh1.8 milioni na kwa waliopo hadi Novemba 14 wamefikisha Sh4 milioni. “Wazazi wa majeruhi hawajiwezi kiuchumi, hivyo uongozi wa wilaya ulishauri watafutwe madaktari bingwa watoe huduma hapa badala ya kuwasafirisha kwenda hospitali za rufaa ili kupunguza gharama,” alisema.

Alisema majeruhi wanne ambao kila mmoja alipoteza jicho moja wanatibiwa majeraha na mipango inafanywa ili fedha zikipatikana wapatiwe miwani ili kuongeza uwezo wao wa kuona kwa jicho lililobaki.

Dk Mariagoreth alisema wanahitaji dawa za ‘antibiotiki’ kwa ajili ya kukausha vidonda vya majeruhi.

Jukwaa la Maendeleo ya Wakazi wa Rulenge na Murusagamba wilayani Ngara llmechangia Sh1.07 milioni kusaidia mahitaji mbalimbali kwa ajili ya majeruhi hao.

Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Michael Mntenjele aliyefika hospitalini kuwajulia hali majeruhi mwishoni mwa wiki, aliwataka wazazi na walezi kuwa na imani na madaktari wanaoshughulikia afya za watoto wao.

Alisema wanafanya jitihada kuhakikisha huduma zinatolewa kwa majeruhi na baada ya kupona utafanyika utaratibu wa kuwarejesha shule.

CCM yafanya uteuzi huu




Chama cha Mapinduzi CCM kupitia Kamati kuu (CC) kwa niaba ya halmashauri kuu taifa NEC, kimefanya uteuzi wa wagombea walioomba kuwania nafasi ya Uenyekiti katika wilaya Sita nchini zikiwemo zile wilaya za kichama.

Wilaya ambazo zimepata wagombea ni Moshi Mjini, Siha na Hai zote za mkoani Kilimanjaro ambapo uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 1-2 mwaka huu. Wilaya ya Makete mkoani Njombe pamoja na wilaya zinazotambulika kichama za Musoma Mjini na Musoma Vijijini mkoani Mara uchaguzi wake umepangwa kufanyika Novemba 25-26 mwaka huu.

Katika Wilaya ya Hai walioteuliwa kugombea nafasi hizo ni Abdullah Hussein Mriri, Magai Wang’uba Maganda na Justice Edmen Elipokea Massawe. Wilaya ya Siha ni Justice Nicodemo Mkita, Wlfred Luka Mossi na Humfrey Joshua Nnko.

Wilaya ya Moshi Mjini ni Absalom Angyeulile Mwakyoma, Joseph Oforo Mtui, Faraji Kibaya Swai na Alhaj Omar Amin Shamba. Wilaya ya Makete ni Aida Menson Chengula, Mwamwite Clemence Njajilo na Onna Amos Nkwama.

Wilaya ya Kichama ya Musoma Mjini walioteuliwa ni Robert Maganya Sylvester, Magiri Benedicto Maregesi, Amina Marumbo Nyamgambwa na Daud Adam Misango. Wialya nyingne ya kichama ya Musoma vijijini wagombea ni Gerald Mfungo Kasonyi, Kananda Hamisi Kananda na Nyabukika Bwire Nyabukika.

Kenya yaiandikia barua Tanzania




Taarifa ya serikali kupitia wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imetibitisha kupokea barua hiyo huku serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiahidi kuijibu na kuitolea ufafanuzi kama ilivyofanya mwanzo.

“Vile vile serikali imepokea barua kutoka Serikali ya Kenya kuhusu masuala haya, na Serikali itaijibu barua hiyo kutoa ufafanuzi”, imeeleza sehemu ya taarifa ya wizara juu ya ufafauzi kuhusu suala la vifaranga pamoja na mifugo iliyoingizwa nchini bila kufuata sheria.

Aidha serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuhakikisha inafuata sheria zote bila kuathiri uhusiano wake na nchi zingine, huku ikizitaka nchi zote duniani, ikiwemo Kenya, kufuata miongozo ya WTO na Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (OIE) kwa kutoa vibali (export permit) kwa mtu yeyote anayetaka kusafirisha mifugo nje ya nchi.

Kabla ya kuteketezwa kwa Vifaranga hivyo serikali imesema Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania alimpigia simu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa Kenya kutaka kujua kama Mamlaka za Kenya zina habari kuhusu vifaranga hivyo ili virudishwe lakini alisema hana taarifa kuhusu vifaranga hivyo na kwamba Kenya haiko tayari kuruhusu vifaranga hivyo kurudishwa nchini mwao.


Zimbabwe: Emmarson Mnangagwa '' Mamba'' atarajiwa kuiongoza





Ni siri iliyofichuka nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kwamba Emmerson Mnangagwa alitaka kumrithi Robert Mugabe kama rais.

Na Bwana Mugabe anaonekana kuwa amekuwa akichezea hisia zake - na amekuwa akimpandisha vyeo katika chama tawala cha Zanu-PF party na hata katika serikali, jambo lililozusha uvumi kwamba Bwana Mnangagwa ''ndie mrithi wake'' lakini baadaye alimshusha cheo huenda baada ya kuonyesha azma yake wazi pengine kupita kiasi.

Lakini baada ya kufutwa kazi, inaonekana kana kwamba subra ya Mnangagwa anayefahamika kwa jina maarufu la "mamba" ilikwisha.

Baada ya kufutwa kazi na Bwana Mugabe kumpuuza na kumshutumu hadharani kwa "usaliti", wafuasi wake katika jeshi waliingilia kati kwa niaba yake.

Lakini yeyote mwenye matumaini kwamba urais wa Mnangagwa utamaliza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Zimbabwe huenda anajitanganya .

Wakosoaji wake wanasema kuwa Kiongozi huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 71- ana damu mikononi mwake.

uhusiano wake na Kongo
Bwana Mnangagwa alizaliwa katika jimbo la Zvishavane na anatoka katika kabila dogo ambalo ni sehemu ya jamii ya Washona

Watu wa Kabla la Karanga ni kabila kubwa katika jamii ya Washona na baadhi wanahisi ni wakati wao sasa wa kuingia madarakani, kufuatia miaka 37 ya utawala wa raia Mugabe anayetoka katika kabila la Zezuru

Uamuzi wa Majaji waigusa Tume ya Uchaguzi Kenya




 Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati.

Tume ya Uchaguzi imefurahia uamuzi wa Mahakama ya Juu na kusema ni dhihirisho la kujitolea kwa tume hiyo kufanikisha uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika.

Imesema kupitia taarifa kwamba inasubiri uamuzi wa kina ambao utaiongoza katika kutathmini uchaguzi huo ulivyokuwa pamoja na mipango yake ya kuimarisha uchaguzi na tume yenyewe.



Vyama vya Siasa vyapewa onyo

Vyama vya Siasa vyapewa onyo



Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevionya vyama vya siasa na kutaka vifanye kampeni kwa kufuata sheria, vikijiepusha na vitendo vya matusi na uchochezi.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Jumapili hii Novemba 19,2017 na Jaji Mutungi amesema maneno ya uongo, matusi na uchochezi kwenye kampeni ni kinyume cha sheria.

Sina shaka na mwitikio wa ushiriki wa vyama vya siasa katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa madiwani unaendelea nchini katika kata 43 zilizoanza Oktoba 26 na zinazotarajiwa kuhitimishwa Novemba 25 mwaka huu, hata hivyo, zimebainika kasoro ndogo ndogo ambazo si ishara nzuri kuelekea uchaguzi wa amani.

Siyo jambo lenye tija kuacha kasoro hizi ziote mizizi, tunastahili kukemea kasoro hizi kwa nguvu zote, hivyo naviasa vyama vya siasa na wagombea wote wanaoshiriki katika uchaguzi huu mdogo wa madiwani kujiepusha na yafuatavyo:-

a) Kuepuka kutumia maneno ya uongo na yenye kuudhi, matusi, uchochezi, kashfa, na mambo yanayofanana na hayo kwani ni kinyume na sheria na , badala yake vyama vinadi sera zao;

b) Kuepuka vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani na kuepuka propaganda ambazo zinawatia hofu wananchi na wapiga kura.

c) Kutochukua hatua za kisheria mkononi na kutojihusisha na vitendo vya uchokozi mfano kuingilia mikutano ya kampeni ya chama kingine, kuchoma ama kuchana bendera/ mabango ya chama kingine ;

d) Kutojihusisha na vitendo vyovyote vya rushwa, mfano kununua wapiga kura au kuuza shahada ya mpiga kura;
e) Kuepuka propaganda ambazo zinawatia hofu wananchi na wapiga kura.

Aidha ni vyema vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huu pia kuelewa kuwa, vina wajibu wa kisheria wa kuwaasa na kuwadhibiti wanachama na wagombea wao kuheshimu na kufuata Sheria zote zinazohusika. Hivyo, kila chama kitekeleze wajibu wake, ili uchaguzi huu ufanyike kwa amani na utulivu.

Pia ninawaomba sana Waandishi wa habari kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya kazi zenu wakati huu wa kampeni na uchaguzi ili kuwasaidia wananchi kupata taarifa sahihi.

Ifahamike kwa wadau wote kwamba, maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wapo katika kata zote 43 wakifanya uangalizi wa karibu kubaini ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za uchaguzi.

Lengo kuu ni kuhakiksha kuwa kunakuwepo uwanja sawa wa ushindani katika uchaguzi, hakuna chama chochote kinachoingilia mikutano ya chama kingine kwa kufanya vurugu, kuepusha matumizi makubwa ya fedha na kuweka uwazi katika matumizi ya fedha na rasilimali nyingine katika kampeni. Hivyo kila chama cha siasa ambacho kinashiriki katika uchaguzi kinapaswa kuwashawishi wananchi kwa sera zake na si vinginevyo.

Miongoni mwa majukumu ambayo yanatekelezwa na maafisa wa ofisi yangu kwa sasa katika kata hizo 43 ni pamoja na kutoa mafunzo elekezi kwa vyama vya siasa, wagombea wa Udiwani, viongozi wao na wananchi kwa ujumla juu ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi na matendo yaliyokatazwa wakati wa kampeni na uchaguzi na kutoa taarifa juu ya mwenendo wa kampeni. Naamini elimu hii itaendelea kuwaongezea Umma ufahamu wa dhamira nzuri ya Serikali katika kukuza demokrasia nchini.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ina jukumu la kisheria la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na Kanuni zake katika chaguzi zote ikiwamo chaguzi ndogo za wabunge na madiwani.

Jaji Francis S.K. Mutungi

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

19 Novemba, 2017

Makonda aiungamkono Kampuni ya ukamataji kazi za Wasanii



MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameipiga jeki Kampuni ya Msama Auction Mart inayojishughulisha na ufuatiliaji na ukamataji wezi wa kazi za wasanii kwa kuchoma CD feki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama alisema Makonda ameamua kuipiga jeki kampeni hiyo kutokana na matunda anayoyaona ya zoezi hilo kuendelea vizuri kwani amezunguka katika jiji lake hasa maeneo ya Kariakoo na kujionea biashara hiyo haramu ya kuchoma CD feki ikiwa imepungua na kuwaomba waendelee na zoezi hilo.

Alisema kutokana na kutiwa moyo na mkuu huyo wa mkoa, Kampuni ya Msama Auction Mart sasa imezidi kupata nguvu ya kuendelea na zoezi hilo popote pale, iwe mafichoni ama pembezoni mwa mji lazima wezi wa kazi za wasanii wakamatwe.
Stori zinazo husiana na ulizosoma