Friday, 15 December 2017

Canavaro kumbe hana wasiwasi na Simba

Beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema licha ya Simba kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, lakini bado kikosi chao kina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa.

Canavaro amesema tofauti ya pointi mbili kati yao na Simba wanaongoza ligi ni kitu kilicho ndani ya uwezo wao kuiweza kuwashusha na sasa wanajipanga vyema kwa hatua hiyo.

Mkongwe huyo alisema mazoezi wanayofanya sasa ni maalum kwa kuhakikisha ligi itakavyoanza wanakuwa tayari ambapo endapo wenzao waliokuwa katika Micchuano ya Kombe la Chalenji watajiunga mapema watakuwa na maandalizi kamili kwa ligi.

Beki Yanga awapasha wakosoaji



 

Beki Yanga awapasha wakosoaji

Beki wa Yanga Juma Abdul amesema matokeo mabaya waliyopata kikosi cha Kilimanjaro Stars, Watanzania hatupaswi kulaumiana bali tunatakiwa kujiuliza tulipokosea.

Abdul ambaye amewahi kuitumikia timu hiyo, amesema hakuna sababu ya kuendeleza lawama kwa makocha na watu wengine, ambapo tathmini ya kina inatakiwa kufanyika kujua wapi tulipokosea kama nchi katika soka letu.

Aidha Abdul amesema bado hajafikiria kuitumikia timu ya taifa, lakini ataendelea kujituma ili kusubiri kuitwa kwa mara nyingine na makocha wa timu za taifa.


Askari mbaroni kwa kumuua mwenzake kisa 'mapenzi

Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia kwa mahojiano askari Magereza wa Gereza la Kisongo jijini Arusha, Koplo Faustine Masanja kwa tuhuma za kumuua mwenzake wakiwa kazini.

Akizungumza na Vyombo vya Habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa limetokea Desemba 14,2017 majira ya saa 2:00 asubuhi.

Kamanda Mkumbo amesema baada ya Masanja kumjeruhi mwenzake kwa risasi, alipelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu ambako alifariki dunia.

Mkumbo ameahidi kutoa taarifa zaidi baada ya uchunguzi kukamilika ili kubaini chanzo na sababu za tukio hilo. Ingawaje taarifa za awali zinaonesha kuwa tukio hilo linaviashiria vya wivu wa mapenzi.

Pogba kurudi dimbani na muonekano mpya


Pogba kurudi dimbani na muonekano mpya 

 

Pogba kurudi dimbani na muonekano mpya

Mshambuliaji  wa Manchester United, Paul Pogba anayetumiakia adhabu ya kukosa mechi tatu, amegeukia mitindo ya nywele ambapo ameonekana akiwa amekoleza rangi kwenye kiduku chake.

Mchezaji huyo aliikosa mechi ya watani ya Manchester United na Manchester City Jumapili iliyopita na hakuwepo kabisa uwanjani. Pia ameikosa mechi ya United na Bournemouth.

Jana Alhamisi, mchezaji huyo mwenye mika 24 alituma picha yake akionyesha mtindo mpya wa nywele kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akijifua mazoezi binafsi ili kuhakikissha anajiweka fiti na mechi zinazofuata.

Thursday, 14 December 2017

Haya ndio majina ya Askari wa JWTZ waliouawa DRC



Haya ni majina ya wanajeshi 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliouawa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wakilinda amani.

Wanajeshi hayo ni  Hamad Haji Bakari, Chazil Khatibu Nandonde, Idd Abdallah Ally, Juma Mossi Ally,  Ally  Haji Ussi, Pascal Singo, Samwel Chenga, Deogratius Kamili, Mwichumu Vuai Mohamed, Hassan Makame, Issa Mussa Juma, Hamad Mzee Kamna, Salehe Mahembano na Nazoro Haji Bakari.

Tayari miili ya marehemu hao imeshaagwa katika viwanja vya ulinzi vilivyopo makao ya jeshi yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wa Serikali wengine waliongoza Watanzania kutoa heshima za mwisho kwa askari hao.

Askari hao 14 walifariki dunia katika mapigano na waasi wa kikundi cha ADF nchini DRC, huku 44 wakijeruhiwa na mmoja akipotea baada ya kambi yao kuvamiwa eneo la Mashariki mwa nchi Desemba 7 wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani.

Kinana awaonya Viongozi wanaowagawa Wananchi



Singida. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewaonya viongozi wa chama hicho ambao amesema wanawagawa wananchi.

Amesema endapo wataendelea kufanya hivyo watavuliwa uongozi.

Kinana amesema hayo leo Alhamisi Desemba 14,2017 akifungua mkutano wa halmashauri kuu ya jimbo unaopiga kura ya maoni kupata mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini.

Katika kinyang’anyiro hicho cha marudio wagombea 22 wamejitokeza kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Lazaro Nyalandu aliyejivua ubunge alioupa akiwa CCM na sasa amejiunga Chadema.

Amesema CCM ipo imara na wapambe wamepungua kwa kiasi kikubwa. Amewataka wagombea wafanye kampeni zinazofaa na mmoja akichaguliwa, wote wawe wamoja ili chama hicho kishinde kwa kishindo.

Kinana akizungumza katika mkutano huo unaofanyika Kijiji cha Ilongero, Singida amesema uchaguzi wa awali uligubikwa na vitendo vya rushwa ndipo uongozi wa juu wa CCM ulipoamua kufuta mchakato.

Ameagiza vitendo hivyo visijirudie akiwataka wajumbe wasirubuniwe kwa aina yoyote; na wagombea wakatae maombi ya wapiga kura ambao mara nyingi huwaambia unatuachaje.

Kinana amempongeza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Hassan Kilimba akisema amekuwa mwaminifu kwa chama hicho hata baada ya kuacha ubunge.

Waziri Nchemba amaliza mgogoro wa Ardhi uliodumu miaka 9 Kondoa


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumaliza mgogoro wa ardhi ambao umedumu kwa miaka zaidi ya tisa ambao ulifikia hadi kuhatarisha amani ya kijiji cha Hurui katika kata kikole jimbo la kondoa vijijini wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma.

Mgogoro huo ambao umesababishwa na baadhi ya watu ambao si wajumbe wa kijiji kuuza eneo la kijiji la malisho mwaka 2009 bila mkutano wa kijiji kushirikishwa na kusababisha hali ya sitofahamu mpaka leo. Jitihada za wananchi kutafuta haki ya eneo hilo kwa njia za kisheria hazikuzaa matunda kwani walishindwa katika kesi zote mbili walizofungua katika Mahakama ya ardhi ya wilaya na mkoa hali iliyopelekea sasa mbunge wa jimbo la kondoa vijijini Dr Ashatu Kijaji kumwita waziri wa mambo ya ndani kusaidia kutuliza taharuki hiyo.

Waziri Dr Mwigulu Nchemba baada ya kusikiliza pande zote za kijiji na serikali ya wilaya ameagiza eneo hilo liendelee kutumika kama lilivyopangwa tangu mwaka 1972 kuwa eneo la malisho, amewataka wananchi na viongozi wa vijiji waache kuuza maeneo kinyemela kwani ndio chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi katika vijiji nchini.

Naye mbunge wa jimbo la kondoa vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa fedha Dr ashatu kijaji amesema amechoka na migogoro ya ardhi katika jimbo lake,yule ambaye atawafikisha katika migogoro watashughulika naye kwa sheria na taratibu za nchi.

Aidha Dr Ashatu amesema kuwa kwasasa hawawezi fanya shughuli za maendeleo katika baadhi ya vijiji kama kujenga madarasa na miundombinu ya maji na umeme kwasababu ya migogoro ya ardhi iliyopo hivyo kwasasa migogoro basi ili wafanye kazi huku akimshukuru Mkuu wa wilaya kwa jitihada kubwa zakusaidia kumaliza migogoro hiyo anayoonyesha

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Hurui Ramadhani Selemani amesema migogoro hiyo imeletwa na baadhi ya wajumbe wa serikali ya vijiji waliopita kwa kuuza maeneo zaidi ya ekari 52 ya malisho bila kushirikisha mkutano wa kijiji hali ambayo imeleta mgogoro mkubwa na kuhatarisha amani ndani ya kijiji.

Wananchi wa kata ya kikole wamemshukuru waziri wa mambo ya Ndani ya nchi kwa kuwarudishia maeneo yao kwani kwasasa amani itarudi tena katika kata yao na maendeleo yatakuja kwani watafanya shughuli kwa amani

Takwimu NBS; Tatizo la ukosefu wa ajira lapungua mwaka hadi mwaka



Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema tatizo la ukosefu wa ajiri nchini limepungua.

Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu, NBS Irineus Ruyoby amesema kwa mujibu wa takwimu walizonazo kwa sasa zinaonyesha tatizo la ukosefu ajira linaenda likipungua mwaka hadi mwaka.

“Takwimu ambazo tunazo zinaonyesha kiwango cha watu ambao hawaja ajiriwa kimepungua mwaka hadi mwaka, sasa hivi tupo katika kufanya tafiti nyingine tutaweza kujua hali halisi sasa ikoje” amesema.

Ameongeza kuwa uchumi wa Tanzania kwa sasa unaendelea kukua kwa kiwango cha wastani wa asilimia saba kwa mwaka na imekuwa hivyo kwa muda mrefu sasa

Kidoa Adaiwa Kurudi kwenye Ufuska,,,



MSANII wa filamu Bongo Asha Salum ‘Kidoa’ ambaye kwa kipindi kirefu alipoa kama maji ya mtungi kutokana na mwandani wake kumpiga ‘stop’ mambo ya kifuska ikiwemo kupiga picha za nusu utupu, amedaiwa kurejea kwenye vitendo hivyo baada ya kumwagana na jamaa huyo.
Kwa mujibu wa chanzo, Kidoa awali alikuwa machachari lakini alivyompata pedeshee ambaye ni kigogo wa serikali
alimpiga ‘stop’ mambo ya kifuska ikiwemo kuuza sura mitandaoni akiwa nusu utupu, pamoja na skendo kwenye vyombo vya habari.
Baada ya kunasa ubuyu huo, mwanahabari wetu alipomtafuta Kidoa, aliangua kicheko na kusema: “Watu wanapenda sana kufuatilia maisha yangu, najua hayo yote yameibuka baada ya kuweka picha Instagram nikiwa na nguo za ndani pekee, mavazi hayo nilikuwa nayapenda kitambo na picha zangu nyingi zilikuwa za hivyo, nikaamua tu nipumzike, si kwamba nimeachwa.”
Kama hujeelekezwa kiotomatiki, bofya

Miezi 11 Mbeya, Songwe yaongoza kwa vifo kwa Kipindupindu



Dar es Salaam. Watu 3,739 wameugua na wengine 71 kufariki dunia kutokana na kipindupindu katika kipindi cha miezi 11 iliyopita, huku mikoa ya Mbeya na Songwe ikiongoza kwa vifo.
Takwimu hizo za Januari hadi Novemba zinaonyesha mkoa wa Mbeya umekuwa na wagonjwa 710 na vifo 14 huku Songwe ikiwa nao wagonjwa 538 na vifo vinne.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu jana aliitaja mikoa mingine iliyoathirika zaidi kuwa ni Morogoro (320 na vifo 11), Dar es Salaam (320 na vifo vitano) Iringa (332 na vifo tisa), Kigoma (314 na vifo vinne). “Takwimu zinatuonyesha bado maambukizi mapya ni tishio kwani kuna ongezeko la idadi ya mikoa na halmashauri zinazotoa taarifa za wagonjwa japokuwa idadi imepungua mwishoni mwa mwaka,” alisema.
Ummy alisema takwimu za tangu mwaka huu uanze zinaonyesha ongezeko la ugonjwa ambapo mikoa 17 ilitoa taarifa za kuwapo kwa wagonjwa.
Hata hivyo, waziri alisema mikoa saba haikuripoti kuwa na ugonjwa huo ikiwamo Mwanza, Shinyanga, Arusha, Lindi, Kagera, Simiyu, Kilimanjaro na Mtwara.
“Nchi yetu inaelekea katika majira ya mvua ambazo zinaweza kuongeza kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu, hivyo tunahitaji kuzidisha juhudi za kuzuia kwa kusimamia kikamilifu maelekezo na miongozo stahiki inayotolewa,” alisisitiza.
Waziri huyo aliwataka wananchi kujenga na kutumia vyoo bora katika maeneo ya makazi, kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kabla ya kula, baada ya kutumia choo na baada ya kuwasafisha watoto waliojisaidia.
“Mamlaka za maji zilizopo nchini zihakikishe upatikanaji wa majisafi na salama kwa wananchi, kunywa majisafi na salama yaliyotakaswa kwa dawa (kama vile water guard) au yaliyochemshwa na kupoa,” alisema.
Ugonjwa wa kipindupindu unachangiwa pia na kutokuwa na vyoo bora, huku ofisa mtendaji wa Kijiji cha Humekwa kilichopo Chamwino mkoani Dodoma, Ashrey Myogoya akisema kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira yenye kaulimbiu “usichukulie poa nyumba ni choo” imesaidia kwa kuwa mpaka sasa kaya zote 349 zina vyoo vilivyoboreshwa. Mkazi wa kijiji hicho, Cecilia Isaya alisema choo chake amekijenga kwa gharama ya Sh55,000.
“Si gharama kubwa nimetumia kwani baadhi ya vifaa nimenunua lakini vingine nimetengeneza mwenyewe ikiwamo matofali,” alisema.
Kama hujeelekezwa kiotomatiki, bofya
hapa .

Wednesday, 13 December 2017

Real kumng’oa neymar psg


Timu ya Real Madrid inaripotiwa wamefikia makubaliano na staa wa Paris Saint-Germains, Neymar, ili akajiunge nayo ifikapo mwishoni mwa msimu ujao.

Mbrazili huyo amekuwa mchezaji ghali zaidi duniani majira ya joto msimu huu baada ya kuhamia PSG akitokea Barcelona kwa uhamisho wa pauni milioni 200.

Licha ya kuanza vizuri msimu huu akiwa na PSG baada ya kufunga mabao 15 na kutoa pasi zilizozaa mengine 11 katika mechi 18 tu, tetesi zimeibuka zikidai kuwa Neymar hana furaha kamili katika mazingira yake mapya.

Ripoti kutoka kwenye chanzo cha habari nchini Hispania Diario Gol, zinadai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekubaliana na Real Madrid na anatarajiwa kutua Bernabeu mwishoni mwa msimu wa 2018-19.

“Neymar anatamani sana kushinda tuzo ya Ballon d’Or na anaamini kuwa atakuwa na nafasi nzuri kutimiza ndoto zake akiwa katika Jiji Kuu la Hispania,” kilieleza chanzo hicho.

Manchester United na Manchester City pia zinasemekana zinavutiwa na mchezaji huyo, ambaye mkataba wake Parc des Princes utafika ukomo mwaka 2022.


Sababu za Wapinzani kuhamia CCM hizi hapa

Sababu za Wapinzani kuhamia CCM hizi hapa

New VIDEO: J Gold Wenga – Yonella

New VIDEO: J Gold Wenga – Yonella

New VIDEO: J Gold Wenga – Yonella

DOWNLOAD