Siku ya leo taarifa ambazo zimeshika vichwa vya vyombo vingi vya habari nchini DR Congo ni kuhusu wandishi wa habari nchini humo kuitisha mgomo usio na kikomo baada ya kutekwa kwa mwandishi mwenzao.
Mwandishi wa habari wa Radio China (CRI), Molelwa Mseke Jide ameripoti kuwa waandishi wa Habari wa mji wa Beni nchini humo walikuwa kwenye kikao cha kuazimia mgomo huo.
Jide amesema kuwa mwandishi aliyetekwa ni Kiongozi Mkuu wa Radio Graben iliyopo mji wa Goma anayeitwa Kasereka Jadomwangwingwi.
Ameeleza kuwa mwandishi huyo alitekwa jana January 11, 2018 saa 11 jioni akiwa ndani ya msafara wa magari yaliyokuwa yakitokea mji wa Kasindi ambao upo mpakani mwa Congo na Uganda akielekea mji wa Beni.
Akisimulia mkasa huo Jide amesema msafara wa mwandishi huyo na watu wengine ulitekwa na majambazi waliovalia sare zilizofanana na za jeshi la taifa, ambapo waliwachukua watu wengine akiwemo na yeye
No comments:
Post a Comment