Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Lushoto imewatia mbaroni watu wawili akiwemo askari mstaafu wa Jeshi la wananchi Sheubua Sempeho pamoja na mwalimu wa shule ya sekondari Edwin Sempeho kwa tuhuma za kufanya uchochezi uliosababisha makundi ya watu kuvamia ofisi ya serikali ya kijiji cha Masange kilichopo kata ya Gale wilayani Lushoto na kuzichana nyaraka zote kisha kuondoka na vitendea kazi kabla ya kuifunga kwa kutumia makufuli yao.
Akitangaza hatua hiyo katika mkutano wa hadhara kabla watuhumiwa hawajatiwa mbaroni,Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Lushoto Januari Lugangika amesema kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria kwa kuazuia watendaji wa serikali wasifanye kazi yao kwa muda wa siku nne hadi sasa.
.
Akielezea sababu zilizosababisha tatizo hilo,Mtendaji wa kijiji cha Masange kilichopo kata ya Gale wilayani Lushoto bwana Amani Sebuye amesema yeye kama mlinzi wa amani siku ya tukio makundi ya watu walitaka kwenda katika taasisi ya St Mary's inayomiliki shule za sekondari na zahanati wakidai kuwa taasisi hiyo ina lengo la kutaka kuchukua eneo lao la ardhi waliloachiwa na vizazi vya ukoo wao vilivyopita .
Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa taasisi ya Masista ya St Mary's sir Kahema amesema wao wanahati ya miaka 99 waliyopewa kisheria lakini hata kama baadhi ya maeneo yamejengwa nyumba na baadhi watu wa kijiji hicho watawaachia maeneo hayo isipokuwa hekari tatu tu kati ya 13 zilizovamiwa wanahitaji ili wajenge zahanati itakayosaidia wakazi hao .
No comments:
Post a Comment