Thursday, 2 November 2017

Mwanamuziki huyu afariki Dunia

Mwanamuziki Keith Wilder(65) amefariki dunia. Wider alikuwa akifanya vizuri na bendi yake ya Heatwave  kipindi cha miaka ya 70.

Kupitia bendi yake hiyo wameshafanya hits song kama “Always and Forever,” “Boogie Nights” na “The Groove Line”, chanzo cha kifo chake kimetajwa kuwa ni matatizo ya kiafya.

Taarifa ya kifo cha mkongwe huyo wa burudani imetolewa na binamu yake Billy Jones, ambaye ameeleza kuwa siku ya Jumapili marehemu alikuwa amelala na ndipo kifo kilipomkuta.

Kupitia band yake wameshawahi kushiriki tuzo kubwa duniani za Grammys mara mbili ila hawakuwahi kushinda tuzo hizo.


Ajira za afya zasitishwa



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu 

Dar es Salaam. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesitisha ajira mpya za kada ya afya zilizoombwa kwa kipindi cha Agosti mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa Oktoba 31 na Tamisemi ikieleza kusitisha ajira hizo kwa walioitwa kazini.

Taarifa hiyo iliwataarifu waajiri na waombaji wote wa nafasi za ajira za kada za afya kuwa imesitisha zoezi hilo kwa muda mfupi ili kukamilisha taratibu za ajira.

“Tafadhali rejeeni tangazo letu lenye Kumb. Na CD. 162/355/01 la tarehe 30 Oktoba, 2017 lililowataarifu waombaji wa kazi wa nafasi mbalimbali za kada za afya walioomba kazi kuanzia 25/07 - 30/08/2017,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imethibitishwa kutolewa na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Zainabu Chaula ambaye aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli wamesitisha kwa muda kwa sababu za kiufundi na halihusiani na madaktari wa Kenya.

Hivi karibuni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kwamba kumekuwa na upungufu wa watumishi wa afya hivyo wapo katika mikakati ya kuhakikisha wanaajiri upya watumishi.

Alisema kwamba wizara yake kupitia kibali cha Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, walitangaza nafasi za kazi 3,152 kwa wahitimu wa kada za afya nchini.

“Wizara ina jukumu la kuwapangia vituo vya kazi waombaji wenye sifa kwa mujibu wa waraka wa maendeleo ya utumishi namba moja wa mwaka 2009 kuhusu muundo wa utumishi ya kada ya chini ya wizara ya afya,” alisema waziri huyo.

Hata hivyo Waziri Ummy alipoulizwa jana kuhusu kusitishwa kwa ajira za kada ya afya katika halmashauri hakujibu chochote na hata alipoulizwa tena idadi kamili na kwa nini ajira hizo zimesitishwa pia hakujibu hadi tunakwenda mitamboni.

Viongozi wawili wa Acacia wajiuzulu



Dar es Salaam. Wakati utekelezaji wa makubalino baina ya Serikali na Barrick ukisubiriwa, Ofisa Mtendaji Mkuu na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Acacia, wametangaza kujiuzulu kuanzia leo Alhamisi.

Kwenye barua yake, Ofisa Mtendaji Mkuu, Brad Gordon amesema anataka kurudi nyumbani Australia kusimamia masuala ya familia yake wakati Ofisa Mkuu wa Fedha, Andrew Wray akisema amepata fursa nzuri zaidi sehemu nyingine.

“Pamoja na uamuzi huo, wote wataendelea kuhudumu kwenye nafasi hizo wakati wakikabidhi majukumu ya ofisi kwa warithi wao,” imesema taarifa ya Acacia iliyotolewa leo Alhamisi asubuhi.

Kuziba nafasi hizo, Bodi ya Wakurugenzi wa Acacia imemtangaza Peter Geleta kuchukua majukumu ya ofisa mtendaji mkuu baada ya Gordon na Jaco Maritz kusimamia masuala yote ya fedha za kampuni hiyo.

Wote wawili walikuwa watendaji wa Acacia kwa muda mrefu. Geleta alikuwa mkuu wa oganaizesheni wakati Maritz alikuwa meneja mkuu wa idara ya fedha.

“Licha ya majukumu ya uendeshaji, Geleta atahudhuria vikao vya bodi vitakavyofanyika mwishoni mwa mwaka huu badala ya Gordon na kuifanya idadi ya wajumbe kuendele akubaki saba,” imesema taarifa hiyo.

MAGAZETI YA LEO 2/11/2017

Mama yake Dogo Janja azungumzia ndoa ya mwanaye


Mama mzazi wa msanii Dogo Janja Bi. Zaituni Omari, amesema habari za mtoto wake kuoa ni za kweli na yeye kama mzazi alimpa baraka zote, vinginevyo asingeweza kuoa.

Mama yake Dogo Janja ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari na kusema kwamba yeye kama mzazi ameridhika kwani pia ametimiza matakwa ya dini.

“Alishawahi kuniambia kuwa anataka kuoa na mimi nikampa baraka zote, alivyokuwa tayari alinijulisha akaniambia kama kuna uwezekano niende isipokuwa kuna mambo yakaingilia kati, ila kwa vile Madee ni kama baba yake na ninamuamini sana nikawaruhusu waendelee, kila anachofanya hafanyi yeye kama yeye lazima kiko nyuma yangu, sio stori za kiki ni kweli kaoa na hawezi kuoa bila kuwasiliana na familia yake”, amesema mama yake Dogo Janja.

Kuhusu suala la tofauti ya umri kati yake na Irene Uwoya, mama yake Dogo Janja amesema kwamba suala la umri halijalishi sana isipokuwa kikubwa ni maelewano.

“Nimeridhika kwa sababu hata dini yetu ya Kiislam Mtume Mohamad alioa mwanamke mkubwa, kwa hiyo umri haujalishi, kikubwa na maelewano”, amesema Mama yake Dogo Janja.

Ijumaa ya wiki iliyopita kulianza kuonekana kwa picha mtandaoni zinazoonyesha Irene Uwoya na Dogo Janja








Tuesday, 31 October 2017

Haji Manara avutiwa na mbinu za kocha wa Yanga

Ni mara chache sana kusikia kiongozi au hata shaki wa Simba na Yanga kusifia timu pinzani kutokana na utamaduni wa vilabu hivyo ulivyo hata kama watatakiwa kupongeza, leo October 31, 2017 Haji Manara amesema waziwazi kukubali mbinu zilizotumiwa na kocha wa Yanga George Lwandamina kwenye mchezo wa Yanga vs Simba Jumamosi iliyopita.

Manara amesema Lwandamina ni mtu wa mbinu na alifanikiwa katika mbinu zake za kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza ambapo  timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1, Simba walianza kupata goli la kuongoza lakini Yanga wakasawazisha dakika mbili baadaye.

“Yanga walicheza vizuri tena kwa nidhamu, kocha wao ni mtu wa mbinu sana alikuja kupaki ‘basi’ kwa heshimba ya kuiheshimu Simba lakini akazitumia vizuri ‘counter attack’, walicheza vizuri bila shaka kwa sababu walikuja kama underdogs wakatuheshimu, wakapaki basi lao vizuri.”

Manara amewaambia Yanga kwamba, kushangilia kwao matokeo ya sare ya 1-1 yanadhihirisha Simba ni klabu kubwa Tanzania.

“Yanga ni imu kubwa, hamuwezi kwenda kucheza na Simba kamawanyonge lakini baada ya matokeo ya 1-1 wakashangilia na hiyo ndiyo inayonipa tatu. Tuliwazidi umiliki wa mpira 58% kwa 42%. Sisi hatukuridhika kutoka sare na Yanga na hatutaridhika kutoka sare na timu yoyote Tanzania kwa sasa hivi kwa sababu tuna kikosi kizuri.”

Zitto Kabwe ameachiwa huru

Zitto Kabwe ameachiwa huru

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa huru kwa dhamana na kutakiwa kuripoti siku ya Jumanne saa tatu asubuhi kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI) jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria wa Zitto Kabwe amesema kuwa mpaka sasa mteja wake anatuhumiwa kwa makosa mawili tofauti likiwepo kuchapisha taarifa kinyume cha sheria ya mitandao lakini kosa jingine ni kutoa takwimu za uongo kinyume na kifungu cha 37 (5) cha sheria ya takwimu ya mwaka 2015 hivyo mwanasheria anasema Zitto Kabwe amehojiwa na kutoa maelezo yake hivyo wanasubiri kujua kama watakwenda mahakamani.

Kwa upande wake Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwa sasa wanasubiri kuona wanapelekwa mahakamani ili waweze kujadiliana huko na kusema kama wao kuna makosa ambayo wanayaona kwake sehemu pekee ambayo wanaweza kwenda kufafanua vizuri ni mahakamani na kudai kuwa kama asingekamatwa angeshangaa kwa kuwa tayari Rais alikuwa ameshatoa agizo.

"Tunasubiri ni lini watatupeleka mahakamani kwa ajili ya kutetea masuala ambayo tumezungumza lakini ya ziada ni kama ambavyo Mwanasheria amezungumza kwa hapa ni makosa mawili ya Sheria ya Takwimu na Sheria ya makosa ya mitandao, wananchama waendelee kuwa watulivu tu kwa sababu kila mtu alitarajia kuwa tutakamatwa kwa kuwa Rais alisema kuwa nikamatwe hivyo tusingekamatwa ningeshangaa, la ziada ni kwamba tusubiri mahakamani itakuaje" alisisitiza Zitto Kabwe
Mbali na hilo kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amewataka wanachama pamoja na viongozi wa chama hicho kuendelea na harakati za uchaguzi mdogo wa udiwani na kusema endapo wakishinda katika uchaguzi huo ni kitu ambacho kitakuwa faraja kwao

Korea Kaskazini: Watu zaidi ya 200 wafariki katika ajali baada ya majaribio

Watu zaidi ya 200 waripotiwa kufariki baada ya handaki moja  kuporomoka nchini Korea Kaskazini

Watu zaidi ya 200 waripotiwa kufariki na wengine kadhaa kukwama baada ya handaki moja likiwa katika ujenzi kuporomoka.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na runinga ya Japan, handaki moja katika ujenzi limeporomoka katika eneo ambalo limetaarishwa kawa ajili ya majaribio la makombora ya nyuklia Punggye-ri.

Taarifa zinafahamisha kuwa watu takriban 200 wamefariki baada ya kuporomoka kwa handaki hilo baada ya jaribio la kombora la nyuklia Korea Kaskazini.

Ajali hiyo  imethibitishwa pia na kituo cha habari cha Korea Kusini Yonhap.

Maporomoko mengine yametokea wakati shughuli za uokozi zikiendele

Manara: Tulinyimwa penati mbili dhidi ya Yanga

Manara: Tulinyimwa penati mbili dhidi ya YangaKLABU ya Simbe imelalamika kunyimwa penalti mbili na refa Hery Sasii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC uliomalizika kwa sare ya 1-1 Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Sunday Manara amesema refa alikwenda na matokeo yake uwanjani.

Manara aliwawekea Waandishi wa Habari video ya mchezo huo kuwaonyesha namna ambavyo refa Sasii hakutoa penalti licha ya mpira kuwagonga mikononi beki, Kevin Yondan na kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi Jumamosi.

Manara aliyewabeza watani wao hao wa jadi, kwamba ni kawaida yao kupendelewa na marefa kila wanapokutana na Simba amesema watapeleka malalamiko Bodi ya Ligi dhidi ya refa huyo na wengine walioionea timu yao katika mechi zilizotangulia.

Akasema huo ni mwendelezo wa matukio ya klabu yake kutotendewa haki na marefa katika mechi za Ligi Kuu msimu huu, akidai walinyimwa pia penalti mbili katika mechi dhidi ya Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, kabla ya wapinzani wao wengine, Singida United kupewa penalti ya utata Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.

Simba ilitoa sare ya 2-2 na Mbao FC kabla ya kushinda 3-1 dhidi ya Stand United, katika mchezo ambao pia walikataliwa bao zuri la mshambuliaji wao, Laudit Mavugo.

Pamoja na hayo, Manara amelalamikia kitendo cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kukataa ombi la klabu, Simba na Yanga kutaka mchezo wao ufanyike Uwanja mkubwa wa Taifa na kuupeleka Uwanja mdogo wa Uhuru.

Manara amesema hali hiyo ilizikosesha klabu fedha kutokana na watazamaji kutojitokeza kwa wingi kwa kuhofia usalama wao kutokana na udogo wa Uwanja wa Uhuru.

Aidha, Manara  amesema kwamba kikosi cha Simba sasa kinaelekeza nguvu zake katika mchezo wake ujao dhidi ya Mbeya City Jumapili Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na  kikosi kitaondoka  Ijumaa kwenda Mbeya na  kitakaa kwa muda mrefu kutokana na kukabiliwa na mechi nyingine pia za Ligi Kuu Nyanda za Juu Kusini.

Harry Kane yupo fiti kuivaa Real Madrid kesho

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa mazoezini na wenzake leo baada ya kupona maumivu ya nyama za paja wakijiandaa na mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho dhidi ya Real Madrid Uwanja wa Wembley, London

Raila Odinga asema hawauatambui uchaguzi wa Uhuru Kenyatta

Raila Odinga asema hawauatambui uchaguzi wa Uhuru Kenyatta


Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Nasa Raila Odinga ameapa kuendelea kufanya maandamano dhidi ya uchaguzi wa Uhuru Kenyatta akisisitiza kuwa upinzani haumtambui.

Odinga anasema kuwa Nasa haitambui uchaguzi huo kwa kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati pamoja na kamishna aliyejiuzulu Roselyn Akombe walithibitisha kwa umma kuwa tume hiyo haiwezi kusimamia uchaguzi ulio huru kutokana na misimamo ya kimapendeleo ya baadhi ya makamishna katika tume hiyo.

Odinga ambaye alikuwa akitoa mwelekeo wa upinzani kwa vyombo vya habari katika jumba la OKoa Kenya jijini Nairobi amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kulikuwa na uingiliaji na uongezaji wa kura katika ngome za chama tawala cha Jubilee.

Anasema kwamba iwapo uchaguzi huo utaruhusiwa na kutambulika utawavunja moyo Wakenya wengi na hivyobasi kuwafanya kutoshiriki katika uchaguzi mwengine wowote.

Mr Odinga pia amesema kuwa hawezi kuwaruhusu watu wawili wanaojigamba kuwa na uwezo kuharibu uhuru na demokrasia ilipatikana.

Amesema kuwa iwapo uchaguzi wa Uhuru utaruhusiwa kuna uwezekano kwamba ataingilia katiba na kuongeza muhula wa kuongoza.

''Tutaendelea kufanya maandamno kila mara'', alisema Raila Odinga.

Bwana Odinga alisusia uchaguzi wa marudio wa urais wiki iliopita kwa sababu anasema kuwa hakuna mabadiliko yaliofanyiwa tume ya uchaguzi ya IEBC baada ya mahakama ya juu kupata makosa na ukiukaji mkubwa wa katiba.

Watu waliojitokeza kupiga kura ni chini ya asilimia 39.

Ametangaza kuwa atazindua bunge la wananchi ambalo litashirikisha jopo litakalochunguza kufeli kwa tume za uchaguzi.

Zitto Kabwe afunguka baada ya kuachiwa

Zitto Kabwe afunguka baada ya kuachiwa



Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema asingekamatwa na polisi angeshangaa.

Amesema hilo linatokana na kauli ambazo zilitolewa na baadhi ya viongozi wa Serikali kuhusu takwimu alizotoa.

"Kila mtu alijua tutakamatwa na kama tusingekamatwa basi tungeshangaa,” amesema Zitto leo Jumanne Oktoba 31,2017 baada ya kuachiwa kwa dhamana na polisi.

Zitto amesema maelezo ya kina na ufafanuzi wa kauli zake zinazodaiwa kuwa za uchochezi atayatoa atakapofikishwa mahakamani.

Ufafanuzi mwingine anaodai atautoa atakapofikishwa mahakamani ni kuhusu masuala ya takwimu na makosa ya mtandao.

Pia, amewataka wanachama wa ACT Wazalendo kuendelea na shughuli zao kama kawaida na hasa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani utakaofanyika Novemba 26, 2017.

Zitto baada ya kuachiwa, mwanasheria wake Stephen Mwakibolwa amesema akiwa Kituo cha Polisi Chang'ombe, mteja wake  alihojiwa kwa kosa la uchochezi alilolifanya wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani Kijichi jijini Dar es Salaam, Jumapili Oktoba 29,2017.

"Pale Chang'ombe alihojiwa kwa uchochezi na baada ya mahojiano aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kurudi Jumatatu ijayo, lakini baada ya kuachiwa alikamatwa tena na kuletwa hapa (kituo cha polisi cha upelelezi wa makosa ya kifedha)" amesema Mwakibolwa.

Amesema makosa aliyohojiwa akiwa katika kitengo hicho ni kuchapisha au kutoa taarifa zisizo sahihi kinyume cha sheria ya takwimu na kusambaza taarifa za uongo kinyume cha makosa ya mitandao.

Mwakibolwa amesema Zitto amepewa dhamana na kutakiwa kurudi Jumanne Novemba 7,2017.

Mwananchi: