Sunday, 10 December 2017

Kiongozi wa mamlaka ya wapalestina akataa kukutana na makamu wa rais wa Marekani



Kiongozi wa mamlaka ya wapalestina Mahmud Abbas hatokukutana na  makamu wa rais wa Marekani Miğke Pence katika ziara yake Mashariki ya Kati.

Mshauri wa nmasula ya kisiasa wa Mahmud Abbas  Bwana Majdi Haldi amesema kuwa uamuzi huo wa kiongozi wa mamlaka ya wapalestina kutokuonana na makamu wa rais wa Marekani umechukuliwa kufuatia uamuzi wa Trump kutangaza kuwa seirikali yake anatambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Mike Pence anatarajiwa kufanya ziara Palestina ili kuzungumzia  mazungumzo ya amani.

No comments:

Post a Comment