Tuesday, 19 December 2017

Polisi wamshikilia Daktari Feki



Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mtu mmoja kwa kosa la kujifanya daktari, katika hospitali ya mkoa Sekou Toure.
Joseph Mbagata 25,mkazi wa mtaa wa Mabatini jijini humo amekamatwa leo Desemba 18 na jeshi hilo baada ya kubainika kwamba sio mwanataaluma na alikuwa akiwatapeli wagonjwa kwa kuwaomba hongo, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Taarifa kutoka kwa jeshi hilo zimesema kwamba mtuhumiwa alikuwa akiwaomba hongo, huku akiahidi kuleta dawa muhimu na pia kufanya mipango ili mgonjwa apate huduma kwa haraka.
Awali zilipatikana taarifa kuwa siku chache zilizopita alionekana mtu aliyevalia mavazi ya udaktari na kujifanya daktari, kisha anapita wodini kuwaona wagonjwa. Pia ilisemekana kuwa mtu huyo tayari amechukua Sh30,000 kwa mgonjwa ili aweze kumpatia matibabu.
Aidha baada ya tuhuma hizo kufika katika uongozi wa hospitali waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa, akiwa amevalia mavazi ya udaktari huku akiwa amesimama nje ya wodi ya upasuaji.
“Tumekuwa tukilalamikiwa kwamba kuna baadhi ya madaktari hapa hawana ujuzi wala hawajitambui, kumbe ni dhahiri kwamba hao watu wapo na kuanzia sasa lazima tufanye ukaguzi wa hali ya juu ili hali hiyo isije ikajitokeza tena maana ni sehemu ya kuhatarisha maisha,” amesema mmoja wa madakatri katika hospitali hiyo ambaye hakutaka kutajwa majina.
Baada ya daktari huyo feki kukamatwa, uongozi wa hospitali ulitoa taarifa polisi, ambapo askari walifika eneo la tukio na kumuweka mtuhumiwa chini ya ulinzi kisha kumfanyia upekuzi kwenye begi alilobeba na kukuta mavazi yanayotumiwa na madaktari katika vyumba vya upasuaji.
Polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi ametoa wito kwa wananchi hususani wagonjwa waliopo hospitalini akiwaomba kuwa makini na watu ambao ni matapeli wa aina kama hiyo wenye nia ovu dhidi yao.
Aidha pia aliwaomba viongozi wa hospitali zote kuendelea kutoa taarifa kwa polisi kuhusiana na watu wanao watilia shaka hospitalini, ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Moyes asema anauwezo Wa kufundisha timu Yoyote duniani



Meneja wa wagonga nyundo wa London West Ham United David Moyes, amesema uwezo alionao kwa sasa anaweza kuifundisha timu yoyote duniani na anataka kuonesha kama ana uwezo huo akiwa na klabu yake ya West Ham United.
Tangu alipoteuliwa kuwa kocha wa West Ham United Moyes, ameisaidia timu hiyo kutoka katika mstari wa timu zinazotakiwa kushuka daraja kwa kutokufungwa michezo mitatu.
"Nina uwezo wa kufanya kazi hii katika klabu yoyote duniani na nina uhakika nitalifanya hili nikiwa na West Ham," alisema kocha huyo.
Kocha huyo raia wa Scotland mwenye umri wa miaka 54, anajaribu kurudisha heshima yake baada ya kufanya vibaya alipoviongoza vilabu vya Manchester United, Real Sociedad na Sunderland.
West Ham kwa sasa iko nafasi ya kumi na tano katika msimamo wa ligi kuu ya nchini England.

Diwani wa Chadema afunguka kuhama chama kwa masharti




Diwani wa (CHADEMA), Kata ya Sombetini, Ally Bananga amesema yupo tayari kurudi (CCM) ikiwa viongozi wa chama hicho ambao wanataka kumnunua ikiwa watamuonyesha watu waliowatuma kumuua Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.
Mbunge wa jimbo la Kibamba, John Mnyika (kushoto) Diwani wa Sombetini Ally Banaga (Katikati) akiwa na Mstahiki Meya wa Ubungo Mhe. Boniface Jacob (Kulia).
Ally Banaga amedai kuwa yeye yupo tayari kurudi CCM kama viongozi hao watatimiza jambo hilo na kusema hiyo ndiyo itakuwa gharama yake kurudi CCM na siyo fedha au mali kama ambavyo wengine wanadaiwa kupewa.
"Ma CCM wanaotaka kuninunua, leo nataja gharama za kurudi CCM. Nionyesheni mliowatuma kumuuwa Mawazo, nitajiunga nanyi siku hiyo hiyo" alindika Ally Banaga
Aidha Banaga ameonyesha masikitiko yake makubwa kwa watu ambao wanakisaliti chama hicho na kusema kuwa wamesahau kuna watu kama kina Mawazo ambao wamekufa wakikipigania chama hicho.
"Nilishika jeneza lako nikikuangalia mwamba umelala. Ndipo nilipoamini kuwa sio stori, mwanaume wa kweli uliyefia vitani ukikitetea chama ambacho kuna Mambwa Koko yanakisaliti, yanakichezea yanakinajisi bila kuhisi maumivu yako ulipotoka roho kukipigania. Nilikuita kwangu Dar es Salaam tupumzike baada ya uchaguzi mkuu ambao CCM walikupora kwa nguvu ushindi wako, kaka ukakataa kwa neno moja " Nikiondoka Makanda watakufa moyo, ngoja niwape tafu, Tukutane Dodoma.....dah! Tukakutania Mwanza kwenye jeneza" alisema Banaga
Novemba 14, 2015 aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Busanda kupitia CHADEMA na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita aliuawa kwa kupigwa mapanga na watu wasiojulikana na kupelekea kifo chake.

Mo Awapa Siri vijana Wa Tanzania



Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group amefunguka na kuwapa siri vijana wa Tanzania kuwa wanapaswa kujikita zaidi katika kilimo kwani ndipo sehemu ambayo ina pesa nyingi sana.


Dewji alisema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na moja ya kituo cha habari na kusema kuwa yeye anatengeneza fedha nyingi zaidi kupitia kilimo ambacho anakifanya na kwamba anatengeneza faidi kubwa kupitia kilimo cha chai, korosho na katani.

"Niwambie siri moja vijana wenzangu kuna pesa nyingi sana kwenye kilimo, mimi nipo kwenye kilimo nipo kwenye katani, nipo kwenye chai, nipo kwenye korosho na ninatengeneza fedha nyingi sana kupitia kilimo" alisisitiza Mo Dewji

Mbali na Mohammed Dewji watu wengine maarufu ambao wamejikita kwenye kilimo ni pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu wa awamu ya nne Mhe. Mizengo Kayanza Pinda, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe.

Facebook na changamoto ya kutoa taarifa ya watumiaji



Mtandao wa Facebook unapambana na changamoto ya kutakiwa kutoa taarifa za watumiaji wake kutoka katika mamlaka mbalimbali duniani.

Ingawa mtandao huo kuna baadhi ya taarifa hauzitoi, idadi ya maombi ya taarifa imeongezeka ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita.

Marekani, India, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zinaongoza kwa kuomba taarifa za watumiaji ikiwa ni asilimia 73 ya maombi yote yanayotumwa.

Hata hivyo, wakati mamlaka zikiongeza maombi, Facebook nao wameongeza orodha ya taarifa ambazo hawawezi kuzitoa.

Zipo taarifa ambazo Facebook kabla ya kuzitoa humtaarifu muhusika lakini zipo ambazo zinatolewa bila mhusika kujulishwa.

“Asilimia 57 ya taarifa zilizoombwa na mamlaka za Marekani hazikuturuhusu kuwataarifu wahusika, ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 ukilinganisha na mwaka jana,” anasema Makamu Kansela wa Facebook, Chris Sonderby.

Mbali na maombi hayo ya mamlaka, Facebook pia imefungua milango ya maombi ya uwajibikaji katika taarifa zinazowekwa katika mtandao huo.

Katika kipindi cha mwaka mmoja jumla ya maombi zaidi ya  200,000 yalitumwa wakihusiana na taarifa za wizi wa hakimiliki na asilimia 68 ya kazi hizo ziliondolewa katika mtandao huo.

Monday, 18 December 2017

Mbaroni kwa kujifanya daktari



Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mtu mmoja kwa kosa la kujifanya daktari, katika hospitali ya mkoa Sekou Toure.
Joseph Mbagata 25,mkazi wa mtaa wa Mabatini jijini humo amekamatwa leo Desemba 18 na jeshi hilo baada ya kubainika kwamba sio mwanataaluma na alikuwa akiwatapeli wagonjwa kwa kuwaomba hongo, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Taarifa kutoka kwa jeshi hilo zimesema kwamba mtuhumiwa alikuwa akiwaomba hongo, huku akiahidi kuleta dawa muhimu na pia kufanya mipango ili mgonjwa apate huduma kwa haraka.
Awali zilipatikana taarifa kuwa siku chache zilizopita alionekana mtu aliyevalia mavazi ya udaktari na kujifanya daktari, kisha anapita wodini kuwaona wagonjwa. Pia ilisemekana kuwa mtu huyo tayari amechukua Sh30,000 kwa mgonjwa ili aweze kumpatia matibabu.
Aidha baada ya tuhuma hizo kufika katika uongozi wa hospitali waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa, akiwa amevalia mavazi ya udaktari huku akiwa amesimama nje ya wodi ya upasuaji.
“Tumekuwa tukilalamikiwa kwamba kuna baadhi ya madaktari hapa hawana ujuzi wala hawajitambui, kumbe ni dhahiri kwamba hao watu wapo na kuanzia sasa lazima tufanye ukaguzi wa hali ya juu ili hali hiyo isije ikajitokeza tena maana ni sehemu ya kuhatarisha maisha,” amesema mmoja wa madakatri katika hospitali hiyo ambaye hakutaka kutajwa majina.
Baada ya daktari huyo feki kukamatwa, uongozi wa hospitali ulitoa taarifa polisi, ambapo askari walifika eneo la tukio na kumuweka mtuhumiwa chini ya ulinzi kisha kumfanyia upekuzi kwenye begi alilobeba na kukuta mavazi yanayotumiwa na madaktari katika vyumba vya upasuaji.
Polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi ametoa wito kwa wananchi hususani wagonjwa waliopo hospitalini akiwaomba kuwa makini na watu ambao ni matapeli wa aina kama hiyo wenye nia ovu dhidi yao.
Aidha pia aliwaomba viongozi wa hospitali zote kuendelea kutoa taarifa kwa polisi kuhusiana na watu wanao watilia shaka hospitalini, ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Mwananchi.
Kama hujeelekezwa kiotomatiki, bofya
hapa 

Mkapa ateuliwa kuwa mwenyekiti Wa CCM kwa muda



Dar es Salaam.Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameteuliwa muda huu mjini Dodoma kuwa mwenyekiti wa muda wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuongoza uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa chama hicho.
Hatua hiyo inatokana na Rais John Magufuli kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho tawala, ili kupisha taratibu za uchaguzi wa nafasi hiyo.
CCM hufanya chaguzi zake, ikiwa ni pamoja na kumchagua mwenyekiti kila baada ya miaka mitano.m
Kama hujeelekezwa kiotomatiki, bofya
hapa .

Watiwa mbaroni Kwa Kosa la Uchochezi



Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Lushoto imewatia mbaroni watu wawili akiwemo askari mstaafu wa Jeshi la wananchi Sheubua Sempeho pamoja na mwalimu wa shule ya sekondari Edwin Sempeho kwa tuhuma za kufanya uchochezi uliosababisha makundi ya watu kuvamia ofisi ya serikali ya kijiji cha Masange kilichopo kata ya Gale wilayani Lushoto na kuzichana nyaraka zote kisha kuondoka na vitendea kazi kabla ya kuifunga kwa kutumia makufuli yao.
Akitangaza hatua hiyo katika mkutano wa hadhara kabla watuhumiwa hawajatiwa mbaroni,Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Lushoto Januari Lugangika amesema kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria kwa kuazuia watendaji wa serikali wasifanye kazi yao kwa muda wa siku nne hadi sasa.
.
Akielezea sababu zilizosababisha tatizo hilo,Mtendaji wa kijiji cha Masange kilichopo kata ya Gale wilayani Lushoto bwana Amani Sebuye amesema yeye kama mlinzi wa amani siku ya tukio makundi ya watu walitaka kwenda katika taasisi ya St Mary's inayomiliki shule za sekondari na zahanati wakidai kuwa taasisi hiyo ina lengo la kutaka kuchukua eneo lao la ardhi waliloachiwa na vizazi vya ukoo wao vilivyopita .
Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa taasisi ya Masista ya St Mary's sir Kahema amesema wao wanahati ya miaka 99 waliyopewa kisheria lakini hata kama baadhi ya maeneo yamejengwa nyumba na baadhi watu wa kijiji hicho watawaachia maeneo hayo isipokuwa hekari tatu tu kati ya 13 zilizovamiwa wanahitaji ili wajenge zahanati itakayosaidia wakazi hao .

Pori la Grumenti lafanikiwa kudhibiti majangili



Kaimu Mkuu wa pori la Akiba la Ikorongo Grumeti lililopo katika wilaya za Bunda na Serengeti Erdwin Njimbi amesema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti tishio la ujangili wa kutumia silaha za moto za jadi na mitego ya kienyeji ya kutumia nyanya ngumu kwa wanyama wadogo na wakubwa kama tembo na faru baada ya kuanzisha kitengo cha iinterejensia na kutumia mbwa wenye uwezo wa kugundua walipo wahalifu hata kama tukio limefanyika kwa siku kadhaa zilizopita na kwamba kufanikiwa kukamata zaidi ya majangili mia moja na sitini katika kipindi cha mwaka 2016/17.
Kaimu mkuu huyo wa pori la akiba la Ikorongo Grumeti amesema palikuwa na tishio kubwa la ujangili hasa wa kutumia mitego ya nyaya ambazo unasa wanyama wa aina zote bila kuchagua lakini baada ya serikali kuanza kutumia mbinu hizo ujangili umepungua kwa kiasa kikubwa na kumekuwa na ongezeko kubwa la wanyama wakiwemo simba pamoja na tembo.
Afisa kutoka Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori TAWA makao makuu Seleman Kirario anasema kuimarika kwa ulinzi kwenye maeneo hayo pia kunachangiwa na uelewa wa wananchi baada ya kuona manufaa yanayo patikana kutokana na uhifadhi pamoja na uanzishwaji wa jumuiya za hifadhi za jamii kwenye maeneo hayo.
Mkuu wa ya Serengeti Nurdin Babu anasema baada ya mafaniko katika uhifadhi halmashauri ya Serengeti imeanza kunufaika ambapo inapata zaidi shilingi milioni miambili tofauti na awali na wawekezaji nao wakataja miradi waliianzisha kwa manufaa ya wananc

Utalii Mpya Wapatikana Ngarongoro



Simba wanaopanda juu ya miti wamekuwa kivutio cha watalii katika eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kuwa ni kitu kipya.
Tabia ya simba imeanza kushangaza watalii na maofisa wanyamapori kwa kuwa si kawaida ya wanyama hao kupanda juu ya miti na kukaa.
Ofisa wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (Tawa), Suleiman Keraryo amesema simba wanaopanda miti walizoeleka katika Hifadhi ya Manyara pekee sasa inaonekana inasambaa hivyo kuhitajika utafiti zaidi.
"Hili si jambo la kawaida linaweza kusababishwa na vitu vingi lakini ni geni na kivutio kizuri kwa watalii," amesema leo Jumapili Desemba 17,2017.
Ofisa wanyamapori mkuu na ushirikishwaji jamii kwenye uhifadhi wa Tawa, Seth Ayo amesema hali hiyo si ya kawaida.
Hata hivyo, amesema jambo hilo linaweza kuwa linasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la joto ardhini.
"Hili ni jambo jipya na linasambaa tumeona simba juu ya miti Grumeti na leo hapa Ngorongoro," amesema.
Idadi kubwa ya watalii walikuwa wakitazama simba katika eneo la Kingo creta ya Ngorongoro ambaye alikuwa amepumzika juu ya mti.

Rayvanny aeleza lini kolabo ya Derulo itatoka



Msanii wa muziki Bongo, Rayvanny amefunguka kinachokwamisha kolabo yake na mkali wa R&B kutoka ardhi ya Trump.
Muimbaji huyo wa WCB ambaye June 26 mwaka huu alionekana studio na Jason Derulo amesema kuwa kazi hiyo ilishafanyika ila anasubiri Derulo aimalizie mixing kisha amtumie.
“Nilifanya ngoma kwenye studio yake lakini ratiba yake inakuwa imebana sana anakuwa anazunguka kwenye miji mingi tofauti, so akaniambia siwezi nikakutumia kitu ambacho hakijakaa proper subiri mpaka tuimix vizuri” amesema Rayvanny.
Hata hivyo Rayvanny ameeleza kuwa katika safari yake ya sasa ya Marekani ambapo ameenda kwa ajili ya ku-shoot video atafuatilia na hilo pia.

Hatua 10 za kuchukua wakati wakutafuta mchumba



Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.
Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.
Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.
Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.
Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.
Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.
Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.
Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.
Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.
Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.
Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.
KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.
Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.
PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.
TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.
NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.
Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.
TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.
Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.
Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.
SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.
Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.
SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana
NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.
TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.
KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.
Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.

Mambo yanayoweza kukuvunjia heshima



HAKUNA kitu kibaya maishani kama kuonekana upo katika daraja la chini na mtu wa kudharaulika kwenye jamii unayoishi. Kisaikolojia kuna madhara makubwa.
Ni imani yangu kuwa kila mwanadamu timamu anapenda kuheshimiwa lakini wengi wetu tunashindwa kupata heshima tunayoitaka kwa sababu hatufahamu jinsi ya kuishi mbele ya wenzetu.
Kitaalamu, hakuna jambo ambalo hutokea maishani bila sababu maalumu hivyo hata kudharauliwa kwako au kwetu ndani ya jamii tunayoishi kunatokana na jinsi tunavyoenenda.
Mwalimu wangu wa somo la maisha na saikolojia, Eric Shigongo, aliwahi kuniambia ‘Nothing happens in the sky, but the elements should be there,’ akimaanisha kuwa hakuna kitokeacho angani pasipo kuwa na dalili au sababu zake.
Naomba nianze kutoa njia za kukusaidia kurejesha heshima yako kwa kuperuzi na wewe baadhi ya dokezo muhimu zinazoweza kukusaidia kujitambua na kuweza kuyaepuka maisha ya kudharauliwa.
MUONEKANO
Kwanza kabisa ni jinsi unavyoonekana. Muonekano ninaouzungumzia hapa ni usafi wa mavazi na mwili kwa ujumla. Hata siku moja hakuna mchafu anayeheshimika katika jamii anayoishi hata kama ana kipaji kikubwa kiasi gani.
Kwa hiyo uchafu wa mavazi na mwili huchangia mtu kudharauliwa katika jamii anayoishi. Linaweza kuwa jambo dogo sana lakini ni moja kati ya sababu kubwa inayochangia kuporomoka kwa thamani yako mbele ya wenzako.
Mazungumzo
Hapa naomba nieleweke kuwa unachokizungumza kinaweza kukujengea heshima au kukubomolea heshima. Kauli zisizo na busara zitakufanya udharaulike kwa kila mtu. Uropokaji usiokuwa na mantiki huchangia kuporomosha heshima yako hasa kama utakuwa muongeaji zaidi. Biblia inasema penye wingi wa maneno hapakosi uovu.
UTENDAKAZI WAKO
Ndugu zangu, siku zote heshima ya mtu ni kazi. Watu wengi hawapendi kufanya kazi kwa bidii huku wengine wakijiendekeza kwa tabia ya kuombaomba, jambo hilo halifai kwa vile huchangia kubomoa heshima yako mbele ya jamii. Fanya kazi usiishi bila kujishughulisha.
KUTOTIMIZA AHADI
Kama una tabia za kuahidi mambo halafu unashindwa kuyatekeleza, basi unajiweka katika nafasi mbaya ya kutunza heshima yako katika jamii unayoishi. Bora ukwepe kutoa ahadi kuliko kuahidi na kutotimiza.
SIFA ZISIZO NA MAANA
Nakumbuka msemo mmoja kutoka kwa mwandishi mwandamizi aliyekuwa mtaalamu wa falsafa za maisha, marehemu Adolf Balingilaki, ambao unasema kwamba:
“Ukitafuta heshima kwa gharama ya juu, basi utalipwa dharau kwa bei nafuu.”
Msemo huu unamaanisha nini? Siku zote ukiwa unafanya mambo yako kwa ajili ya kusifiwa au mazungumzo yako kuwa ya kujiinua, watu watakudharau.
KUTOKUWA MWAMINIFU
Suala la uaminifu ni pana, kuna uaminifu wa fedha, siri, dhamana na mambo kama hayo, hivyo ni vema kila unachoaminiwa lazima ukitunze kwani ukiwa mtu wa kuvunja uaminifu fahamu kuwa utashusha heshima yako.