Wednesday, 17 January 2018

Seven ‘fuel thieves’ face the music, appear in court


SEVEN people, including former staff of the Tanzania Zambia (TAZAMA) Oil Pipeline Company, Samwel Nyakirang’ani (63), allegedly linked to the theft of fuel destined for the Tanzania Ports Authority (TPA), appeared before a Dar es Salaam Court yesterday, facing three counts.


Other accused persons at the Kisutu Resident Magistrate’s Court in the city were Nyangi Mentaro, a teacher at Ufukoni Primary School; Farijia Ahmed, a businesswoman; Malaki Mathias, a businessman; Kristomsi Angelusi, a businessman; Pamfili Nkoronko, a masson and Henry Fredrick, a businessman.

Before Principal Resident Magistrate Thomas Simba, the accused were not allowed to enter plea to the charges of “unlawful connection of fuelpipeline and damaging property which is used for the purpose of providing a necessary service.

” This is because they have been charged under the Eco-nomic and Organised Crime Control Act. The Magistrate ordered the accused to be remanded in custody because the Director of Public Prosecutions (DPP) has filed a certificate to deny them bail on grounds of public interest.

The case will be mentioned on January 30, this year, as investigations into the matter, according to the prosecution led by Principal State Attorney Peter Maugo and State Attorney Majigo Lulumanywa, have not been completed.

Reading the counts, the prosecution told the court that between 2015 and January 8, this year, at Tungi Muungano area within Kigamboni District in the city, jointly and together, all accused persons connected their one inch in diameter stainless steel pipeline without the consent of the licensee, the TPA.T

he court was further told that within the same period and place in Kigamboni District, Dar es Salaam Region, jointly and together, the accused perforated and damaged a 24 inches in diameter pipeline, the property of TPA, used to supply diesel fuel.

It is alleged also that within the same period and place at Kigamboni District in the city, jointly and together, all the accused perforated and damaged a 28 inch in diameter pipeline, the property of TPA, used for supplying crude oil.

Police investigations suggest that Nyakirang’ani is the owner of the house from which the pipe was allegedly connected drawing oil from the TPA pipeline.

The accused were arrested at Kigamboni area immediately after the theft was discovered.


Trump's mental ability is okay, says White House doctor


BBC quoted White House Doctor Ronny Jackson as saying, “I have no concerns about his cognitive ability or neurological functions.

" President Trump, 71, had a three-hour medical check-up, few days after the release of a controversial book about the US Head of State’s mental health. Dr Jackson revealed to reporters that Donald Trump overall health was “excellent.”

"All data indicates the president is healthy and will remain so for the duration of his presidency," BBC quoted the White House doctor.

However, Dr Jackson said that Mr Trump could benefit from a lower-fat diet and more exercise.


Sunday, 14 January 2018

Azam yatwaa ubingwa Mapinduzi Cup


Mbele ya Rais wa Zanzibar, Ali Mohammed Shein aliyekuwa mgeni rasmi, Azam FC wametimiza kile walichokitaka Watanzania wengi baada ya kubeba ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Kikosi cha Azam FC kimeshinda kwa mikwaju 4-3 ya penalti dhidi ya URA ya Uganda katika mechi ya fainali ya Mapinduzi iliyochezwa jana usiku katika uwanja wa Amani kisiwani huko.

URA ilikuwa kama imekuwa kiboko ya Watanzania, kwa kuwa ndiyo iliitoa Simba katika michuano ya Mapinduzi, baadaye ikafanya hivyo kwa kuing'oa Yanga pia.

Lakini, tayari ilikuwa imeishinda Azam FC katika hatua za makundi. Lakini leo mambo yalikuwa magumu baada ya dakika 90 kwisha kwa sare ya bila mabao.

Dakika za nyongeza bado mambo yalikuwa magumu baada ya sare ya 0-0.

Walipoingia katika mikwaju ya penalti, kipa wa Azam FC, Razack Abarola ndiye alikuwa shujaa kwa kupangua mikwaju miwili ya Waganda hao.

Azam iliingia fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Singida United kwa bao 1-0, huku URA wao wakitinga fainali baada ya kuichpa Yanga kwa mikwaju ya penati 5-4. Kwa ushindi huo wa jana Azam inakuwa imetwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo lakini pia wakitwaa ubingwa wao wa kwanza ndani ya msimu huu.


Perez bado ana imani kubwa na Zidane



Klabu tajiri huwa zinawekeza ili kupata makombe tu, hawataki kitu kingine chochote, hawataki kukuza vipaji wala kutafuta nafasi ila kinachotakiwa ni kombe tu na hiyo ndio sera ya Real Madrid.

Jana Real Madrid wametoka kupoteza mchezo wao dhidi ya Villareal, kwa matokeo haya sasa Real Madrid wanabaki na alama 32 na vinara wa ligi Barcelona wakishinda mechi ijayo watawapita Madrid kwa alama 19.

Pamoja na yote hayo lakini sio rahisi kwa Florentino Perez kumfukuza Zinedine Zidane na hawezi kukaa muda mrefu kama Arsene Wenger ama Sir Alex Ferguson lakini kwa siku za karibuni anaonekana hawezi kuondolewa.

Bodi nzima ya Real Madrid ikiongozwa na Rais mwenyewe Florentino Perez pamoja na wachezaji wote wa Real Madrid inasemwa kwamba wako upande wa Zidane na wana imani naye katika timu hiyo.

Habari kutoka Hispania zinasema kwamba Florentino Perez anajipanga kutoa fungu kubwa la pesa kwa Zinedine Zidane kwa ajili ya usajili wa mwezi huu wa January na lile dirisha kubwa la usajili baada ya msimu wa ligi.

Zidane anaweza kuendelea kupewa nafasi na imani katika kikosi cha Real Madrid lakini yeye mwenyewe kama asiporidhishwa na kiwango cha klabu hiyo anaweza kuamua kuachana nayo kwa hiari yake.

Kenyatta, Odinga wampongeza Olunga mitandaoni



Michael Olunga amekuwa Mkenya wa kwanza kufunga goli katika ligi kuu ya Uhispania ~La Liga. Olunga amefunga magoli matatu (Hat-trick) dhidi ya Las Palmas na kuweka rekodi ya kuwa Mkenya wa Kwanza kufunga hat-trick kwenye Laliga.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kuona taarifa hiyo hakukaa kimya kupitkia ukurasa wake wa Facebook akampongeza Michael Olunga kwa kusema “Ongera Michael Olunga kwa kuweka historia kuwa Mkenya wa kwanza kufunga goli katika ligi ya Hispania La Liga na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwa klabu ya Girona katika ligi ya Spain”

Nae kiongozi wa Muungano wa Upinzania nchini Kenya Raila Odinga amepost katika ukurasa wake wa Twitter kumpongeza Olunga.



Mafaza wa Yanga sasa kukiona cha moto


Panga kubwa ambalo litaondoka na mafaza kadhaa linakuja ndani ya Yanga, hii inatokana na mabadiliko makubwa yaliyoonyeshwa na wachezaji vijana kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Habari za ndani ya Yanga zinasema kwamba benchi la ufundi linafikiria kufanya hivyo mwishoni mwa msimu huu ili kuongeza ufanisi pamoja na kubadilisha aina ya uchezaji wa Yanga, ambao kwa kipindi kirefu ulikuwa unategemea wachezaji wakongwe wa ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa wachezaji hao wakongwe wamekuwa mzigo kutokana na kusumbuliwa na majeruhi kwa kipindi kirefu huku wakiwa wanaigharimu klabu. Miongoni mwa mafaza wanaotajwa ni pamoja na Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Nadir Haroub Canavaro na Amisi Tambwe.

VIJANA WAFUNIKA MAPINDUZI

Katika michuano ya Mapinduzi iliyomalizika jana usiku, Yohana Nkomola, ambaye alisajiliwa na Yanga katika kipindi cha dirisha dogo msimu huu akitokea kikosi cha Taifa ya Vijana Serengeti Boys ni miongoni mwa vijana waliotamba pamoja na Ramadhani Kambwili na Said Musa.

Nkomola ametamka kuwa baada ya mwaka mmoja Jangwani itatisha kwa sababu itakuwa na kikosi cha vijana ambacho kitakuwa na ushindani mkubwa, huku kocha wake Shadrack Nsajigwa naye akikiri hilo.

“Mimi kama mmoja wa wachezaji vijana ninaamini baada ya mwaka mmoja tutaweza kuifanyia Yanga mambo makubwa zaidi, mashabiki wetu wazidi kutusapoti ilikuweza kufanya vyema zaidi. “Tunashukuru kocha wetu ametupa nafasi kwenye Mapinduzi na vijana tumeweza kuonekana na sisi tutapambana hatutamuangusha tutazidi kupambana na kuwa bora,” alisema Nkomola.

Hata hivyo, Nsajigwa ambaye aliwanoa wachezaji hao kuanzia kwenye timu ya vijana, alisema kiwango kilichoonyesha na wachezaji wote chipukizi kwenye Mapinduzi ni ishara kuwa wakiongeza juhudi watakuwa matata sana siku zijazo na wataibadili sura ya Yanga.

“Wachezaji chipukizi wamejitahidi kuonyesha uwezo na ilikuwa ni nafasi yao ya kucheza kwani tulitumia michuano hiyo kama sehemu ya mazoezi ya kujiandaa na ligi pamoja na michuano ya kimataifa. “Tunashukuru kuona kila mmoja ameonyesha kiwango cha juu hata wale ambao walikuwa hawapati nafasi ya kucheza walifanya vyema, hivyo inatupa nafasi ya kuamini kuwa tunaweza kufanya vyema zaidi,” alisema Nsajigwa.


Ujue Ugonjwa wa UTI



UTi ni ugonjwa ambao unasumbua watu wengi; watoto, vijana na watu wazima. UTI ni kifupisho cha Urinary Tract Infection. Huu ni ugonjwa ambao hushambulia figo (kidneys); ureters; ambayo ni mirija inayounganisha figo na kibofu cha mkojo, kibofu cha mkojo (bladder) na urethra; sehemu inayotoa mkojo toka kwenye kibofu cha mkojo hadi nje ya mwili.

Kwa kifupu ugonjwa wa UTI hushambulia viungo vinavyohusika katika kupitisha mkojo kabla haujatoka nje ya mwili. Hebu tuvitazame viungo hivi kabla ya kueleza chanzo cha ugonjwa na tiba ya UTI baadaye hapa chini.

Kuelewa vizuri tunachokizungumzia hapa tazama picha ya viungo hivi na kwa kifupi hapa tutatoa maelezo ya picha hiyo. Figo ni viungo viwili vilivyopo kimoja kila upande wa uti wa mgongo eneo la kiunoni. Figo hufanya shughuli nyingi katika mwili wa binadamu ikiwepo ya kutoa uchafu na maji ya ziada katika damu, na huvitoa vitu hivi kama mkojo. Kwa sababu hii, figo ni muhimu sana katika kuweka msukumo wa damu kwenye kiwango kizuri.

Figo pia husikia mapema sana mabadiliko ya kiwango cha sukari mwilini na mabadiliko katika kiwango cha msukumo wa damu (blood pressure). Kiwango cha sukari na msukumo wa damu vikizidi, vyote huweza kuleta madhara kwenye figo.

Ureters ni mirija miwili myembamba yenye urefu wa yapata nchi 10 hivi kila mmoja ambayo huchukua mkojo kutoka kwenye figo na kuumwaga ndani ya kibofu cha mkojo.

Kibofu cha mkojo ni kijimfuko kidogo kinachopokea mkojo kutoka kwenye mirija ya ureters na kuuhifadhi. Mkojo ukifikia kiwango fulani ndani ya kibofu cha mkojo, tunasikia haja ya kuupunguza (kukojoa) na ndipo misuli ya nje ya kibofu cha mkojo hujibana na kuukamua mkojo nje ya kibofu.

Urethra ni mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na nje ya mwili.
Sehemu yo yote katika hizi tulizozitaja hapa juu, inaweza ikapata maambukizi ya UTI na kadri maambukizi hayo yatakavyokuwa ndani zaidi ukitokea nje, ndivyo ugonjwa huu utakavyokuwa umefikia hali mbaya zaidi. Wasichana na akina mama hupata maambukizi haya kwa wingi zaidi kuliko wavulana au akina baba. Asilimia kama 40 ya wanawake na asilimia 12 ya wanaume hupata maambukizi haya ya UTI katika maisha yao.

Chanzo Cha UTI Ni Nini?
Mkojo kwa kawaida ni kitu kisicho na wadudu wo wote wabaya. Maambukizi yanakuja pale wadudu wanapoingia kwenye mkondo wa mkojo kupitia kitundu cha kutolea mkojo nje ya mwili na kufuata mkondo huo kuelekea kwenye figo. Wadudu hao wakisha ingia huanza kuzaliana.

Asilimai 90 ya maambukizi yasiyo mabaya sana huwa ni ya bacteria waitwao Escherichia Coli au kwa kifupi E.Coli. Kwa kawaida bacteria hawa huishi katika utumbo au karibu na maeneo ya mkundu. Wadudu hawa wanaweza wakatembea kutoka eneo la mkundu wakaelekea kwenye tundu la mkojo na kuingia. Lakini, kutojisafisha kwa namna nzuri (kwa mfano, kutawadha kuanzia nyuma kuja mbele) au ngono ndizo njia mbazo huambukiza bacteria hawa kirahisi zaidi.

Wanawake hupatwa zaidi na maambukizi haya kwa sababu ya ukaribu wa mkundu na kijitundu cha kutolea mkojo na kwa sababu ya ufupi wa urethra katika miili yao ukilinganisha na wanaume. Wanawake wanaoshiriki ngono mara nyingi na watu tofauti hupatwa na maambukizi zaidi kuliko wale wanaoshiriki kwa kiwango kidogo.

Wanawake wanaotumia diaphragms kama njia ya uzazi wa mpango hupatwa zaidi na tatizo hili pia akina mama waliokoma hedhi kwa sababu ya ukosefu wa homoni ya estrogen. Kukosekana kwa estrogen kunasababisha mabadiliko katika mkondo wa mkojo na kuufanya uweze kuambukizwa kwa urahisi zaidi.

Matatizo yo yote yanayosababisha mkojo usitoke nje kwa urahisi huongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UTI. Mifano ni; watoto kuzaliwa na matatizo katika mikondo yao ya mkojo ambayo huzuia mkojo usitoke nje kirahisi, matatizo ya kidney stones na prostate kukua kupita kiasi; na watu wanaotoa mkojo kupitia kifaa maalumu (catheter).

Tendo la kukojoa huwatoa bacteria hawa nje ya mwili lakini wakiwa wengi sana, kukojoa hakuwezi kuwatoa wakaisha. Wadudu hawa husafiri kwenye urethra hadi kwenye kibofu cha mkojo ambako watazaliana. Wanaweza kuendelea kusafiri kupitia ureters hadi kwenye figo ambako pia watazliana na kuleta matatizo makubwa endapo tiba nzuri haitatolewa kwa wakati muafaka.

Ni Nini Dalili Za UTI?
Dalili za ugonjwa huu huwa tofauti kulingana na hatua ambayo ugonjwa umeshafikia.

Lower UTI ni hatua ya ugonjwa kushambulia maeneo ya urethra na kibofu cha mkojo (bladder). Katika hatua hizi, mgonjwa atasikia dalili zifuatazo:


Maumivu wakati wa kukojoa
Kujisikia kukojoa mara kwa mara lakini kutoa mkojo kidogo tu
Damu katika mkojo
Mkojo wenye rangi ya chai
Mkojo wenye harufu kali
Maumivu ya kiuno kwa wanawake
Maumivu ya sehemu za nyuma kwa wanaume


Upper UTI ni maambukizi ya ndani ya figo. Hii ni hatua mbaya sana endapo bacteria wataanza kuingia kwenye mkondo wa damu kutoka kwenye figo – SEPSIS. Sepsis huweza kusababisha msukumo wa damu kuwa mdogo sana (Low Blood Pressure), mshituko au kifo.

Dalili za upper UTI ni:

Maumivu ya maeneo ya juu ya mgongo
Homa
Kusikia baridi
Kusikia kichefuchefu
Kutapika


Hatua Za Kujikinga Na UTI
Kuna hatua unazoweza kuchukua ili usipatwe na maambukizi ya ugonjwa huu kirahisi. Hii ni pamoja na kujifuta au kutawadha ukianzia mbele kwenda nyuma baada ya haja kubwa au ndogo. Kunywa maji mengi, glasi 6 hadi 8 za maji kila siku na kuhakikisha unakunywa maji baada ya kushiriki tendo la ndoa. Haifai kuubana mkojo kwa muda mrefu, timiza haja mara itokeapo. Kusafisha maeneo nyeti mara kwa mara. Kuoga kupitia bomba la mvua ni bora zaidi kuliko kutumbukia kwenye josho. Ni vema kuvaa chupi zilizotengenezwa kwa pamba.

BREAKING NEWS: Ndumbaro ashinda ubunge Songea



Mgombea Ubunge jimbo la Songea Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dr. Damas Ndumbaro ameshinda Uchaguzi kwa kupata kura 45162 sawa na 97% akifuatiwa kwa mbali na mgombea Wa CUF aliyepata kura 608.

Matokeo rasmi yametangazwa na mkurugenzi wa uchaguzi jimbo la Songea mjini.


MAGAZETI YA LEO 14/1/2018






































Friday, 12 January 2018

Joh Makin akana kuwa na bifu na Fid Q



Kama wewe ni mpenzi au mdau wa muziki wa Hip Hop hapa Bongo, basi hakuna ubishi kuwa kolabo kubwa inayosubiriwa na mashabiki ni kolabo kati ya Joh Makini na Fid Q.

Je, unajiuliza kolabo hii huenda ikatokea? ukweli ni kwamba ondoa shaka kwa hilo kwani Joh Makini amesema kuwa ni muda tu unasubiriwa kwani wawili hao hawajahi kukaa pamoja kuzungumzia ishu za kolabo lakini endapo ikitokea nafasi ya kufanya hivyo watafanya.

“Mimi na Fid Q hatuna matatizo kama ambavyo watu wanafikiri, kwa sababu mimi mwenyewe binafsi sijawahi kuwa na matatizo naye na wala sijawahi kuona kama anamatatizo na mimi. Kwa hiyo mimi kama msanii na yeye kama msanii Chochote kinaweza kutokea anytime,“amesema Joh Makini kwenye kipindi cha Playlist cha Times FM huku akielezea kikwazo cha muda

“Ni vile labda hatujawahi kukutana kwenye hiyo vibe, hatujawa bado kwenye hiyo Chemistry ya kusema tufanye ngoma pamoja so you never know..hakuna mipaka 2018,“amemaliza Joh Makini.

Waziri awaapisha bodaboda kuwalinda watoto wa kike


Madereva Bodaboda wa wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamekula kiapo cha uaminifu cha kuwalinda watoto wa kike dhidi ya vitendo vya ngono na mimba za utotoni zinazo sababisha kukatisha haki yao ya kuendelezwa.

Kiapo hicho kimeongoza na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Kampeni ya “Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima” iliyozinduliwa tarehe 11 Oktoba, 2017 kwa lengo la kuhamasisha wananchi kupambana na kuzuia matukio ya mimba za utotoni katika jamii zetu.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa ili kufanikisha kutokomeza mimba za utotoni hatuna budi kuweka ushirikiano baina ya wazazi, walezi, jamii, Serikali na wadau wengine ili kuwaepusha watoto wa kike kupata vishawishi vya mahusiano ya kingono katika umri mdogo na hatimaye kupata mimba za utotoni.

Ameongeza kuwa lengo la Kampeni ya “Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima” imelenga kuunganisha nguvu za pamoja za wanajamii wakiwemo madreva wa Bodaboda kushirikiana na Serikali kuzuia na kutokomeza matukio ya mimba za utotoni katika ngazi ya jamii na shuleni.

“Niseme kampeni hii itasaidia kwa asilimia kubwa kuunganisha nguvu zetu kama wananchi na sisi Serikali katika kutokomeza vitendo hivi viovu”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amewaasa madereva hao kuondokana na tamaa za kujihususha na mahusiano na kingono na watoto wadogo bali wao kuwa walinzi wao katika kutokomeza suala mimba kwa watoto wetu.

Amewataka kufichua vitendo vyovyote vyenye ushawishi wa mahusiano yanayosababisha mimba kwa watoto wa kike ili Sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kuweka mikakati ya kupambana na wanaume na vijana wakware wanaotumia fursa zao kuwa na mahusiano maovu na watoto wa kike katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ambao ndio unaoongoza kitaifa kwa kuwa na asilimia 45.

Mmoja wa dereva Boda boda wa Wilaya ya Mpanda Bw. Juma Salum kwa wakati tofauti wameishukuru Serikali kwa kuandaa Kampeni hiyo itakayowajengea uelewa wananchi kusaidiana katika kuwalinda watoto wa kike kwa kuweka miundo mbinu salama ya kusomea na kujifunzia ili kupunguza kiwango cha mimba za utotoni kwa silimia 50 ifikapo mwak 2021/22.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) alikuwa na ziara ya siku mbili mkoani Katavi kuhamasisha wananchi kupambana na kuzuia mimba za utotoni kupitia “Kampeni ya Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima”.




Staa wa Soka Nigeria awa kichaa



Ijumaa ya January 12 2018 katika mitandao ya kijamii zimeenea taarifa za kusikitisha kuhusu staa wa zamani wa soka wa kimataifa wa Nigeria aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya Wilson Oruma kuripotiwa kuwa amepata ukichaa.

Oruma ameripotiwa kupata ukichaa baada ya kutapeliwa na mchungaji (Pastor) wake Naira bilioni 1.2 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 75 za kitanzania, ambapo mchungaji huyo alimshauri Oruma ampatie pesa hizo ili wafanye uwekezaji katika biashara ya mafuta.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Wilson Oruma licha ya kuiongoza Nigeria U-17 kama nahodha na kutwaa Ubingwa wa dunia 1993, amewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya kama Olympique Marseille, Sochaux, Servette na Lens.


Wandishi DRC waanzisha mgomo baada ya mwenzao kutekwa


Siku ya leo taarifa ambazo zimeshika vichwa vya vyombo vingi vya habari  nchini DR Congo ni kuhusu wandishi wa habari nchini humo kuitisha mgomo usio na kikomo baada ya kutekwa kwa mwandishi mwenzao.

Mwandishi wa habari wa Radio China (CRI), Molelwa Mseke Jide ameripoti kuwa waandishi wa Habari wa mji wa Beni nchini humo walikuwa kwenye kikao cha kuazimia mgomo huo.

Jide amesema kuwa mwandishi aliyetekwa ni Kiongozi Mkuu wa Radio Graben iliyopo mji wa Goma anayeitwa Kasereka Jadomwangwingwi.

Ameeleza kuwa mwandishi huyo alitekwa jana January 11, 2018 saa 11 jioni akiwa ndani ya msafara wa magari yaliyokuwa yakitokea mji wa Kasindi ambao upo mpakani mwa Congo na Uganda akielekea mji wa Beni.

Akisimulia mkasa huo Jide amesema msafara wa mwandishi huyo na watu wengine ulitekwa na majambazi waliovalia sare zilizofanana na za jeshi la taifa, ambapo waliwachukua watu wengine akiwemo na yeye