Tuesday, 19 December 2017

Mo Awapa Siri vijana Wa Tanzania



Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group amefunguka na kuwapa siri vijana wa Tanzania kuwa wanapaswa kujikita zaidi katika kilimo kwani ndipo sehemu ambayo ina pesa nyingi sana.


Dewji alisema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na moja ya kituo cha habari na kusema kuwa yeye anatengeneza fedha nyingi zaidi kupitia kilimo ambacho anakifanya na kwamba anatengeneza faidi kubwa kupitia kilimo cha chai, korosho na katani.

"Niwambie siri moja vijana wenzangu kuna pesa nyingi sana kwenye kilimo, mimi nipo kwenye kilimo nipo kwenye katani, nipo kwenye chai, nipo kwenye korosho na ninatengeneza fedha nyingi sana kupitia kilimo" alisisitiza Mo Dewji

Mbali na Mohammed Dewji watu wengine maarufu ambao wamejikita kwenye kilimo ni pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu wa awamu ya nne Mhe. Mizengo Kayanza Pinda, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe.

No comments:

Post a Comment