Kama wewe ni mpenzi au mdau wa muziki wa Hip Hop hapa Bongo, basi hakuna ubishi kuwa kolabo kubwa inayosubiriwa na mashabiki ni kolabo kati ya Joh Makini na Fid Q.
Je, unajiuliza kolabo hii huenda ikatokea? ukweli ni kwamba ondoa shaka kwa hilo kwani Joh Makini amesema kuwa ni muda tu unasubiriwa kwani wawili hao hawajahi kukaa pamoja kuzungumzia ishu za kolabo lakini endapo ikitokea nafasi ya kufanya hivyo watafanya.
“Mimi na Fid Q hatuna matatizo kama ambavyo watu wanafikiri, kwa sababu mimi mwenyewe binafsi sijawahi kuwa na matatizo naye na wala sijawahi kuona kama anamatatizo na mimi. Kwa hiyo mimi kama msanii na yeye kama msanii Chochote kinaweza kutokea anytime,“amesema Joh Makini kwenye kipindi cha Playlist cha Times FM huku akielezea kikwazo cha muda
“Ni vile labda hatujawahi kukutana kwenye hiyo vibe, hatujawa bado kwenye hiyo Chemistry ya kusema tufanye ngoma pamoja so you never know..hakuna mipaka 2018,“amemaliza Joh Makini.
No comments:
Post a Comment