Tuesday, 31 October 2017

Muigizaji akiri kushiriki mapenzi ya jinsia moja



 Muigizaji mkongwe kutoka Uingereaza Kevin Spacey amefunguka kwa mara ya kwanza na kukiri kushiriki mapenzi ya jinsia moja.

Kevin ambaye ni maarufu pia katika tamthilia ya ‘House of Cards’ ameamua kutoa kauli yake baada ya muigizaji na msanii wa muziki Anthony Rapp kudai kuwa amekuwa akisumbuliwa na Spacey toka aliwa na umri wa miaka 14, wakati huo Kevin ana miaka 26.

Kauli ya Rapp(46) imetoka wakati akifanyiwa mahijiano na Buzzfeed, Hata hivyo Spacey(58) amefunguka na kuadai kuwa alimuomba radhi kijana huyo na kumtaka asionge ila anashangazwa na Rapp kuamua kusema sasa.

Ajibu ajazwa zawadi Jangwani



Mwigizaji na msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi maarufu kama ‘Ray’, amewaongoza mashabiki wa Yanga SC kutoka kundi la ‘Yanga For Life’ kwenye mtandao wa WhatsApp kutoa zawadi kwa wachezaji wa timu hiyo.

Ray na wenzake wametoa zawadi ya fedha, viatu na ‘Shin Gard’, mchana wa leo kwa wachezaji watatu, waliofanya vizuri katika michezo ya Ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu.

Miongoni mwa wachezaji waliopata zawadi hizo ni mshambuliaji Ibrahim Ajib ambaye amepewa kiasi cha Tsh Milioni moja, baada ya kuibuka nyota wa mchezo kwenye mechi mbili za Kagera Sugar na Stand United.

Kiungo kutoka DRC Papy Kabamba Tshishimbi, ambaye aliibuka nyota wa mchezo wa watani wa Jadi jumamosi iliyopita amepewa zawadi ya shilingi laki tano huku kipa Youthe Rostand, akipata shilingi laki mbili, viatu na ‘Shin Gard’. 

Baada ya kukabidhi zawadi hizo Ray amesema nia ya kundi lao ni kuwapa hamasa wachezaji wao ili waweze kutetea ubingwa wao wa ligi na kutwaa mara ya nne mfululizo

Rais Magufuli afunguka mazito kuhusu wanaohama CCM

Rais Magufuli afunguka mazito kuhusu wanaohama CCM




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

"Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele" alisisitiza Rais Magufuli

#Updates : Zitto Aachiwa, Polisi Wamkamata Tena

#Updates : Zitto Aachiwa, Polisi Wamkamata Tena



Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, ameruhusiwa kwa kudhaminiwa na watu wawili hapa Kituo cha Polisi Chang'ombe, Temeke, Dar es salaam.

Polisi wamemkamata tena baada ya kudhaminiwa kwa amri ya DCI, na muda huu anapelekwa kuhojiwa katika Kituo cha Polisi Kamata.

Ado Shaibu
Katibu - Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma
ACT Wazalendo
Oktoba 31, 2017

Miili 9 iliyokatwakatwa yapatikana kwenye nyumba Tokyo Japan

Miili 9 iliyokatwakatwa yapatikana kwenye nyumba Tokyo Japan




Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamume mmoja baada ya kupata viungo vya miili tisa katika nyumba yake iliyo Zama huko Tokyo.

Polisi walipata vichwa viwili kwenye jokovu nje ya nyumba ya mshukiwa kwa jina Takahiro shiraishi, wakati wakichunguza kutoweka kwa mwanamke mmoja.

Pia walipata viungo vya watu saba kwenye majokovu yaliyo ndani ya nyumba yake.
Mtu huyo wa umri wa miaka 27 anashtakiwa kuwa ndiye alitupa miili hiyo.

Polisi walikuwa wamepata miili ya wanawake 8 na mwanamume mmoja, mingine tayari ikiwa imeanza kuoza.

"Niliwaua na nikaifanyia kazi miili yao ili kuficha ushahidi," shirika la habari la NHK lilimnukuu akisema.

Jirani wake alisema kuwa alikuwa ameanza kuhisi harufu mbaya kutoka kwa nyumba yake tangu Bw. Shiraishi ahamie nyumba hiyo mwezi Agosti.

Polisi walifanya ugunduzi huo walipokuwa wakimtafuta mwanamke wa umri wa miaka 23 ambaye amekuwa hajulikani aliko tangu tare 21 mwezi Oktoba.

Wachunguzi waligundua kuwa Bw. Shiraishi amekuwa akiwasiliana na mwanamke huyo baada ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikuwa anataka kujiua


Profesa Jay atupa jiwe gizani

Profesa Jay atupa jiwe gizani

Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ametoa ujumbe unaoonekana kama ushauri kwa vyama vya siasa huku ukilenga matukio ya hivi karibuni ya wanasiasa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine.

Katika Ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Profesa Jay ameandika “Mkimaliza hiyo HOJA yenu Mfu ya UFISADI, leteni tuhuma za wote waliobaki huko na Muwatimue mapema msisubiri waondoke wenyewe... TUMEELEWANA”?

Ujumbe huu wa Profesa Jay umekuja ikiwa ni chini ya saa 24 toka Mbunge wa Singida Kaskazini kupitia CCM, Lazaro Nyalandu ajiuzulu Ubunge pamoja na nyadhifa zingine ndani ya chama ikiwemo kujivua uanachama.

Kwa upande mwingine ujumbe huo umechukuliwa kama jibu kwa Chama cha Mapinduzi ambacho kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kilijibu suala la Nyalandu kuhama kwa hoja ya kuwa ni miongoni mwa wanachama wengi wasio waadilifu ambao wameamua kuondoka kabla ya Panga kuwafikia.

Hata hivyo Profesa Jay amegoma kufafanua undani wa ujumbe huo iwapo umelenga kupuuza hoja hiyo ya Ufisadi. Awali Profesa Jay aliandika ujumbe wa kumpongeza Nyalandu kwa uamzi wake na kumkaribisha Chadema. “Hongera sana my brother Lazaro Nyalandu kwa Ujasiri na kusimamia kile unachokiamini!! KARIBU SANA KIUMENI SPEAK YOUR MIND”, aliandika Profesa Jay.

Kiongozi wa Catalonia aliyefutwa "aenda Ubelgiji"



Rais wa Catalonia aliyefutwa Carles Puigdemont ameenda nchini Ubelgiji, wakili wake aliye chini humo anasema.

Wakili huyo Paul Bekaert, hakuzungumzia ripoti kuwa Bw. Puigdemont anajiandaa kuomba kupewa hifadhi.

Mwendesha mashtaka nchini Uhispania ametaka mashataka ya uasi kufunguliwa dhidi yake na viongozi wengine ya kura ya maoni iliyopogwa marufuku.

Serikali ya Uhispania ilichukua udhibiti kamili wa Catalonia siku ya Jumatatu, kuchukua mahala pa viongozi waliofutwa.

Ilifuta utawala wa eneo hilo na kuitisha uchaguguzi mpya baada ya Bw Puigdemont na serikali yake kujitangazia uhuru wiki iliyopita.

Wakili huyo wa Ubelgiji Paul Bekaert alisema kuwa Bw. Puigdemont kwa sasa yuko mji mkuu wa Ubelgiji Brussels.

Mbona Puigdemont akaenda Ubelgiji?
Uhispania ilikuwa imekumbwa na mzozo wa kikatiba tangu kura ya maoni iliyopangwa na serikali ya Bw. Puigdemont, ilipoandaliwa tarehe mosi Oktoba kinyume na amri ya mahakama iliyoamua kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na katiba.

Serikali ya Ctalonia ilisema kuwa asilimia 43 ya wapiga kura walishiriki huku asilimia 90 ya wapiga kura hao wakiunga mkono uhuru

Siku ya Ijumaa bunge la Catalonia likatangaza uhuru, Kisha waziri mku wa Uhispania akatangaza kuvunjwa kwa bunge la eneo hilo na kuondole kwa Bw. Puigdemont kama kiongozi wa Catalonia.

Sababu za kukamatwa Zitto hizi hapa



JESHI la Polisi linaendelea kumshikiria Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa mahojiano kwa kosa ya kutoa kauli za uchochezi katika mkutano wa hadhara alioufanya Kata ya Kijichi, Temeke,

Zitto alikamatwa mapema leo asubuhi nyumbani kwake na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Chang’ombe kwa mahojiano kwa makosa hayo ambayo anadaiwa kufanya katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani wa kata ya Kijichi.

Kwa mujibu wa viongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto anahojiwa kwa kutoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani kwa wananchi na kujenga chuki kwa serikali yao.

Maneno hayo yaliyopelekea Zitto kushikiliwa na kuhojiwa ni pamoja na kusema: “Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.”

Zitto pia anadaiwa kusema: “Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.”

Timu ya mawakili wa chama cha ACT-Wazalendo na ndugu na jamaa wa Zitto wapo pamoja naye katika mahojiano hayo na wataendelea kutoa taarifa kila kinachoendelea

900 wasimamishwa shule, kisa binti mmoja

900 wasimamishwa shule, kisa binti mmoja


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, karibu wanafunzi 900 wa Shule ya Sekondari Kabale katika Manispaa ya Kabala nchini Uganda wamesimamishwa masomo kutokana na vurugu kubwa zilizoibuka shuleni hapo, chanzo kikielezwa ni kumgombea kimapenzi binti mmoja ambaye pia ni mwanafunzi shuleni hapo.

Wanafunzi hao waliibua vurugu kubwa na kuanza kupigana mchana wa Ijumaa iliyopita shuleni hapo. Inaelezwa kuwa, mwanafunzi wa kidato cha sita aliomba kuwa na uhusiano na binti ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi mwingine wa kidato cha nne.

Kutokana na kuvuja kwa taarifa hizo, makundi mawili ya wavulana hao yaliibua uhasama ulioishia kupigana. Ugomvi huo haukuishia kwa wanafunzi tu, waliharibu pia mali za shule na hata za majirani wanaoishi karibu na shule hiyo.

Kutokana na hali hiyo, jeshi la Polisi lililazimika kuingilia kati kutuliza ghasia kwa kutumia mabomu ya machozi na silaha nyingine kutawanya wanafunzi hao. Kaimu Ofisa anayeshughulikia usalama wilayani Kabale, Kenneth Birungi amethibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kuongeza kuwa, timu ya wanausalama baadaye ilikutana na uongozi wa shule na kukubaliana kuwasimamisha masomo wanafunzi hao, huku Bodi ya Shule ikitarajiwa kutoa uamuzi juu ya hatima yao.

Jokate kuachana na mambo ya muziki

Jokate kuachana na mambo ya muziki


MWANAMITINDO na msanii wa Bongo Fleva, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa, ‘soon’ ataachana na muziki huo, bila kutaja sababu ya kufanya hivyo.

Jokate aliiambia Full Shangwe kuwa, anajipanga kuachia wimbo mmoja wa mwisho kisha anaachana kabisa na Bongo Fleva.

“Nafikiria kutoa wimbo moja wa mwisho, halafu baada ya hapo nitakuwa nimestaafu kufanya muziki, sina sababu ya msingi ila ni maamuzi yangu tu,” alisisitiza Jokate.

Aliyepanga kumuua Rais wa Urusi ajeruhiwa






Amina Okuyeva na mumewe walipigana dhidi ya makundi yanayoiunga mkono Urusi

Mwamamue moja kutoka Chechenia ambaye analaumiwa kwa kupanga kumuua rais wa Urusi Vladimir Putin amejeruhiwa na mke wake kuuliwa wakati wa shambulizi karibu na mji mkuu wa Ukrain Kiev.

Adam Osmayev alijeruhiwa lakini anaweza kuishi baada ya gari alilokuwa akilitumia kumiminiwa risasi kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya ukrain.

Wizara hiyo ilisema kuwa mke wake Osmaye, Amina Okuyev aliuawa wakati wa shambulizi katika kijiji cha Hlevaha.

Mwaka 2012 maafisa nchini Urusi walisema kuwa Bw. Osmayev alikuwa sehemu ya njama ya wanamgambo kumuua Bwa Putin.

Vyombo vya habari vya Urusi viliripoti wakati huo kuwa watu walipanga kutega mabamu kwenye barabara ya Kutuzovsky mjini Moscow, inayotumiwa na Bw Putin kila siku.

Urusi baadaye iliitaka Ukrain kumsalimisha Bw. Osmayev lakini mamlaka nchini Urusi zikakataa kufanya hivyo, zikisema kuwa zilitaka kungoja hadi mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya kuamua kuhusu ombi lake la kupinga kusalimishwa kwa Urusi.

Mwezi Juni alinusurika jaribio la kumuua mjini Kiev. Mshambuliaji kisha akapigwa risasi na kujeruhiwa na Bi Okuyeva.

Hii inakuja chini ya wiki moja baada ya mbunge wa Ukrain kujeruhiwa kwenye shambulizi la bomu kwenye mji mkuu Kiev.

Mlinzi wa Ihor Mosiychuk na mtu mwingine waliuawa wakati wa mlipuko huo.

Bi Okuyeva wakati moja alifanya kazi kama mshauri wake

Nafasi za kazi leo October 31

Mwakibinga amfananisha Zitto Kabwe na Harmorapa




KIJANA kutoka Kundi la Vijana Wazalendo nchini, James Mwakibinga, amekuja juu na kumshukia kiongozi wa Chama cha Act- Wazalendo, Zitto Kabwe na kusema anatafuta kiki kama Harmorapa kwa kupingana na kasi ya Rais Dk .John Pombe Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi uliofanyika katika madini nchini.

Mwakibinga amesema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa mambo yanayofanywa na kiongozi huyo siyo ya kizalendo na hayafai kufumbiwa macho na mtu yoyote mwenye akili na mwenye dhamira ya kweli kwenye taifa lake.

“Nadiliki kusema kuwa game changer amebadilisha mchezo hivyo wanasiasa wanashindwa kufanya kazi katika majimbo yao na kazi yao imekuwa kufanya upotoshaji  juu ya kazi zilizofanywa na Rais Dk John Pombe Magufuli hasa katika swala zima la kuokoa mali za Watanzania katika sekta ya madini,” amesema Mwakibinga.

Amesema Zito anatakiwa kufanya siasa za kistaarabu na kuacha kupayuka tu kwani hii ni miaka miwili bado mitatu hivyo zama hizi zimebadilika hakuna utaratibu tena wa mashirika kuwahonga viongozi wa kisiasa.

Mwakibinga amesema kuwa vijana wazalendo wako nyuma yake watamlinda na kusimamia misingi yote ya kulinda rasilimali za wananchi zisiendelee kuibwa.