Monday, 22 January 2018

Ushirika Mara kukaguliwa mali zake


Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa amesema Serikali itatuma wakaguzi kwa ajili ya kukagua  mali za chama cha ushirika mkoa wa Mara.

Amesema Serikali imeanza kufuatilia mali za vyama vya ushirika nchini zikiwemo za chama hicho.

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo jana, Januari 21 mwaka 2018 katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani hapa.

Amesema ukaguzi huo utakwenda sambamba na kufuatilia fedha wanazodai waliokuwa watumishi wa chama hicho.

“Kumekuwa na matatizo makubwa ndani ya vyama vya ushirika kiasi cha kudumaza maendeleo ya wananchi,” amesema.

Pia, amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mhandisi  Elius Mwakalinga kufanya tathimini  ya ubora ya jengo la kituo cha pamoja cha forodha cha Sirari kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Amesema mkurugenzi huyo afanye tathmini na kuishauri Serikali kama jengo hilo linafaa kutumika.

Januari 17, Waziri Mkuu alikagua kituo hicho kilichopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara na kusema hajaridhishwa na ujenzi wake  kwa kuwa upo chini ya kiwango.

Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2011 na kukamilika mwaka 2014.

Basi la Mkombozi laua wawili na kujeruhi watatu Mwanza


Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa katika ajali ya gari baada ya basi dogo la abiria kampuni ya Mkombozi kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Walawi katika eneo la Kamanga jijini Mwanza.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa dereva wa basi la Mkombozi pamoja na abiria mwingine wamepoteza maisha hapo hapo.

"Ni kweli imetokea ajali hiyo na kusababisha vifo vya watu wawili akiwepo dereva la basi dogo la kampuni ya Mkombozi ambaye alifariki hapo hapo baada ya ajali pamoja na abiria mwingine, lakini pia wapo majeruhi watatu ambao wamepelekwa kwa matibabu zaidi"

Jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kujua chanzo za ajali hiyo

Makumbusho ya Taifa yamzungumzia binadamu wa kwanza

Makumbusho ya taifa la Tanzania iliyopo jijini Dar es salaam imeandaa mafunzo ya onesho la chimbuko la binadamu Afrika yanayotarajiwa kutolewa kesho.

Mkurugenzi wa Makumbusho ya taifa Prof. Audax Mabula  mafunzo na onesho hilo yanatokana na tafiti mbalimbali zinazofanyika bonde la hifadhi ya Olduvai na Laetol katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.

Aidha Prof. Audax  ameeleza onesho hilo litafanyika kesho jijini Dar es salaam na litafunguliwa na waziri wa Mali asili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na litahudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Katika onesho hilo wananchi pia wataweza kuona mambo mbalimbali ya kale ambayo binadamu wa kwanza aliweza kuyafanya katika nyanja tofauti katika maisha yake.

Mwenyekiti UVCCM amtupia kombora Salum Mwalimu


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Kheri James amemfananisha Mgombea Ubunge, Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CHADEMA, Salum Mwalimu sawa na bibi harusi na kuwa wao CCM watashinda uchaguzi huo.

James amesema kuwa Watanzania wanakipenda sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati huu kuliko wakati mwingine wowote hivyo ni lazima Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya (CCM), Maulid Mtulia ashinde.

"Kinondoni tunakwenda kushinda nimesikia Kamati ya harusi imemchagua Bibi harusi mmoja, hawa wanacheza siasa ya diblo dibala mara wamo mara hawamo lakini faida tuliyopata safari hii wametuletea mtu mwenye historia ya kushindwa, kaomba Ubunge kwao huko visiwani kapigwa, kaomba Ubunge wa Afrika Mashariki kapigwa na Kinondoni atapigwa, nachohitaji Kinondoni nataka kipigo kitakatifu ili baada ya kushindwa Salum Mwalimu aache siasa atafute biashara nyingine" alisema Kheri James

Mbali na hilo Mwenyekiti wa UVCCM amedai kuwa Salum Mwalimu ni mbuzi wa kafara wa CHADEMA kuwa kila shughuli ngumu wanamtuma yeye ili akafe wao wabaki.

Shule ya Makuti Mtwara yaanza kukarabatiwa


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mtwara QS Omary Kipanga, amesema ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Mitambo iliyopo kata ya Msimbati ambayo iliripotiwa kuwa na madarasa ya makuti, unaendelea shuleni hapo.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Bw. Kipanga mesema ujenzi huo ni wa vyumba vitatu vya madarasa ambao serikali inasimamia, na kimoja ambacho kinajengwa kwa nguvu ya wananchi, pamoja na nyumba ya mwalimu.

“Vyumba vipo na vya matofali na vimeezekwa majengo matatu, lakini kuna ujenzi ambao unaendelea kwa nguvu za wananchi wa darasa moja, lakini na sisi halmashauri katika bajeti yetu ya mwaka 2017/18 tumetenga bajeti kwa ajili ya madarasa mawili na nyumba ya mwalimu, mpaka sasa vyumba vya madarasa vinavyotumika ni vyumba viatu, vingine vitatu vipo kwenye ujenzi”, amesema Mkurugenzi Kipanga.

Sambamba na hilo Mkurugenzi amekiri uwepo wa upungufu wa walimu, ambapo amesema tatizo hilo ni la nchi nzima na sio kwenye halmashauri yake peke yake, hata hivyo serikali inafanya jitihada za kutatua changamoto hiyo.

“Tuna changamoto ya walimu sio kwenye halmashauri yangu tu, ni nchi nzima, kwa sababu mimi katika halmashuri yangu nina upungufu karibu mia 5 na kitu, pale walimu 7, wanafunzi 437 na madarasa 7 yaani la kwanza mpaka la saba”, ameendelea kufafanua Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wa elimu ya sekondari Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mtwara amesema ana tatizo kubwa la kuwepo kwa upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi, kwani kwenye halmashauri yake ina uhaba wa walimu 71 wa masomo ya sayansi.

“Kwa upande wa sekondari masomo ya sanaa hatuna tatizo sana, ila kwa masomo ya sayansi mimi kwenye halmashauri yangu ina upungufu wa walimu takriban 71 kwa shule zote, lakini bado tuna mikakati ya kuhakikisha tunapata walimu wa mazoezi ili tuweke priority kwenye masomo ya sayansi”, amesema Mkurugenzi huyo.

Shule ya Mitambo ilianzishwa mwaka 2009, ambapo mwaka 2015 walihitimu wanafunzi wa darasa la saba kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa.

EATV.

Rais Magufuli apokea hati za mabalozi sita nchini


Rais Dkt John Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka Mabalozi 6 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Vanessa kuinufaisha familia ya Mbaraka Mwishehe


Msanii wa muziki Vanessa Mdee amebainisha kwa nini familia ya marehemu Mbaraka Mwishehe itanufaika kwa mauzo ya albamu ya Money Monday kwa njia ya mtandao na sio kwa mauzo ya kawaida (CD).

Mrembo huyo amebinbisha hayo kupitia mahojiano aliyofanya na Bongo5 na kusema kuwa ameamua maamuzi hayo yamekuja baada ya kutoa kionjo katika ngoma ya ‘Jogoo la Shamba’ ya marehemu Mbaraka na kukitumia katika ngoma yake ya ‘ Pumzi ya Mwisho’ aliyowashirikisha marapa wawili amabo ni Cassper Nyovest na Joh Makini.

“Familia ya mubaraka itanufaika kwa mauzo ya kimtandao kwa sababu soko letu lina hamia kimtandao Zaidi hivyoi ni meona ni busara kutumia njia hiyo,” amesema Vanessa.

AUDIO Audio | Lava Lava – Kizunguzungu | Mp3 Download

AUDIO
Audio | Lava Lava – Kizunguzungu | Mp3 Download

AUDIO
Audio | Lava Lava – Kizunguzungu | Mp3 Download

DOWNLOAD Mp3

New VIDEO: Stonebwoy – Bawasaaba

New VIDEO: Stonebwoy – Bawasaaba

New VIDEO: Stonebwoy – Bawasaaba



DOWNLOAD VIDEO

New VIDEO: Nameless – Volume (Voloyoom)

New VIDEO: Nameless – Volume (Voloyoom)

New VIDEO: Nameless – Volume (Voloyoom)


DOWNLOAD VIDEO

Mtoto wa Navy Kenzo awa kivutio kwa watu


MTOTO wa wanamuziki wa kishua wanaounda Kundi la Navy Kenzo, Emannuel Mkono ‘Nahreel’ na Aika Mareale waliompa jina la Gold, amegeuka kivutio kwa watu mbalimbali baada ya wawili hao kuachia picha yake mtandaoni.

Wanamuziki hao ambao ni kapo ya muda mrefu walionesha picha ya mtoto huyo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na kusababisha watu wengi kuichua na kuweka katika kurasa wakimsifia.

Mama wa Gold, Aika aliiambia Over Ze Weekend, kuwa anafurahi kuona watu wengi wamefurahishwa na ujio wa mwanaye, jambo ambalo kwao ni baraka kubwa katika safari yao ya kimaisha.

Mnyeti atoa agizo mbunge wa Kiteto akamatwe



Kiteto. Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Alexander Mnyeti amemuagiza mkuu wa wilaya ya Kiteto, mhandisi Tumaini Magessa kumkamata mbunge wa Kiteto (CCM), Emmanuel Papian endapo atabainika kuwa anachochea migogoro ya ardhi.

Mnyeti amesema hayo Ijumaa Januari 19, 2018 wakati akihitimisha ziara yake ya siku saba alipotembelea wilaya ya Kiteto.

Amesema  endapo Papian anasababisha migogoro ya ardhi kwa kuchochea wananchi walime kwenye hifadhi, anapaswa kuchukuliwa hatua.

"Mkuu wa wilaya wewe ndiye mteule wa Rais kwenye eneo hili la Kiteto. Endapo mtu mwingine hata kama ni mbunge wa jimbo akiwa anachochea migogoro ya ardhi, uwe unawakamata na kuwaweka ndani," amesema Mnyeti.

Amesema migogoro ya ardhi kwenye wilaya ya Kiteto  haitaweza kumalizika endapo wanasiasa wataendelea kuwachonganisha wakulima na wafugaji.

"Mbunge asiote mapembe na kupanda kichwani kwako, wewe ndiye mtawala wa hapa. Nataka  siku nyingine unipigie simu kuwa umemkamata na kumweka ndani mbunge ili asirudie hilo," amesema Mnyeti na kuongeza,

"Mkuu wa wilaya unapozungumzia mgogoro wa kijiji zungumza sehemu husika na kama mbunge akiendelea kuchochea umkamate," amesema Mnyeti.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi, Papian hakukubali wala kukataa juu ya yeye kuchochea na kusababisha migogoro ya ardhi, ila amesema muda utaongea.

"Hapa tunavyozungumza nipo kwenye gari, ila suala hilo uliloniuliza litajulikana huko mbeleni tunakokwenda hivyo tujipe muda tuu itabainika," amesema Papian.

TPSF yaiomba Serikali kufanya marekebisho muswada wa ardhi



Dar es Salaam. Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imeiomba Serikali kuondoa mabadiliko ya Sheria ya Ardhi yaliyomo katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ili kuepuka madhara ya kiuchumi yanayoweza kusababishwa na mabadiliko hayo iwapo yatapitishwa.

Katika kuhimiza hilo, TPSF imemuandikia barua Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ikimtaka kuwashirikisha wadau kabla ya muswada huo kujadiliwa na Kamati ya Bunge.

Msimamo wa TPSF unafanana na wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambacho kimesema iwapo marekebisho hayo yatapitishwa na sheria kuanza kutumika, yataathiri mfumo wa rehani nchini.

Mjumbe wa Kamati ya Katiba na sheria ya TLS, John Seka alisema kwa muda mrefu wananchi wengi wamekuwa wakitumia mashamba kama rehani kwenye taasisi za fedha.

Alisema wamewasilisha maoni yao Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria inaouchambua muswada huo unaomtaka mmiliki wa shamba ambalo halijaendelezwa au kuendelezwa kidogo, kutumia fedha anayokopa kuliendeleza zaidi.

Jana, mkurugenzi mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye alisema muswada huo unapaswa kuondolewa kabisa bungeni kwani endapo kosa lolote litafanyika, madhara yake ni makubwa kwenye uchumi.

“Inawezekana Serikali ina lengo zuri, lakini hatukushirikishwa. Uwekezaji utakufa nchini kwa sababu wengi hukopa ili kuendeleza biashara walizonazo jambo linalozuiwa kwa sasa,” alisema Simbeye.

Kwa hali hiyo, alisema sekta ya kwanza kuanguka itakuwa ya benki na taasisi za fedha ambazo zitakosa wateja.

TPSF imeipongeza Serikali kwa juhudi za kuboresha mazingira ya biashara hasa kwa kurahisisha upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya kuwekeza, lakini imetoa angalizo kwa marekebisho yanayopendekezwa.

TPSF imepokea malalamiko kutoka kwa wanachama, benki na taasisi za fedha, wamiliki wa viwanda pamoja na wakulima kuhusu mabadiliko yanayopendekezwa, inasema barua hiyo.

Miongoni mwa hoja zilitolewa na taasisi hiyo ni kutoshirikishwa kwa wadau katika utungaji wa mabadiliko hayo ili wawasilishe maoni yao.

Imesema kwa namna muswada huo ulivyoandaliwa, Serikali inaweza isipate mafanikio inayoyatarajia na mapendekezo ya vifungu hivyo vitatu yanaweza kuwa na athari kwa uchumi wa nchi.

“Kwa barua hii, tunaiomba wizara yako iuondoe mara moja muswada huo kabla haujajadiliwa na Kamati ya Bunge au Bunge lenyewe mpaka wadau, ikiwamo TPSF watakaposhirikishwa,” inasema barua hiyo.

Muswada huo unapendekeza kufanya marekebisho katika sheria tano ambazo ni Sura ya 25 ya Sheria ya Ufilisi, Sura ya 439 ya Sheria ya Bajeti, Sura ya 113 ya Sheria ya Ardhi na Sura ya 238 ya Sheria ya Utumishi wa Umma ili kuondoa mapungufu mbalimbali yaliyomo katika utekelezaji wa sheria hizo.

Marekebisho ya Sheria ya Ardhi ambayo TPSF inapendekeza maoni yao yazingatiwe, inabadili masharti yaliyopo kwenye Kifungu cha 45 kwa kuongeza adhabu ya ukiukwaji wa masharti kwa mtu anayeweka dhamana ya miliki ya ardhi.

Kwenye sheria inayofanyiwa marekebisho, vifungu vya 120A, 120 B na 120 C vimeongezwa kuwezesha fedha zinazopatikana kutokana na mkopo uliotolewa kwa dhamana ya miliki ya ardhi Tanzania zitumike kuendeleza sehemu ya ardhi iliyowekwa rehani kwa miliki zote ambazo hazijaendelezwa.

Marekebisho hayo yanawataka wote wawili; mkopaji na mkopeshaji, kuwasilisha taarifa kwa kamishna wa ardhi. Licha ya hilo, yanataka fedha itakayopatikana iwekezwe Tanzania.

Aidha, muswada unataka benki na taasisi zote za fedha zinazotoa mkopo husika; ndani na nje ya nchi kuwasilisha tamko kwa kamishna wa ardhi kwamba fedha hizo zitawekezwa Tanzania.

Maana yake, mkopo wa fedha zozote zitakazokopwa kwa dhamana ya ardhi ya Tanzania kisha zikawekezwa nje, utakuwa batili.

Waziri Lukuvi amewataka wadau wenye maoni kuhusu marekebisho yanayopendekezwa kwenye muswada huo kuyawasilisha kwenye kamati husika ya Bunge.

“Huo ndio utaratibu. Kama kuna malalamiko yoyote, ni vizuri yawahishwe wakati huu vikao vinapoendelea, yatachambuliwa,” alisema.