Wednesday, 24 January 2018

New AUDIO | Lil Wayne – Big Bad Wolf

New AUDIO | Lil Wayne – Big Bad Wolf

New AUDIO | Lil Wayne – Big Bad Wolf

Lil Wayne is reloaded. As he prepares to drop Dedication 6: Reloaded, Weezy unleashes four minutes of freestyle fire in the form of “Big Bad Wolf.” Over a stripped-down beat, the Young Money boss huffs and puffs with bar after bar, barely coming up for air.

“When the shit get ugly, I go Pretty Ricky,” he spits. “I don’t fuck with rats, neither Minnie, Mickey / I don’t fuck with cops, that’s the piggly wiggly / Fuck my bitch’s friends and they friendly friendly.”

D6: Reloaded serves as the follow-up to Wayne’s DJ Drama-hosted mixtape Dedication 6, which arrived on Christmas Day and featured collaborations with Nicki Minaj and Zoey Dollaz. He is also fresh off collaborations with DJ Spin and Whiiite, Hot Boy Turk, and Kodak Black.

Listen to Weezy blow the house in.


Majimaji yatua Dar kuvaana na Simba




KIKOSI cha Majimaji leo Jumatano kinatarajia kuingia jijini Dar ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuvaana na wapinzani wao Simba katika pambano la ligi ambalo litapigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa.

Majimaji wanaodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet, inatua Dar ikiwa na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo na Sim­ba ambapo mchezo wao wa mwisho waliilazimisha sare Singida United ya kufungana bao 1-1.

Kocha msaidizi wa timu hiyo iliyo katika nafasi ya 12, Habibu Kondo ame­liambia Championi Jumatano, kuwa wamekuja Dar kuhakikisha wanaendele­za mwendo wa kukusanya pointi kama walivyofanya kwenye michezo yao miwili ya mwisho dhidi ya Azam na Singida United kabla ya kuivaa Simba.

“Kesho (leo) Jumatano ndiyo tunatara­jia kufika huko Dar kwa ajili ya kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya kucheza na wenyeji wetu Simba, tunawaheshimu wapinzani wetu kama timu kubwa lakini tunataka kufanya vizuri mbele yao.

“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tumejipanga vyema kwa ajili ya kupata pointi mbele ya wenzetu hao, tunakuja tukiwa kamili kwa maana ya kikosi chote na siku chache ambazo tutakaa huko zitatufanya kuzoea mazin­gira kabla ya kupambana na wapinzani wetu,” alisema Kondo.

Jini Kabula aibuka, afunguka siri ya kunawiri kwake


BAADA ya mwaka jana kuugua na kwenda kupumzika kwao Mwanza na sasa kuonekana kuwa na hali nzuri, msanii wa filamu za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ameibuka na kuanika siri ya kunawiri kwake.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Jini Kabula alisema kunawiri kwake kunatokana na kupumzika kwa miezi mitatu bila mikikimikiki huku akila vinono nyumbani kwa kaka yake alikoenda kwa mapumziko na hivi karibuni ana mpango wa kurejea tena Dar kwa ajili ya kufanya biashara ili kujiendeshea maisha na siyo sanaa tena kwa sasa.

“Jamani kunawiri kwangu ni kwamba ninakula vinono kwa kaka yangu huku Mwanza, sina stress maisha yanaenda tu vizuri, nimeshapumzika miezi mitatu kama daktari alivyoshauri na ninajiandaa kurudi kwa ajili ya mishe nyingine za kimaisha,” alisema Jini Kabula.

Jaji Mkuu awataka Viongozi kutoingilia utendaji wa Mahakama


Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amewataka wanasiasa na viongozi wa serikali wenye mamlaka ya kikatiba na sheria kutoingia utendaji wa Mahakama na kuheshimu Muhimili huo.

Jaji Ibrahimu ameyasema hayo jijini Dar es salaam, wakati akifafanua siku ya maadhimisho ya siku ya sheria nchini itakayo adhimishwa Februali Mosi Mwaka huu.

“Nadhani hayo ni mambo ambayo yamekuwa yanatakiwa kwa mujibu wa Katiba unapokuwa na Katiba kazi moja ni kugawa mamlaka na mamlaka moja inapoingia kwenye mamlaka nyingine tayari unaondoka kwenye misingi ya Katiba.Mimi naomba Mahakimu ambao amri zao zinavunjwa na hawaonekani wakichukua hatua nadhani tuwe tunafanya kama Bunge wanavyofanya ukiingia kwenye anga la Bunge utaitwa mbele ya Kamati utaulizwa maswali na hatua huwa zinachukuliwa,” alisema Jaji Mkuu.

“Ninawasihi viongozi wote wa Serikali wenye mamlaka za kikatiba na kisheria wabaki ndani ya maeneo yao ya kikatiba na wajiepushe na kingilia maeneo yaliyo ndani ya haki, hadhi na mamlaka ya kikatiba ya Mahakama.”

“Mahakama tuna nguvu kama hiyo na sio Jaji ndio Mwenye nguvu hiyo ila nguvu hiyo iko kwenye kila Mahakama asitokee mtu akajivika kofia ya kimahakama atachukuliwa sheria”,aliongeza.

Wiki ya sheria mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Dully Sykes `kuufikisha mtandao wa simu Mahakamani



MKONGWE kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Anthony Wayson ‘Dully Sykes’ ameeleza kuwa anatarajia kuuburuza mahakamani mtandao maarufu wa simu za mkononi Bongo kwa madai kwamba umeshindwa kulinda nyaraka zake muhimu.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Dully alisema kuwa, mtandao huo umesababisha matapeli kutumia laini yake ya simu kufanya utapeli kwa watu wake mbalimbali.

“Kuna mtu ame-renew laini yangu, akapewa ushirikiano mkubwa na kampuni hiyo ya simu, aka-hack’ facebook yangu kisha akawaomba watu pesa na picha za utupu kwa wanawake, lazima niushtaki mtandao huu kwani unahusika,” alisema Dully Sykes.

Aslay afunguka Idadi ya ngoma alizotoa tangu kuondoka Yamoto Band




Mwanamuziki Aslay amefunnguka idadi ya nyimbo alizotoa tangu kuondoka Yamoto Band.

Muimbaji huyo ameiambia Power Breakfast ya Clouds Fm kuwa hadi sasa ametoa nyimbo zipatazo 16 na kufanya hivyo kwa kipindi kifupi kimemsaidia katika show zake.

“Imenisadia kwa namna moja au nyingine kwenye show zangu, nikienda kufanya show nafanya nikiwa na nyimbo zangu mimi kama mimi na show inakamilika, nina nyimbo 16 sasa hivi,” amesema Aslay.

Kwa sasa Aslay anafanya vizuri na wimbo ‘Subal kheir’ alioshirikiana na Nandy ambao awali uliimbwa na Culture Group kutoka visiwani Zanzibar.

Nafasi za kazi leo Jan 24

Vurugu za Kidini zasababisha Wanafunzi kuchomana visu Kenya



Mamia ya wanafunzi nchini Kenya katika shule ya Sekondari ya Jamhuri jijini Nairobi wapo katika hali mbaya ya kiafya baada ya usiku wa jana kutokea vurugu ya kidini kwenye shule hiyo.

Taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini Kenya zinaeleza kuwa wanafunzi hao walikuwa wakizozana kati ya Waislamu na Wakristo.

Kwenye mzozo huo Wanafunzi wa dini ya Kiislamu walikuwa wanawalazimisha wenzao wakristo kubadilisha dini (Kuslimu) na ndipo vurugu zilipoanzia.

Taarifa za awali zinaelezakuwa vurugu hizo zimetokea usiku wa kuamkia leo na mamia ya Wanafunzi wamejeruhiwa kwa kuchomwa visu huku vitanda na madawati yakivunjwa kwenye vurugu hizo.

Hata hivyo tayari Jeshi la Polisi jijini Nairobi limefika shuleni hapo asubuhi hii kufuatilia tukio hilo ili kutoa taarifa rasmi idadi ya wanafunzi waliojeruhiwa.

Source:Bongo 5


Thierry Henry bifuni na mashabiki wa Arsenal


Thierry Henry kwa sasa amepachikwa majina mengi ya kejeli na mashabiki wa Arsenal kutokana na madai ya kumshawishi Alexis Sanchez kujiunga na Manchester United.

Wengine wamekuwa wakimuita nyoka msaliti na mengine mengi. Kocha huyo msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji na mchezaji wa zamani wa Arsenal amekana kuwa hakuwahi kumshauri Sanchez kufanya maamuzi hayo.

Henry ametoa taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter, ameandika, “Ninajua sihitaji kuelezea hili kwa mashabiki wengi wa Arsenal lakini kinyume na uvumi hakuna muda wowote nilimwambia Alexis Sanchez aondoke Arsenal. Sikujua kwamba angeenda kusajiliwa na Man Utd mpaka nilipoona kwenye habari kama wengine.”

Baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Man United, Alexis Sanchez alithibitisha kwa kuandika ujumbe kuwa alipokea ushauri wa kuondoka Arsenal na kujiunga na Manchester kutoka kwa Henry.

“Nakumbuka leo, mazungumzo niliyokuwa nayo na Henry, mchezaji wa kihistoria wa Arsenal, ambaye alibadilisha klabu kwa sababu hiyo hiyo na leo ni wakati wangu,” aliandika Sanchez.

Bushoke afunguka kuhusu Q Chief


Msanii Bushoke ambaye aliwahi kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Bongofleva katika kipindi cha nyuma amefunguka na kukana taarifa za yeye kugombana na Q-chief na kudai wanaweza kutofautiana lakini siyo kuzinguana kabisa.

Bushoke ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo fununu kuwa wakongwe hao kwa sasa ni kama paka na panya licha ya kuwa karibu hapo awali na hata kurekodi wimbo mmoja studioni lakini mpaka sasa kazi hizo zimefungiwa studio.

"Some times' tunaweza kutofautiana lakini siyo kivile kwa hiyo namshukuru Mwenyezi Mungu yaani tupo karibu hata huko kutofautiana inawezekana mmoja wetu siku ameamka vibaya kwa hiyo ndio vitu hivyo lakini kugombana hatujawahi", alisema Bushoke.


Rais wa TFF aguswa na msiba wa Kocha wa Mwadui


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Jumanne Ntambi na wachezaji wa Mwadui kwa kuondokewa na kocha wao usiku wa kuamkia leo huku akiwataka wafiwa wawe na moyo wa subira

Rais Karia amesema hayo katika salamu zake zilizotolewa rasmi na Shirikisho hilo huku akisema ameshtushwa kupata taarifa hizo kwani marehemu Ntambi alikuwa na mchango mkubwa katika soka la Tanzania.

"Kifo cha Kocha Ntambi kimenishtua sana na kwa niaba ya Shirikisho natoa pole kwa wafiwa, nawaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu kwao kumpoteza mpendwa wao. Hakika alikuwa kocha aliyejitahidi kuibua vipaji na amekuwa na mchango mkubwa katika mpira wa miguu ambao bado alikuwa anautumikia mpaka kifo chake," alisema Rais Karia.

Enzi za uhai wake Jumanne Ntambi aliwahi kufundisha timu za Kahama United ya Shinyanga, Mlale JKT ya Ruvuma, Panone ya Kilimanjaro, timu ya mkoa wa Shinyanga Igembe Nsabo na mpaka mauti yanamkuta alikuwa akiifundisha Mwadui ya Shinyanga akiwa kocha msaidizi.

Serikali yatakiwa kupiga marufuku mifuko ya plastiki


Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeiagiza Serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kutoka nje ya nchi ili kulinusuru Taifa na madhara yanayotokana na mifuko hiyo.

Maagizo hayo yalitolewa baada ya kamati hiyo jana kukutana na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Akizungumza jana, mwenyekiti wa kamati hiyo, Sadiq Murad alisema walipata maelezo kutoka serikalini kuwa uzalishaji katika viwanda 41 vya plastiki nchini ulikuwa ni tani 73 katika mwaka 2016.

Hata hivyo, alisema mifuko iliyoingia nchini kupitia bandarini na mipakani ilikuwa tani 1,375.

“Kamati ilishauri ipigwe marufuku mifuko ya plastiki kutoka nje ya nchi na iwekwe tahadhari katika mipaka yetu,” alisema.

Alisema kamati inaitaka Serikali kufanya uhakiki wa uzalishaji katika viwanda vya nchini ambavyo vimepunguza uzalishaji ili waweze kukaa chini na kuzalisha mifuko ambayo itakayokidhi mahitaji na vigezo.

“Na hii itakuwa ni ya muda kuzalisha mifuko hiyo kwa masharti ya vigezo baadaye Tanzania isiwe na uzalishaji wa mifuko hii tena inayoharibu mazingira,” alisema.

Murad alisema zipo nchi nyingine kama Kenya, Rwanda, Uganda na Zanzibar ambazo zimepiga marufuku uzalishaji na uingizaji wa mifuko hiyo na kutafuta mifuko mingine inayotengenezwa na nguo, karatasi na majani.

Alisema mfano mzuri ni Zanzibar ambayo imepiga marufuku mifuko hiyo tangu mwaka 2016 na mtu anapoingia na mifuko hiyo bandarini hunyang’anywa na kupewa mingine.

“Tueleweke kabisa sisi kama kamati hatutaki kiwanda chochote kifungwe, tunataka uzalishaji kwa kufuata masharti na vigezo. Tunaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za kuipeleka nchi katika uchumi wa viwanda lakini vigezo na masharti lazima yazingatiwe,” alisema.

Akizungumzia agizo hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alisema hawaja japelekewa rasmi hayo mapendekezo. Hata hivyo alisema watapiga marufuku mifuko yote ya ndani na nje. “Wenye viwanda wajiandae maana yake dhamira ya Serikali wanaijua tangu mwaka 2016,” alisema

Aliyekua kipa wa Yanga azikwa Burundi


 Kipa wa zamani wa Yanga, Ismail Suma enzi za uhai wake.

KIPA wa zamani wa Yanga, Ismail Suma amezikwa nchini Burundi baada ya kukosa msaada wa kiuchumi kumrejesha nchini.

Habari za awali zilizopatikana Jumanne asubuhi zilisema kwamba Suma alifia kwa rafiki yake alipokuwa amekwenda kumsalimia.

Baada ya kutokea tatizo hilo, wadau wakaanza kupambana kusaka fedha za kurejesha mwili Tanzania lakini jioni, zikatumwa picha kwenye mitandao ya Burundi kwamba ameshazikwa kulekule.

Habari zinasema kwamba alizikwa kidini na idadi ndogo ya watu kwavile alikuwa hafahamiki.

Akifanyiwa maombi kabla ya kuzikwa.