Monday, 16 October 2017

Rais Magufuri Apongezwa

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana wa UVCCM Taifa Shaka Hamidu, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kurejesha mwamko ndani ya chama.
Shaka amesema kuwa katika uongozi wa Rais Magufuli kama Mwenyekiti wa Chama cha CCM, UVCCM imeweka rekodi ya kupokea maombi mengi zaidi ya watu wanaowania nafasi ya Uenyekiti Taifa kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Jumla ya vijana 113 kutoka Tanzania bara na Zanzibar wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.
“Katika uongozi wa Dkt, Magufuli akiwa Mwenyekiti wa chama limekuwa ni jambo la historia inaonyesha jinsi gani vijana wamekuwa na mwamko na hamu ya kukitumikia chama, kwakweli anastahili pongezi na hizi ni dalili nzuri kwa Chama”, amesema Shaka.
Kwa upande mwingine Shaka amesema hivi sasa zoezi linaloendelea ni usaili wa wagombea wote walioonesha nia ya kuwania uongozi ili kuwabaini na kuwapitisha wenye sifa sitahiki. Moja ya sifa kuu ya kugombea uongozi ndani ya UVCCM ni kuwa na miaka 30 au chini ya hapo ili katika uongozi wako usizidi miaka 35 kwani kila awamu ni miaka mitano.
Nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo ambao mchakato wake umeanza tangu mwezi April kwa ngazi za Shina na Tawi ni Mwenyekiti, na Makamu wake, Wajumbe watano wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC), wajumbe watano wa baraza kuu la umoja huo Taifa na wawakilisha wa Jumuiya hiyo katika Jumuiya nyingine ndani ya chama.

Ibrahim Ajib Namba 10 Amekuja yanga wakati muafaka,,,

WAKATI mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC walipoichapa KageraSugar FC 2-1 katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba Jumamosi iliyopita na ‘kufunga’ gepu la pointi na viongozi wa ligi, kiungo-mshambulizi, Ibrahim Ajib ameendelea kuwathibitishia mashabiki wa klabu hiyo kuwa hahitaji sana muda ili kuanza kuwaonyesha ‘thamani’ yake.
Yanga ilikuwa timu pekee kati ya 16 kupata ushindi katika michezo ya mzunguko ya sita na alama hizo tatu walizozipata ugenini zimewafanya kufikisha pointi 12 sawa na Simba SC, Mtibwa Sugar FC na Azam FC ambao wote walishindwa kupata ushindi wakati michezo saba ya raundi hiyo ilipomalizika kwa matokeo ya sare/suluhu.
Magoli matatu ya Ajib, pointi 9 za Yanga
Yanga imeangusha pointi mbili tu katika michezo mitatu waliyocheza ugenini hadi sasa. Wamefanikiwa kufunga katika viwanja vya Sabasaba, Njombe (goli moja), Majimaji, Songea (goli moja) na wikendi iliyopita walipandisha kiwango chao kiufungaji kwa mara ya kwanza msimu huu walipofanikiwa kutikisa nyavu za golikipa Juma Kaseja mara mbili.
Ajib amehusika katika magoli matatu kati ya manne ambayo timu yake imefunga ugenini, huku akiongoza chati ya ufungaji katika kikosi hicho cha kocha Mzambia, George Lwandamina akiwa na magoli matatu kati ya sita ambayo timu yake imefanikiwa kufunga katika michezo sita iliyopita katika VPL.
Alifunga goli lake la kwanza akiwa mchezaji wa Yanga na kuisaidia timu yake kushinda 1-0 dhidi ya Njombe Mji FC. Goli hilo ni la kwanza la mpira uliokufa msimu huu. Akafunga tena katika ushindi wa 1-0 vs Ndanda FC katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Na sasa ametoka kufunga goli lake la tatu katika michezo sita ya ligi kuu, huku akipiga pasi ‘ya video’ kwa Obrey Chirwa aliyefunga goli la kwanza vs Kagera Sugar.
Hadi sasa Ajib amekuwa na mchango mkubwa sana katika kikosi cha Yanga hasa wakati huu ambao safu yao ya mashambulizi inatetereka kutokana na majeraha ya mara kwa mara yanayowaandama, Mrundi, Amis Tambwe, Mzimbabwe, Donald Ngoma na Chirwa.
Kuendelea kwake kufunga magoli kunaipa nafasi timu yake kuendelea kupanda juu kimsimamo kwani licha ya kufunga magoli sita tu katika michezo sita iliyopita ila safu ya ulinzi imekuwa imara na hata magoli matatu waliyoruhusu hadi sasa hajawaathiri sana.
Ajib ni namba 10
Uwepo wa Pius Buswita katika kikosi cha Yanga hivi sasa kumekumeongeza ufanisi wa timu katika utengenezaji wa nafasi. Buswita anaenda sana kurahisisha mpira kwa pasi zake zake fupifupi za ‘one-two’. Katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar kocha Lwandamina aliwapanga washambuliaji wawili-Ajib na Chirwa.
Upande wa kushoto alimpanga Geofrey Mwashuiya, Buswita akawa anaibia katika wing ya kulia-huku akisogea sana katikati wakati wakishambulia ili kumpa nafasi beki namba mbili Juma Abdul kupanda kwa ajili ya kupiga krosi pasi.
Ajib alikuwa akipata uhuru wa kushuka hadi eneo la kati la kuichezesha timu kama vile ni kiungo mchezeshaji, alipiga pasi ya juu ya kupenyeza akitokea na mpira eneo la kati na mpira ule aliuchopu na ukaangukia nyuma ya walinzi wa Kagera Sugar, Juma Nyosso na patna wake Juma Shemvuli, na kitendo cha wao kugeuka wakamkuta tayari Chirwa anautazama mpira uliodondoka mbele yake huku golikipa Kaseja akisubiri nini atafanya.
Nimeandika makala kadhaa na nimekuwa nikisisitiza Lwandamina anapaswa kutumia washambuliaji wawili wa kati wakati huu ambao nyota wake wa mashambulizi wakipambana na majeraha. Na faida niliyokuwa naitaraji ndiyo ile ambayo Ajib alionyesha. Kupiga pasi za mwisho zisizotarajiwa akitokea kati mwa uwanja, na kufunga magoli muhimu.
Baada ya kumalizika kwa mchezo wa Kagera Sugar naamini sasa, Lwandamina atakuwa amemshuhudia namba kumi bora ambaye anaweza kucheza vizuri sambamba na Chirwa au Tambwe ambao wanauwezo mkubwa wa kusimama na kutengeneza nafasi wakicheza kati zaidi. Hakika Ajib tayari ameanza kujibu matarajio ya wengi ambao waliamini angeweza kuyafanya baada ya kusajiliwa kutoka Simba msimu huu.
Alicheza akimzunguka Chirwa huku akili yake akionyesha kuwa na haraka katika kufikiria, huku akifikia maamuzi ya hatari kwa kila pasi yake iliyoelekea golini kwa timu pinzani. Aligusa mpira kiufundi, huku kiwango chake cha utendaji kazi kikiwa juu. Huyu ni namba 10 sahihi aliyekuja Yanga katika wakati mwafak

Akamatwa Akisafirisha mabomu kwenye madumu ya maji,,,,

Askari walimshtukia kijana huyo baada ya kupita kwenye vituo vitatu bila kusimama huku gari hilo likielekea kwenye kambi ya majeshi ya Umoja wa Mataifa kwa spidi kali.
Polisi mjini Kabul wamesema walitumia nguvu kubwa kumsimamisha kwa kulishambulia gari lake kwa risasi.
Kijana huyo akiwa mikononi mwa wanajeshi wa UN.
Wanajeshi wa UN nchini humo wamesema kuwa mabomu hayo yalichanganywa na mbolea na kuwekwa kwenye madumu huku mengine yakiwa kwenye maboksi ya nyanya hii ni baada ya kufanyiwa ukaguzi.
Hata hivyo, mpaka sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lilitoa tamko juu ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa UN nchini Afghanistan mamia ya raia wanauawa kila mwezi na makundi ya kigaidi ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Septemba watu 1,584 wameshauawa kwenye matukio mbalimbali ya mashambulizi ya kigaidi.

Zitto amkumkumbuka Mh. Filikunjombe ‘Ni majaribu makubwa kukubali kuwa haupo nasi’

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amemkumbuka marehemu Mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe ambae alifariki dunia baada ya helikopta aliyokuwa akiitumia kwaajili ya kampeni kupata ajali kwenye msitu wa Selous.
Mbunge Zitto amesema kuwa Filikunjombe alikuwa rafiki yake na ndugu yake hivyo bila uwepo wake ni majaribu makubwa.
Rafiki yangu, Ndugu yangu. Miaka miwili Sasa bila kuwa nawe. Ni majaribu makubwa kukubali kuwa haupo nasi. Mola akuweke mahala peponi. Naendelea kuombea familia moyo wa subira.
Ninakukumbuka Ndugu yangu Deo Haule Filikunjombe
Mhe. Deo Filikunjombe na abiria wengine walikuwa kwenye helikopta yenye namba 5Y-DKK wakitokea Dar kuelekea Ludewa.

Ndege ya AirAsia yageuka na kurudi Australia baada ya hofu ya hitilafu

Ndege ya shirika la Indonesia ya AirAsia imelazimika kugeuka na kurudi Australia baada ya marubani kujulishwa kuwa kulikuwa na tatizo la hewa katika eneo la abiria la ndege hiyo.
Ndege hiyo ya QZ535, iliyokuwa safarini kwenda kisiwa cha Bali nchini Indonesia, ilirudi Australia dakika 25 baada ya kupaa siku ya Jumapili.
Airbus A320 iliyokuwa na abiria 151 ilitua salama kwenye uwanja wa Perth, AirAsia ilisema kuwa ndege hiyo ilikumbwa na matatizo ya kiufundi, huku vyombo vya habari nchini Australia vikisema kuwa ilionekana kushuka.
Kanda ya video iliyorekodiwa na kupeperushwa na vyombo va hahari, ilionyesha vifaa vya hewa vikining'inia kutoka kwa dari la ndege.
AirAsia iliwaomba msamaha abiria kwa tatizo lolote lililosababishwa na hitilafu hiyo.
Mwezi Juni ndege ya AirAsia iliyokuwa safarini kwenda Bali, ililazimika kurudi uwanja wa Perth baada ya hitilafu ya injini yake kusababisha ndege hiyo kutingishika kama mashine ya kuosha.
Mwezi Disemba mwaka 2014 ndege ya AirAsia ilianguka baharini na kuwaua watu wote 162 waliokuwa ndani yake

Lissu Amfaliji Nyalandu,,,,

Baada ya kukaa hospitali kwa zaidi ya mwezi mmoja Lissu
akipatiwa matibabu, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amekiri kuona tabasamu la Mbunge huyo aliyepigwa risasi mwezi uliopita na kuwataka watanzania waendelee na maombi.
Kupitia mtandao wake wa Instagram Nyalandu amesema kwamba shauku aliyonayo Lissu ndani ya moyo wake ni kuiona siku iliyo njema pia kufurahia siku kila asubuhi.
Nyalandu ameandika "Tuendelee kumwombea ndugu yetu Tundu Lissu. Nimeliona tabasamu la uso wake leo, na hakika Mungu anaendelea kujibu maombi ya Watanzania, na wote wanaomkumbuka katika sala na dua zao katika majira na saa hii ya kujaribiwa kwake".
"Tusimame pamoja naye, kwa kuwa shauku ya moyo wake ni kuiona siku iliyo njema, aweze kuifurahia kila asubuhi kama apendavyo Mungu".
Lissu alipigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa wasiojulikana tangu Septemba 07 akiwa mjini Dodoma nje ya nyumba yake alipokuwa ametoka Bungeni kutekeleza majukumu yake na sasa bado yupo hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea na matibabu.

Mwanafunzi Aua wenzie 5 kwa Risasi,,,,

Wanafunzi watano na mlinzi wa shule wameuawa kwa kupigwa risasi na mwanafunzi mwenzao, huku wengine 17 wakijeruhiwa katika shule ya sekondari ya Lokichogio iliyopo kaunti ya Turkana, nchini Kenya.
Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki hii ambapo mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina la Abraham mwenye asili ya SUdan Kusini alikwenda shuleni akiwa na wenzake, na kuanza kuwamiminia risasi wanafunzi ambao walikuwepo kwenye shule hiyo, kwa kinachoaminika kuwa ni kulipiza kisasi baada ya kusimamishwa sule kwa utovu wa nidhamu.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanafunzi huyo alifanikiwa kuingia shuleni hapo baada ya kumuua mlinzi na kisha kuingia bwenini, na kufanya shambulio lililopelekea vifo hivyo na kujeruhi wengine.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema kuna ulazima wa kukagua wanafunzi wanaotoka maeneo ya karibu kabla hawajawasajili kwenye shule zao, ili kujiepusha na matukio kama hayo kuendelea kutokea.
Mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza alikamatwa na polisi akijaribu kukimbia kuelekea kwenye kambi ya wakimbizi ya SUdan Kusini, na kumpeleka kituo cha polisi, lakini baada ya muda wananchi walivamia kituo hiko na kukishambulia, wakitaka kumuua kwa mawe.
Kufuatia tukio hilo uongozi wa shule hiyo umetangaza kuifunga shule hiyo kwa muda, ili wanafunzi wakae sawa kisaikolojia, kufuatia kile walichokishuhudia.

Austria kumchagua kiongozi mwenye umri mdogo zaidi duniani,,,,,

Mkuu wa chama cha kihafidhina nchini Austria cha People's Party, Sebastian Kurz, anaelekea kuwa kiongozi wa taifa mwenye umri mdogo duniani, baada ya ushindi wake katika uchaguzi mkuu hapo jana.
Kurz aliye na umri wa miaka 31 amepungukiwa na uwingi , lakini yupo katika nafasi nzuri ya kuunda serikali ya muungano.
Haijulikani wazi iwapo atafikiria kuunda serikali ya muungano na chama kinachopinga uhamiaji Freedom Party, kilichoibuka nafasi ya tatu kwa kishindo katika uchaguzi huo.
Akihutubia wafuasi wake Bw Kurz alisema: "Ni wakati wa kuleta mabadiliko kati nchi hii. Leo ni siku muhimu kwetu kuibadilisha nchi hii na ninasema asante kwa wale wamewezesha hili".
"Nina furaha, nimejitolea kuifanyia kazi Austria."
Sebastian Kurz ni nani?
Kabla ya uchaguzi Bw. Kurz lihudumu kama waziri mwenye umri mdogo zaidi wa mashauri ya nchi za kigeni barani ulaya, baada ya kuteuliwa mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 27.
Mwezi Mei mwaka 2017 akawa kiongozi wa chama cha People's Party. Alianza taaluma yake ya siasa katika tawi la vijana wa chama kabla ya kwenda kuhudumu katika baraza la manispaa la mji wa Vienna.
Akipewa jina "Wunderwuzzi" linalomaanisha mtu anayeweza kutembea juu ya maji, amefananishwa na viongozi vijana wa Ufaransa na Canada, Emmanuel Macron na Justin Trudeau.
Sawa na Macron, Bw Kurz amejiundia wafuasi wanaomzunguka, kukibadilisha chama cha People's Party, ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 30

Muda wa kiongozi wa Catalonia kutangaza msimamo waelekea kuisha

Kiongozi wa eneo la Catalonia amesalia na saa chache kabla ya kumalizika muda wa mwisho uliowekwa na serikali kuu kuthibitisha wazi ikiwa ametangaza uhuru au la.
Ikiwa atakiri kuwa ametangaza, atakuwa na hadi Alhamisi kufuta tangazo hilo au Catalonia ambayo imekuwa ikijisimamia iongozwe moja kwa moja na Uhispania, Tarehe ya mwisho iliyotolewa kwa Carles Puigdemont ni leo 08:00 GMT.
Baada ya kura ya maoni ya uhuru wiki mbili zilizopita ambayo ilitangazwa kuwa iliyo kinyume na sheria na mahakama ya katiba ya nchi hiyo, Bw Puigdemont alisaini tangazo la uhuru lakini akafuta kutekelezwa kwake, Alisema alitaka mazungumzo na serikali ya Madris lakini hilo halijafanyika.

7,602 wakutwa na saratani ya shingo ya kizazi

Jumla ya wanawake 187,267 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi huku 7,602 wakipatiwa matibabu katika mradi uliofadhiliwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates baada ya kukutwa na ugonjwa huo.
Mradi huo uliokuwapo kwa miaka mitano ulikuwa ukitekelezwa na taasisi za Marie Stopes Tanzania (MST), Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (Umati) na PSI.
Akizungumza wakati wa kufunga mradi huo juzi, Mkurugenzi Mkazi wa MST, Anil Tambay alisema idadi hiyo ya wanawake imetoka katika mikoa 22 ambako mradi huo ulikuwa ukitekelezwa.
“Mradi huu ulijikita kupunguza athari za saratani na shingo ya kizazi kwa wanawake, tumefanya uchunguzi na kutoa matibabu,” alisema Tambay.
Alifafanua kuwa wakati wa kuanza kwa mradi huo walitoa mafunzo na kupata watoa huduma 210 waliohudumia vituo 79 vilivyoanzishwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Afya ya Uzazi wa Wizara ya Afya, Dk Hussein Kidanto alisema asilimia 38 ya wagonjwa waliofika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road mwaka 2015 walikuwa na saratani ya shingo ya kizazi.

Uchaguzi Liberia: Weah na Boakai kuelekea duru ya pili ya uchaguzi wa rais

Nyota wa zamani wa soka George Weah na makamu wa rais Joseph Boake, wanaelekea duru ya pili ya uchaguzi kwenye uchaguzi wa rais nchini Liberia.
Karibu matokeo yote kwenye uchaguzi wa siku ya Jumanne yamehesabwa, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.
Bw. Weah ambaye ni mwafrika wa kwanza kushinda tuzo la kandanda la Ballon D'Or, anaongoza kwa asilimia 39 huku Bw. Boakai akiwa wa pili kwa asilimia 29, Duru ya pili kati ya wawili hao inatarajiwa mwezi ujao.
Wanaongoza wagombea wengine 20 ambao wanataka kuchukua nafasi ya Ellen Johnson Sirleaf, mwanamke wa kwanza kuchaguliwa rais barani Afrika na mshindi wa tuzo la amani la Nobel, Weah na Boakai wote walikuwa wametabiri kuwa wangeshinda duru ya kwanza.
Meneja wa zamani wa Bw. Weah akiwa mcheza kandanda, Arsene Wenger, mapema wiki iliyopita alipotoshwa na habari kuwa Weah tayari alikuwa amechaguliwa rais.

Rais MagufuliJP atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya KADCO, Balozi Kibelloh



Mchezaji afariki kwa kugongana uwanjani Indonesia

Mlinda mlango wa klabu ya ligi kuu ya Indonesia amefariki baada ya kugongana na mchezaji mwenzake uwanjani.
Choirul Huda, mwenye miaka 38, alikimbizwa hospitalini siku ya Jumapili lakini muda mfupi baadae ilitangazwa kwamba amefariki dunia.
Katika taarifa iliyotolewa na tovuti ya klabu yake Persela FC , daktari wa timu Yudistiro Andri Nugroho amesema mchezaji huyo alifariki baada ya kupata madhara makubwa kifuani.
Anasema mgongano huo ulisababisha kushindwa kupumua kwa Huda.
Ameongeza kuwa madaktari walijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio, Mchezo huo uliisha kwa Persela kuifunga Semen Padang 2-0.
Maelfu ya mashabiki wamefika hospitalini alipofia mchezaji huyo aliyecheza michezo 500 ya ligi kuu kwa klabu yake pekee.